Buriani Mzee Ruksa: Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,013
115,120
Wanabodi
20240303_145349.jpg
Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya malalo ya makao ya milele.

Mara ya Kwanza Kulisikia Jina la Ali Hassan Mwinyi.
Kwa mara ya kwanza jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977 nikiwa darasa la 3 shule ya msingi, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake aliyejiuzulu kutokana na kashfa hiyo, bali Makamo wa pili wa rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa!, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa!. Wakafuatiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma!, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Samweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma, na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza pia akapumzishwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa sio mtu wa mchezo hata kidogo!, kwani baada ya kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua mjini Mwanza, likaanzia kumfagia Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, kwanza wote wakafutwa kazi, kisha wakarejeshwa vijijini kwao, kwa kusombwa na Land rover 109 usiku usiku na kurudishwa kwenye their places of domicile na mwisho wa siku walikuwa kushitakiwa kwenye ile kesi maarufu, "Kesi ya Mauaji Mwanza" ya mwaka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri wa wakati huo, Wakili Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote, walikwenda na maji na walikula mvua za kutosha!. Ni kupitia tukio hilo ndipo nilipoanza kulisikia jina la Ali Hassan Mwinyi. Hiki kisa cha Kesi ya Mauaji Mwanza pia nilikihadithia kwenye bandiko hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Mwaka 1976 kule Mwanza kwenye eneo la Kigoto, watuhumiwa wa mauaji ya vikongwe walikuwa tortured to death na maofisa wa polisi!.

Mzee wangu, Andrew Mayalla (RIP) akiwa RSO wa Mwanza, akawanusuru watuhumiwa wawili, Masanja Makhula Mazengenuka na Isaak Mwanamkoboko kutoka eneo la Kigoto baada ya mateso makubwa, wakiwa njiani wakamweza hawajala chochote kwa muda wa siku 3 za mateso ya usiku na mchana!.

Akaamua kuwapeleka Bugando, on their way akasimama mahali kuwanunulia soda na kitafunio, soda waliweza kunywa, kutafuna walishindwa!.

Bugando akawakabidhi kwa Dr. Nkulila. The next day they were both died!, hivyo mtuhumiwa mkuu wa kuhusika na vifo hivyo, ni aliyewapeleka hospitali na sio wale waliowatenda na kuwa tortures!.

Hizo ni enzi za Nyerere, tulikuwa tukiishi Isamilo ya chini, next door ni RPC alikuwa akiitwa Mkwawa, nyumba ya tatu ni DSO na nyumba ya nne ni RMO, Mzanzibari mmoja akiitwa Dr. Dahoma!.

Baada ya Taarifa kumfikia Nyerere, kuanzia Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, Rashid Mfaume Kawawa aliondolewa na kushushwa cheo!. Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alipoteza uwaziri kwa kujiuzulu!. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu, anyeshughulikia TISS, Peter Siyovelwa, alijiuzulu!. Watendaji wakuu wakiongozwa na IGP wa wakati huo Samweli Pundugu alipoteza kazi, kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma!. Mkurugenzi wa TISS, Emelio Mzena, alipoteza kazi, kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma!. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo, alipoteza kazi, DC wa Mwanza pia alimwaga unga!

Ikaja kwa Mzee, RSO, RPC, DSO na OCD wa Mwanza wote walistaafishwa kwa manufaa ya umma, tulihamishwa usiku usiku na kurudishwa kijijini (detention fulani za Nyerere).

