Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Hali hiyo inafanya wenye kueleza experience zao humu ziwe kama story za kubuni tu kwenu maana ni vitu vigeni kwenye maisha ya kila siku.

Huwa mnachagua kuja kueleza yale matukio ambayo yanahalalisha msimamo wenu tu.
Una muda?
 
Kwahiyo mkuu kwa ufahamu wako ni kwamba uchawi umekuwa hauna uthibitisho kwa miaka yote hii kwa sababu hauna matokeo kama huo mfano uliyotoa?

Ushajiuliza baada ya kuamka hauna hizo nywele ndio utaweza kuelezea kwa jinsi gani huo uchawi umeweza kuondoa hizo nywele?
Utaweza kuthibitisha kuwa ni uchawi tu ndio ulitoa hizo nyewele na si kitu chengine?

Sioni utaweza vp kuwa tofauti na visa vya watu wanavyoeleza kuhusu uchawi humu ila mnawaambia hakuna uthibitisho au ni nocebo tu.
Mkuu uchawi kwa lugha nyepesi ni “maajabu”…….. yaani mambo kutokea kinyume na kanuni za nature(sayansi)

Mimi sitaki kujua jambo imekuaje likatokea……..maana nikijua itakua ni sayansi

Mimi nataka kuona tu hayo maajabu yametokea nijiridhiashe kweli uchawi upo.

Kuna mambo mengi sana yanatokea na tunayaona lakini kisayansi bado haijulikani yanayokeaje.

Hakuna mahali popote Duniani uchawi umewahi kuthibitishwa kutokea zaidi ya ngonjera za madai ya kuwa imetokea

Mimi nimeishi kijijini na nilipokuja town nilifikia uswahilini sehemu ambazo watu kwa 99% wanaamini uchawi lakini Sijawahi kuthibitisha popote kama upo japo wanaodaiwa wachawi wapo na wanaodai kurogwa wapo lakini hakuna ushahidi wowote

Sasa basi tuachane na madai ya matokeo ya watu, unaweza kuthibitisha upo? Au wewe kazi yako ni kuamini wanaosimulia wameona matokeo ya uchawi?
 
Sasa humu watu wenye kueleza experience zao kwenye mambo yenye kuhusishwa na uchawi ni watu wenye kuamini uchawi tu ila wenye kudai hakuna uchawi wao hawajawahi hata kushuhudia hayo matukio yenye kuhusishwa na uchawi yani hawajawahi hata kusikia tu matukio hayo hata kwa ndugu ama rafiki zao.

Na hapo ndipo panapo nishangaza, najiuliza wote tunaishi afrika hii hii ama?
Changamoto kubwa ya IMANI yoyote ile huwa haitaki matumizi sahihi ya akili………… huwa inataka kuamini tu.

Yaani kwasababu unaamini uchawi upo hivyo mtu akikwambia kuna bibi ni mchawi nilimuona kwa macho yangu anageuka fisi wewe utakubali tu?

Yaani kwenye IMANI kila kitu kinawezekana…….. namaanisha kila kitu
Ukitumia akili kikamilifu hautakaa ukubaliane na Imani yoyote ile ikiwemo uchawi
 
Umemalizaa kwenye imani kitu chochote kinawezekana

Na ajabu ili upate matokeo unaambiwa lazima uamini kwanza
 
Mkuu uchawi kwa lugha nyepesi ni “maajabu”…….. yaani mambo kutokea kinyume na kanuni za nature(sayansi)

Mimi sitaki kujua jambo imekuaje likatokea……..maana nikijua itakua ni sayansi

Mimi nataka kuona tu hayo maajabu yametokea nijiridhiashe kweli uchawi upo.

Kuna mambo mengi sana yanatokea na tunayaona lakini kisayansi bado haijulikani yanayokeaje.

Hakuna mahali popote Duniani uchawi umewahi kuthibitishwa kutokea zaidi ya ngonjera za madai ya kuwa imetokea

Mimi nimeishi kijijini na nilipokuja town nilifikia uswahilini sehemu ambazo watu kwa 99% wanaamini uchawi lakini Sijawahi kuthibitisha popote kama upo japo wanaodaiwa wachawi wapo na wanaodai kurogwa wapo lakini hakuna ushahidi wowote

Sasa basi tuachane na madai ya matokeo ya watu, unaweza kuthibitisha upo? Au wewe kazi yako ni kuamini wanaosimulia wameona matokeo ya uchawi?
Twende taratibu tu.

