Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti ya habari,sanaa utamaduni na michezo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO, MHESHIMIWA JOSEPH OSMUND MBILINYI (MB), KUHUSU BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18


1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, naomba kuwasilisha mbele ya bunge lako maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika Wizara hiyo, mwaka wa fedha 2017/18.

Mheshimiwa Spika, kabla sijawasilisha maoni hayo, napenda kutumia fursa hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema, na kuniwezesha kusimama hapa kufanya kazi hii muhimu kwa taifa, ya kuhakikisha misingi ya kikatiba ya kulinda na kuenzi haki na uhuru wa kutoa na kupata habari inalindwa na kuenziwa katika nchi yetu.


Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani kwa Naibu Waziri Kivuli wa Wizara hii, Mheshimiwa Devota Minja (Mb) kwa ushirikiano mkubwa anaonipa, lakini kipekee kwa kutumia taaluma yake kama mwanahabari, kutoa ushauri wa kitaalam ambao umesaidia sana katika maadnalizi ya hotuba hii. Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hii kuwapongeza wanahabari na wasanii wote nchini, kwa uvumilivu na ujasiri wao wa kufanya kazi bila woga licha ya changamoto na vikwazo vingi vinavyowakabili kipindi hiki. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazipongeza timu za michezo mbalimbali na wanamichezo wote ambao kwa nyakati tofauti wanaipatia nchi yetu heshima kubwa kwa kushiriki na kutuwakilisha katika mashindano mbalimbali ya ndani na ya kimataifa yaliyofanyika katika mwaka huu wa fedha unaomaliza muda wake pamoja na kuwa na msaada kidogo kutoka serikalini.


Mheshimiwa Spika, dunia haitanielewa kama sitatambua mchango mkubwa wa Wana Mbeya ambao umenifanya niwe nilivyo leo. Sitasahau heshima kubwa wana mbeya waliyonipa ya kunifanya kuwa Mbunge wa kwanza Tanzania Bara na Visiwani kupata kura nyingi kuliko Mbunge yeyote katika Bunge hili katika uchaguzi Mkuu wa 2015. To cut the story short Mr. Speaker, I am the most voted Mp in this house and I am proud of it. Nasema asanteni sana wana Mbeya kwa heshima hii kubwa mliyonipa, na kazi hii ninayoifanya hapa ni mojawapo ya ishara kwamba; naitendea haki heshima mliyonipa.


Mheshimiwa Spika, baada ya salamu hizo za utangulizi, naomba sasa nianze kuzungumzia masuala ya kisera na kibajeti katika Wizara hii ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.






2. UHURU WA KUJIELEZA NA KUTOA MAONI

Mheshimiwa Spika, Wakati tarehe tatu Mei wiki hii dunia imeadhimisha siku ya uhuru wa habari, tasnia ya habari Tanzania inapita katika majaribu makubwa kuliko wakati wowote katika historia ya nchi yetu. Uhuru wa kupata na kutoa habari hapa nchini umeporomoka kwa kasi ya kutisha hasa baada ya Serikali hii ya awamu ya tano kuingia madarakani.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ripoti ya The Freedom Press ya mwaka 2017 iliyochapishwa katika gazeti la The Citizen la tarehe 3 Mei,2017 ni kwamba; Tanzania haina uhuru kamili wa habari, na kwamba imeshuka kwa alama tatu kutoka alama 61 mwaka 2016 hadi 58 mwaka huu wa 2017. Kushuka huko kumeifanya Tanzania kushika nafasi ya 122 kati ya nchi 198 duniani zilizofanyiwa utafiti kuhusu uhuru wa habari.

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa ya Tanzania kushuka katika viwango vya uhuru wa habari ni kutungwa kwa sheria zinazodhibiti uhuru wa habari yaani Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Cyber Crimes Act) ya mwaka 2015; Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari (Media Services Act) ya mwaka 2016 pamoja na kushtakiwa na kufungwa kwa waandishi wa habari na wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers).

Mheshimiwa Spika, ripoti hiyo ya The Freedom Press, inasema kwamba pamoja na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuendesha kampeni kubwa ya kupambana na rushwa lakini

Serikali yake imekuwa haina uvumilivu (tolerance) wa kukosolewa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba mwishoni mwa mwaka 2016 takriban watu 10 walikuwa wameshtakiwa kwa kilichodaiwa kumkashifu Rais, chini ya sheria ya makosa ya kimtandao. Aidha, mwanzilshi mwenza wa mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo, naye alikamatwa na kushtakiwa chini ya sheria hiyo. Matukio haya ya ukamataji, kuwashtaki na kuwafunga watu ambao wametumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao, kumeipotezea sifa nchi yetu katika medani za kimataifa na kuiweka katika orodha ya nchi zinazokandamiza uhuru wa habari duniani.


Mheshimiwa Spika, Mkutano Mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1946 uliazimia na kueleza yafuatayo kuhusu uhuru wa habari, naomba kunukuu;

“Freedom of information is a fundamental human right and……the touchstone of all the freedom to which the United Nations is consecrated”

Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba, uhuru wa kupata taarifa ni msingi wa haki zote za binadamu.

Mheshimiwa Spika, Tamko la Umoja wa Mataifa linafafanua pia kuwa kila mmoja ana haki ya kujieleza na kutoa maoni ikiwa ni pamoja na haki ya kutoa maoni bila kuingiliwa na ikijumuisha pia kutoa na kupokea taarifa kutoka kwenye chombo chochote cha habari.

“Everyone has the right to freedom of opinion and expression, this right includes freedom to hold opinions without interference and to seek, receive and impart information and through any media and regardless of frontiers”.

Mheshimiwa Spika, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 inakazia tamko hilo la Umoja wa Mataifa ambapo inaeleza kuwa; naomba kunukuu;

“kila mtu-

(a) Anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(b) Anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi;

(c) Anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na

(d) Anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na kuhusu masuala muhimu kwa jamii.



Mheshimiwa Spika, tamko hili la Umoja wa Mataifa linaonekana kuwa kitendawili kisichokuwa na majibu kwa serikali ya awamu ya tano. Hii ni kutokana na matukio kadhaa yanayoashiria kukiuka misingi ya uhuru wa habari na haki kutoa maoni ndani ya nchi kutokana na matukio kadhaa nitakayoeleza;



i. Kupotea kwa Ben Saanane na Kukamatwa na Kuteswa kwa Wananchi

Mheshimiwa Spika, toka mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka 2016 ambapo ni takribani miezi sita sasa Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Ben Saanane, hajulikani aliko na vyombo vya dola vimekuwa kimya juu ya tukio hilo.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa kabla ya kupotea kwa Ben, miezi kadhaa ya nyuma alitumia mtandao wa facebook kuhoji uhalali wa serikali kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma, na kutoa rai kwa viongozi wakuu nao vyeti vyao kuhakikiwa ikiwemo PhD ya Mkuu wa nchi. (Nimeambatanisha sehemu ya maandiko ya Ben ya Facebook kwenye vielelezo kabla hajapotea).

Mheshimiwa Spika, Baada ya andiko la Ben ulijitokeza mjadala mkali kiasi cha kujitokeza watetezi wengi dhidi ya hoja za Ben Saanane kutoa maoni yake akiwemo Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo. Kushindwa kujibu kwa hoja maandiko ya Ben Saanane vikaibuka vitisho mbalimbali dhidi yake ambapo taarifa zake zilipelekwa Polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa (Nimeambatanisha taarifa ya Vitisho kama alivyoandika Ben Saanane Mwenyewe).

Mheshimiwa Spika, mtu aliyemtishia Ben Saanane kupitia simu namba 0768 797982 katika ujumbe wake wa vitisho ambao Ben aliuripoti Polisi aliitaja Serikali kuwa mhanga wa uhuru wa maoni wa Ben. Katika ujumbe huo mtishaji alisema, na nitanukuu “Ben unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata. Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefika hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia. Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu?. You are too young to die. Tunajua utaandika na hili. Andika lakini next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha. Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia. Andika Ben. Andika sana, ongea. Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu.”

