Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Kwenye nchi zilizoendelea kwasasa kuna uhaba mkubwa wa vijana wa kufanya kazi lakini wakati huohuo kuna janga kubwa la vijana wasikuwa na kazi Tanzania. Pamoja ni jitihada nyingi za serikali za kusaidia vijana kupata kazi na kufanya shughuli za kilimo ni lazima vijana nao wajiongeze walau kuweka mikakati ya muda wakati serikali ikijipanga vizuri hasa kwenye viwanda na mashamba ya mikakati. Badala ya kushinda vijiweni huu ni wakati wa serikali kufikiria zaidi ya Tanzania kwenye mambo ya ajira.

Tatizo tofauti na jamii za nchi jirani kama Kenya na Uganda watu wengi Tanzania wameweka utamaduni wa kuaminisha vijana wakienda nje tu kutafuta maslahi eti sio wazalendo. Ni bora wabaki vijiweni na kupuyanga wakati hawana uwezo wa kuchangia chochote kwa familia zao na wazazi wao. Naomba mlielewe siongelei vijana wote lakini nacho sema hapa tusiweke madongo kwa wale wanaotafuta maslahi nje ya nchi. Je, kuna fursa zipi hasa na nashauri nini. Hii ni kwa wale vijana wasio na kazi wala vipato

1. Serikali msione aibu kuongea na kampuni kubwa za teknologia ambazo zinaajiri watu nchi nyingine. India mfano wanafanya kazi nyingi sana za nchi nyingine kuanzia engineering design, accounting, programming, computer coding, technology training. Sasa je, ni kwanini hakuna jitihada zozote za kuwezesha Watanzania waweze kuajiriwa wakiwa Tanzania. Nasema hivyo kwasababu mimi nipo USA na naona hizi nchi kuna watu wengi sana wanafanya kazi kutoka nchi nyingine. Kuna kampuni ya Houston, Texas ambayo ina wafanyakazi zaidi ya 100 na wanafanyia kazi India!. sasa hawa wametuzidi nini. Mawaziri wetu wa teknologia hata kujiangaisha au kufikiria haya hawafanyi.

2. Serikali iweke uhusiano mzuri na diaspora na kuwawezesha diaspora wenye nafasi za kiungozi kuweza kuajiri Watanzania. Tatizo kwasasa hakuna sheria ambazo ziko wazi mfano kama manager diaspora yupo Canada na anataka kumpa kazi kijana Mtanzania na afanyie kazi kutoka Tanzania je ni sheria gani za kikodi na uwazi zipo kwasasa ili yule mwajiri aweze kuwa na uhakika anafuata sheria? Je tunasheria za hivi au hatuna? mafao na kodi zinalipwa vipi?

3. Watanzania vijana wahangaikie kazi za muda. Nchi nyingi zina kazi za muda kuanzia kwenye kilimo, meli za wageni, hospitali, mahoteli.. na hata ujenzi. Vijana badala ya kushinda mitandaoni na kuendesha bodaboda kwa Tsh 10,000 kwa siku tumia muda wako kutafuta kazi nje. Hizi kazi ni za mikataba mwaka mpaka miaka mitatu halafu unaweza kurudi wakati serikali nayo imejipanga. Mjue tu miaka ya 1995-2000 kuna watanzania wengi tu walienda USA kwenye program ya summer camp. walitafuta wenyewe lakini vijana wa siku hizi ni wepesi kulalama badala ya kutafuta fursa.

4.Vijana tafuteni " mentor" au washauri wenye uzoefu. Kuna Watanzania Dunia nzima wewe ni kijana wa miaka 20's badala ya kulalama tafuta mtu mzima wa kukushauri ambaye anafanya kitu ambacho wewe unapenda. Tatizo leo mnashinda kufikiri na kutaka kuwa kama Diamond au Nandy badala ya kutafuta wataalamu au wafanyabiashara ambao unataka kuwa kama wao. Sio lazima wawe Tanzania. Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi? Hata hapa vijana kuna watu wengi wakuwapa mawazo lakini mnakimbilia kupiga madongo!madongo yanakusaidia nini?

