Madai ya Wanafunzi wa Rutabo kupewa chakula kidogo, Afisa Elimu asema 'tatizo ni siku ya Wali na Nyama'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Baada ya member wa JamiiForums.com kuripoti kuwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rutabo hawapewi Chakula cha Kutosha kutokana na uhaba wa Chakula na kudai kuwa hatua hazichukuliwi, Serikali imechukua hatua.

Awali member alidai Shule hiyo inawapikia Wanafunzi Chakula kidogo hali inayowalazimu kugombania na kuomba hela nyumbani mara kwa mara kwa.

Andiko liko hapa - Wanafunzi wa Rutabo High School (Kagera) hawapewi chakula cha kutosha

Afisa Elimu Sekondari Kagera, Michael Lugola amesema alimuagiza Afisa Elimu Kata ambaye ameenda kwenye shule hiyo na kumpa ripoti hii:

Nimefika katika Shule ya Sekondari Rutabo, tumefanya kikao na Wanafunzi tukawapa nafasi ya kueleza changamoto zinazohusiana na chakula.

Walichokieleza kilikuwa cha kawaida, sio kikubwa kama kinavyoripotiwa kwenye Mtandao, tatizo kidogo lilielezwa siku za Wali na Nyama kuwa wakati mwingine hawashibi lakini walikiri kuwa ugali unatosha.

Tumeweka mkakati mpya ikiwa ni pamoja na usimamizi wa chakula kutoka kinapokuwa stoo mpaka jikoni.

Kuongeza Walimu wa kusimamia na kuonja ubora wa chakula, kuongea na Wapishi ili kuhakiki wanaandaa chakula kizuri na kuhakikisha hakuna hujuma ya chakula sehemu ya jiko.

Wanafunzi viongozi kutoa taarifa ya mapungufu ya chakula kwa Mwalimu au Mkuu wa Shule haraka sana yanapojitokeza ili yafanyiwe kazi.

Na Mimi nimeahidi kufika mara kwa mara shuleni saa za Wanafunzi kupata chakula ili kujionea hali halisi.
 
Mara zote Siku za Wali nyama shuleni, Chakula kilikuwa hakitoshi.

Hii inatokana na baadhi ya Wanafunzi Viongozi kubeba chakula cha kutosha ili wale na Jioni.

Wanafunzi ambao walikuwa hawatokei Siku ya Ugali maharage Kwa kwenda kula canteen za Shule nao kujumuika Siku ya wali Nyama.

Nakumbuka wakati niko Shule, Siku za Wali nyama ziliongezwa kutoka Siku 1 Kwa wiki hadi Siku 3 Kwa Wiki.

Hii ilifanya Wanafunzi tuongeze Utulivu na kufocus na Masomo zaidi ๐Ÿ˜…๐Ÿค—
 
Baada ya member wa JamiiForums.com kuripoti kuwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rutabo hawapewi Chakula cha Kutosha kutokana na uhaba wa Chakula na kudai kuwa hatua hazichukuliwi, Serikali imechukua hatua.

Awali member alidai Shule hiyo inawapikia Wanafunzi Chakula kidogo hali inayowalazimu kugombania na kuomba hela nyumbani mara kwa mara kwa.

Andiko liko hapa - Wanafunzi wa Rutabo High School (Kagera) hawapewi chakula cha kutosha

Afisa Elimu Sekondari Kagera, Michael Lugola amesema alimuagiza Afisa Elimu Kata ambaye ameenda kwenye shule hiyo na kumpa ripoti hii:

Nimefika katika Shule ya Sekondari Rutabo, tumefanya kikao na Wanafunzi tukawapa nafasi ya kueleza changamoto zinazohusiana na chakula.

Walichokieleza kilikuwa cha kawaida, sio kikubwa kama kinavyoripotiwa kwenye Mtandao, tatizo kidogo lilielezwa siku za Wali na Nyama kuwa wakati mwingine hawashibi lakini walikiri kuwa ugali unatosha.

Tumeweka mkakati mpya ikiwa ni pamoja na usimamizi wa chakula kutoka kinapokuwa stoo mpaka jikoni.

Kuongeza Walimu wa kusimamia na kuonja ubora wa chakula, kuongea na Wapishi ili kuhakiki wanaandaa chakula kizuri na kuhakikisha hakuna hujuma ya chakula sehemu ya jiko.

Wanafunzi viongozi kutoa taarifa ya mapungufu ya chakula kwa Mwalimu au Mkuu wa Shule haraka sana yanapojitokeza ili yafanyiwe kazi.

Na Mimi nimeahidi kufika mara kwa mara shuleni saa za Wanafunzi kupata chakula ili kujionea hali halisi.
Hili nalo tunahitaji msaada kwa nchi zilizoendelea,
 
Yani balaa nakumbuka nilikuwa waziri kwenye kitengo flani siku hiyo nakuwa na bakuli special kwaajili ya kula kesho yake kama kiporo na hakuna wa kuniuliza ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ufisadi ulianza muda mrefu kumbe sio tu kwenye familiya
 
Kwani wali na Nyama sio Chakula ?

Hivyo ni kweli kuna tatizo za watu kutokushiba siku za wali na nyama..., ni kama kungekuwa na tatizo la wanafunzi kutokula kabisa akasema hapana siku za keki asubuhi ndio huwa hazipo hence watu hawali......
 
Ufisadi ulianza muda mrefu kumbe sio tu kwenye familiya
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Nilikuwa na watoto kama wote mm ndo mama Yao ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€naandaa na kachumbari tunagawana ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€sema nilijuta siku walivunja sheria nikawamaind undugu ukafa wakaanza kusema Hadi wali nilowapa nimevunja sheria washenzi sana wale ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Yani balaa nakumbuka nilikuwa waziri kwenye kitengo flani siku hiyo nakuwa na bakuli special kwaajili ya kula kesho yake kama kiporo na hakuna wa kuniuliza ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Wewe Waziri wewe ๐Ÿ˜…

Tukikupa Wizara ya Afya tafadhali usiondoke na dawa zetu tu Wazee ๐Ÿ˜œ
 
Back
Top Bottom