Mheshimiwa Spika, zipo dhana kadhaa kuhusu kupotea kwa Ben Saanane kunakotokana na ujumbe huo wa mtishaji.

(i) Dhana ya Kwanza ni kuwa mtuma ujumbe ana uhusiano wamoja kwa moja na Serikali ama kwa kuwa afisa wa Serikali au kutumwa na Serikali kutuma ujumbe huo kwa sababu aliyehojiwa kuwa na PhD ni kiongozi mkuu wa nchi.

(ii) Dhana ya pili: Hakuna rekodi zozote kutoka Serikalini za kukanusha kuhusika na ujumbe huo dhidi ya Ben, pamoja na kuwa aliripoti katika vyombo vya Serikali, hivyo ukimya wa Serikali unaleta mashaka kuwa inafahamu mahali Ben alipo na ndio maana inashindwa kuhitimisha zoezi la utafutwaji wa Ben.

(iii) Dhana ya tatu ni kushangazwa kwa mtishaji kuwa hakutarajia Ben kwa kiwango chake cha elimu afikie hatua ya kuhoji uhalali wa PhD ya mkuu wa nchi kwa kuwa ndio jambo la mwisho Ben kuhoji katika rekodi za mitandao yake ya kijamii, hivyo hisia za umma ni kuwa Serikali ina siri kali juu ya hatma ya Ben.

(iv) Dhana ya nne; ni kuwa mtishaji wa Ben alikuwa na mpango wa kuondoa uhuru wa Ben kwa kusema kuwa “Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu.” Hivyo kupotea kwa Ben kunaashiria kuwa alitekwa nyara.

(v) Dhana ya tano ni kuwa; baada ya kukamilisha hatua za utekaji nyara wa Ben, hatua zilizopangwa na mtishaji wa Ben ni kutekeleza mpango wa mauaji dhidi yake kutokana na kumtishia awali kuwa “You are too young to die.”

(vi) Dhana ya sita ni kuwa, mtishaji wa Ben anadhihirisha kuwa ni muuaji mzoefu kwa kitendo cha kumtishia Ben kuwa hata rafiki yake alitangulia.


Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali, ithibitishe ukweli wowote juu ya dhana hizi sita za kupotea kwa Ben Saanane. Tunasema hivi kwa sababu vyombo vya dola vimejizolea sifa ya kuendelea kuwakamata vijana mbalimbali na kuwafungulia mashitaka ya uchochezi kutokana na kuamua kutumia uhuru wao wa kikatiba kutoa maoni. Sifa hizo ndio zinachagizwa na mtishaji wa Ben kuitaja Serikali katika vitisho vya ujumbe mfupi wa simu na kuwa Serikali haiwezi kukwepa kutoa taarifa za mahali alipo Ben Rabiu Saanane.

Mheshimiwa Spika, ukiacha suala la Ben Saanane wapo vijana wengi ambao wamekuwa wakikamatwa na kuteswa hasa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi na Kituo cha Polisi cha Oysterbay Dar Es Salaam, kutokana na kuandika na kutoa maoni yao mtandaoni ambayo huonekana ikikosoa serikali. Hivi karibuni alikamatwa kijana kutoka Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe Mdude Nyagali pamoja na Nicas David, ambapo baada ya Mdude kukamatwa huko Mbozi aliteswa bila kupelekwa hospitali na baadae kusafirishwa kwenda Dar es Salaam ambapo pia alipata mateso akiwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay bila ya kupelekwa Mahakamani.

Mheshimiwa Spika, ni baada ya Wakili msomi na Rais wa TLS Mhe. Tundu Lissu (Mb) kuwaeleza Polisi kuwa angepeleka maombi Mahakama Kuu ya Habeas Corpus ndipo aliporudishwa tena Mbozi na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi ambapo mwezi wa Aprili mwaka 2017 Mahakama imemkuta bila hatia yoyote.

Mheshimiwa Spika, mwendelezo wa Serikali kutumia Sheria ya “Cyber Crime” ya mwaka 2015 umekuwa mwiba mchungu wa watu kutoa maoni yao ndani ya nchi yao. Ni ishara kuwa serikali haipendi matumizi ya mitandao ya kijamii na ndiyo maana Rais wa nchi wakati anapokea ndege za Bombadier Jijini Dar es Salaam alisema kuwa anatamani malaika washuke kuizima mitandao hiyo na kusahau kuwa wakati wa uchaguzi mkuu 2015 alitumia mitandao hiyo hiyo kujinadi na kutafuta kura.

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa Sheria ya Cyber Crime ya mwaka 2015 inatumika kama malaika kuzuia uhuru wa kutoa maoni kwenye mitandao ya kijamii. Mamlaka makubwa waliopewa Polisi kukamata computer au simu za mikononi tuliyaeleza kwa kirefu wakati sheria hiyo ilipokuwa inapitishwa Bungeni kwenye Bunge la kumi. Ndiyo maana mpaka sasa nchi washirika wa maendeleo na Jumuiya ya Kimataifa, wameikosoa sheria hiyo kuwa inakiuka misingi ya demokrasia na utawala bora; na kwa sababu hizo Serikali ya Marekani iliamua kuinyima Tanzania fedha za miradi ya MCC jumla ya Dola milioni 500.

Mheshimiwa Spika, orodha ya vijana wa Kitanzania ambao tayari walishapandishwa kizimbani kutokana na Sheria hii ya Cyber Crime kwa kuikosoa Serikali ya awamu ya Tano na hususan Kiongozi Mkuu wa Nchi, orodha hiyo ya vijana ni kubwa kuliko matumizi ya vifungu vingine vya Sheria hii, jambo linaloifanya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iamini kuwa utunzi wa Sheria hii ulilenga kuzuia uhuru wa kujieleza ili Serikali hii iendelee na vitendo vya ukandamizaji wa haki nyigine na ikose kabisa watu wa kuikosoa.

Mheshimiwa Spika, naomba kueleza rasmi kwamba, Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Cyber Crime Act) ya 2015 ni ya kibaguzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, makada wa Chama cha Mapinduzi wanatoa matusi kwa viongozi wa Vyama vya Upinzani lakini sheria hiyo haitumiki kuwachulia hataua (nimeambatanisha kielelezo). Kutokana na hali hiyo, mtu yeyote anaweza kujenga hoja kuwa sheria hiyo wametungiwa wapinzani pekee na si upande mwingine. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kuleta marekebisho ya sheria hiyo ili kuondoa vifungu kandamizi ambavyo vinalalamikiwa na wadau na wananchi kwa ujumla.



1. SERIKALI KUINGILIA VYOMBO VYA HABARI

i. Kuvamiwa kwa Kituo cha Clouds TV na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Mheshimiwa Spika, tarehe 17 mwezi Machi mwaka 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye inasemekana jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite, alivamia kituo cha luninga cha Clouds kinachomilikiwa na Kampuni ya Clouds Media Group akiwa ameambatana na askari wenye silaha za moto na kuingia moja kwa moja kwenye chumba cha habari (news room).

Mheshimiwa Spika, imeelezwa na kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa lengo la uvamizi huo lilikuwa kuwatisha na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha “Weekend Chat Show” maarufu kama Shilawadu. Kitendo hicho cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni cha kulaaniwa na watu wote wanaopenda na kujali misingi ya uhuru wa habari.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua za serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Habari wa wakati huo Mheshimiwa Nape Nnauye kuunda kamati ya uchunguzi na kamati hiyo kuwasilisha taarifa yake Serikalini, badala ya kuchukua hatua dhidi ya Mkuu huyo wa Mkoa, ikaamua kumfukuza kazi na kutupa kapuni taarifa ya Kamati pamoja na juhudi alizochukua Mheshimiwa Nape Nnauye kulinda maslahi mapana ya uhuru wa vyombo vya habari.

