Ushauri: Benki Kuu anzisheni Bondi maalumu kwa diaspora

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Mimi kama diaspora nimeona fursa kubwa sana kwa nchi yetu na bank kuu yetu.

Kwasasa hakuna utaratibu wowote wa kumwezesha;

1. Diaspora kurudi nyumbani miaka ya baadae kwa kuwekeza nyumbani.

2. Utaratibu wa serikali kupata pesa za uhakika kutoka kwa diaspora.

Sasa nini kifanyike;

1. Serikali kwa kupitia Benki Kuu fungueni bondi maalumu kwa ajili ya diaspora ili wawekeze na pesa hiyo iende kwenye miradi ya kimaendeleo kama madini. Wakati huohuo diaspora wanajihakikishia kwenye uzee wao pesa itakuwepo.

2. Serikali kama walivyofanya wenzetu wa Ethiophia kwenye bwawa tunaomba pesa za bondi hii ziende kwenye madini na kilimo kwenye miradi ya mkakati.

Uzuri wa bondi ni kuwapa serikali pesa ya uhakika kwa muda mrefu tena pesa ya kigeni, lakini kwa diaspora watapata pesa ya uhakika wakati wakirudi nyumbani.

Hizi account za CRDB za kuweka pesa kwa diaspora hazina tija kwa nchi wala diaspora. Zimetumika kuwaibia pesa diaspora tu.
 
Back
Top Bottom