Je, Serikali inazungumziaje suala la wanafunzi kukaa na njaa shuleni hadi usiku?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,926
45,386
Hivi Mwanafunzi anayeshinda na njaa kuanzia Asubuhi hadi usiku saa tatu.

Hapa Dar es Salaama unakuta 90% ya wanafunzi wa shule za serikali wanaamka saa kumi na moja na kuanza kugombania daladala na wakifika shule hamna uji Wala chakula na mwanafunzi ili Afike kwao Mbagara, Gongo la Mboto au Kigamboni lazima afike usiku wa saa tatu au saa-mbili.

Wanafunzi hapa Dar salaam wamekuwa wakiugua vidonda vya Tumbo udumavu wa Akili. Kama naongea uongo naomba mtafute mtoto wa miaka 17/16 anayesoma ukimuangalia umbo Kama la mtoto wa miaka 9 au 10.

Naomba Serikali itengeneze Mfumo rafiki wa either Mzazi/mlezi kuchangia kiasi kidogo Cha pesa ili mtoto wake Apate chakula mashule mbona nyie wana-siasa watoto wenu wanakula vizuri tu wana Afya nzuri tu.

Pia watoto wa shule za serikali kutokana na Njaa hawaelewi masomo yenyewe na mwisho wa siku Mtu anamaliza shule 0-0

NB: Pia wazazi wenyewe wapo kwa wahidi mshahara hauzidi laki mbili.
 
Naomba Serikali itengeneze Mfumo rafiki wa either Mzazi/mlezi kuchangia kiasi kidogo Cha pesa ili mtoto wake Apate chakula mashule mbona nyie wana-siasa watoto wenu wanakula vizuri tu wana Afya nzuri tu.

Hapo wazazi ndo huwa hawaelewi kitu
Wanawaumiza Sana watoto
 
Sijui kama wanawapa shilingi ngapi
Mtu analipwa laki mbili kwa wahindi hivi unadhani ataweza kumtengea mtoto wake nauli Go and return 600 na hapo hela ya kula?

Sio Rahisi na katika hiyo laki mbili you suppose to pay ur all bills
Kodi
Umeme
Chakula

Tujitahidi kuvaa viatu vyao ndo tutasolve hili tatizo.
 
Hivi Mwanafunzi anayeshinda na njaa Kuanzia Ahsubui hadi usiku saa tatu...
Nilisha shuhudia baadhi ya wazazi kuleta watoto wao walio chaguliwa form one waliiletwa shule waanze wa kiwa hawana sare viatu au madaftari ya shule.

Hiyo aina ya wazazi ndo wachangia chakula cha watoto wao wale mashuleni, siasa za hapa ziliharibu elimu mtu anaina ni jukumu la serikali kusomesha mwanae kwa 100%.
 
Nilisha shuhudia baadhi ya wazazi kuleta watoto wao walio chaguliwa form one waliiletwa shule waanze wa kiwa hawana sare viatu au madaftari ya shule...
KPwanza tambua hakuna mtu anapenda shida na Maisha Magumu hata ao wanasiasa wanajisahau tu na kutoa Dhihaka kwa wananchi wao.

Watu wanaishi Maisha Magumu Sana kutokana na mifumo ya nchi yetu kuwa na Maisha mazuri ni kama bahati.
 
Kwanza tambua hakuna mtu anapenda shida na Maisha Magumu hata ao wanasiasa wanajisahau tu na kutoa Dhihaka kwa wananchi wao...
Kwahiyo serikali ina uwezo wa kulisha hao watu wote?

Kama mtu hawezi kununuliwa mwanae madaftari wewe unategemea ataweza kumnunulia chakula kweli kila siku?
 
Back
Top Bottom