Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Kaka Manyanza kwanza asante kwa kutenga muda wako kuandika na kisha kushare hapa Shukrani sana bro

1 Nikianza na hilo tukio la ajali, ambalo kwa kawaida ni tukio halisi kwa sababu ajali ilitokea na kila mtu aliona madhara ya hiyo ajali
Madhara hayo yalionekana mpaka kufikia hatua ya wewe kulala kwa siku zote hizo bila fahamu

2. Kuhusu huyo dada kukuambia umepata ajali na umeumia sehemu fulani

Hili halipaswi kuwa jambo la ajabu sana kwa sababu eti hukuwahi kumuona hapo kabla

Nasema hivi kwa sababu ulipata ajali kwenye mazingira ambayo kulikuwa na watu, na watu waliona au walisikia kuhusu hiyo ajali
Sasa kaka vipi kama huyo dada alisikia au alipewa taarifa kutoka kwenye chanzo ambacho wewe hukijui?
Huýo Dada hata hakusikia chochote aisee na mambo ya mitandao hayakuwa yameshika sana nafasi japo ile ajali ilitangazwa na Marehemu Ephraim Kibonde kipindi cha Jahazi wakati ule. Maana nilipata ajali na mfanyakazi wa ile media sehemu tofauti kabisa na jijini. Yule Dada ni mtu wa mikoa ya kusini magharibi na alikuwa ni mshamba sana kipindi kile 🤭 13 years ago
Kuhusu kufanyiwa kisomo, nadhani hii ni issue ya chano, sio?
Mtu mwenye majini hulishwa chano kwa mtindo kama huo
Mara nyingi hutumika vitu kama halua, tende na vinginevyo
Nimeona haya mambo ya chano kwa sababu familia yangu ni pure Muslim
Sina ufahamu sana na hayo mambo ya chano. Lakini kwa sababu ni kisa nimeshare hapa na wewe umezungumzia vitu vipya itabidi nitafute ilimu. Mashallah kwa kuwa kwenye imani yenye haki. Na mimi nilienda huko pia, pekee yangu na watu huwa wanashangaa Msukuma gani ni Muislam.
Sasa kuhusu issue ya kutapika baada ya kisomo ukizingatia pia ulikuwa unaumwa na ulikuwa na maumivu ya kichwa, vipi kama zile ngoma na kelele za dufu zilikukera ukahisi kizunguzungu na hatimaye ukatapika?
Hapa kuna mambo magumu sana 😢 na ukizingatia kwa kipindi ananiambia tayari nilikuwa nimeingia hofu lakini siwezi eleza sana maana vitu vyenye sukari nyingi mimi ni mwepesi kukinai
Inawezekana pia vile ulivyovitapika vilitokana na hali hiyo
Hapana havikutokana na ile hali maana ni kama viini vya yai kabisa mfano wake na ni yai la kienyeji kabisa how come nile mkate, tende,haluwa ,ndizi nichovye kwenye asali nitapike viini vya njano ? Sijui labda kama ilikuwa ni kiini macho
Lakini licha ya yote hayo bado kuna kosekana ushahidi wa kutosha kua ni kweli
Hili nilishalisema ushahidi sana ushahidi hakuna
wewe uli rogwa na hao inaosemekana walikua hawapendi unavyo interact na watu na maisha yako kwa ujumla na hii ni kwa mjibu wa huyo dada mganga
😂😂😂 kuna tukio lilitokea hapa sema ukiandika itaonekana kama unafurahisha au unadanganya watu lakini ndio ukweli na mimi huwa nachukia sana uongo japo ukweli huwa Unanifanya mpaka nichukiwe lakini huwa sibadilishi kile nilichokuwa na uhakika nacho
So kwa mkanganyiko huu na kukosekana ushahidi strong basi uchawi unabaki kama dhana (theory)
Nimekwambia hata leo ni "dhana "
 
Huýo Dada hata hakusikia chochote aisee na mambo ya mitandao hayakuwa yameshika sana nafasi japo ile ajali ilitangazwa na Marehemu Ephraim Kibonde kipindi cha Jahazi wakati ule. Maana nilipata ajali na mfanyakazi wa ile media sehemu tofauti kabisa na jijini. Yule Dada ni mtu wa mikoa ya kusini magharibi na alikuwa ni mshamba sana kipindi kile 🤭 13 years ago
Ahaaaa kumbe ni muda mrefu hivyo
13yrs ago nilikua mdogo ila tayari najitambua
Sina ufahamu sana na hayo mambo ya chano. Lakini kwa sababu ni kisa nimeshare hapa na wewe umezungumzia vitu vipya itabidi nitafute ilimu. Mashallah kwa kuwa kwenye imani yenye haki. Na mimi nilienda huko pia, pekee yangu na watu huwa wanashangaa Msukuma gani ni Muislam.
Msukuma wa kuchovya wewe (jokes
Hapa kuna mambo magumu sana 😢 na ukizingatia kwa kipindi ananiambia tayari nilikuwa nimeingia hofu lakini siwezi eleza sana maana vitu vyenye sukari nyingi mimi ni mwepesi kukinai