Mheshimiwa Spika, kitendo alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam si tu kinakiuka uhuru wa vyombo vya habari bali kinakiuka misingi ya utawala bora na kimeonesha kuwa Mkuu huyo wa Mkoa hana chembe ya maadili ya uongozi wa umma kwa mujibu wa kiapo alichokula kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kwa mujibu wa Sheria lakini hana mamlaka ya kuamuru namna ya askari wa Jeshi la Polisi, Magereza au Uhamiaji kufanya kazi zao. Kwa namna inavyoonekana hata Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam CP Simon Sirro hana haja ya kuwepo kwa sababu Mkuu wa Mkoa ndiye amekuwa akiagiza askari kufanya majukumu yao kinyume kabisa na Sheria ya Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inaunga mkono kauli na uamuzi wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari kususia kuripoti taarifa zinazomhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili iwe fundisho kwa viongozi wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakiwanyanyasa waandishi wa habari wakati wanapotekeleza majukumu yao.





ii. Kuvamiwa kwa Waandishi wa Habari na Wafuasi wa Prof. Lipumba

Mheshimiwa Spika, Tarehe 22 Aprili 2017 katika Hoteli ya Vina iliyopo Mburahati, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam lilitokea tukio la kusikitisha ambapo waandishi wa habari walivamiwa wakati wakitekeleza majukumu yao kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na kiongozi wa Wilaya wa Chama cha Wananchi CUF.

Mheshimiwa Spika, waandishi wa habari walipigwa na kuumizwa na kikundi kilichoratibiwa na Prof. Ibrahim Lipumba ambaye amekuwa chanzo cha mgogoro ndani ya Chama ambacho alitangaza hadharani kuachia ngazi zake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, mmoja wa wanakikundi cha Prof. Lipumba Ndugu Abdul Kambaya alikiri hadharani kuwa vijana waliowavamia waandishi wa habari ni vijana wanaotokana na genge lao. Cha kushangaza zaidi ni kuwa toka, matamshi hayo ayatoe hadharani amekaa muda mrefu mtaani bila kuchukuliwa hatua yoyote hali inayoonesha kuwa serikali inajua vema uwepo wa watu hao ambao wamewaumiza waandishi wa habari.

Mheshimiwa Spika, Baadhi ya waandishi wa habari kama vile Asha Bani wa gazeti la Mtanzania na Fredy Mwanjala wa kituo cha runinga cha Channel ten, ni miongoni mwa waandishi ambao wameumizwa na kikundi hicho cha Prof. Lipumba.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawashauri waandishi wa habari kutotoa taarifa zinazomhusu Prof, Lipumba na watu wake kama wambavyo wamefanya kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba huo ni mkakati wa serikali wa kutaka kuvigombanisha vyombo vya habari na vyama vya Upinzani nchini hasa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inalaani matukio yote yanayoashiria kuvuruga amani ya nchi yetu.



iii. Kukamatwa kwa Waandishi wa Habari kwa amri za Wakuu wa Wilaya

Mheshimiwa Spika, ukiacha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yupo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ambaye naye amekuwa akiwanyanyasa waandishi wa habari. Tarehe 21 Desemba 2016 aliamuru Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Ndugu Halfan Lihundi kukamatwa na kuwekwa ndani kwa saa 24 kwa sababu ya kutoa na kuripoti taarifa mbalimbali zinazohusu matatizo ya wananchi hasa migogoro ya ardhi na tatizo la Maji bila kuishirikisha au kupata kibali cha Serikali ya Wilaya.

Mheshimiwa Spika, taarifa zinaonesha kuwa Halfan Lihundi alihojiwa na Jeshi la Polisi na kufunguliwa jalada la uchochezi. Baada ya kelele za wadau ilipofika tarehe 22 Desemba 2016 mwandishi huyo wa habari aliachiwa huru na Jeshi la Polisi bila masharti yoyote. Huu ni uonevu ndani ya Taifa letu. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kueleza itaacha lini uonevu wa kiasi hiki? Aidha, Serikali sasa iwapatie semina elekezi wakuu wa Mikoa na Wilaya ili watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia sheria.

Mheshimiwa Spika, Kama hiyo haitoshi tarehe 7 Februari, 2017 waandishi wa habari wawili walikamatwa na kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Usa River mkoani Arusha, kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti. Waandishi waliokamatwa ni Bahati Chume wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Kilimanjaro na Dorine Alois kutoka kituo cha Sunrise Radio cha jijini Arusha.


Mheshimiwa Spika, Waandishi hao walikamatwa walipokuwa wakifuatilia habari ya mgogoro kwenye machimbo ya kokoto katika Kijiji cha Kolila mpakani mwa Wilaya za Arumeru na Hai.

Baadaye waliandika maelezo juu ya madai kuwa waliingia katika kijiji hicho bila taarifa ya mkuu wa Wilaya Mnyeti.


Mheshimiwa Spika, ikumbukwe pia kuwa ni Mnyeti na Makonda ambao wote kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakitoa maneno ya kulidharau Bunge kinyume na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na wameshakwisha kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya masuala hayo na Bunge kuazimia kuwasamehe.

Mheshimiwa Spika, Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga Godwin Gondwe ambaye ni Mwandishi wa habari wa siku nyingi na anayetambua kazi za habari, aliamuru Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani waandishi wa habari wawili waliokuwa wakifuatilia tukio la kufukuzwa kwa wachimbaji wadogo 3,000 eneo la mlima wa Mazigamba, Kijiji cha Nyasa Wilayani Handeni.

Mheshimiwa Spika, Tukio hilo lilitokea tarehe 5 Novemba 2016, majira ya saa 8 mchana ambapo mwandishi wa Clouds Tv Salehe Masoud na mwadishi wa Star Tv MacDonald walikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 8 huku mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Nasra Abdallah akifanikiwa kutoroka.

Mheshimiwa Spika, Agizo la Gondwe kutaka waandishi hao wakamatwe lilitokea baada ya wanahabari hao kufika katika eneo la mgodi na kupata picha ambako nyumba za wakazi wa eneo hilo zimechomwa moto na baadhi ya mali kuteketea.


Mheshimiwa Spika, Baada ya wanahabari kufika eneo hilo Polisi waliwaamuru kuzima Kamera zao kutokana na kupewa amri ya Mkuu wa Wilaya. Mmoja wa Askari Polisi alihoji waandishi hao kwanini wamekwenda kwenye eneo hilo bila ruhusa ya Mkuu wa Wilaya, hivyo kutaka waondoke kwakuwa hawana kibali wala taarifa za ujio wao.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, waandishi hao waliwaeleza Polisi kuwa hawalazimiki kuwa na vibali kufika kwenye matukio ya aina hiyo na kwamba wamekwenda ili kufahamu tukio hilo kwa undani, kwani kuna taarifa kuwa baadhi ya wananchi wameuawa kwenye operesheni hiyo na maiti zao bado hazijaondolewa.

Mheshimiwa Spika, Baada ya mabishano kama dakika 45 ndipo mmoja wa mapolisi hao aliwaongoza waandishi kwa Mkuu wa Operesheni ambapo nae alikataa kuzungumza chochote na kuwataka waende kwa Mkuu wa Polisi kituo cha Handeni.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na kwamba waandishi hao waliomba kupiga picha kwanza ndipo waende huko, lakini walikataliwa ambapo Polisi huyo aliwaamuru waliopo chini yake kuwaondoa waandishi eneo hilo huku wakiwasindikiza na mitutu ya bunduki na wengine wakiendelea kupiga mabomu.

Mheshimiwa Spika, Baada ya kukamatwa waandishi hao walipelekwa kituo cha polisi Handeni ambapo walikaa huko kuanzia saa 8 mchana hadi saa 3 usiku ambapo walitolewa kutokana na juhudi za wahariri akiwemo Katibu wa Jukwaa la wahariri Neville Meena kuzungumza na Gondwe.


Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Wilaya wanaonekana kutumia madaraka yao vibaya kunyang'anya uhuru wa waaandishi wa habari na kuwanyima wananchi haki ya kujua kinachoendelea nchini. Matumuzi mabaya ya madaraka yanawafanya baadhi ya wakuu wa Wilaya kuwa wahariri kwenye vyombo vya habari na papo hapo, kuwa walalamikaji na waamuzi ambao wanaweza kuamua mtu kuswekwa ndani kwa amri zao.

Mheshimiwa Spika, viongozi hawa na wengine wenye tabia kama hizi hawafai kuwepo katika utumishi wa umma. Ni rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa serikali kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafukuza kazi kwa sababu wametenda makosa ya kukiuka uhuru wa vyombo vya habari, kutumia madaraka yao vibaya pamoja na kukiuka Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuileta Bungeni Sheria inayowapa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya uwezo wa kuwaweka rumande raia kwa masaa 48 ili sheria hiyo tuifute kwa kuwa haina maslahi kwa Taifa na hutumiwa na Serikali kukandamiza haki za kiraia ndani ya Taifa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe maelezo ni wapi Askari Polisi wametoa mamlaka ya kuwazuia waandishi wa habari kufanya shughuli zao za kutafuta habari ambazo huzifanya kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na sheria zilizopo.



iv. Kufungiwa kwa Magazeti na Stesheni za Radio

Mheshimiwa Spika, Katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha 2016/2017 tulieleza masikitiko yetu kufuatia uamuzi wa serikali kupitia Gazeti la serikali namba 03 juzuu ya 97 wa kufuta gazeti la Mawio katika orodha ya magazeti nchini bila hata kusikiliza wamiliki na waendeshaji wa gezeti hilo. Hata hivyo, mwezi Machi mwaka huu 2017, Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam ilikosoa uamuzi wa Serikali wa kulifungia gazeti hilo. Mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu alinukuliwa akisema kuwa uamuzi wa Serikali kulifungia gazeti la Mawio ni mwendelezo wa falsafa ya “Nyonga kwanza kusikiliza baadae”.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kauli ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulaani Serikali kulifungia gazeti la Mawio, bado Serikali ikalifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 na mpaka sasa bado lipo kifungoni na waandishi wa habari wa gazeti hilo kuendelea kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Spika, vituo vya radio navyo havijawa salama kutoka kwenye mkono wa Serikali, kwa sababu tarehe 29 Agosti mwaka 2016 vituo vya radio Five na Magic FM vilifungiwa na Waziri mwenye dhamana ya habari ili kuchunguzwa na Kamati ya Maudhuo ya TCRA. Kitendo cha kuvifungia vituo hivyo vya radio kwa sababu za jumla kuwa vimekuwa vikitangaza habari za uchochezi, ni kitendo cha uonevu na mwendelezo wa falsafa ile ile ya nyonga kwanza sikiliza baadae.


v. Utekaji nyara na Ukamataji holela wa Wasanii Nchini

Mheshimiwa Spika, tarehe 26 Machi, 2017 Msanii Emmanuel Elibariki alias ‘Ney wa Mitego’ alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi kwa kuueleza umma ukweli juu ya kukosekana kwa uhuru wa kujieleza kupitia wimbo wake maarufu “WAPO”. Kutokana na hali hiyo, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) liliamua kupiga marufuku wimbo wa WAPO usichezwe mahali popote. Hata hivyo, baadaye serikali iliruhusu wimbo huo upigwe bila kutoa sababu za kuukataza katika hatua ya kwanza. Jambo hili linaifanya Serikali kuonekana kufanya mambo bila mpangilio na hivyo kuifanya kutoaminika katika maamuzi yake.

Mheshimiwa Spika, Utamaduni wa kuwakamata wasanii haukuishia kwa Msanii Ney wa Mitego. Msanii Roma Mkatoliki alitekwa na kurejeshwa kwa namna ya utatanishi sana ambayo mpaka sasa kuna maswali mengi ambayo hayajapatiwa majibu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina juu ya watekaji wa ROMA Mkatoliki na Jeshi la Polisi liwasake na kuwakamata watu wote waliohusika na utekaji huo ili wafikishwe Mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao. Ni vema sasa serikali ikachukua hatua ya kuwakamata watekaji hao kuonesha kwamba kweli ina mkono mrefu.

Mheshimiwa Spika, Aidha Kambi Rasmi ya Upinzani tunampa ujasiri ROMA atoke mbele ya jamii aeleze kwa uwazi yaliyomkuta na aliyofanyiwa, hii itasaidia katika kutambua ni kikundi gani kinafanya vitendo hivyo na kujua kuwa wanafanya hivyo kwa niaba ya nani.

vi. Bunge Live bado Kizungumkuti

Mheshimiwa Spika, tarehe 27 Januari 2016 serikali kupitia Waziri wa Habari wakati huo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ilitoa kauli hapa Bungeni kuwa imezuia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kurusha moja kwa moja vipindi vya Bunge kutoka Dodoma.

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa iliyotolewa wakati huo ilikuwa ni gharama kubwa ya kurusha matangazo hayo kwa sababu Serikali ilikuwa imeamua kubana matumizi na kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kauli wadau kadhaa ikiwemo Kampuni ya Uhai Media na asasi zingine binafsi zilijitokeza na kuonesha nia ya kurusha matangazo ya Bunge moja kwa moja, serikali ilikuja na sababu nyingine kwamba wananchi wanashindwa kufanya kazi kutokana na kuangalia mijadala ya Bunge, hivyo imesitisha matangazo hayo ili wananchi wapate nafasi ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, niliihoji serikali kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika hotuba yangu ya mwaka wa fedha uliopita, kuwa kama tatizo ni fedha ni kwa nini hawaruhusu mashirika binafsi kurusha matangazo ya Bunge? Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kusisitiza kuwa, uamuzi wa kutorusha matangazo ya Bunge sio unawakosesha wananchi haki yao kwa mujibu wa ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali pia inarudisha nchi yetu nyuma kwa kuondoa utamaduni tuliokwisha kujijengea kwa muda mrefu wa wananchi kuona namna wawakilishi wao wanavyotekeleza majukumu yao na serikali ikiwajibika kwao kupitia Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, badala ya vyombo vya habari vya umma kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi waweze kufuatilia vikao vya Bunge, tena kwa kipindi hiki muhimu cha kujadili Bajeti ya Serikali, sasa hivi vyombo hivyo vimekuwa vikirusha matangazo yanayomuonesha Mkuu wa nchi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Ni dhahiri kuwa sasa kuna watu katika nchi hii wanaona wana sifa za pekee kuliko Mhimili wa Bunge na hivyo ni wao tu ndio wanastahili kuonekana moja kwa moja wakitekeleza majukumu yao. Huu ni ubaguzi na ubinafsi wa hali ya juu kufanywa na viongozi wakubwa wa nchi.

Mheshimiwa Spika, taarifa zinaonesha kuwa tayari Bunge limepata leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuruhusu Channel yake kufanya kazi ya kurusha matangazo. Kwa kuwa ilionekana ni gharama kulitumia Shirika la Utangazaji Tanzania, na kwa sasa kama nilivyoeleza channel ya Bunge imepata leseni na ithibati kutoka TCRA ni rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa Kamisheni ya Bunge kwa kushirikiana na wadau kurudisha utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ili wananchi waendelee kupata haki yao ya kuona na kujua kinachoendelea Bungeni.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ina uhakika kwamba Bunge kwa kurusha mubashara matangazo yake, wadhamini wengi watajitokeza na hivyo channel hiyo itakuwa inafanya biashara nzuri na hivyo miradi mingi ya Maendeleo ya Bunge ambayo ilikuwa imesimama kwa ukosefu wa fedha itaweza kuendelea.