Kuna vitu viwili, kuna athari ya matokeo ya mambo yenye kuaminika ni kutokana na nguvu ya uchawi na kuna uthibitisho wa huo uchawi wenyewe. Mvutano mkubwa kwenye hili suala la kuhusu uchawi upo kwenye uthibitisho, usifikiri watu wote wenye kuamini uchawi basi walikuwa wakiamini hivyo toka zamani, hadi sasa kuna watu wanakubali kuamini uchawi baada ya kushuhudia na kujiridhisha wenyewe ilhali watu hao walikuwa wakipinga kabisa kuwepo kwa uchawi. Kwahiyo hata wewe ambaye haujashuhudia uchawi huko tokea huko kijijini mpaka mjini binafsi sioni ajabu maana wapo pia wenye kuamini uchawi ila hawajashuhudia huo uchawi na wapo ambao walikuwa wakipinga ila wakaja kushuhudia.

Ndio maana nasema mvutano mkubwa upo kwenye uthibitisho, na ndio maana unasema duniani hakujawahi kuthibitishwa kutokea uchawi na hiyo kwa sababu ya hoja ya uthibitisho na si kwamba hakuna hayo maajabu.

Ndio maana nikakupa tafsiri ya uchawi na kutoa mifano ili kuonyesha kwamba hata wewe unaweza kufanya ili kujiridhisha mwenyewe kama ni kweli au ni ngonjera tu ila cha ajabu mkuu bado unashikilia kutaka mimi ndio nikuthibitishie kwa kutaka nikuroge.
 
Changamoto kubwa ya IMANI yoyote ile huwa haitaki matumizi sahihi ya akili………… huwa inataka kuamini tu.

Yaani kwasababu unaamini uchawi upo hivyo mtu akikwambia kuna bibi ni mchawi nilimuona kwa macho yangu anageuka fisi wewe utakubali tu?

Yaani kwenye IMANI kila kitu kinawezekana…….. namaanisha kila kitu
Ukitumia akili kikamilifu hautakaa ukubaliane na Imani yoyote ile ikiwemo uchawi
Sasa na mimi nakwambia tumia akili pia kutafakari kwamba kwanini watu hawaamini kila kitumaana kuna utofauti wa mambo ambayo watu wanaamini? Kwanini watu hubadili imani zao na wakati mwengine hukosoa walichokuwa wakiamini mwanzo?

Halafu chengine imani ni sehemu ya maisha ya binaadamu hakuna mwenye kuweza kujitenga na imani, imani si Mungu,dini wala uchawi.
 
Mkuu mimi nimezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya IMANI kwa asilimia 100+…………… Naijua IMANI sababu maisha yangu yote toka mtoto hadi nakua na akili timamu nimeiishi IMANI

Unapozungumzia kubadili imani hata mimi nimebadili so sina haja ya kujiuliza kwanini wanabadili imani sababu naimekwiisha pita huko kitambo kabla ya kubaini hizo ni hekaya tu za kusadikika

FACT huwa ni moja tu kwa jambo moja mkuu…… watu wanabadili imani kwasababu wanabaini ni uongo tu, na huko wanakokwenda wanakuta yale yale tu ila kwasababu toka utoto wao saikolojikali akili zao zimekua brainwashed wanalazimika kuwa kwenye imani yoyote ili mradi kukidhi matakwa ya nafsi zao kua imani ni lazima
 
Twende taratibu tu.

Kuna vitu viwili, kuna athari ya matokeo ya mambo yenye kuaminika ni kutokana na nguvu ya uchawi na kuna uthibitisho wa huo uchawi wenyewe. Mvutano mkubwa kwenye hili suala la kuhusu uchawi upo kwenye uthibitisho, usifikiri watu wote wenye kuamini uchawi basi walikuwa wakiamini hivyo toka zamani, hadi sasa kuna watu wanakubali kuamini uchawi baada ya kushuhudia na kujiridhisha wenyewe ilhali watu hao walikuwa wakipinga kabisa kuwepo kwa uchawi. Kwahiyo hata wewe ambaye haujashuhudia uchawi huko tokea huko kijijini mpaka mjini binafsi sioni ajabu maana wapo pia wenye kuamini uchawi ila hawajashuhudia huo uchawi na wapo ambao walikuwa wakipinga ila wakaja kushuhudia.

