ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,571
- 41,678
- Thread starter
- #381
Hilo linawezekanaNADHANI UNA UVIVU WA KUFUKIRIA MTOTO WEWE
Ila sijakuzidi wewe
Hilo linawezekanaNADHANI UNA UVIVU WA KUFUKIRIA MTOTO WEWE
Hahaha hii si sawa kabisa 😂😂😂Kaka hapa nakuona ulivyokua una vimba wakati unapokea maua kutoka kwa cuzo
Shaka ondoa 😃Kaka wewe pia ni msukuma 😅sikujua kuhusu hili please nipe mwaliko nije mwanza nile samaki fresh wa ziwani
Kwanini utamani ? Na hilo tukio ni la kweli ?Hilo tukio lako ni story fulani ya kusisimua 😢
Natamani nikuamini 🤔
Huyu jamaa ndio Dr William wa kule Facebook mropokaji?Hilo linawezekana
Ila sijakuzidi wewe
Weee ulikua waonekana kicwaHahaha hii si sawa kabisa 😂😂😂
Kuna sehemu vijana nilikuwa nawahoji mpaka nikawa naitwa Zitto Kabwe kipindi hicho yuko CHADEMA
Nataka nijionee sio kuambiwa😅Shaka ondoa 😃
Kwanini utamani ? Na hilo tukio ni la kweli ?
Kwamba...
Noma sanaaisee
Sina uhakika broHuyu jamaa ndio Dr William wa kule Facebook mropokaji?
ShesRise_1 msome na Uncle Pascal Mayalla hapa
Wanabodi
Japo uchawi upo na wachawi wapo na wanaloga!, anayeruhusu hicho kilogo kikufikie, au uchawi ukufikie, na kulogeka ni wewe mwenyewe bila kujijua, wewe unao uwezo wa kuzuia kulogeka bila kwenda kwa mganga yeyote au bila kutumia zindiko lolote bali ni kwa kujitambua tuu kwa kutumia Imani! na ukawa hata ulogwe na mchawi gani au uchawi gani, unakuwa hulogeki!. Hata ukitupiwa uchawi, unadunda na kurudi kule ulikotoka au kumrudia yule aliyekuloga na unamtandika yeye aliyekuloga!.
View: https://youtu.be/ZnvyUD1WlI0?si=SwyhaQapWdmV6DVq
Paskali
Update
Mchango very objective
Kwamba...
- Pascal Mayalla
![]()
- imani kuzuia uchawi uchawi upo ukawa wachawi wapo wewe
- Replies: 37
- Forum: Jamii Intelligence
Ujuaji tu wa Kisukuma 😂😂😂Weee ulikua waonekana kicwa
Nilishakwambia Matukio yapo lakini ushahidi ndio huwa unabakia kwenye dhana tuNataka nijionee sio kuambiwa😅
Mambo yapo kwenye DNA 😅Ujuaji tu wa Kisukuma 😂😂😂
Huwa unamuona Joseph Kasheku (Msukuma) kule bungeni ?
Luhaga Mpina pia
Au Braza PCM Waziri wa Michezo
Yes uchawi ni dhanaNilishakwambia Matukio yapo lakini ushahidi ndio huwa unabakia kwenye dhana tu
😂😂😂Mambo yapo kwenye DNA 😅
HakikaYes uchawi ni dhana
Kuna dada mmoja ni msukuma aliniambia kijijini kwao ukiongea kiswahili ukiwa ni binti unaambiwa umeanza umalaya😅😅😂😂😂
Ukiwa kijijini ndichi kabisa ukiongea kisukuma unaonekana unawadharau na wao huwa wanatakakuongea kiswahili eti
Hakika
Bhanaa nitarudi na kisa kingine baadaye tuache wasukuma na misifa yetuKuna dada mmoja ni msukuma aliniambia kijijini kwao ukiongea kiswahili ukiwa ni binti unaambiwa umeanza umalaya😅😅
Kaka acheni hizo bana🤣
Karibu ku share kaka 😊Bhanaa nitarudi na kisa kingine baadaye tuache wasukuma na misifa yetu
Imechukua muda kwa sababu nilikuwa naipangilia vyemaKaribu ku share kaka 😊
Safii nasoma sasa asanteImechukua muda kwa sababu nilikuwa naipangilia vyema
Kaka Manyanza kwanza asante kwa kutenga muda wako kuandika na kisha kushare hapa Shukrani sana broKuna mwaka fulani, nilipata ajali mbaya sana ambayo ilinifanya nipoteze fahamu kwa takribani siku kumi kutokana na brain concussion. Baada ya hapo nilianza kipindi cha recovery, na kwa bahati nzuri hali yangu iliendelea kuimarika taratibu.