Wakati yote haya yakifanyika, mimi nilikuwa mdogo sana sikujua ni nini kinaendelea ili kilichofuatia ni mpaka ilipoanza kuunguruma, Kesi ya Mauaji Mwanza, na kulisoma jina la Dingi Gazetini, ndipo nikafunguka macho nini kilitokea, na thanks God, mtu pekee aliyenasuka ni Dingi, Andrew Mayalla, kufuatia kazi kubwa na mzuri iliyofanywa na Wakili Murtaza Lakha, na sijui kama Tanzania, tuna mawakili wa kiwango chake!.
Paskali
Sijui uwajibikaji wa aina hii ya enzi za Nyerere, ulikuja kupotelea wapi, siku hizi watuhumiwa wanakufa mikononi mwa polisi, and no body cares!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, jijini Dar es Salaam, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza! alikuwa darasa moja na mtoto wa Malecela, Seche. Kitendo cha mtoto wa rais na mtoto wa Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu John Malecela kusoma shule moja, na halikuwa jambo dogo!, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati huo hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kukubali misaada ya masherti na kugeuka nyuma akageuka jiwe, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Ali Hassan Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa!.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wenye siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali pamoja, na wanyama wengine kwasababu nguruwe ni haramu kwa Waislamu,
na isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni haramu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembecha miaka kadhaa baadae.

Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja wa wana vuguvugu hawa ni mshikaji wangu sana wa deski moja sekondari ya Tambaza, akiitwa Hassan.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akaruhusu mitumba, akaruhusu Chai Maharage, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko, market economy.

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma Watanzania tunaendelea kuzifaidi rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na kale ka copy pale Zanzibar!, cha mtu rahimu kama yeye!.

Akina sisi, tayari tumeisha mshauri Mama, kama hoja Hivyo kama HII sauti ni sauti ya kweli, na kama vipi 2025, ataona ni parefu, hakuna ubaya, akikapisha kale ka Copy kule kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun
(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
 
Ni kipindi cha nguo kupigwa viraka,Enzi hizo watu wanavaa nguo imepigwa viraka vya rangi tofauti tofauti

Watu walivaa nguo zilizotoboka ,Ilikuwa hakuna kumshangaa mtu

Wanafunzi wanaenda shule peku peku bila viatu na unawakuta wanakimbia mchaka mchaka kwa uzalendo

Enzi hizo sherehe za Chrismass na Idi zilikuwa sherehe kweli

Watu kabla ya miezi miwili christmass au idd mnaanza kutafuta mchele na kuuhifadhi ndani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe,Unaweza enda siku ya sherehe sokoni ukakosa vinywaji na vyakula
 
Kuna kipindi alipwaya mpaka Nyerere aliamua kumsaidia.

Alishindwa kabisa kucontrol bunge , serikali ilikua inaanguka.

Anyways nitamkumbuka kwa kuuza Loliondo kwa waarabu.

Familia yake ina bahati sana ya Uongozi ila ni vilaza.
 
Kuna kipindi alipwaya mpaka Nyerere aliamua kumsaidia.
Hapana hakupwaya ila ni Mchonga ndie alikuwa akimuungilia kwenye Uraisi wake kwasababu kifikra hawa walikuwa ni Viongozi wawili waliokuwa na MITIZAMO tofauti kabisa.

Kuna STORI👈 zinasema Mzee Rukhsa kidogo ajiuzulu URAISI kwa sababu ya Mchonga Interference.

Mwinyi alikuwa ni Mliberali Nyerere alikuwa ni Mkomunisti.
 
Hapana hakupwaya ila ni Mchonga ndie alikuwa akimuungilia kwenye Uraisi wake kwasababu kifikra hawa walikuwa ni Viongozi wawili waliokuwa na MITIZAMO tofauti kabisa.

Kuna STORI👈 zinasema Mzee Rukhsa kidogo ajiuzulu URAISI kwa sababu ya Mchinga Interference.
Kulikua na resistance bungeni alishindwa kucontain chama na serikali yake.

Nyerere akaamua kuingilia kati.

Jamaa alikua shallow sana ila ndio hivyo tena , kawa Rais na watoto wake wawili pia ni marais.
 
Kulikua na resistance bungeni alishindwa kucontain chama na serikali yake.

Nyerere akaamua kuingilia kati.

Jamaa alikua shallow sana ila ndio hivyo tena , kawa Rais na watoto wake wawili pia ni marais.
Kwanyinyi Wakomunisti mliokuwa mumetuingiza kwenye Siasa za Kijinga zilizofeli Duniani hamkufurahi, lakini sisi Waliberali siasa za Mzee Mwinyi ndio tulichakarika na kupata Mitaji.
 
