Twende haraka kwenye mada.
Mama mwenye Upendo Kwa wanae, Yuko radhi ashinde njaa, ajinyime kununua kipande Cha kanga Ili mtoto wake apate kula chakula na kupata mahitaji muhimu, Watoto mashuleni katika shule za kata ni watoto wa Serikali wawapo mashuleni.
Viongozi wengi wa juu waliopo sasa ni mashuhuda kuwa zamani wanafunzi tulikula mashuleni Bure uji, ugali wa wanga, Hadi maziwa, tulionekana Kwa nje maskini lakini tulipata huduma muhimu ya CHAKULA muhimu shuleni na Elimu ilipaa na kuthaminika sana. Nini kimetokea, mbona mmebadilika ghafula?
Wazazi wanapokabidhi watoto wao Kwa Serikali kupitia shule za kata Ili wapewe Elimu, ni JUKUMU la Serikali kuhakikisha watoto wanapatachochote kitu tumboni Ili masomo yaeleweke na kumrahisishia mwalimu kufundisha Kwa muda wawapo shuleni.
ELIMU Bora inachagizwa na Mazingira Bora ya kufundishia kama madarasa, walimu wenye Viwango Bora, Madawati, nk nk
Uwezo wa kulisha wanafunzi wetu tunao, Nia tunayo? Ari tunayo kuhakikisha watoto wanapata chakula Bure mashuleni.?
Kuna watoto shule za msingi na sekondari wanatembea zaidi ya 5km kwenda na kurudi shuleni, na hurudi jioni saa kumi Hadi 12 jioni bila kula chochote shuleni, kusoma imekuwa ADHABU?
Nikisema Serikali itoe chakula Bure mashuleni, haimaanishi Bure, wazazi wanalipa Kodi serikalini Kwa njia mbalimbali.
Pia wazazi wengi Hasa wazazi wakulima wanalima chakula na kikiuza katika maghala ya Serikali.
Hivyo pakiwepo Nia thabiti, tunaweza kuhakikisha tunaanza japo na UJI mashuleni, wanafunzi wapate japo kikombe kimoja.
Shule Zina Utaratibu wa kuwafungia watoto mashuleni Hadi jioni saa kumi bila kula chochote.
Nauliza, hivi mtoto wa MKULIMA aliyetoka nyumbani bila kula chochote nyumbani wazazi wakienda shambani kulima, anawezaje kuelewa nasomo darasani bila kula chochote ?
Narudia tena, Serikali haitapata HASARA yoyote kuhakikisha wanafunzi wanapata japo kikombe Cha uji mashuleni Nchi nzima.
Kiongozi wetu mkuu wa sasa ni mama na mwenye vichengerwa kadhaa, tafadhali unaweza kukumbukwa hata Kwa hili jambo dogo lenye mchango mkubwa sana mbeleni.
Angalizo: Katika chaguzi zijazo msipokuja na HOJA nzito na muhimu kama Chakula mashuleni, maji safi, Nishati ya umeme shule za vijijini Kwa wanafunzi kujisomea usiku,sahauni kuchaguliwa.
Karibuni, Amen.