Ndio maana nasema mvutano mkubwa upo kwenye uthibitisho, na ndio maana unasema duniani hakujawahi kuthibitishwa kutokea uchawi na hiyo kwa sababu ya hoja ya uthibitisho na si kwamba hakuna hayo maajabu.

Ndio maana nikakupa tafsiri ya uchawi na kutoa mifano ili kuonyesha kwamba hata wewe unaweza kufanya ili kujiridhisha mwenyewe kama ni kweli au ni ngonjera tu ila cha ajabu mkuu bado unashikilia kutaka mimi ndio nikuthibitishie kwa kutaka nikuroge.
Nilikuambia natamani sana kuujua uchawi mkuu lakini hukunielekeza namna ya kuufanya

Tafadhali nifundishe hapa niufanye ili nijiridhishe 🙏🙏
 
Mkuu mimi nimezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya IMANI kwa asilimia 100+…………… Naijua IMANI sababu maisha yangu yote toka mtoto hadi nakua na akili timamu nimeiishi IMANI

Unapozungumzia kubadili imani hata mimi nimebadili so sina haja ya kujiuliza kwanini wanabadili imani sababu naimekwiisha pita huko kitambo kabla ya kubaini hizo ni hekaya tu za kusadikika

FACT huwa ni moja tu kwa jambo moja mkuu…… watu wanabadili imani kwasababu wanabaini ni uongo tu, na huko wanakokwenda wanakuta yale yale tu ila kwasababu toka utoto wao saikolojikali akili zao zimekua brainwashed wanalazimika kuwa kwenye imani yoyote ili mradi kukidhi matakwa ya nafsi zao kua imani ni lazima
Wewe umesema kwenye imani mtu hatumii akili kwamba mtu anaamini chochote tu ndio maana nikasema ingekuwa hivyo basi tusingetofautiana kwenye kuamini wote tungekuwa tunaamini tu kila kitu, maana si hatutumii akili kwamba.

Huyo asiyeamini kabisa je, yeye aliwezaje kujua kuwa imani zote duniani ni uongo hadi akifikia hitimisho la kutokuamini? Binafsi sioni tofauti ya anayeamini na asiyeamini kwa sababu huyu asiyeamini unakuta labda kaona baadhi ya mambo katika hiyo imani ambayo hayapo sawa basi mtu huyo anaenda moja kwa moja kujiingiza kwenye makundi au msimamo wa kupinga Mungu,miungu,uchawi n.k na atalazimika kutetea huo msimamo kwa hali yeyote ile maana ndio huo msimamo unavyotaka.

Mkuu sote tumezaliwa na kukuta wenye kuamini na kupinga, wote tunapita kwenye mitazamo ya waliyotutangulia huko.
 
Nilikuambia natamani sana kuujua uchawi mkuu lakini hukunielekeza namna ya kuufanya

Tafadhali nifundishe hapa niufanye ili nijiridhishe 🙏🙏
Mimi natamani kujua unachokijua wewe kuhusiana na issue ya uchawi, mimi nataka kuelewa haya ambayo tunaita uchawi je ni nini? Maana mpaka sasa ukitoa madai ya uthibitisho bado sijaona cha kunielimisha kuwa nachoamini ni uchawi kwamba si uchawi bali ni kitu chengine ambacho sikijui.

Maana mpaka upo hapa unabisha kuwa hakuna uchawi ni wazi umeshajiridhisha kuwa hakuna na mimi ndio nataka kujifunza toka kwako.
 
Sasa ni RASMI umeishiwa na HOJA mkuu

Mijadala ya watu wote wa IMANI ukiwabana huwa wanaishi kukutaka wewe ndio UTHIBITISHE Imani hiyo haipo

Kitu ambacho HAKIPO ni hakipo tu na kilichopo kipo tu

Wajibu wa THIBITISHA kitu upo kwa anayesema kitu hicho kipo wakati HAKIONEKANI

Leo hii ukisema umegundua dawa ya Saratani itakua ni wajibu wako kuthibitisha inatibu nasio kuwataka wanao hoji kuthibitisha haitibu

BTW si wewe umesema utanifundisha uchawi na mimi nijaribu kuufanya nijiridhishe upo? Au umeghairi?
 