2. KUYUMBA KWA UCHUMI NA ATHARI ZAKE KATIKA TASNIA YA HABARI



Mheshimiwa Spika, kumekuwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa na athari katika ukuaji wa sekta binafsi. Hii ni pamoja na uamuzi wa kuondoa au kupunguza matangazo ya serikali kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu binafsi.



Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo kufungwa kwa biashara nyingi katika miji na majiji nchini kumepunguza matangazo mbalimbali ya biashara katika vyombo vya habari hali inayopelekea vyombo vingi vya habari kuyumba kimapato. Hii si ishara njema katika sekta ya habari nchini, Kambi Rasmi ya Upinzani inadhani kuwa huu ni mkakati wa serikali kuviua vyombo vya habari binafsi ili kuendelea kutumia vyombo vya habari vya umma pekee.



Mheshimiwa Spika, ukisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka fedha 2016/2017, moja ya sababu zilizochangia Mashirika ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania) na TSN (Kampuni ya Magazeti ya Serikali) kushindwa kukusanya maduhuli pamoja na mambo mengine, serikali inakiri yenyewe kuwa ni kushuka kwa biashara sokoni kutokana na baadhi ya biashara kufungwa na makampuni mengi kubana matumizi na kupunguza bajeti.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kuangalia namna bora ya kuhakikisha kuwa pamoja na kupenda sana matumizi ya vyombo vya habari inatoa sera na kodi ambazo ni rafiki katika ukuaji wa sekta hii ikiwemo na vyombo vinavyomilikiwa na serikali. Kambi ya Upinzani inapenda kutoa tahadhari kuwa, kama hatua hazitachukuliwa, tutarajie vyombo vingi vya habari kufunga shughuli zao na waaandishi wengi wa habari pamoja na waajiriwa wengine wa sekta ya habari kusimamishwa kazi kutokana na ukata.



Mheshimiwa Spika, ni lazima serikali itambue kuwa sekta ya habari inategemea ukuaji wa uchumi na sekta binafsi kwa upande mwingine, hivyo ni lazima kwa mwaka ujao wa fedha Bunge liangalie namna bora ya kuishauri serikali kwenye masuala ya kodi na ukuaji wa biashara ili kuweza kuchochea ukuaji wa sekta ya habari.



Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge inaitaka serikali kuhakikisha kuwa inavipa bajeti ya kutosha vyombo vinavyomilikiwa na umma na kuacha kuviingilia ili viwe na ubunifu wa namna bora ya kuhimili ushindani wa soko kwa sababu moja ya changamoto katika vyombo hivyo ni kushindwa kuhimili soko la habari. Haishangazi kuona Rais anawasiliana kwa karibu na vyombo vya habari binafsi na sio mashirika ya habari ya umma kwa sababu ya kukosa weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao. Kambi ya Upinzani haishangai kuona TBC wakitangaza habari za uongo zilizopikwa mitandaoni bila kufanya tafiti za kina kabla ya kuzitoa kwa umma. Ni lazima TBC ijitathmini kuacha ushabiki wa kisiasa na kuegemea kwenye taaluma.


3. WIZI WA KAZI ZA WASANII

Mheshimiwa Spika, wakati wa serikali ya awamu ya nne nilizungumza kwa kirefu namna ya kulinda kazi za wasanii nchini. Moja ya pendekezo ambalo baadae lilichukuliwa na serikali ni kutumia stika maalumu ambazo zitatoa utambulisho wa kazi halisi za wasanii kuzuia wizi wa kazi za wasanii. Pamoja na serikali kutumia stika za Mamlaka ya Mapato (TRA) bado tatizo hili halikupata ufumbuzi. Hii ni kutokana wizi wa kazi za wasanii kuendelea kuwepo.


Mheshimiwa Spika, Pamoja na kuwa sisi Kambi Rasmi ya Upinzani ndio chanzo na msingi wa hoja ya matumizi ya stika katika kulinda kazi za wasanii, napenda kusisitiza na kuieleza serikali na Bunge lako tukufu kuwa kwa sasa dunia imekwenda mbele zaidi kwa sababu kwa sasa biashara ya muziki na filamu inafanyika kwa kutumia mitandao zaidi na wasanii duniani kote sasa wanafanya biashara ya muziki kwa kutumia mitandao kama vile Youtube, iTune na mitandao mingine kusambaza na kuuza kazi zao.Mheshimiwa Spika, kwa hapa nchini wasanii wanaojitambua wamekuwa wakitumia mtandao maarufu wa MKITO, Blogs, Websites zingine na biashara zao kuendelea na kuwanufaisha kiuchumi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa na kauli na hatua za kipropaganda anazofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kutangaza kuwa anazuia kazi za wasanii wa filamu kutoka nje ya nchi, hii inatokana na kutokufahamu kuwa kuzuia filamu za nje sio kinga ya kuzuia wizi wa kazi za wasanii au hata kuboresha soko la kazi zao bali njia pekee ni kuhakikisha kuwa wanaboresha kazi zao kwa kuongeza ubunifu na kutumia njia za kisasa kuuza na kutangaza kazi zao.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kuacha kuitazama mitandao ya kijamii kwa jicho hasi na badala yake waione kama sehemu ya ajira kwa wasanii wetu ili kuwasaidia kukuza kipato chao na kujitangaza kimataifa. Aidha Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawaasa wasanii kutotumika kisiasa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye hata hivyo amesusiwa na vyombo vya habari kutokana na matendo yake yasiyokuwa ya kimaadili na matumizi mabaya ya madaraka yaliyopitiliza.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kulieleza Bunge lako tukufu kuhusu agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam la kazuia kazi za wasanii wa nje kuingia nchini kama ndio msimamo wa serikali au ni kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee na kama anayo mamlaka kisheria kutoa agizo alilotoa au ni kujitaftia umaarufu baada ya kukataliwa na tasnia ya habari.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa rai kwa wasanii nchini kuimarisha vyama vyao vilivyopo kama vile TUMA, CHAMUDATA, BONGO MOVIE! Na vingine ili kusimamia maendeleo yao halisi na sio kutumika kisiasa na watu ambao hawana uelewa wa kazi ya sanaa na zaidi ya kutaka kujipa umaarufu wa kisiasa. Kambi Rasmi ya Upinzani inapenda kusisitiza kuwa kazi za sanaa na sheria zinazosimamia hati miliki ni za kitaifa na kimataifa na katika masuala hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa agizo ambalo hajui athari zake katika kazi ya sanaa hasa kwenye mikataba ya kimataifa.


4. SEKTA YA MICHEZO

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza hoja yake kwa mwaka uliopita kuwa, ili tuweze kuendeleza michezo ni lazima serikali iwekeze katika michezo. Serikali haiwezi kutegemea mafanikio katika michezo kama fedha za maendeleo kwenye Wizara mpaka Februari 2017 imetolewa kwa asimili 6 pekee.


Mheshimiwa Soika, Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa michezo kwa kiwango kikubwa Duniani ni biashara na sio burudani kama ambavyo hapa Tanzania inavyochukuliwa.Kwa dhana hiyo ya michezo ni biashara, ni lazima tufanye uwekezaji, kwani biashara yoyote ile, ili iende vizuri ni lazima uwekezaji wa maana ufanyike.


Mheshimiwa Spika, katika uwekezaji huo ni lazima uanzie kwenye ngazi ya chini, kwa kuwatayarisha watoto wetu kuwa wachezaji wazuri wa michezo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, katika hilo naomba kunukuu ushauri uliotolewa na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, kwa Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuhusu nini kifanyike ikiwa ni mwanzo wa uwekezaji katika michezo;

“Mheshimiwa Spika, Shughuli za Michezo na utamaduni katika halimashauri zinakuwa chini ya idara ya Elimu ya Msingi ambayo ina majukumu makubwa sana ya kushughulikia elimu ya Msingi na sehemu kubwa ya bajeti yake ya matumizi ya kawaida inatoka serikali kuu. Kitengo cha Michezo na utamaduni kinakuwa kimemezwa na shughuli za Elimu ya Msingi hivyo kushindwa kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.



Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaishauri serikali kuunda idara mpya ya Michezo na utamaduni katika halimashauri hapa nchini ili kuinua na kuhamasisha shughuli za Michezo na utamaduni katika nchi yetu kwavile zitalazimisha serikali kuu na Halimashauri kutenga fedha za kutosha katika bajeti kwa ajili ya idara hiyo ya Michezo na utamaduni”.



Mheshimiwa Spika, kwa mwaka uliopita, tulisisitiza kuwa ni lazima tuhakikishe kuwa Viwanja vya Michezo vinaboreshwa ili kukidhi mahitaji ya sekta ya michezo. Aidha tunapenda kurudia kuwa, ni lazima viwanja vyote vilivyopokwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku wakijua kuwa ni mali ya wananchi wote kwa kuwa vilipatikana kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza. Ni lazima baadhi ya Halmashauri na Serikali Kuu ivichukue viwanja vya CCM kwa kuwa Chama hicho kimeshindwa hata kuviendeleza.



5. SEKTA YA UTAMADUNI

Mheshimiwa Spika, serikali hii bado haijaona umuhimu wa kuendeleza sekta ya utamaduni nchini. Ieleweke kuwa utamaduni si tu ni utambulisho wa utaifa bali pia sekta hiyo ikiboreshwa vizuri inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa kuvutia watalii wa nje na ndani.

Mheshimiwa Spika, wakati wa awamu ya nne serikali iliunda Kamati iliyokuwa inaratibu na kukamilisha mchakato wa vazi la taifa. Kamati hiyo ilitumia fedha lakini hatujaweza kujulishwa kama mchakato huo ulikamilika..Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kueleza mbele ya Bunge hili mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi na nini hatma yake.



6. UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara hii ilitengewa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, hadi kufikia Februari mwaka huu Wizara ilipokea shilingi 190,324,000 sawa na asilimia 6 pekee. Hii ina maana kwamba, bajeti ya maendeleo haijatekelezwa kwa asilimia 94.


Mheshimiwa Spika, kutotekeleza bajeti ya maendeleo katika wizara hii kwa asilimia 94, ni dharau na kunaonyesha jinsi Serikali isivyothamini sekta ya habari, michezo na utamaduni. Ikumbukwe kwamba Chama cha Mapinduzi na Serikali yake ndio wanufaikaji wakubwa wa sekta hii hasa kipindi cha kampeni za uchaguzi kinapofika. Kipindi cha kampeni utaona jinsi CCM inavyojikomba kwa wasanii na kuwatumia katika kampeni zao, lakini uchaguzi unapopita wanawasahau wasanii na wanamichezo kwa ujumla. Kutenga bajeti ndogo kwa sekta hii na mbaya zaidi kutoitekeleza kwa asilimia 94 ni majibu tosha kwamba sekta hii sio kipaumbele kwa Serikali. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawatahadhariha wasanii na wanamichezo wote nchini, kuwa makini na ulaghai unaofanywa na CCM na serikali yake kwa kuwapa vijizawadi kipindi cha kampeni kuonyesha kwamba inawajali, lakini ‘deep down’ haina mpango nao kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa mwendo huu wa utoaji fedha za miradi ya maendeleo ni ishara kuwa serikali haina nia ya kuendeleza sekta zilizopo ndani ya Wizara hii.



7. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie hotuba yangu kwa kumnukuu msomi na mwanafalsafa wa fasihi andishi wa nchini Marekani, Jill McCorkle aliyesema: “By limiting or denying freedom of speech and expression, we take away a lot of potential. We take away thoughts and ideas before they even have the opportunity to hatch. We build a world around negatives – you can’t say, think, or do this or that”



Mheshimiwa Spika, kwa tasfiri isiyo rasmi ni kwamba, kwa kuminya uhuru wa habari na kujieleza tunaondoa mambo mengi yenye faida. Tunatupilia mbali mawazo na fikra kabla hata hayajafikia hatua ya kuzaliwa. Tunajenga mazingira katika ulimwengu hasi ambapo huwezi kusema chochote, huwezi kufikiri, huwezi kufanya hiki wala kile. Kwa maneno mengine Mheshimiwa Spika, ni kama uko kwenye ulimwengu wa giza, na kwa hali hiyo hakuna hatua yoyote ya maendeleo inaweza kupigwa.


Mheshiiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuachilia uhuru wa habari Tanzania. Tunataka haki na uhuru wa maoni na kujieleza ambao msingi wake ni kikatiba ya nchi yetu uheshimiwe. Tunataka vyombo vya habari kama mhimili wa nne wa dola viachwe vifanye kazi kwa uhuru. Tunataka vyombo vya habari vya umma vinavyoendeshwa na kodi ya watanzania virushe matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Tunataka vitendo vya utekaji na utesaji wa wasanii vikomeshwe. Tunataka mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe. Tunataka vitendo vya ukamataji, kushtakiwa na kufungwa kwa waandishi wa habari kwa kesi za kubambikwa za uchochezi vikomeshwe. Tunataka matukio ya uvamizi wa vyombo vya habari kwa malengo ya kushinikiza habari fulani itoke au isitoke yakomeshwe. Tunataka matukio ya kuwashambulia na kuwaumiza na hata kuwauwa waandishi wa habari wakiwa wanatekeleza majukumu yao yakomeshwe. KWA KIFUPI TUNATAKA UHURU WA HABARI TANZANIA. “We urge the Government of Tanzania to bring back our freedom of Press”.


Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha.



Joseph Osmund Mbilinyi (Mb)

WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI

YA UPINZANI BUNGENI, KATIKA WIZARA YA HABARI,

UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO

5 Mei, 2017






KIELELEZO A: MAONI YA BEN SAANANE KUHUSU UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK

Sakata la vyeti feki na hali ya PHD ya maganda ya korosho ya Mhe.Magufuli.::

Angalizo:Hasira hazitasaidia hapa.
Uchochezi ni kushindwa kufafanua kitu ulichokitetea mbele ya Maprofesa.
Najadili Sakata la Vyeti Feki na hali ya Ph.D ya Mhe.Magufuli.
Tuanzie hapa kwanza ndio tusonge mbele.Wale watakaomtetea sitaki kusikia eti tulimuona kwenye Korido za Chuo au Canteen au mara nilikua pale Chuoni wakati anasoma hapo.
Huo sio utetezi wa Kisomi.Jihadhari!

Kabla wale Malaika hawajatushukia kuzima mitandao na pia Wakati tunaendelea kusubiri atoe nyaraka alizoahidi miezi 5 iliyopita kuhusu Mshahara wake twaweza kuendelea kihivi ili akitoka hadharani atoke na nyaraka na ushahidi wa hili pia

Kwa kulitendea haki zoezi la Uhakiki wa Vyeti linaloendelea ,Naamini Watumishi wote wa Umma kuanzia Rais ,Nasisitiza kuanzia Rais uhakiki huo ulipaswa upite huko.

Najua Urais hauhitaji hiyo taaluma yake lakini nataka tuibue hoja ya uhalali wa Ph.D na suala la Uadilifu kitaaluma.

Ni jambo la Msingi sana katika vita hii ya kupambana na Mafisadi wa Elimu .

Ofisi kuu lazima ioneshe mfano na Rais Magufuli kama Raia namba moja ni lazima akaguliwe asiache shaka yoyote katika kuhakikisha kile anachojiita kuwa ndiye(Daktari wa Falsafa katika Kemia) .Alionesha mfano katika ukaguzi wa Silaha na pia suala la Usafi.Zoezi la Silaha limepita sasa ni ukaguzi wa vyeti Mkuu wetu.Sitarajii urudi nyuma

Niliwahi kuuliza kama Shahada ya Uzamivu ya Mhe.John Pombe Magufuli ni halalali na kama imekidhi vigezo Aliingia Lab kweli?Alienda kui-defend kweli kwenye Baraza la Taaluma mbele ya Maprofesa? Council ilikua imeundwa na akina nani? Sitaki kuhusisha maamuzi yake na suala lake la Academic maana haihusiani na İntelligence but just to be curious kipindi hiki anapotakiwa kuonesha mfano tu Kuna waziri wa Ulinzi wa Ujerumani nadhani Karl-Zu aliwahi kukutwa amedesa Ph.D yake ikamgharimu Uwaziri Suala hili linapaswa kujibiwa na Magufuli mwenyewe na sio msaidizi au Prof.Aliyemsimamia.

