Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Hapo unamkusudia mtu ambaye anaamini tu uchawi na kushuhudia hayo yenye kuaminika kuwa ni uchawi, je vp kwa wale ambao hutenda kabisa hayo mambo? Yani mtu anajua nikifanya hivi na kile ni uchawi ambao nitapata matokeo fulani niliyokusudia?
Huyo mtu anayeweza kufanya hivyo bila kumdhuru mtu kwa kificho kisha aseme kubwa amefanikisha kichawi, hayupo.
Kama yupo mwbie afanye kwangu
 
Hapo umeigusa point muhimu. Tatizo ni kuanza na msimamo kabla ya kuangalia ushahidi.

Mtu akisema “uchawi upo” bila ushahidi, na mwingine akisema “uchawi haupo kabisa” bila kuchunguza madai, wote wanaweza kuwa wanaanzia kwenye IMANI, si ushahidi.
Umeeleza vizuri kabisa mkuu.
 
Huyo mtu anayeweza kufanya hivyo bila kumdhuru mtu kwa kificho kisha aseme kubwa amefanikisha kichawi, hayupo.
Kama yupo mwbie afanye kwangu
Kwanza mkuu ondoa dhana ya kwamba uchawi ni issue ya kuleta madhara kwamba uchawi ni suala la kumdhuru mtu, hiyo sio sahihi.
 
Dada nakushauri soma dinni yako utajua uchawi ni nini?
Mtume alishaeleza haya mambo kane zimepita huko nyuma
 
Tukiangalia hii hoja ya kwamba uchawi ni saikolojia tu tutaona kwamba inatumika kwa wale ambao wenye kuamini uchawi kisha ikatokea matatizo yao yakahusishwa na uchawi kwa wao kuambiwa tu hivyo nao wakaamini, lakini tukiangalia upande mwengine wapo wenye kuamini uchawi na kufanya kivitendo.

Hawa ambao wanaamini uchawi wamejifunza kufanya huo uchawi, je hao wanapotenda hayo wanayoamini ni uchawi iwe kwa kudhuru au kimanufaa ni kwa vp saikolojia inahusika kwa upande wao?
 
Tukiangalia hii hoja ya kwamba uchawi ni saikolojia tu tutaona kwamba inatumika kwa wale ambao wenye kuamini uchawi kisha ikatokea matatizo yao yakahusishwa na uchawi kwa wao kuambiwa tu hivyo nao wakaamini, lakini tukiangalia upande mwengine wapo wenye kuamini uchawi na kufanya kivitendo.

Hawa ambao wanaamini uchawi wamejifunza kufanya huo uchawi, je hao wanapotenda hayo wanayoamini ni uchawi iwe kwa kudhuru au kimanufaa ni kwa vp saikolojia inahusika kwa upande wao?
Uchawi unafunzwa wapi kwa vitendo?
Kuna darasa?
 
Sijui wanaelewaje
Mi najua kuhusu na vyoelewa mimi
Kuwa na fikra huru mkuu, penda kujielimisha hata usivyoviamini pia.

Kwa wenzetu wazungu wana madarasa na kuna maelfu ya vitabu yenye kufundisha uchawi kwamba ukifanya hivi na vile utapata matokeo haya.
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi



Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Kwa kuwa unayo akaunti ya dolari hapo uswisi unabofya Tu na top up onakuwa tayari Acha wa 2100 nao wajiachie!
 
Kuwa na fikra huru mkuu, penda kujielimisha hata usivyoviamini pia.

Kwa wenzetu wazungu wana madarasa na kuna maelfu ya vitabu yenye kufundisha uchawi kwamba ukifanya hivi na vile utapata matokeo haya.
Wewe unadhani sipendi kujielimisha?
Nasoma Bible na Qur’an
Hata hivyo vifungu sijavichukua kwa AI nimesoma hivyo vitabu viwili
Baada ya hapo nimefikia kuamini hivyo ninavyo amini

Issue za uchawi na majini
Nimeshuhudia watu wakisema wanapandisha majini
Nimeshuhudia watu wakilishwa chano nk.....
 
Sawa dada yangu nauliza ukifa na ukakuta haya uliyoambiwa na mola wako katika kitabu chake kitukufu ni ya kweli na unayaona kwa macho yako itakuwaje?
Mola wangu atanilaumu kwa kusema uchawi ilikua ni dhana?
 
R

ndo alisema hivi kwenye kitabu chake
Unajua shida ipo wapi Mungu aliweka vitu kwa mafumbo vingekua wazi wala kusingekua na sintofahamu sana

Mpaka watu wengine kufikia hatua ya kusema Mungu hayupo
 
Mola ameweka kila kitu
Unajua shida ipo wapi Mungu aliweka vitu kwa mafumbo vingekua wazi wala kusingekua na sintofahamu sana

Mpaka watu wengine kufikia hatua ya kusema Mungu hayupo
mola ameweka kila kitu kwa dalili na ushahidi mfano amesema miongoni mwa alama zangu ama uwepo wangu ni kuwepo kwa jua na mwezi usiku na mchana uwepo wa siku ya mwisho nikushauri dada yangu soma dini vizuri
 
Back
Top Bottom