5. Vijana msisubiri serikali. Serikali haijawahi kusaidia vijana kama wakati huu lakini vijana wa huko nyuma miaka ya 1990's na 2000's walienda kutafuta vyuo na maslahi huko nje wenyewe na marafiki zao sio kwa msaada wowote wa serikali. Tatizo vijana mnasubiri sana serikali ambayo itachukuwa muda sana kuweka mambo ya ajira sawa. Nawashauri tafuteni kazi popote Duniani ilimradi unasaidia familia yako. Lakini usisahau nyumbani

Kukaa nyumbani vijiweni na kulalama siku hadi siku sio uzalendo. Na usijidanganye kuwa wewe ni mzalendo kuliko yule kijana anayetuma pesa kusaidia familia yake.

Nishatoa ushauri huu

Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria.

Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea Tanzania? inawezekana kabisa lakini kunatakiwa kuwa na makubaliano na hizi kampuni.

Nashauri serikali ifanye mwaliko wa hawa maguru na wakubwa wa hizi kampuni ili wafungue data center Tanzania waweze kuajiri wataalamu tofauti hasa kwenye teknolojia. Tusione aibu kuandikia barua na kualika hata kama wakisema hawana muda tunaweza kubahatisha mmoja.

Niongezee tu kwenye soko la hisa za Marekani 50% ni kampuni za teknolojia hizo hapo ni thamani za kampuni mfano Apple hapo ni $T2.3 na Oracle ni $240B

bolCompanyCap Rank
1-27-23
Market Cap
1-27-23
1d Chg
1-27-23
1m Chg
1-27-23
12m Chg
1-27-23
AAPLApple12,311.01.4%12.2%-8.3%
MSFTMicrosoft21,848.00.1%4.7%-17.2%
GOOGLAlphabet31,294.3-0.9%-1.1%-34.6%
AMZNAmazon41,042.6-1.6%-10.6%-48.1%
BRK-ABerkshire Hathaway5682.80.0%1.7%1.9%
TSLATesla6561.811.0%63.0%-35.6%
NVDANvidia7501.02.8%44.2%-7.2%
TSMTaiwan Semiconductor8483.9-0.2%25.5%-19.8%
VVisa9477.23.0%12.2%12.3%
XOMExxonMobil10476.1-1.8%4.9%53.9%
UNHUnitedHealth11454.1-1.3%-8.6%5.3%
JNJJohnson & Johnson12439.8-0.4%-5.2%-1.4%
JPMJPMorgan Chase13411.60.2%6.5%-3.4%
METAMeta14397.93.0%29.8%-48.5%
WMTWalmart15386.50.8%-0.4%5.5%
MAMastercard16359.6-0.9%8.1%6.7%
CVXChevron17347.0-4.4%-0.1%32.6%
PGProcter & Gamble18331.6-0.4%-8.7%-11.7%
LLYEli Lilly19325.1-1.7%-6.2%44.5%
HDHome Depot20322.80.9%-0.9%-11.1%
BABANvidia21313.4-1.8%31.7%5.9%
BACBank of America22284.40.3%9.0%-22.0%
MRKMerck23267.2-1.4%-6.0%30.8%
ASMLASML24266.6-2.4%24.2%5.2%
KOCoca-Cola25261.6-0.5%-5.8%1.4%
ABBVAbbVie26258.7-0.8%-10.3%7.6%
AVGOBroadcom27247.0-1.3%6.8%9.0%
PFEPfizer28245.8-1.0%-14.4%-18.0%
ORCLOracle
Larry Ellison-Oracle Corporation
1675091721306.png

Tesla-Elon Musk
1675091739883.png

Microsoft-Satya Narayana Nadella
1675091764181.png

Alphabet-Google-Sundar Pichai
1675091784044.png

SAP CEO Christian Klein
1675091807608.png

IBM CEO Arvind Krishna's
1675091826399.png
 
Yaani nchi kama Kenya ni wiki iliyopita imesaini mkataba na USA, Germany na Qatar/ Saudi Arabia,kuexport human resource zao , kwenye kazi mbalimbali, zinazohitaji watu kwenye nchi hizo....Nyie Bongo endeleeni tu na siasa za kutelekeza nguvu kazi ya vijana wakibakia kuendelea kubakia kushabikia , bongofleva, Yanga/Simba na promotion za vijana kuendelea kubet tu Kwa bidii....... Kwa kweli safari yetu, bado ni ndefu na tutafika tumechooka.....
Waambie hao! Vijana msilale, serikali isilale. Dunia iko kasi mnoo.
 