Tena Prof.Akijitokeza tutamuuliza kama kuna Publication yoyote aliyofanya kabla ya VİVA.

Ha ha ha!

Miaka hiyo nikiwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili niliposikia Waziri Magufuli katunukiwa Ph.D,kwa ufahamu tu wa kitaaluma na pengine kiherehere tu kilichoniandama niliwahi kuhoji hata kule JF kuhusu Duration ya Ph.D yake.Sikupata majibu.Tunalifufua tena kipindi hiki kwa kuwa yeye ni msema kweli ndio maana Prof.Ndalichako kama waziri wa Elimu ana ujasiri wa kukemea vyeti feki na alikemea wabunge na Mawaziri.

Niliuliza kama kuna Chapisho(Publication) yoyote aliyofanya kwenye journals

Najua sio lazima iwe Public maana nyingine zinawekwa kwa Journals tu na baadhi ya watu kushindwa kupata access lakini hata kama ingekua hivyo kwa sababu Mhe.Magufuli anajinasibu kuwa Muwazi na ana guts za kuita wengine vilaza sasa atoke hadharani atoe chapisho lake

Mimi ni member kule Research gate.Nimetafuta chapisho.lake lolote hakuna

Halafu nimefukua kwa UDMS nikakutana na Sharti kwenye Prospectus ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye İbara ya 2.7.7 kwamba muda wa chini kabisa kwa mwanafunzi wa Ph.D ni Miaka 3 akiwa Mwanafunzi wa muda wote(Fulltime) na pia miaka 5 kwa mwanafunzi ambae sio full time Mhe.Magufuli yeye alisoma Ph.D kuanzia 2006-2009 akafanya research na kutetea tasnifu(Thesis) yake

Halafu kuna kitu naendelea kuki-study kwa undani hapa kisha naweza kutangaza Dau la mtu yeyote atakayeleta Publication ya Magufuli tangu amalize Ph.D

Kuna utafiti unaofanana sana na wa Magufuli uliofanywa na mwanafunzi mwingine Dr. J.Y. Philip na wote wanaonekana walisimamiwa na Prof. Buchweishaija katika utafiti uliokuwa unashabiiana sana wote wakitafuta namna maganda ya korosho yanaweza kutumika kuzuia kutu.

Dr.J.Y. Philip yeye anaonekana alikuwa na Sandwich programme kule Sweden iliyomuwezesha kukaa miezi 8 halafu minne UDSM kwa kila mwaka. Dr. P. Magufuli yeye anaonekana alikuwa ni full time student pale Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam peke yake. Alikuaje Fulltime akiwa Mbunge na Waziri?Kwa wanafunzi wa Ph.D wanajua mziki wake.

Halafu kuna kitu İnteresting hapa kuhusu huyu Dr.Y J Philip na (Dr?) Magufuli . Wote walimaliza shule muda mmoja mwaka 2009.Je, Ni kwanini Dr. P. Magufuli hana hata paper moja kwenye "Peer reviewed journal" kutokana na thesis aliyoandika?

Nimemkuta Dr.Philip kwenye Data zake.Twende kwa facts.Hakuna hasira wala mihemko.

Dr. J.Y. Philip
  • 2005 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2009 Ph.D. (Chem.), University of Dar es Salaam, Tanzania ( Sandwich programme with Swedish University)
  • Peer reviewed articles: 2

Philip, J.Y., Buchweishaija, J., Mkayula, L.L. and Ye, L., 2007. Preparation of molecularly imprinted polymers using anacardic acid monomers derived from cashew nut shell liquid. Journal of Agricultural and Food Chemistry, 55 (22), 8870-8876.

Haya kisha tena huku

Philip, J.Y., Da Cruz Francisco, J., Dey, E.S., Buchweishaija, J., Mkayula, L.L. and Ye, L., 2008. Isolation of anacardic acid from natural cashew nut shell liquid (CNSL) using supercritical carbon dioxide. Journal of Agricultural and Food Chemistry, 56 (20), 9350-9354.

Halafu sasa Mhe.Magufuli ikawa hivi

Dr. P. Magufuli
  • 2006 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 2009: PhD (Chemistry); University of Dar es salaam
  • Peer reviewed articles: 0

    Nani alimuiga mwenzie?

    A Luta Continua,Victory Ascerta...

    Ben Saanane





    KIELELEZO B: VITISHO ALIVYOPOKEA BEN SAANANE BAADA YA KUJADILI SAKATA LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA

    Safari inaendelea. Vitisho.Haya ndiyo maisha yetu ya Kila siku.Mengine tumetoa Ripoti Polisi huko

    Kuna watu hawa miongoni mwa wengi .Yeye anaandika " Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata.Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia.Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu .You are too young to die. Tunajua utaandika na hili.Andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha.Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia.Andika Ben.Andika sana ,ongea.Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

    He's such a coward.Muoga.Muaji anayejitangaza nae ana hofu tupu

    Nimemshukuru lakini nimemjibu kwa namba yake hii 0768797982 ambayo ipo polisi.

    Haya tunasonga mbele Watanzania.Kama ni Uchochezi sidhani kama upo uchochezi mkubwa zaidi ya huu.

    As long as tupo hai,Sauti zetu hazitakoma.Tutaandika,Tutasema,Tutahutubia na tutafanya vitendo

    Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa Damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katikati ya mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya Radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai,watesaji,wakandamizaji wa haki.Watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza tororo la Unyanyasaji,unafiki na ubakaji wa taaluma na dhamiri zao kitaaluma na kiimani

    Yesu Kristu aliishi miaka 33 tu duniania.Nina Mwaka Mmoja bado .He faught the right cause.Alikuja Duniani kimungu.Kila mtu anaishi kutokana na makusudi ya Mungu.Mwenyezi Mungu huruhusu kila jambo kwa makusudi yake.Sisi ni akina nani tukatae makusudi yake?Hatukujileta Duniani na hatutaishi milele.

    Wasichojua watu hawa ni kuwa nilizaliwa na kubatizwa hatari siku hiyohiyo kama Mkatoliki.Ubatizo wa kifo(Hatari) 13 Desemba miaka hiyo,nikapona kwa fadhila zake Muumba.Nimepata fadhila sana Machoni pa Mwenyezi Mungu hadi muda huu.Wanajisumbua!Nimeishi beyond that favour

    Oh nakupenda mpenzi wangu Tanzania.I love you more than words can wield the matter,dearer than eyesight,space and Liberty.Oh I love you Tanzania.My Pride ,My fountain of inspiration."

    Mlale salama marafiki zangu wapendwa.

    Mapambano na Yaendelee,Ushindi U Dhahiiri(Aluta Continua,Victory Ascerta)

    Pumzika kwa amani Rafiki yangu kipenzi Alphonce Mawazo.Hukukopa,Ulijiandaa kulipa gharama.Ukalipa Deni. Tunasonga Mbele! Nitalitaka Jeshi la Polisi liunganishe ujumbe uliotumwa na kifo chako katika hatua za uchunguzi.

    Ben Saanane

    KILELEZO C: MAONI YA BEN SAANANE AKIMJIBU PROF. KITILA MKUMBO KUHUSU SAKATA LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA

    Nimesoma Hoja ya Prof.Kitila kuhusu PhD ya Magufuli.