Wewe umesema kwenye imani mtu hatumii akili kwamba mtu anaamini chochote tu ndio maana nikasema ingekuwa hivyo basi tusingetofautiana kwenye kuamini wote tungekuwa tunaamini tu kila kitu, maana si hatutumii akili kwamba.

Huyo asiyeamini kabisa je, yeye aliwezaje kujua kuwa imani zote duniani ni uongo hadi akifikia hitimisho la kutokuamini? Binafsi sioni tofauti ya anayeamini na asiyeamini kwa sababu huyu asiyeamini unakuta labda kaona baadhi ya mambo katika hiyo imani ambayo hayapo sawa basi mtu huyo anaenda moja kwa moja kujiingiza kwenye makundi au msimamo wa kupinga Mungu,miungu,uchawi n.k na atalazimika kutetea huo msimamo kwa hali yeyote ile maana ndio huo msimamo unavyotaka.

Mkuu sote tumezaliwa na kukuta wenye kuamini na kupinga, wote tunapita kwenye mitazamo ya waliyotutangulia huko.
Kuna Miungu zaidi 1000 Duniani na kila mtu ANAAMINI Mungu wake ndio SAHIHI na Miungu ya wenzake ni Ubatili na laana kuiabudu kwani watakumbana na adhabu ya milele

Na kila mtu anaamini Mungu wake ndio amempa Afya, mke na watoto, anampa riziki, anampa pumzi ya bure nk nk

Na tusio amini hizo hekaya tunapata vyote hivyo LAKINI watu wa Imani kila mmoja anaamini Mungu wake ndio anatuonea huruma tusio amini ndio maana anatupa sisi😂

Sasa sijui nitakwenda kuhukumiwa na Mungu gani huko “mbinguni”

Hizi ndio AKILI za watu wa IMANI

Watu wa imani sio kama hawana akili timanu, Wanazo sana…………. Isipokua linapokuja swala la Imani Akili huwa wanaiweka pembeni

Hii ni replies karibu ya 10 nakuomba jambo moja tu UTHIBITISHO kwamba Uchawi Upo au THIBITISHA uchawi unafanya kazi lakini naona blah blah tu unaruka ruka tu kuhamisha swali la msingi

Haiwezekani wewe ujue uchawi upo halafu ushindwe kueleza upo kivipi
 
Sasa ni RASMI umeishiwa na HOJA mkuu

Mijadala ya watu wote wa IMANI ukiwabana huwa wanaishi kukutaka wewe ndio UTHIBITISHE Imani hiyo haipo

Kitu ambacho HAKIPO ni hakipo tu na kilichopo kipo tu

Wajibu wa THIBITISHA kitu upo kwa anayesema kitu hicho kipo wakati HAKIONEKANI

Leo hii ukisema umegundua dawa ya Saratani itakua ni wajibu wako kuthibitisha inatibu nasio kuwataka wanao hoji kuthibitisha haitibu

BTW si wewe umesema utanifundisha uchawi na mimi nijaribu kuufanya nijiridhishe upo? Au umeghairi?
Kwanza hakuna nilipotaka uthibitishe chochote mkuu bali nimetaka kujua kutoka kwako kwa namna gani umejiridhisha kuwa hakuna uchawi, lengo ni kujifunza kuona upande ambao pengine mie sijauona bado. Na ndio maana humu nikagusia issue ya kwamba watu wenye kupinga uchawi hawaelezi experience zao katika matukio ambayo yanaaminiwa kama ni uchawi iwe kwao wenyewe,familia au hata watu wa karibu tu ili tusikie wao wanashughulikia vp mambo hayo tofauti na sisi.

Ni sahihi kuwa kitu kama kipo ni kipo tu na kama hakipo hakipo tu, huo ni UKWELI na UKWELI huwa hautegemei uthibitisho. Maana uthibitisho ni kwa ajiri yetu sisi ndio maana kuna leo tunaweza hatuna uthibitisho kuhusu jambo fulani ila baada ya muda tukapata uthibitisho ila UKWELI upo vilevile tu maana hautegemei uthibitisho.

Tunapozungumzia huo wajibu wa anayetakiwa kuthibitisha basi pia si tu kwa anayedai kitu kipo tu, bali hata anayedai kujua kuwa kitu fulani hakipo anawajibu wa kuthibitisha. Sasa hicho kibachoitwa uchawi kina sifa ya kutoonekana, akija mtu na kudai anajua hicho kitu (kisichoonekana) hakipo atapaswa kuthibitisha.