Yaani nchi kama Kenya ni wiki iliyopita imesaini mkataba na USA, Germany na Qatar/ Saudi Arabia,kuexport human resource zao , kwenye kazi mbalimbali, zinazohitaji watu kwenye nchi hizo....Nyie Bongo endeleeni tu na siasa za kutelekeza nguvu kazi ya vijana wakibakia kuendelea kubakia kushabikia , bongofleva, Yanga/Simba na promotion za vijana kuendelea kubet tu Kwa bidii....... Kwa kweli safari yetu, bado ni ndefu na tutafika tumechooka.....
Tz mabalozi wenyewe sasa😅😅
 
Kukaa nyumbani vijiweni na kulalama siku hadi siku sio uzalendo. Na usijidanganye kuwa wewe ni mzalendo kuliko yule kijana anayetuma pesa kusaidia familia yake.
Naomba kwanza kabla ya kutulaum sisi vijana unijumlishie Jumla ya gharama ya passport na visa na nauli ya safari kutoka Tanzania hadi Kuwait kwa mfano.

Baada ya hapo uje kutulaum sisi vijana
 
1. Serikali msione aibu kuongea na kampuni kubwa za teknologia ambazo zinaajiri watu nchi nyingine. India mfano wanafanya kazi nyingi sana za nchi nyingine kuanzia engineering design, accounting, programming, comouture coding, technology training.... sasa je ni kwanini hakuna jitihada zozote za kuwezesha Watanzania waweze kuajiriwa wakiwa Tanzania. Nasema hivyo kwasababu mimi nipo USA na naona hizi nchi kuna watu wengi sana wanafanya kazi kutoka nchi nyingine. Kuna kampuni ya Houston, Texas ambayo ina wafanyakazi zaidi ya 100 na wanafanyia kazi India!. sasa hawa wametuzidi nini. Mawaziri nmwetu wa teknologia hata kujiangaisha au kufikiria haya hawafanyi.
2. Serikali iweke uhusiano mzuri na diaspora na kuwawezesha diaspora wenye nafasi za kiungozi kuweza kuajiri Watanzania. Tatizo kwasasa hakuna sheria ambazo ziko wazi mfano kama manager diaspora yupo Canada na anataka kumpa kazi kijana Mtanzania na afanyie kazi kutoka Tanzania je ni sheria gani za kikodi na uwazi zipo kwasasa ili yule mwajiri aweze kuwa na uhakika anafuata sheria? Je tunasheria za hivi au hatuna? mafao na kodi zinalipwa vipi?.....
3. Watanzania vijana wahangaikie kazi za muda. Nchi nyingi zina kazi za muda kuanzia kwenye kilimo, meli za wageni, hospitali, mahoteli.. na hata ujenzi. Vijana badala ya kushinda mitandaoni na kuendesha bodaboda kwa Tsh 10,000 kwa siku tumia muda wako kutafuta kazi nje. Hizi kazi ni za mikataba mwaka mpaka miaka mitatu halafu unaweza kurudi wakati serikali nayo imejipanga. Mjue tu miaka ya 1995-2000 kuna watanzania wengi tu walienda USA kwenye program ya summer camp. walitafuta wenyewe lakini vijana wa siku hizi ni wepesi kulalama badala ya kutafuta fursa.
4. Tatufeni " mentor" au washauri wenye uzoefu. Kuna Watanzania Dunia nzima wewe ni kijana wa miaka 20's badala ya kulalama tafuta mtu mzima wa kukushauri ambaye anafanya kitu ambacho wewe unapenda. Tatizo leo mnashinda kufikiri na kutaka kuwa kama Diamond au Nandy badala ya kutafuta wataalamu au wafanyabiashara ambao unataka kuwa kama wao. Sio lazima wawe Tanzania. Jioulize Je una account ya linked ? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi? Hata hapa vijana kuna watu wengi wakuwapa mawazo lakini mnakimbilia kupiga madongo!madongo yanakusaidia nini?
5. Vijana msisubiri serikali. Serikali haijawahi kusaidia vijana kama wakati huu lakini vijana wa huko nyuma miaka ya 1990's na 2000's walienda kutafuta vyuo na maslahi huko nje wenyewe na marafiki zao sio kwa msaada wowote wa serikali. Tatizo vijana mnasubiri sana serikali ambayo itachukuwa muda sana kuweka mambo ya ajira sawa. Nawashauri tafuteni kazi popote Duniani ilimradi unasaidia familia yako. Lakini usisahau nyumbani
Naunga mkono hoja
P
 
