Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 17,371
- 33,019
Mwanaye DAS wa Morogoro, mwingine kashinda kura za maoni Kawe kawashinda magwiji😂😂😂, Jesca yupo kwenye kazi nzuri EWURAWadau,
Huu ni uzi wa swali.
Nimefuatilia kwa karibu kuona jinsi Rais Magufuli anavyoilea familia yake na nikaona kuna mfanano fulani na jinsi hayati baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyoilea familia yake.
Kwanza sijaona mama yetu Janet Magufuli akiwa na taasisi yake Kama wake wengi wa marais waliopita haswa awamu ya tatu na nne. Mama Janet yuko bize kumsaidia mumewe kwenye yale yaliyopangwa kwenye ilani. Hi inatoa fursa ya kutokumuhusisha au kumpaka Rais matope kwa kupitia taasisi ya mkewe.
Watoto wa Rais Magufuli ni Kama hawapo. Ninamfahamu Jesca tuu na huyu nilimfahamu kipindi kill cha ishu ya wanafunzi wa udom.
Kwa uelewa wangu hili halitokei kwa bahati mbaya bali kwa Rais aliyepo madarakani kutotaka kushea uongozi wake na familia yake. Mwalimu Nyerere ni mfano mzuri katika hili.
Amani