Kutokuwepo kwa uthibitisho, sio uthibitisho wa kutokuwepo.
 
Kuna Miungu zaidi 1000 Duniani na kila mtu ANAAMINI Mungu wake ndio SAHIHI na Miungu ya wenzake ni Ubatili na laana kuiabudu kwani watakumbana na adhabu ya milele

Na kila mtu anaamini Mungu wake ndio amempa Afya, mke na watoto, anampa riziki, anampa pumzi ya bure nk nk

Na tusio amini hizo hekaya tunapata vyote hivyo LAKINI watu wa Imani kila mmoja anaamini Mungu wake ndio anatuonea huruma tusio amini ndio maana anatupa sisi😂

Sasa sijui nitakwenda kuhukumiwa na Mungu gani huko “mbinguni”

Hizi ndio AKILI za watu wa IMANI

Watu wa imani sio kama hawana akili timanu, Wanazo sana…………. Isipokua linapokuja swala la Imani Akili huwa wanaiweka pembeni

Hii ni replies karibu ya 10 nakuomba jambo moja tu UTHIBITISHO kwamba Uchawi Upo au THIBITISHA uchawi unafanya kazi lakini naona blah blah tu unaruka ruka tu kuhamisha swali la msingi

Haiwezekani wewe ujue uchawi upo halafu ushindwe kueleza upo kivipi
Na ndio maana nasema hakuna tofauti, anayeamini anaamini Mungu wake ndio sahihi katika hiyo miungu 10000 ambayo mengine hata haijui, na asiyeamini naye anaona miungu yote hiyo 1000 sio sahihi na mengine hata hajawahi kuisikia.

Suala la uthibitisho nishalielezea hapa na ndio maana hata wewe ulivyotaka nikuroge nikakwambia hilo haitosaidia kuwa uthibitisho, ukasema unataka kujiridhisha kama kweli upo na si kujua unafanyaje kazi maana hiyo itakuwa sayansi.

Tatizo hamuwezi kujadili haya mnayoyapinga tofauti na kung'ang'ania uthibitisho tu, binafsi huwa sikatai kuwa hakuna uthibitisho na nalieleza wazi ila bado mtaendelea kudai uthibitisho hapo huwa mnanifurahishaga sana.
 
Narudia tena kukujibu kwamba mkuu IMANI naijua kwasababu NIMEIISHI kwa zaidi ya nusu ya maisha yangu………..yaani niliaminishwa na nikaamini kila jambo jema lilitokea kwenye maisha yangu ni kazi ya Mungu.
Na kila jambo gumu lililo nitokea nilitumia IMANI kutafuta sababu kwa kuunganisha dots na kufikia muafaka kwamba ama ni kazi ya Shetani ama nimerogwa……….pengine kwasababu nilikwanzana na ndugu au jirani tukatupiana maneno “si unajifanya mjanja wewe tutaona”

LAKINI wakati nilipoamua kuweka IMANI pembeni na kuanza kutumia akili(Logic) ndio wakati nilipobaini IMANI ni UJINGA kama ujinga mwingine

Mwisho umemalizia kwa kuanzika “Kutokuwepo kwa uthibitisho, sio uthibitisho wa kutokuwepo”
Hapa ndipo ujinga wenyewe ulipo kwamba ukiambiwa mimi nyumbani kwangu usiku anakuja Mtume Mohammed na Yesu kristo napiga nao sana stori kuhusu Mungu utakubali tu? Kwamba kitumbua kinageuka Prado, kwamba mtu anageuzwa fisi na unakubali tu?………… ndio maana nikakwambia ujinga wa imani ni kwamba KILA KITU KINAWEZEKANA sababu haihitajiki uthibitisho………just a blind believe
 
Na ndio maana nasema hakuna tofauti, anayeamini anaamini Mungu wake ndio sahihi katika hiyo miungu 10000 ambayo mengine hata haijui, na asiyeamini naye anaona miungu yote hiyo 1000 sio sahihi na mengine hata hajawahi kuisikia.

Suala la uthibitisho nishalielezea hapa na ndio maana hata wewe ulivyotaka nikuroge nikakwambia hilo haitosaidia kuwa uthibitisho, ukasema unataka kujiridhisha kama kweli upo na si kujua unafanyaje kazi maana hiyo itakuwa sayansi.

