Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Wanafunzi wa kidato cha sita wanalipa michango mbalimbali. Baadhi ya michango hiyo ni mchango wa mlinzi. Je walinzi wa shule siyo waajiriwa wa serikali? Na kama siyo waajiriwa wa serikali wanapolipwa na wanafunzi wanalipwa kama vibarua? Kama ni vibarua wanahudumu kwa miaka mingapi kama vibarua? Mafao yao yanapelekwa NSSSF?Kwa mfumo gani?
Nauliza haya maswali kwa sababu wapo walinzi wa shule miaka yote ni wale wale na sheria za nchi zinakataza mtu kuajiriwa zaidi ya miezi sita bila kusajili kwenye mfumo rasmi na pia bila kuchangia mifuko ya jamii. Kwenye private sector ukikutwa na kibarua zaidi ya miezi sita lazima wachukue maokoto au wakushtaki . Je serial inaruhusiwa?
Eneo la pili ni michango ya wapishi wa shule, je hawa pia maisha yao yote wanakuwa vibarua na kwamba wanafunzi ndio wanapaswa kuwalipa? Inakuwaje tunaruhusu watoto wapikiwe chakula na vibarua badala ya kutafuta wapishi ambao wamesomea? Afya za watoto hawa hazipo hatarini?
Ukienda kwenye sector ya hotel kwa kuzingatia usalama wa walaji chakula, mpishi lazima awe amesomea upishi na eneo lake la huduma linalindwa kudhibiti watu wasiostahili kuingia mara kwa mara. Kwanini serikali inadhani ni sahihi shule zake kuuwa na wapishi wasioajiriwa?
Lakini swali lakujiuliza tunazo shule ngapi za sekondari zinazohitaji wapishi na walinzi wakuajiriwa hadi tushindwe kuwaajiri tukachukue vibarua kinyume na taratibu za ajira? Waziri wa elimu na waziri wa TAMISEMI naamini haya maswali hayapo kwenye program na mikakati yenu lakini nayaleta kwenu yaanze kuchakatwa kabla hawa vibarua hawajaleta madhara kwa wanafunzi au awajawasilisha madai yao mahakamani kwamba wanadhulumiwa na serikali.
Nirudi kwenye hoja, je serikali haina uwezo wa kulipa umeme kwa shule zetu nchini? Kwanini liwe jukumu la mwanafunzi kulipia umeme? Tunaamini mtoto wa mkulima na mfugaji wataweza hizi gharama?
Nimecheki jumla ya michango kwa kidato cha sita ni laki tatu na arobaini na tano bado ujaweka nauli na matumizi binafsi. Je kwa mfumo huu kwanini hizi fedha zisingewekwa kama ada then serikali inawajibika kulipia hizi huduma pamoja na kuajiri? Nasema hizi kwa sababu kama unachukua pesa kwa wanafunzi inazitumia kuajiri vibarua kwanini usichukue hizi fedha ukatumia kutoa ajira rasmi?
Kwa matajiri wa humu ndani naamini michango ya laki tatu itaonekana ni michache ila wapo wanafunzi hata uniform wanashindwa kuwa nazo. Na tukumbuke ukiizaliwa na mzazi asiyewajibika haimaanishi nawewe hautawajibika. Serikali inapoweka haya mambo ijaribu kufanya analysis. Haiwekana kuna wababu leo wanaitwa walinzi wa shule lakini kiukweli hakuna wanavyolinda. Kuna wapishi siyo wapishi hii yote ni kutokana na mwanya huu uliowekwa kwenye usalama wa afya na mwili wa watoto wetu.
Umofia Kwenu