Kwa kweli hiyo ni fursa kubwa ingawa viongozi wetu hasa balozi zetu wamelala bado usingizi wa pono kupata tu hati ya kusafiri vizuizi lukuki unaambiwa ulete mpka barua ya mwaliko sasa huo kama sio ujima ni kitu gani mwaliko wa kazi gani kama mtu kaamua kwenda kufata fursa ughaibuni? Kamishna wa uhamiaji mwenyewe anaona sawa tu katika miaka kadhaa kutoa hati za kusafiria chini ya 200,000 tuko na safari ndefu Sana bado watu wako usingizini.​
 
Unalinganisha maendeleo ya technology ya India na TZ au Africa? India has always been a tech powerhouse.

TZ kupata tu passport ni changamoto. Hawataki watu watoke, waingie wala uraia pacha. Nchi ya kiwaki sana hii. Kuna lawama vijana wanachukua ila ni kidogo sana compared to serikali ambayo haina mazingira wezeshi ya watu kujiongeza.
 
Kama navyosema sisi tumewezaje kuja huku miaka ya 1990’s ! Kwani passport ilikuwa rahisi kupata wakati huo kuliko sasa🤔 . Tatizo lenu kizazi hiki mnasubiri kufanyiwa kila kitu na kupenda kulalama. Nenda katafute passport ukishidwa uje hapa usime tatizo ni nini badala tu ya kujiaminisha kupata ni ngumu.
 
Naomba kwanza kabla ya kutulaum sisi vijana unijumlishie Jumla ya gharama ya passport na visa na nauli ya safari kutoka Tanzania hadi Kuwait kwa mfano.

Baada ya hapo uje kutulaum sisi vijana

Nakumbuka sisi watoto wa form six miaka hiyo 1997 wakati nakuja. Tulitafuta shule wenyewe bila mitandao tulienda america culture center/ usaid pale , tulifanya mitihani ya toefl mzizima wenyewe, tulituma application kwa DHL wenyewe, interview wenyewe na tumekuja hizi nchi hatufahamu watu na tuna miaka 20 tu. Wazazi walikuwa hawjui lolote zaidi ya kusaidia nauli! Wewe unataka mimi eti ndiye nikupe gharama inaonyesha uvivu wa kizazi hiki ulipofikia.

Dogo mimi sina shida hapa naandika kuwasaidia nyie na kama mnaona huu ni utani Mungu wangu anajua najaribu kurudisha na kuelimisha jamii🙏.
 
Kama navyosema sisi tumewezaje kuja huku miaka ya 1990’s ! Kwani passport ilikuwa rahisi kupata wakati huo kuliko sasa🤔 . Tatizo lenu kizazi hiki mnasubiri kufanyiwa kila kitu na kupenda kulalama. Nenda katafute passport ukishidwa uje hapa usime tatizo ni nini badala tu ya kujiaminisha kupata ni n
Nafikiri zama zimebadilika na vitu vingi vimebadilika pia miaka ya 90 tofauti Sana na sasa enzi hizo matishio kama ugaidi hayakuwepo/ hayakusikika kama miaka ya 2000 na kuendelea hata nchi nyingi zimezidi kubadilisha taratibu na sera za mambo ya nje kutokana na mazingira ya sasa. Lakini hiyo haiondoi fursa kwa vijana wengi kujaribu kutafuta maisha nje ya nchi yao hasa mataifa ya magharibi kiukweli balozi zetu zimekaa kisiasa zaidi kuliko uhalisia wenyewe ni ngumu kwa wao kutafuta fursa na kiziweka bayana kwa wenzao walioko nyumbani
 