Hapana havikutokana na ile hali maana ni kama viini vya yai kabisa mfano wake na ni yai la kienyeji kabisa how come nile mkate, tende,haluwa ,ndizi nichovye kwenye asali nitapike viini vya njano ? Sijui labda kama ilikuwa ni kiini macho
Labda mchanganyiko wa hivyo vitu ndiyo ulitengeneza hivyo viini ya yai 🤭

Ila mie nae mbishi😅 AkA tomaso
Hili nilishalisema ushahidi sana ushahidi hakuna

😂😂😂 kuna tukio lilitokea hapa sema ukiandika itaonekana kama unafurahisha au unadanganya watu lakini ndio ukweli na mimi huwa nachukia sana uongo japo ukweli huwa Unanifanya mpaka nichukiwe lakini huwa sibadilishi kile nilichokuwa na uhakika nacho
dah andika bhana au basi utanisimulia wakati mwingine
Nimekwambia hata leo ni "dhana "
Exactly my brother
 
Ahaaaa kumbe ni muda mrefu hivyo
13yrs ago nilikua mdogo ila tayari najitambua
Hahaha nilikuwa kwenye 24/25 hahaaa
Msukuma wa kuchovya wewe (jokes

Labda mchanganyiko wa hivyo vitu ndiyo ulitengeneza hivyo viini ya yai 🤭
😂😂😂 Yawezekana
Ila mie nae mbishi😅 AkA tomaso
Matukio mengi mimi yana ushahidi wa picha na audio
dah andika bhana au basi utanisimulia wakati mwingine

Exactly my brother
Sawa 😄
 
Je, katika hali ya kawaida, unaweza ukatafuna wembe ukasagikia mdomoni bila kupata maneraha hata kidogo na ukaumeza na usidhurike??

Ikiwa, mtu akakuka mizizi ya miti Fulani, kisha akakupa wembe utafune, ukatafuna vizuri, wembe ukasagika na akakwambia umeze na ukameza bila kudhurika hata kidogo..
Je, hiyo tuiteje??
Kwa anaetaka kuthibitisha aseme na awe tayari kusafiri
 
Katika hali ya kawaida
Jibu ni :haiwezekani
Ikiwa, mtu akakuka mizizi ya miti Fulani, kisha akakupa wembe utafune, ukatafuna vizuri, wembe ukasagika na akakwambia umeze na ukameza bila kudhurika hata kidogo..
Je, hiyo tuiteje??
Wewe umewahi kufanya hivyo?
Kwa anaetaka kuthibitisha aseme na awe tayari kusafiri
Ni wapi huko tupange safari mkuu
 
Uchawi upo... tena duniani. Neno witchcraft limo ndani ya lugha ya kiingereza, inamaanisha hata wao wachawi wanao - Ila siku hizi wanabandika majina mbalimbali ili uchawi flani uheshimike, kwa mfano - Freemasons. Itikadi zao ni kichawi, hata hizo kafara tunazosikia.

Uchawi Afrika, una vyeo vyake. Binafsi, uchawi unategemea uoga na imani yako kuhusiana na uchawi. Yule muoga na tayari anaamini flani mchawi, aweza ugua mchawi wake akimkodolea macho mbaya sana.

Niko nawe uliposema kwa nini wasitupaishe ... ila sasa ndege zao balaa, afu sijui ni masharti, lakini hutamuona mchawi tajiri hata kama yeye anaganga wengine watajirike. Ama kwa nini?

Huku kupaa, wazungu watuambia uchawi ni mbaya, lakini wao wanatafiti TELEPORTATION (kuibuka mji mwingine tokea kwako)... hawa wachawi wetu katika kupaa wanaita kusafiri, lakini fumba macho fumbua ushafika.
sasa najiuliza hii ni teleportation ama usafiri ndani ya WARP SPEED ama imechanganya vyote viwili.

Hapa kwetu,
Je yule mtabiri na vitunguli vyake ni mchawi?
Je mganga wa kienyeji anaeongea lugha zake na kukufanyia mamboz - kuku wa rangi flani wa kafara nk, ni mchawi?

Waafrika tumeamini sana uchawi, na ni moja ya sababu upo. Wapo biasharani vizuri tu kwa sababu sisi waswazi tuna tabia za kichawi.... yaani mtu kutaka mwenzake adhuriwe kwa sababu ni mkali shuleni, ama anajenga bonge la mjengo, kurukia maaumizu huyu kalogwa kisa kichwa kinamuuma mara nyingi kama wenye ugonjwa MIGRAINE na kuanza kumuona mchawi kwanza kabla ya kwenda sipitali. Hizi tabia ndo zarutubisha uchawi.

