Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Mimi huo uchawi siamini kama upo naamini ni dhana tu

Vp wewe una amini uchawi upo
Sina sababu ya kusema uchawi upo kama nguvu halisi isiyo ya kawaida, kwa sababu haujathibitishwa kisayansi. Kwa hiyo, kwenye suala hili naegemea upande wako.

Uchawi unaonekana zaidi kuwa dhana/imani ya kitamaduni kuliko jambo lililothibitishwa kisayansi.
 
Umemaliza bro 🤝
 
Hakuna uchawi bali ujinga juu ya jambo flan ambalo mwamini uchawi analiita uchawi na kwakuwa halijuwi jambo hilo, na kulieleza atakieleza in a distorted way.
NO WITCHCRAFT BUT KNOWLEDGE GAP.
Uchawi ni sehem ya science, uchawi ni sayansi ifanyikayo kwa local way, mfano wachawi hutumia mkusanyiko wa chemical compound ya viumbe mbali mbali ajili ya kukamilisha chemical reaction zao japo hata wao sidhani kama wanajua wafanyacho in sehem ya science
 
Sina sababu ya kusema uchawi upo kama nguvu halisi isiyo ya kawaida, kwa sababu haujathibitishwa kisayansi. Kwa hiyo, kwenye suala hili naegemea upande wako.

Uchawi unaonekana zaidi kuwa dhana/imani ya kitamaduni kuliko jambo lililothibitishwa kisayansi.
Mkuu uchawi upo, na noi sehem ya science, japo hufanyika kwa njia za kienyeji
 
Wazungu kutambua neno uchawi sio uthibitisho kua uchawi upo kweli

Ndio maana nikasema sijui uchawi
ila naelewa neno uchawi kama dhana tu ni kitu kinachohisiwa lakini uhalisia wake baado haujathibishwa

So kusema wazungu wanatambua neno uchawi haina maana kweli uchawi upo

Ningependa kujua ni kina nani walioandika vitabu vya dini
Maana Muslim ni Waarabu
Inamana wao ndiyo waliandika

Bibilia nayo kwa kiasi kikubwa inaonekana iliandikwa mashariki ya kati

Hao sio wazungu ndiyo lakini huku tumezoea mtu yoyote kuita mzungu bila kujali anatokea bara gani
Screenshot 2026-08-22 193833.jpg

View: https://youtu.be/txytY6LuD5k?si=viOH1SNgvUlaAxp6
 
Naam, ni sahihi kabisa, lazima kuwepo na kitu ambacho muamini uchawi atakihusisha, na kitu hicho kwakuwa hakijuwi, basi atakieleza kwa namna iliyo tofauti na uhalisia.
Hapo unamkusudia mtu ambaye anaamini tu uchawi na kushuhudia hayo yenye kuaminika kuwa ni uchawi, je vp kwa wale ambao hutenda kabisa hayo mambo? Yani mtu anajua nikifanya hivi na kile ni uchawi ambao nitapata matokeo fulani niliyokusudia?
 
Wazungu kutambua neno uchawi sio uthibitisho kua uchawi upo kweli

Ndio maana nikasema sijui uchawi
ila naelewa neno uchawi kama dhana tu ni kitu kinachohisiwa lakini uhalisia wake baado haujathibishwa

So kusema wazungu wanatambua neno uchawi haina maana kweli uchawi upo

Ningependa kujua ni kina nani walioandika vitabu vya dini
Maana Muslim ni Waarabu
Inamana wao ndiyo waliandika

Bibilia nayo kwa kiasi kikubwa inaonekana iliandikwa mashariki ya kati

Hao sio wazungu ndiyo lakini huku tumezoea mtu yoyote kuita mzungu bila kujali anatokea bara gani
Wazungu waliuwana sana kutokomeza imani za kichawi.
 
Hatuwezi kuchukua tukio fulani, tukaliita uchawi, halafu moja kwa moja tukasema ni saikolojia bila kulichunguza.

Mfano: mtu anaumwa baada ya kudai amerogwa. Kuna uwezekano akawa:

1. Ana ugonjwa wa kawaida.

2. Hofu na imani vimemsababishia dalili (nocebo).

3. Kuna sababu nyingine ambayo bado haijagunduliwa.

Kwa hiyo, “kuchunguza ushahidi” nilimaanisha kuangalia tukio lenyewe na kutafuta chanzo chake kabla ya kulipa jina.

Hii haimaanishi kwamba ninajua au nina ushahidi kwamba uchawi unafanya kazi. Sina ushahidi huo. Nilikuwa nasema tu tusihitimishe chanzo cha tukio kabla ya kulichunguza.
Issue ni kwamba watu wameshajichagulia upande kwamba ima uwe mwenyewe kuamini uchawi au uwe wenye kupinga uchawi, hivyo unakuta mtu anapinga uchawi si kwamba ana sababu za msingi bali ni msimamo tu ambao kauchagua hivyo anausimamia.
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Uchawi upo na saikolojia ipo sema ww hujalogwa ila ulihisi umelogwa ndio mana ulivyopotezea ukatafuta dawa hospital ukapona ila UCHAWI NA SAIKOLOJIA ni vitu viwili tofauti
 
Uchawi upo na saikolojia ipo sema ww hujalogwa ila ulihisi umelogwa ndio mana ulivyopotezea ukatafuta dawa hospital ukapona ila UCHAWI NA SAIKOLOJIA ni vitu viwili tofauti
Umewahi kukutana na tukio la uchawi kwenye mazingira gani mpka ukaamini?
 
Nilikutana na uchawi mdogo sana nilifika usukumani ilikuwa siku ya alhamis watoto walikuwa wanarudi nyumban kutoka shule njian njia panda zilitupwa peni tatu katika sehemu nilipofikia jirani yetu watoto wake wawili wakaokota kalamu mbili mwingine akaokota kalamu 1 wakafika wakala na kurud shule sanane kumbe zile kalamu zilitegwa na bibi flan Huwa ukiumwa anakuagua watoto walipofika shule na kuanza kuzitumia walipagawa ikatokea taharuki
 
Basi wazazi wakafuatwa mara moja tukaona wanafunzi wanakuja nyumban na kwajiran wakatoa taarifa nilipofikia kwa mzee makoye aliposikia hivyo akasikiliza maneno ya wanafunzi na yey akarejea kumbu kumbu zake akachukua panga hajabahatisha akafika aka noa panga nje ya yule bibi watu wakapiga yowe akawa anataka kumfeka badae akatulia akamwambia nakupa nusu saa mwanangu awe mzima la sivyo ww Leo mwisho wako kweli watoto walipona siku hiyo hiyo
 
Yaani hapana bana 🤔
 
Issue ni kwamba watu wameshajichagulia upande kwamba ima uwe mwenyewe kuamini uchawi au uwe wenye kupinga uchawi, hivyo unakuta mtu anapinga uchawi si kwamba ana sababu za msingi bali ni msimamo tu ambao kauchagua hivyo anausimamia.
Hapo umeigusa point muhimu. Tatizo ni kuanza na msimamo kabla ya kuangalia ushahidi.

Mtu akisema “uchawi upo” bila ushahidi, na mwingine akisema “uchawi haupo kabisa” bila kuchunguza madai, wote wanaweza kuwa wanaanzia kwenye IMANI, si ushahidi.
 
Back
Top Bottom