Hello jamii intelligence 👋
Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an
Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:
Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi
Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi
kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana
Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje
Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.
Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla
Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa
Sasa najiuliza...
Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?
Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?
Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?
Kuna hii pia👇
Ooh, wachawi wanapaa usiku...
Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?
Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa
Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?
Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?
Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu
Basi kuna mtu akamwambia mama:
Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔
Heh! 🤔
Nikastuka
Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?
Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine
Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.
Usiku naogopa kulala mwenyewe.
Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja
Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo
Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha
So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo
Mara nione hiki...
Mara nisikie kile...
Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?
Asieee!
Nikakaa nikasema:
Hapana, hizi mbona kama fix?
Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win
Nikaacha kabisa huo upuuzi
Nikaamua ku-clean akili yangu
Kuanzia hapo nikiambiwa
Njoo kwenye visomo
Nawaambia
Mimi sina tatizo lolote
Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu
Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku
Nikatumia zangu dawa nikawa fresh
Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu
Sioni mauza mauza wala nini
Naishi vizuri kabisa
Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu
Wala hakuna cha uchawi wala nini
Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake
Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...
Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?
Mashetani wana migodi yao huko?
Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi
Je, uchawi ni nguvu halisi?
Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?
Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...
Kwanini usitumike kinyume chake?
Au kama wachawi wanaweza kupaa...
Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?
Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?
ShesRise_1 ✋️
Ulichokieleza kuhusu maumivu ya kichwa na sababu za kiafya ni sawa: si kila tatizo ni uchawi, na ni muhimu kutafuta sababu za kiafya kwanza. Lakini
Biblia na Qur’an hazisemi kwamba kwa sababu baadhi ya mambo yanaelezeka kisayansi au kisaikolojia, basi uchawi haupo kabisa.
Biblia:
Kutoka 22:18 inasema:
“Usimwache mchawi kuishi.”
Hii yenyewe inaonyesha Biblia haikuchukulia uchawi kuwa hadithi tupu.
Pia
Matendo 8:9-11 inamtaja mtu aliyeitwa Simoni ambaye alikuwa akifanya uchawi na kuwashangaza watu. Na
Matendo 16:16-18 inasimulia msichana aliyekuwa na “pepo wa uaguzi” na watu walipata faida kupitia utabiri wake.
Qur’an:
Al-Baqarah 2:102 inasema kuhusu watu waliofundishwa uchawi na hata inaeleza kwamba uchawi huo unaweza kutumika kuleta madhara, kama kutenganisha mtu na mwenzi wake. Qur’an pia inasema:
Al-Falaq 113:4: “Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni.”
Kwa hiyo Qur’an haikanushi kuwepo kwa uchawi; inatuonya dhidi ya shari yake.
Lakini kuna jambo muhimu:
Biblia na Qur’an hazifundishi kwamba kila ugonjwa, kila kushindwa shuleni, kila ndoto au kila tatizo ni uchawi. Huwezi kuchukua mfano wa mtu aliyegundulika ana upungufu wa damu, kisha ukatumia huo kuthibitisha kwamba uchawi wote haupo. Huo ni kama kusema, “Baadhi ya watu hudhaniwa wamepagawa lakini kumbe wana ugonjwa, kwa hiyo mapepo hayapo.” Hiyo haifuati.
Na swali lako la:
“Kama uchawi upo, kwa nini usitumike kufanya genius awe genius zaidi au kupunguza foleni kwa kupaa?” — hilo ni dhana yako kuhusu uchawi, si mafundisho ya Biblia wala Qur’an. Vitabu hivyo havisemi kwamba uchawi ni
teknolojia yenye matumizi yoyote tunayoyataka. Vinauhusisha na mambo ya siri, udanganyifu na madhara.
Hata Biblia inatofautisha
uchawi na miujiza ya Mungu. Kwa mfano, Kutoka 7:11-12 inataja waganga/wachawi wa Misri waliweza kufanya mambo yao, lakini nguvu zao hazikuwa sawa na uwezo wa Mungu.
Kwa hiyo hoja sahihi si:
“Kwa nini mchawi hapandishi watu angani?”
Hoja sahihi ni:
Biblia na Qur’an zote zinatambua uchawi kama jambo lililokuwepo, lakini zinakataza kuufuata na kuutumia. Na pia si sahihi kuita kila tatizo la kiafya au kisaikolojia “uchawi.”