Pia kuna wakati flani, marekani zamani waliua wachawi, kwa tuhuma tu. Wengi walouawa hawakuwa wachawi, ila vitendo vyao kuwa tofauti na wakristo wakali viliwaponza. Unafikiri hili likitokea bongo, si wataacha uchawi, ama?
Kwa hiyo ina maana, kwa sababu hata sirikalini kuna wachawi, fani itaendelea bila kupingwa sana.
 
Nimesoma hii comment yako kuna baadhi ya sehemu nimeshindwa kukuelewa mkuu

Hii ya kuhusu uchawi kwamba hata kwa wazungu upo inaweza kua kweli kwani wazungu wao si ni wanadamu kama sisi ?

Si hata hivyo vitabu vya dini vimeanzia huko huko kwao
Lakini ni ukweli usiofichika wao hiyo dhana ya uchawi wameiacha ama kuipuuza na pengine ni baada ya kugundua haina faida yoyote

Ndiyo maana wao wameamua ku focus kwa mambo yana yo onekana kwa macho wote tunaona jinsi sayansi inavyoifanya dunia iwe bora kila kukicha japo changamoto hazikosi

Sasa uchawi wenyewe una nini ?
Kwanza unakuta mtu anaeulezea mwenyewe hawezi kuuthibisha
Zaidi atakuambia amini tu

Mimi nashangazwa na watu wanaokumbatia hii dhana ya kale isiyo na tija kwa mtu binafsi au kwa jamii dhana isiyoweza kuleta matokea chanya kwenye jamii

Unakuta mtu anasema ni mchawi na ana uwezo mkubwa wa kichawi lakini ni maskini wa kutupwa
Guys huu uchawi wa hivi ni wa nini 🙌

NB: anae amini aamini ila mimi hapana kila nikijaribu kufikiria nashindwa kabisa
Kukubali hii dhana (Uchawi)
 
Kwahiyo hapo unakubali yale mambo yenye kusemwa kuwa ni nguvu ya uchawi yapo kweli ila ule si uchawi ni jambo lengine tu ambalo hao watu wamekosa uelewa nalo?
Naam, ni sahihi kabisa, lazima kuwepo na kitu ambacho muamini uchawi atakihusisha, na kitu hicho kwakuwa hakijuwi, basi atakieleza kwa namna iliyo tofauti na uhalisia.
 
Nimesoma hii comment yako kuna baadhi ya sehemu nimeshindwa kukuelewa mkuu

Hii ya kuhusu uchawi kwamba hata kwa wazungu upo inaweza kua kweli kwani wazungu wao si ni wanadamu kama sisi ?

Si hata hivyo vitabu vya dini vimeanzia huko huko kwao
Lakini ni ukweli usiofichika wao hiyo dhana ya uchawi wameiacha ama kuipuuza na pengine ni baada ya kugundua haina faida yoyote

Ndiyo maana wao wameamua ku focus kwa mambo yana yo onekana kwa macho wote tunaona jinsi sayansi inavyoifanya dunia iwe bora kila kukicha japo changamoto hazikosi

Sasa uchawi wenyewe una nini ?
Kwanza unakuta mtu anaeulezea mwenyewe hawezi kuuthibisha
Zaidi atakuambia amini tu

Mimi nashangazwa na watu wanaokumbatia hii dhana ya kale isiyo na tija kwa mtu binafsi au kwa jamii dhana isiyoweza kuleta matokea chanya kwenye jamii

Unakuta mtu anasema ni mchawi na ana uwezo mkubwa wa kichawi lakini ni maskini wa kutupwa
Guys huu uchawi wa hivi ni wa nini 🙌

NB: anae amini aamini ila mimi hapana kila nikijaribu kufikiria nashindwa kabisa
Kukubali hii dhana (Uchawi)
Hakuna uchawi bali ujinga juu ya jambo flan ambalo mwamini uchawi analiita uchawi na kwakuwa halijuwi jambo hilo, na kulieleza atakieleza in a distorted way.
NO WITCHCRAFT BUT KNOWLEDGE GAP.
 
Nimesoma hii comment yako kuna baadhi ya sehemu nimeshindwa kukuelewa mkuu

Hii ya kuhusu uchawi kwamba hata kwa wazungu upo inaweza kua kweli kwani wazungu wao si ni wanadamu kama sisi ?

Si hata hivyo vitabu vya dini vimeanzia huko huko kwao
Lakini ni ukweli usiofichika wao hiyo dhana ya uchawi wameiacha ama kuipuuza na pengine ni baada ya kugundua haina faida yoyote

Ndiyo maana wao wameamua ku focus kwa mambo yana yo onekana kwa macho wote tunaona jinsi sayansi inavyoifanya dunia iwe bora kila kukicha japo changamoto hazikosi

Sasa uchawi wenyewe una nini ?
Kwanza unakuta mtu anaeulezea mwenyewe hawezi kuuthibisha
Zaidi atakuambia amini tu

Mimi nashangazwa na watu wanaokumbatia hii dhana ya kale isiyo na tija kwa mtu binafsi au kwa jamii dhana isiyoweza kuleta matokea chanya kwenye jamii

Unakuta mtu anasema ni mchawi na ana uwezo mkubwa wa kichawi lakini ni maskini wa kutupwa
Guys huu uchawi wa hivi ni wa nini 🙌

NB: anae amini aamini ila mimi hapana kila nikijaribu kufikiria nashindwa kabisa
Kukubali hii dhana (Uchawi)
Dada, lugha ikiwa na neno 'uchawi' basi kuna wachawi. Ughaibuni, kwa mfano lugha ya waingereza, wana neno 'witchcraft' ambalo linamaanisha uchawi... kwa hiyo basi wachawi wapo. Pia kuna historia mbalimbali zimeandikwa kuhusu mambo ya uchawi. Marekani ilipokuwa mpya ya wazungu wahamiaji, kulikuwa na BOSTON WITCH HUNT, japo ilizushwa na shutma na hujuma. Pia historia ya kanisa la katoliki ina maandishi mengi tu ambayo walishutumu wanasayansi kuwa wachawi... hawa hawa kina Galileo kina Archimedes... Inaonyesha enzi za zama chochote kile kisichoeleweka kiliitwa uchawi, nasi Afrika / Bongo hatuko tofauti. Maybe, it is human nature....

Ila nilisema kuna uchawi ughaibuni umegubikwa na jina la kifahari ama mengineyo... nilitoa mfano FREEMASONS, kama mganga chatu kule kigamboni kadai kuku rangi flani kumtoa kafara, na freemasons tunaambiwa wanatoa kafara... basi si wote ni wachawi tu? Ama

Ningependa kukuambia dada angu, wazungu si waloandika vitabu vya dini. Tena ni jamii ya mwisho kuingia dini, walikuwa wapagani maridadi, na walipoingia dini walileta upagani wao na sikukuu zao. Tafiti hili, manake tunasherehekea nao eti sikukuu za dini zisizo ila za miungu yao.

Niliandika hili swala la wachawi kuwa maskini... sielewi. Labda ni masharti yao.
 
Wazungu kutambua neno uchawi sio uthibitisho kua uchawi upo kweli

Ndio maana nikasema sijui uchawi
ila naelewa neno uchawi kama dhana tu ni kitu kinachohisiwa lakini uhalisia wake baado haujathibishwa

So kusema wazungu wanatambua neno uchawi haina maana kweli uchawi upo

Ningependa kujua ni kina nani walioandika vitabu vya dini
Maana Muslim ni Waarabu
Inamana wao ndiyo waliandika

Bibilia nayo kwa kiasi kikubwa inaonekana iliandikwa mashariki ya kati

Hao sio wazungu ndiyo lakini huku tumezoea mtu yoyote kuita mzungu bila kujali anatokea bara gani
 
Mara nyingi kinachoonekana kama uchawi kinaweza kuelezwa na saikolojia kama placebo, hofu, imani, suggestion na coincidence.

Lakini si sahihi kusema kila tukio linaloitwa uchawi ni saikolojia bila kuchunguza ushahidi wa tukio husika.
 
Wewe unaweza kuweka ushahidi kua uchawi unafanya kazi kwa namna gani
Ili tuache kuchanganya na saikolojia?
 
Hatuwezi kuchukua tukio fulani, tukaliita uchawi, halafu moja kwa moja tukasema ni saikolojia bila kulichunguza.

Mfano: mtu anaumwa baada ya kudai amerogwa. Kuna uwezekano akawa:

1. Ana ugonjwa wa kawaida.

2. Hofu na imani vimemsababishia dalili (nocebo).

3. Kuna sababu nyingine ambayo bado haijagunduliwa.

Kwa hiyo, “kuchunguza ushahidi” nilimaanisha kuangalia tukio lenyewe na kutafuta chanzo chake kabla ya kulipa jina.

Hii haimaanishi kwamba ninajua au nina ushahidi kwamba uchawi unafanya kazi. Sina ushahidi huo. Nilikuwa nasema tu tusihitimishe chanzo cha tukio kabla ya kulichunguza.
 
Mimi huo uchawi siamini kama upo naamini ni dhana tu

Vp wewe una amini uchawi upo
 
Back
Top Bottom