Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Ungekua specific ni jambo gani hilo la kichawi limetoa hayo matokeo tungejadili vizuri

Kwa hapa kwetu Tz Imani ya uchawi ni jambo linalochukuliwa kama ni jambo BAYA sana………… uchawi unadhana kwamba mtu anatumia miujiza KUMDHURU mwingine

Sasa kumtafuta mtu “mchawi” akathibitisha huwa anawaroga kuwadhuru wengine inakua mtihani kidogo(labda wale wa mchongo kwa Manabii na mitume)

Kwahiyo utakuta burden of proof inaangukia kwa watu wanaodai wamerogwa………… hapa ndio pana viroja

Kama uchawi upo basi ni lazima iwe rahisi sana kuuthibitisha upo………….. lakini kwa bahati mbaya sana wasio “wachawi” ndio watu wa kwanza kutetea uchawi upo kwa kuweka ugumu kwamba uchawi hauthibitiki kirahisi kwa masharti yake as if wao ndio wachawi na wanajua kanuni zake
Uchawi yeyote yule anaweza kuutenda na si lazima hadi awe mchawi, hata waganga hufanya uchawi wa ubaya au uzuri na ndio maana hao wasio wachawi hutetea uchawi kwa sababu wanaweza kumroga mtu kupitia kwa mganga na waganga wapo wazi wanajitangaza ni tofauti na wachawi.

Kwahiyo kuthibitisha tu inawezekana ila utake uthibitisho wenye vigezo vya kisayansi.
 
Labda unifafanulie UCHAWI ni nini mkuu?………….. kwa maelezo yako haya inawezekana hata wewe ukawa ni mchawi pia au unaweza kuufanya.

Kwamba mtu yeyote anaweza kuufanya uchawi?…………….. to be honest mimi binafsi nataka kuujua na ku practice huo uchawi

Hebu “thibitisha” huo uchawi upo mkuu
 
Nasubiri jibu lake pia
 
Tukitumia tafsiri ya kutoka kwenye kamusi ya kiswahili inasema hivi kuhusu uchawi: Ufundi wa kutumia dawa au vitabu vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe.

Kwa tafsiri hiyo ina maana kwa mfano hata wewe ukielekezwa matumizi ya dawa fulani ili kusababisha madhara(kuroga) labda kugombanisha watu au kumuadhibu aliyekuibia na ukafanya hivyo hivyo basi huo ni uchawi teyari maana umeroga hapo.

Kuna vitabu kibao tu vya wazungu na vya wabongo ambavyo vinafundisha matumizi ya dawa ama visomo katika namna ya kufanya uchawi.

Binafsi sioni kama nalazimika kukuthibitishia kuwepo uchawi, nachofanya ni kueleza ni namna gani unaweza mwenyewe ukathibitisha matokeo ya huo unaoitwa uchawi ila kama wewe unataka tu uthibitishiwe uchawi basi mie sio jukumu langu.
 
Mkuu hiyo tafsiri yako ya UCHAWI ina walakini.

Tukiwa na nafsiri sahihi ya UCHAWI tutaweza kukinzana vizuri kwa hoja……….. tafsiri yako imepelea, ufundi ni sayansi
 
Hiyo sio tafsiri yangu bali ni tafsiri ya kamusi, TUKI.

Suala la tafsiri sahihi ya uchawi huo ni mjadala mwengine maana kuna tafsiri nyingi kutoka kwenye kamusi na zipo tafsiri binafsi za watu, ila hapa hoja yetu sio tafsiri sahihi.

Kwani wewe tafsiri yako ya uchawi ni ipi?

Ufundi ni ujuzi au uhodari.
 
Ufundi ni UJUZI aka Skills/knowledge

Uhodari ni umahiri/ukakamavu/ushupavu

Turudi kwenye mada 😂

Uchawi HAUPO ispokua watu wanaamua kukubali jambo fulani ni la kichawi bila kuwa na uthibitisho wowote thabiti
 
Ndio maana kuna hii mada ili tujadili hiyo mitazamo aina mbili ya watu, mtazamo wa uchawi upo na mtazamo wa kwamba hakuna uchawi.

Kama mtu anafanya jambo analoamini ni uchawi na anapata majibu aliyokusudia kutokana na hicho alichokifanya, basi kuna haja ya kutolewa maelezo kuwa kilichofanyika ni nini? Hata kama si uchawi basi kuwe na maelezo kuwa si uchawi bali hiki ama kile ili wenye kuamini uchawi waelewe maana uchawi si simulizi za zamani bali ni kitu ambacho watu wanatenda.
 
Hivi UGUMU wa KUTHIBITISHA UCHAWI upo wapi haswaa

Wewe si unajua uchawi?………… hebu niroge huku nilipo tukate mzizi wa ftna hapa

Nakubaliana na wewe ukitumia neno WANAAMINI……………IMANI haijawahi kuwa FACT hata siku moja mkuu, you can believe in whatever you want
Imani yako haifanyi kitu kisichokuwepo kuwa kipo.