    Prof.Kitila ni Rafiki yangu sana.Yeye ni kaka yangu na ananichukulia kama mdogo wake.

    Katika Kuchangia Mjadala wa PhD ameandika "UDSM hakuna namna mtu kupata Cheti Fake na huwa hatuangalii sura ya Mtu...". Kwa hiyo. .. "PhD ya Magufuli haina kasoro"...

    Vilevile kuna watu Mwanzo walisema masuala ya Machapisho hayana maana lakini cha ajabu wameweka waliyoita Machapisho ya Magufuli na pia kuweka Picha akiwa amevaa mavazi ya Graduation kama vile ndio Authentification ya PhD ya Magufuli.

    Nataka kugusia hoja ya Prof.Kitila kuhusu kuwa hakuna namna ya kufanya Udanganyifu UDSM .

    1-Prof.Kitila anaweza kuwa Mwaadilifu sana katika kusimamia taaluma na kazi yake kama Mhadhiri Chuoni.

    Lakini ni kosa kubwa ku-assume kila mtu ni mwadilifu.

    Tukienda hivyo tutaua nchi na ndio maana wengine tunasizitiza sana Kuimarisha Taasisi zetu na mifumo.

    Hapo ni kama vile ku-assume kuwa kila mtu ni mpigaji.Hivyo tunasizitiza haja ya kuimarisha taasisi na mifumo ambayo itadhibiti mafisadi na watu wasio waadilifu baadala ya ku-assume kila mtu ni mtakatifu .

    Kama watu waliweza ku-forge documents Serikalini na Kuchota Fedha Za EPA au ESCROW ni mechanism gani itakayozuia PhD za Mbeleko vyuoni kwetu hasa zinazohusu wanasiasa?

    Tena katika mazingira yanayoashiria mbeleko kwa Mbebaji kumshusha aliyembeba nae akambeba kwa kumteua kushika ujumbe wa Bodi?

    2-Kama Seif-Al Islam Mtoto wa Ghaddafi alikuja kuibuliwa kwa kashfa ya kuhonga na kupata PhD ya mbeleko Kule London School of Economics(LSE) sass UDSM ina mfumo gani thabiti wa kuepuka fraud kuliko LSE?

    Kwa Mujibu wa Academic Perfomance Center chuo kikuu cha London School of Economics kilishika nafasi ya pili kwa miaka kadhaa mfululizo kwa ubora duniani wakati UDSM ikishika nafasi ya 1618 kati ya Vyuo 2,000.

    3-UDSM imewahi kukumbwa na staff waliofanya Udanganyifu kwenye taaluma na Prof.Maboko aliwahi kuutangazia Umma.

    UDSM hii hii imeshawahi kutoa wanafunzi waliofanya udanganyifu na baadhi yao kuvuliwa Degree zao

    Charles I . Ng'imba aliwahi kuvuliwa Digrii yake aliyoipata kwenye Graduation ya Tarehe 29 August ,1987.

    4-Kuna hao walioleta machapisho waliodai ni Ya Magufuli na kudai kuwa alistahili PhD kwa sababu alishaandika tangu 2003.

    Tena nimeona ameshirikiana baadhi na huyo Superviser wake.

    Sasa watuambie alifanya PhD by Publication?

    Sweden ,Australia na hata Uholanzi(Najua Unafahamu) inaruhusiwa PhD by Publication.

    Kwa faida ya mjadala tu: Ni kuwa PhD by Publication zinakusanywa paper zote na kuziandikia Covering Essay na jumla na paper iwe na maneno si chini ya 20,000 ikiwa condition na masharti mengine ya submission yapo constant.

    Pia inazingatiwa ni paper ngapi umeandika mwenyewe na ni ngapi umeshirikiana(Co-Author).

    Na katika kushirikiana ni ipi jina lako limekua la kwanza maana inabeba uzito wa synopsis.

    Sasa Katika hizo Paper alizoweka the so called (Dr.!?) Chahali ni Tatu tu anazooneshwa kaandika yeye na zipo kwenye vijarida vya uchochoroni tu sio kwenye respectable Journals huko.

    So swali la PhD Candidate huyu kuipata PhD kwa miaka 3 akiwa Part time Candidate kinyume na Prospectus halijajibiwa.

    Ingawa Prof.Kitila umetoa maoni yako tu kama mchangiaji na Sio Authority ya UDSM au Supervisor wake(Ofcourse hawezi kujitokeza tena maana ni mteule wa Bodi) lakini naheshimu maoni yako uliyotoa kistaarabu bila matusi kama hao waliomtetea kwa vitisho na matusi kwa hoja zao za kula nae Canteen au kumuona amevaa vazi la graduation.

    UDSM kama vilivyo vyuo vingine au taasisi nyingine nchini haina kinga thabiti dhidi ya Academic Fraud hasa zinazohusisha wanasiasa na vigogo serikalini.

    Hoja ya Prof.Buchweshwaija kuwa co-author kwenye pepa yake kisha kuja kuwa Supervisor wake na kisha kuja kuwa mteuliwa wa Waziri aliyeteuliwa na yeye mwanafunzi wake tunaweza kuli-debate left-right-center hasa tunapoangalia mfumo wetu wa elimu na uadilifu.

    Ofcourse nakiri kuwa wakati wa kuanza PhD yangu niliwahi kukuambia nilipata headache sana kuhakikisha kuwa napata Supervisor maahiri ndani yawanakamati.

    I knew as PhD candidate,Institution'll gain through my presence by gaining credibility,profile and funding. Why should I allow them to treat me as an inconvinient ,Incompetent fool?

    So kwa Case ya Magufuli na SUP wake twaweza kui-debate kweli kuanzia co-authorship.

    Sijui independence ya Mwanafunzi huyo ilikuaje hata kama ilikua ni Ph.D by Publication.

    Baadae tena Kaka. ...

    [HASHTAG]#MagufuliHakikiPhDyako[/HASHTAG]

    [HASHTAG]#MagufuliVerifyYourPhD[/HASHTAG]

    [HASHTAG]#MagufulideclareyourPaytubes[/HASHTAG]

    A Luta Continua,Victory Ascerta.....

    Ben Saanane


 
Haya sasa tumeisoma hotuba yote nyie maccm, kama hamtaki kuisoma shauri yenu, hotuba imetulia utadhani imeshuka kutoka mbinguni kama amri za Mungu
Ukweli siku zote ni mchungu na hautangamani na ghiliba.
 
Eti wanatupangia cha kusoma, muda sio mrefu watatupangia cha kufikiri wakati wenyewe hawana hata chembe ya mawazo mbadala. ...mjinga tu asiyejua kuwa hakiwezekani!
 
Eti wanatupangia cha kusoma, muda sio mrefu watupangia cha kufikiri wakati wenyewe hawana hata chembe ya mawazo mbadala. ...mjinga tu asiyejua kuwa hakiwezekani!
Ukiisoma hotuba yote hakuna sehemu hata moja ambayo ina maneno ya uongo ama ambayo hayajulikani kwa watanzania , sasa sijui wanataka hotuba za kuisifia serikali au wanataka za aina gani , Bunge limejigeuza na kuwa dola .......badala ya kuithibiti dola linajithibiti lenyewe
 
anayejua alipo ben sanane ni said kubenea
 

Attachments

  • tmp_13013-IMG-20170429-WA0035-1184017259.jpg
    tmp_13013-IMG-20170429-WA0035-1184017259.jpg
    96.2 KB · Views: 51
hivi ben si ndio yule aliyekuwa anatembea na sumu mfukoni amlishe Zitto? ben ana maadui wengi mno ndani ya chadema na upinzani
 
Eti wanatupangia cha kusoma, muda sio mrefu watatupangia cha kufikiri wakati wenyewe hawana hata chembe ya mawazo mbadala. ...mjinga tu asiyejua kuwa hakiwezekani!
mnayafanya wenyewe chumbani mkija huku nje mnawageuzia wengine. poor you
 
Back
Top Bottom