Siku ya leo, tunampunzisha Mzee wetu, Rais Mtaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kwa jina maarufu la Mzee Rukhsa, kwenye nyumba yake ya milele.

Kwa mara ya kwanza Jina la Ali Hassan Mwinyi, nililisikia mwaka 1977, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Nyerere, alipolazimika kujiuzulu kutoka na kashfa ya vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, huko Mwanza mwaka 1976.

Mwinyi hakuwa peke yake, bali Makamo wa pili wa Rais na Waziri Mkuu, Rashidi Mfaume Kawawa, pia aliondolewa, Waziri wa Ofisi ya Rais, anyeshughulikia Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa aliondolewa, wakafutiwa na watendaji wakuu wa vyombo vya usalama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emelio Mzena, akastaafishwa kwa manufaa ya umma, Mkuu wa Polisi, IGP Swamweli Pundugu akastaafishwa kwa manufaa ya umma.

Baada ya Baba wa Taifa kuwafagia kule juu, fagio la chuma, likatua Mwanza, Mkuu wa Mkoa Peter Kisumo, akaenda na maji, RPC wa Mwanza, RSO, OCD, na DSO wa Mwanza, wakafutwa kazi na kushitakiwa kwenye kesi maarufu ya Mauaji Mwanza yam waka 1976. Mtu pekee aliyesalimika kati ya hao washtakiwa ni mtu mmoja tuu, aliyeitwa Andrew Mayalla, na salama yake, mdogo wake anayetwa Mathew Kasanga, kumuwekea wakili mahiri Murtaza Lakha, kumtetea kaka yake, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha!.

Tukio hilo lilileta mageuzi makubwa nchini mwetu, kwanza Idara ya Usalama wa Taifa, ilifumuliwa na kusukwa upya kwa kufanyiwa mabadiliko makubwa, ikaletwa sheria ya usalama wa Taifa, ya 1976, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na katiba mpya ya mwaka 1977.

Jina la Ali Hassan Mwinyi, nikaja kukutana nalo tena shule ya msingi, tukisoma na mtoto wake Hussen Mwinyi (Dr)aliyenitangulia madarasa mawili. Baada ya ya shule ya Msingi nikajiunga shule ya sekondari ya Tambaza, ile mwaka 1985 Rais Mwinyi anakuwa Rais wa Tanzania, yule mtoto wake Hussein Mwinyi alikuwa anasoma PCB Tambaza!, kitendo cha mtoto wa rais kusoma shule moja, halikuwa jambo dogo, sasa ndio nikazidi kumfahamu Ali Hassan Mwinyi kwa karibu, wakati hapo Tambaza pia tuko na mtoto wa Nyerere na Mtoto wa Mkapa, darasa moja.

Mwanzo wa Mwinyi Kutwa Mzee Ruksa.

Wakati Mwinyi anachukua urais ile 1985, hali yetu ya Uchumi ili dhollfu bin taaban, baada ya vitavya Kager ana Mwalimu Nyerere kutangaza miezi 18 ya kufunga mikanda, mambo kiukweli yalikuwa magumu, tumekula unga wa Yanga, kutoka Marekani ambao kule kwao ni chakula cha mifugo!, Watu wamevaa magunia, sandarusi hadi sisi wanafunzi nchi nzima tumevaa uniforma ya kitambaa cha madurufu, ambacho nip amba chafu ya kutupa!.

Mahitaji muhimu yote ni kwa resheni kupitia maduka ya kaya, tulikuwa tunapanga foleni siku nzima kusubiria kuuziwa kilo mbili mbili za sukari, hivyo Watoto wote mnatumwa, ili kuwahi foleni, watu walidamka asubuhi na kupanga mawe, gari linaweza kuja saa 10 jioni au siku nyingine kutoka bila bila, haliji kabisa.