Ukiamini mjomba wako kakuroga figo sababu alikuomba msaada hukumpa hiyo ni wewe tu mkuu……..ila huwezi kuthibitisha zaidi ya kutumia sababu ya mgogoro wako na mjomba wako
 
Sasa mkuu unavyoniambia nikuroge hivyo ndio kuthibitisha uchawi? Unaweza ukaeleza ni kwa vp huo uchawi utathibitika kwa mimi kukuroga wewe? Tuchukulie mimi nimekuroga kweli na wewe ukakubali kweli umerogwa, je hiyo ndio itakuwa uthibitisho wa kuwepo uchawi? Au itakuwa umekubali tu kuamini uchawi?

Ndio maana mimi nataka tujadili uchawi kwa yale mambo ambayo mtu anafanya kwa makusudio maalum na kweli anapata matokeo vilevile alivyokusudia. Kwa sababu yapo mambo ambayo hufanyika au hutokea ambayo ninyi mnaopinga uchawi mnasema ni saikolojia tu, tricks tu n.k

Tujadili kwa upana mkuu tusishikilie tu misimamo yetu kwa kukariri neno la uthibitisho.
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
kwani hujashuhudia uchawi wa kizungu kwenye SGR DOM to Dar masaa 3?
 
Sasa mkuu unavyoniambia nikuroge hivyo ndio kuthibitisha uchawi? Unaweza ukaeleza ni kwa vp huo uchawi utathibitika kwa mimi kukuroga wewe? Tuchukulie mimi nimekuroga kweli na wewe ukakubali kweli umerogwa, je hiyo ndio itakuwa uthibitisho wa kuwepo uchawi? Au itakuwa umekubali tu kuamini uchawi?

Ndio maana mimi nataka tujadili uchawi kwa yale mambo ambayo mtu anafanya kwa makusudio maalum na kweli anapata matokeo vilevile alivyokusudia. Kwa sababu yapo mambo ambayo hufanyika au hutokea ambayo ninyi mnaopinga uchawi mnasema ni saikolojia tu, tricks tu n.k

Tujadili kwa upana mkuu tusishikilie tu misimamo yetu kwa kukariri neno la uthibitisho.
Mkuu ukiniambia kesho nakuroga utaamka hauna nywele kichwani na kweli nikaamka sina hizo nyewele si Iitakua ndio UTHIBITISHO(matokeo kuonekana) kwamba nilikua na nywele lakini umezitoa “kimiujiza”

Lakini ukiniambia nakuroga mwaka huu lazima utaumwa hapo utakua unacheza na saikolojia kwa kutumia possibly ya mimi kuumwa ndani ya mwaka inawezekana kabisa….. so siku nikiumwa niamini umeniroga
 
Kwahiyo mkuu kwa ufahamu wako ni kwamba uchawi umekuwa hauna uthibitisho kwa miaka yote hii kwa sababu hauna matokeo kama huo mfano uliyotoa?

Ushajiuliza baada ya kuamka hauna hizo nywele ndio utaweza kuelezea kwa jinsi gani huo uchawi umeweza kuondoa hizo nywele?
Utaweza kuthibitisha kuwa ni uchawi tu ndio ulitoa hizo nyewele na si kitu chengine?

Sioni utaweza vp kuwa tofauti na visa vya watu wanavyoeleza kuhusu uchawi humu ila mnawaambia hakuna uthibitisho au ni nocebo tu.
 
Basi wazazi wakafuatwa mara moja tukaona wanafunzi wanakuja nyumban na kwajiran wakatoa taarifa nilipofikia kwa mzee makoye aliposikia hivyo akasikiliza maneno ya wanafunzi na yey akarejea kumbu kumbu zake akachukua panga hajabahatisha akafika aka noa panga nje ya yule bibi watu wakapiga yowe akawa anataka kumfeka badae akatulia akamwambia nakupa nusu saa mwanangu awe mzima la sivyo ww Leo mwisho wako kweli watoto walipona siku hiyo hiyo
Uchawi ni dhana lakini nimekumbuka zamani sana , Kuna Bibi mmoja huko kijijini kwetu alijigeuza fisi ghafla akawa anakimbizwa barabarani kabisa saa 10 jioni yaani huyo fisi alikuwa anakimbizwa kwa Wanakijiji kupokezana na walikuwa wakinyoosha mkono kumpiga mawe au fimbo mikono ilikuwa inakufa ganzi

Huyo fisi route yale ilikuwa ndefu sana nikianza kufikiria huo umbali kama km 15 wanakijiji pumzi zinakata ma wengine wanaunganisha kumkimbiza nao pumzi zinakata. Sio chini ya 20 mpaka 30 km
 
Aisee
 
Back
Top Bottom