Siku moja, nikiwa natembea kwa miguu, nilikutana na dada mmoja ambaye sikuwahi kumfahamu wala kuonana naye kabla. Aliniita:
“Kaka, mambo?”
Nikajibu, “Poa.”
Kisha akaniambia:
“Kaka yangu, sikujui wala hatufahamiani, lakini lete mkono wako.”
Nilimpa mkono wangu. Akaanza kuangalia kiganja changu kwa muda, kisha akaniambia mambo ambayo kwa wakati huo yalinishtua sana.
Aliniambia kuwa nilikuwa nimepata ajali mbaya ya gari, kwamba nilikuwa nimeumia upande wa kushoto wa kichwa, na kwamba kulikuwa na tatizo kwenye mkono wangu wa kushoto kiasi kwamba haukuwa ukifanya kazi vizuri.
Nilishangaa sana kwa sababu hayo yalikuwa mambo ambayo kweli yalikuwa yametokea kwangu.
Nikamwambia:
“Ndiyo dada yangu, ni kweli.”
Kwa sababu tayari nilikuwa nimetoka kwenye ajali na nilikuwa bado kwenye kipindi cha recovery, maneno yake yalinifanya niingiwe na hofu.
Akanieleza kwamba kesho yake asubuhi niende nyumbani kwake nikiwa na tende, haluwa, asali, sukari ya mawe, ndizi mbivu mbili na mkate. Pia akaniambia niende na sarafu za mia mbili ili niwape watoto wataokuwepo.
Alisema anataka kunifanyia kisomo.
Kesho yake nilienda na vitu hivyo mpaka nyumbani kwake. Kisomo kikaanza. Kulikuwa na watoto waliokuwa wakisaidia, wengine wakipiga dufu. Vile vyakula viliandaliwa pamoja kwenye sahani, nami nikaambiwa nile.
Wakati kisomo kikiendelea, ghafla nilianza kutapika.
Nilitapika vitu vilivyofanana na viini vya mayai vilikuwa kama vinne na vilikuwa vikubwa. Koo lilianza kuuma sana. Baadaye nilitapika kitu kilichofanana na damu nyeusi.
Nilipoteza nguvu kabisa. Mwili ulikuwa hauna nguvu, nilikuwa na maumivu makali na nikaanza kulia kwa sababu ya maumivu.
Yule dada akanishika mabegani na kunitoa nje huku mwili wangu ukiwa umelegea.
Aliendelea kunisomea huku mimi nikiendelea kuhisi maumivu makali na mwili wangu ukawa kama unabanwa.
Baadaye akachukua wallet yangu, akatoa hela na kwenda sokoni kununua jogoo mwekundu. Alimchinja hapo hapo, ingawa wakati huo hali yangu ilikuwa mbaya kiasi kwamba sikuweza kufuatilia vizuri kila kilichokuwa kinaendelea.
Baada ya muda, hali yangu ilianza kurudi taratibu kwenye hali ya kawaida.
Baadaye yule dada akanieleza tafsiri yake ya kile kilichotokea.
Aliniambia kwamba nilikuwa nimetupiwa vitu vibaya vya kijini na kwamba kulikuwa na mambo ya kichawi yaliyokuwa yamefanywa dhidi yangu. Sababu aliyotoa ilikuwa kwamba kuna watu ambao hawakupenda maisha yangu na namna nilivyoishi na watu.
Hicho ndicho kisa nilichowahi kukipitia miaka kadhaa iliyopita.
Lakini ninapokifikiria leo, huwa najiuliza swali moja muhimu:
Je, kile nilichokipitia ni ushahidi wa uchawi, au ni tukio lililotokea ambalo baadaye lilipewa tafsiri ya kichawi?
Kwa upande wangu, narudi na hoja kuwa kuna tofauti kubwa kati ya tukio na tafsiri ya tukio.
Tukio lenyewe ni jambo nililoliona na kulipitia: nilikuwa na historia ya ajali, nilipata hali mbaya ya mwili wakati wa hicho kisomo, nilitapika, nilihisi maumivu makali, nikadhoofika na baadaye nikapata nafuu.
Lakini kusema kwamba chanzo cha tukio hilo kilikuwa ni “uchawi”, “jini” au mtu fulani kunitupia kitu kibaya ni tafsiri ya tukio.🤔
Na hapo ndipo ninapoona mjadala wa uchawi unakuwa mgumu.
Kwa sababu mtu anaweza kusema:
“Niliona hiki, kwa hiyo uchawi upo.”
Lakini kuona tukio na kulipa jina fulani si sawa na kuthibitisha chanzo chake
Inawezekana mtu akawa amepitia tukio la kweli kabisa, lakini maelezo aliyopata kuhusu chanzo cha tukio hilo yakawa hayana ushahidi wa kutosha.