Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike"

"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa
 
Ni sawa kuwa mwema kwa binadamu wenzio hasa ukiwa katika nafasi aidha ya uongozi ama kifedha lakini si sawa kubagua misaada yako iwe kwa walionazo tu na si makapuku wanaostahili hasa msaada wako.

Samia ni mwema sana kwa matajiri/watu maarufu na wanasiasa lakini walio chini kabisa kila siku wanazidi kulia kwa hali mbaya na ugumu wa maisha.
 
Ilisemekana kuwa marehemu alikuwa tajiri sana. Pamoja na hayo ana stahili yake za kulipiwa tiba yeyote kama mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu. Mataamshi haya yana weza kutafsiriwa kama alipewa upendeleo na Mheshimiwa Rais kitu ambacho ni vigumu kuamini kwa sababu kugharamiwa tiba na serikali ilikuwa ni haki yake. Labda kama kuna kitu sijaelewa.

Amandla...
 
Back
Top Bottom