Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Kwa muktadha huu, kitu/jambo lisipoonekana kwa macho maana yake halipo?
Hapana kitu sio lazima kionekane kwa macho ndiyo uthibitisho wake uwepo
Ila tunathibisha kwa matokeo yake
Mf: pumzi sio rahisi kuiona kwa macho lakini matokeo yake ni halisi
Paragraph ya mwisho kabisa, umeisoma vizuri ukaielewa Twin?
Nimeelewa twin swali langu jibu lake ni ile paragraph yako ya mwisho
 
Inawezekana ukawa sahihi lakini sio sana, maana kutokujua kwako majibu hakumaanishi kuwa hiyo mifumo haipo au haikuathiri Mkuu.
Kama ni miungu, mizimu na uchawi mimi nina uhakika 100% kuwa havipo.

Tukisema tujadili tutatoka sana nje ya hii mada.

Ila kuhusu uwepo wa jambo flani "supernatural" linalotawala dunia, labda lipo. Kama linatuathiri ni sawa tu.
 
1.Kijana A alimtukana kijana B halafu kijana A(Mtukanaji) akapindishwa mdomo on the spot na kijana B(Mtukanwaji) tena alimwambia kabisa "Mimi huwa situkanwi"
Aisee🤔
2. Kuna mchawi mmoja mwaka huu huu alijaribu kutunishiana misuli na mimi kwa kujaribu kuniua kwa kunisababishia ajali mbaya ya gari. Ajali haikutokea kwa sababu ya Ulinzi ninaolindwa nao 24/7. Nikiri tu kwamba under normal circumstances mimi sikupaswa kuwa hai. Nimekingwa na mashambulizi ya kichawi mengi sana na mengine ni kutoka kwa ndugu zangu wa damu!
Umekingwa na nini ?
Au Mungu mwenyewe?
3. Mwingine alinijia usiku mnene nikiwa nimelala ili aniwangie akidhani simuoni kumbe namuona fully. Nilichofanya ni kumkata jicho tu kisha akatokomea kwa hofu
Yaan nakosa hata cha kusema aisee
Yatosha kwa leo!

UJUMBE: Kuna tofauti kati ya kuamini uwepo wa Uchawi na kuishi kwa kuutumainia uchawi. Wengi huwa wanachanganya Kati ya haya mawili. Wapo ambao wanaamini kwamba kutoamini uwepo wa Uchawi ni Njia ya wao kuwa salama dhidi ya Uchawi Jambo si kweli.
Sasa hapa unawasemea watu ujue
watu wasioamini uchawi ni kweli hauwatesi wala hawaujui kabisa
ndiyo maana hata wakija hapa watakuambia wanaishi maisha bila hayo mauza uza na kila kitu kinaenda
Ukweli ni kwamba kama mtu hana Ulinzi wa Kristo Yesu ndani yake basi hata ajilinde vipi hayupo 100% safe dhidi ya hatari mbalimbali za kiroho ukiwemo Uchawi na za kimwili pia

ZABURI 91
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

YOHANA 10
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Tena mkuu hakuna watu wanaongoza kulalamika kulogwa na mambo kama hayo kama watu wa imani shida inakua wapi?
 
Hapana kitu sio lazima kionekane kwa macho ndiyo uthibitisho wake uwepo
Ila tunathibisha kwa matokeo yake
Mf: pumzi sio rahisi kuiona kwa macho lakini matokeo yake ni halisi
Kama unakubali kuwa pumzi haionekani lakini matokeo yake ni halisi, kwanini unakataa uwepo wa uchawi au nguvu za kiroho kwa kigezo cha kutoziona?
 
Kama ni miungu, mizimu na uchawi mimi nina uhakika 100% kuwa havipo.

Tukisema tujadili tutatoka sana nje ya hii mada.