Nchi za mabeberu zilimpa Mwalimu Nyerere masherti magumu ya kutupa misaada, ndipo Mwalimu akaamua kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, bora aachie ngazi, kwa mtindo wa kung’atuka na kumpisha Mwinyi. Hivyo Mwinyi aliipokea nchi ikiwa kwenye dhiki kubwa.

Baada ya ya kuingia rais Muislamu, kukaibuka vikundi vya Waislamu wa siasa kali, kwanza waligomea Nguruwe wasichinjiwe mahali panoja, na nyama ya nguruwe isiuzwe bucha zile zile za nyama ya kawaida.

Vikundi hivyo vikaleta vurugu za kulazimisha nyama ya nguruwe ipigwe marufuku kwasababu ni harafu, na kuanzishwa mihadhara ya kashfa, kwa wanazuoni wa Kiislamu kuikosoa Biblia na kusema nguruwe hata kwenye Biblia ni Haramu. Vurugu hizo zikapelekea kuvamia mabucha ya nguruwe na kuvunja kisha kukimbilia kujificha misikitini kulikopelekea vurugu za Msikiti wa Mwembechai. Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa, wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, ikiwemo Msikiti wa Mwembechai Kuvamiwa, tena ikatokea mmoja waw ana vuguvugu haw ani mshikaji wangu sana wa sekondari ya Tambaza, Hassan Mkokola.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akalipindua Azimio la Arusha lililoweka miiko ya uongozi na kuleta Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kufanya biashara na kumiliki mali na hapa sasa ndio viongozi wa umma wakaanza kuwa matajiri na kuupindua uchumi wetu kutoka uchumi wa kijamaa na kuingia kwenye uchumi wa kibepari wa nguvu ya soko,

Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzia kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa!, Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!.

Japo Rais Mstaafu, Ali Haasan Mwinyi, Mzee wa Rukhsa, ametutoka kwa kutangulia mbele ya haki, huku nyuma rukhsa zake, tutanzienzi milele, na tena sio tuu ametuachia Rukhsa, pia ametuachia na copy pale Zanzibar, cha mtu rahimu kama yeye!, kama vipi 2025, kama Mama ataona ni parefu, hakuna ubaya, akimpisha kale ka Copy kaje huku kutufungulia ruksa nyingine zote zilizobakia!.

Buriani Ali Hassan Mwinyi, Mwendo Umeumaliza.

inna lillahi wa inna ilayhi rajiun (in arabic إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)

Paskali.
Emilio Mzena and Andraw Mayalla.Hospital ya Mzena,Paskali Mayalla kuna uhusiano?.
 
Kuna kipindi alipwaya mpaka Nyerere aliamua kumsaidia.

Alishindwa kabisa kucontrol bunge , serikali ilikua inaanguka.

Anyways nitamkumbuka kwa kuuza Loliondo kwa waarabu.

Familia yake ina bahati sana ya Uongozi ila ni vilaza.
Hakupwaya,
Ni Nyerere ndio alikuwa na wivu, na hakuwa anataka Mwingi afanye vitu bila kumshirikisha, eg Mwinyi alipoamua kukubali mashart ya IMF ikiwemo kudevalue currency hio ilimuuma sana Nyerere, and btw, Nyerere bado alikuwa na wafuasi wengi sanaaaa, so kitendo cha Mwinyi kwenda against sera za Nyerere kilileta maneno mengi sanaaaaa
 
Hapana hakupwaya ila ni Mchonga ndie alikuwa akimuungilia kwenye Uraisi wake kwasababu kifikra hawa walikuwa ni Viongozi wawili waliokuwa na MITIZAMO tofauti kabisa.

Kuna STORI👈 zinasema Mzee Rukhsa kidogo ajiuzulu URAISI kwa sababu ya Mchinga Interference.

Mwinyi alikuwa ni Mliberali Nyerere alikuwa ni Mkomunisti.
Nyerere alikuwa anazingua, alikuwa mkosoaji mkuu wa Mwinyi, alitamani mwiny akaze kwenye ujamaa
 
Back
Top Bottom