Tatizo hamuwezi kujadili haya mnayoyapinga tofauti na kung'ang'ania uthibitisho tu, binafsi huwa sikatai kuwa hakuna uthibitisho na nalieleza wazi ila bado mtaendelea kudai uthibitisho hapo huwa mnanifurahishaga sana.
Sijui hata umejibu nini hapa

Hebu nieleze kwa utuo mkuu, wewe ulijuaje na kisha kijiridhisha pasi na shaka ya ziada kwamba UCHAWI kweli upo?

Kwa ufahamu wangu lazima kutakua na kitu kinachopelekea kujua jambo fulani lipo……….kitu hicho ndio kinatwa UTHIBITISHO mkuu

Naomba jibu hoja tafadhali🙏
 
Narudia tena kukujibu kwamba mkuu IMANI naijua kwasababu NIMEIISHI kwa zaidi ya nusu ya maisha yangu………..yaani niliaminishwa na nikaamini kila jambo jema lilitokea kwenye maisha yangu ni kazi ya Mungu.
Na kila jambo gumu lililo nitokea nilitumia IMANI kutafuta sababu kwa kuunganisha dots na kufikia muafaka kwamba ama ni kazi ya Shetani ama nimerogwa……….pengine kwasababu nilikwanzana na ndugu au jirani tukatupiana maneno “si unajifanya mjanja wewe tutaona”

LAKINI wakati nilipoamua kuweka IMANI pembeni na kuanza kutumia akili(Logic) ndio wakati nilipobaini IMANI ni UJINGA kama ujinga mwingine

Mwisho umemalizia kwa kuanzika “Kutokuwepo kwa uthibitisho, sio uthibitisho wa kutokuwepo”
Hapa ndipo ujinga wenyewe ulipo kwamba ukiambiwa mimi nyumbani kwangu usiku anakuja Mtume Mohammed na Yesu napiga nao sana stori kuhusu Mungu utakubali tu?………… ndio maana nikakwambia ujinga wa imani ni kwamba KILA KITU KINAWEZEKANA sababu haihitajiki uthibitisho………just a blind believe
Hayo uliyoeleza hapo kuhusu imani si kila imani inaamini hayo, wakati wewe ulipokuwa unaamini hivyo kuna waumini wengine walikuwa wanakuona mjinga kwa hivyo ulivyokuwa ukiamini. Binaadamu ni kiumbe cha hisia na imani na hakuna asiyetumia logic ni sehemu ya ubongo wa mwanadamu.

Watu hutofautiana tu tunayoamini, hutofautiana logic zetu na tunapozitumia. Kwahiyo wewe kuacha kuamini Mungu,dini na uchawi sio kwamba ndio kipimo cha logic kwamba ukitumia logic lazima utafikia hitimisho la kuacha kuamini hivyo vitu, kuna watu wanatumia logic na hufikia hitimisho tofauti na hivyo.

"Kukosekana kwa uthibitisho sio uthibitisho wa kutokuwepo"

Shida ni kwamba mnafanya ushahidi na ukweli kuwa kitu kimoja ilhali hivyo ni vitu viwili tofauti, ushahidi unaweza ukawa hakuna kwa sababu kwa sasa bado haujapatikana au ni ngumu kupatikana huo ushahidi kutokana na aina ya huo ushahidi wenyewe, ila hiyo haiathiri ukweli bado ukweli utabaki kama ulivyo.

Ni kosa la kimantiki kutumia kukosekana kwa ushahidi kufanya kuwa ni ushahidi wa kutokuwepo, kwahiyo sisemi ukubali kitu bila ushahidi ila tusifanye kukosekana ushahidi kuwa ni ushahidi.
 
Kwahiyo tunakubaliana HAKUNA UTHIBITISHO kwamba uchawi upo?
 
Wengi hatuielewi dhana ya uchawi coz hatuwazi nje ya box, dhana ya uchawi inatekelezwa kwa material ambayo yapo proved scientifically, mfano MTU anataka kukusababishia ugumba, ataandaa chemical compound ya mimea au viumbe wengine ajili ya kuleta madhara ktk mfumo wa uzazi, ila kwa kua yote haya hufanyika locally ndo maana kuna ukinzani was mitizamo
 
Back
Top Bottom