Ila kuhusu uwepo wa jambo flani "supernatural" linalotawala dunia, labda lipo. Kama linatuathiri ni sawa tu.
Kwani hiyo nguvu unayoikubali wewe ina utofauti gani na kile wengine wanachoita miungu au uchawi?
 
Kwa sababu hakuna matokeo dhahiri twin kama ilivyo kwa pumzi
ndiyo maana kwangu inabaki kama theory tu
Unachotaka wewe Twin ni empirical evidence kwenye mambo ya kiroho na kisaikolojia, kitu ambacho hakiwezekani!

Mbona hata upendo, stress, au chuki havina matokeo dhahiri yanayofanana kwa kila mtu?

Mtu mmoja akipata stress akapungua unene, mwingine akanenepa, na mwingine akapata vidonda vya tumbo, tutasema stress ni theory kwa sababu haina matokeo yanayofanana?
 
Kuna metaphysical aspect ambayo inafanya kazi kwa laws za quantum mechanics... Lakini pia katika maswala hermetic principles.. Toka kale sana na zimefichwa kwa njia za uongo wa physics ili watu wa amini katika tangible reality
zimeficwa kwa manufaa gani sasa?
Wewe umejuaje na zilificwa ?
 
Mbona hata upendo, stress, au chuki havina matokeo dhahiri yanayofanana kwa kila mtu?
Twin matokeo hayafanani ila yana thibitika
Mtu mmoja akipata stress akapungua unene, mwingine akanenepa, na mwingine akapata vidonda vya tumbo, tutasema stress ni theory kwa sababu haina matokeo yanayofanana?
Twin nachotaka ni matokao yanayoweza kuthibitika

Uchawi hauna matokeo yana yothibitika
 
Shukran mkuu asante kwa maoni
Na wanaosema uchawi upo wakisimama kushuhudia huo uchawi, wakihusisha kitu unachokifahamu, utashangaa.
Mimi ni dentist by profesion, miaka ladhaa iliyopita nikwa nafanya shughuli zangu mkoa fulani niliingia makubaliano ya kuhudumia kituo kingine cha pembezoni, ndani ndani. Ktk huduma zilizokuwa natoa mojawapo ni re-habilitation kwa kutengenezea mhusika neno ya bandia.
Kutengeneza meno ya bandia huwa tunafanya kipimo kwa kuchukua impression ya meno mdomoni, then tuna cast na kupata model ya meno ya mhusika. Mhusika alishapewa meno yake, model inatupwa.
Sasa bwana kwenye kituo hicho cha pembezoni ikatokea mhudumu mmoja akaokota ile model, kwakuwa hana ufahamu wowote juu ya meno bandia, akaibeba na kuwashirikisha wenzake 2 ambao nao hawakuwa na ufahamu, isipokuwa walitambua kubwa ni meno ya binadamu. Wakajenga dhana ya uchawi, wakimtuhumu mwenzao mmoja kuwa ni mchawi na amekuwa akiwaroga kwa kutumia neno ya binadamu, walimu washia moto hadi kutaka kumpiga. Ilibidi akimbilie kwa mkuu wa kituo ambaye alinipigia simu ili nitoe ufafanuzi kwani naye alikuwa hajui, ingawa alihisi kubwa hiyo model inaweza kuhusika na kazi zangu. Hiyo ndio ikawa ponapona yake yule mhudumu aliyetuhumiwa kuwaroga wenzake kwa meno ya binadamu!
Nilipotembelea tena pale kituoni ilibidi nitenge muda kuwapa ufahamu wa neno ya bandia.
 
Homie huoni huoni tatizo lilianzia kwenye kuelekezwa ?
Kulikua na ulazima gani kuelekezwa huo uchawi ambao hauna faida yoyote?

Allah aliwawekea mitego waumi wake kwanini
Kuelekezwa kulikuja na maelekezo Ukifanya hivi umekufuru

Si tunataka pepo basi Mitihani ni sehemu ya maisha wajulikane walio amini na wasio amini
 
Back
Top Bottom