Kama navyosema sisi tumewezaje kuja huku miaka ya 1990’s ! Kwani passport ilikuwa rahisi kupata wakati huo kuliko sasa🤔 . Tatizo lenu kizazi hiki mnasubiri kufanyiwa kila kitu na kupenda kulalama. Nenda katafute passport ukishidwa uje hapa usime tatizo ni nini badala tu ya kujiaminisha kupata ni ngumu.

FYI hata sisi tupo USA so you're preaching to the choir. Sijasema vijana hawabebi lawama kabisa ila nimesema serikali inabeba lawama zaidi. Ni wazi kupata passport bongo ni kazi wakati nchi zingine passport ni haki yako. Serikali ambayo haitaki hata paypal utaiambia nini kuhusu kuvutia tech companies? Unadhani ni kwanini Microsoft, google, twitter, BBC, Visa, FB hadi NALA kampuni ya mbongo kabisa are headquartered in Kenya badala ya TZ? Hapo napo utalalamikia vijana? Ndo maana nasema 80% ya shortcomings za vijana in the tech world ni sera mbovu za serikali.

Nisome hapa: Diaspora Hawatoi connection?
 
Nakumbuka sisi watoto wa form six miaka hiyo 1997 wakati nakuja. Tulitafuta shule wenyewe bila mitandao tulienda america culture center/ usaid pale , tulifanya mitihani ya toefl mzizima wenyewe, tulituma application kwa DHL wenyewe, interview wenyewe na tumekuja hizi nchi hatufahamu watu na tuna miaka 20 tu. Wazazi walikuwa hawjui lolote zaidi ya kusaidia nauli! Wewe unataka mimi eti ndiye nikupe gharama inaonyesha uvivu wa kizazi hiki ulipofikia.

Dogo mimi sina shida hapa naandika kuwasaidia nyie na kama mnaona huu ni utani Mungu wangu anajua najaribu kurudisha na kuelimisha jamii🙏.
Kadri teknolojia inavyokua na IQ za watu wanaotumia teknolojia hiyo inapungua. Vijana sasa wanaenda na move... Kwenye wengi n wao wanajichomeka hapohapo. Maisha yamebadilika sana, watu wafikirie beyond the Common. Hili ndo lifanyiwe kampeni na serikal Kwa sasa
 
FYI hata sisi tupo USA so you're preaching to the choir. Sijasema vijana hawabebi lawama kabisa ila nimesema serikali inabeba lawama zaidi. Ni wazi kupata passport bongo ni kazi wakati nchi zingine passport ni haki yako. Serikali ambayo haitaki hata paypal utaiambia nini kuhusu kuvutia tech companies? Unadhani ni kwanini Microsoft, google, twitter, BBC, Visa, FB hadi NALA kampuni ya mbongo kabisa are headquartered in Kenya badala ya TZ? Hapo napo utalalamikia vijana? Ndo maana nasema 80% ya shortcomings za vijana in the tech world ni sera mbovu za serikali.

Nisome hapa: Diaspora Hawatoi connection?
Sahihi kabsa hati ya kusafiria tu kizungumkuti eti unaambiwa fomu za maombi uambatanishe na barua ya mwaliko mambo ya kijima kabsa haya mwaliko inawahusu nini vikwazo lukuki wakati kila raia mwenye uhitaji anapaswa kuwa na hati ya kusafiri pia ni chanzo kikubwa cha mapato hebu fikiria wizara ya mambo ya ndani idara ya uhamiaji ingetengeneza kiasi gani cha mapato kama kamishina na wasaidizi wake wakija na mkakati wa kutoa hati za kusafiria 2,000,000 kwa kila mwaka. Lakini unashangaa watu wako maofisini wanashindwa kuja na mipango kazi inayoeleweka kazi zinafanyika kwa mazoea bora liende rushwa ndo inazidi nchi inakosa mapato na fursa zinachangamkiwa na vijana wa nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom