KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Nimefarijika sana kuona kile nilichokuwa natamani kifanywe muda mrefu sasa kinakwenda kufanywa na kikiwa kimesemwa na viongozi wa kiroho na kiimani, ni ishara jambo hilo ni la kiimani zaidi.
Ni muda mrefu nilikuwa nawaza Kwa mazuri anayofanya Rais Samia ni vyema atambuliwe rasmi kama Mama wa Taifa. Tangu alipoingia madarakani ametenda kama Mama anavyotakiwa kufanya Kwa familia na hapa familia ni nchi yetu.
Nikizungumza kwa mifano, mama ni mtu wa karibu sana kwa watoto na hapa ndio wazo la kumtambua Rais Samia kama Mama wa Taifa liliponijia baada ya ishara hii. Rais Samia amekuwa karibu sana na vijana ambao ni kama watoto kwenye familia. Rais Samia ndiye kiongozi aliyeteua vijana wengi uongozini na pia anatoa ajira nyingi na kuwawezesha vijana wengi kiuchumi kwenye maeneo mbalimbali, yaani kajitoa sana Kwa ajili ya wanawe( vijana). Kwetu vijana tunajisikia fahari kubwa Rais Samia kutambuliwa kama Mama wa Taifa.
Baada ya Rais Samia kutambuliwa kama Mama wa Taifa sasa ni dhahiri familia hii(Tanzania) itakuwa imepata muunganiko wa kiroho wenye nguvu zaidi.
Mama wa Taifa ni heshima kubwa katika kutambua mchango mkubwa alionao Rais Samia katika ujenzi wa nchi yetu kama kiongozi wa kwanza mwanamke na shujaa wa uchumi na maendeleo.