Kisa cha kwanza
Mwaka 2006 nikiwa nipo below 20 nilienda sehemu fulani kwa ndugu yangu aliyekuwa ameolewa. Nikakuta kuna hali ya unafiki na uonevu nikashindwa kuvumilia nikawa namchana makavu yule Ba mjengo mpaka akawa anajifanya anasema nitamuuwa kwa presha akawa anasusa mpaka kula 😅
Na ana watoto wakubwa tu mwanae wa kwanza kanizidi kama miaka 12 hivi halafu ni mwanamke na akawa ananikubali sana yaani cuzo unachofanya nasikia burudani sana maana huyu mzee ni mchwawi tu 😂😂😂
Basi ulivyofika muda wa kwenda shule nikaondoka pale nikaenda mkoa mwingine kuendelea na shule, sasa nikiwa huo mkoa kuna siku nikaota ndoto yule Ba mjengo anaenda baiskeli tena phoenix chakavu kanipitia miguuni kanigonga aisee nilitoa ukulele ile siku mpaka nikaamka.
Nilipoamka nikaona miguu imeanza kuvimba na iliendelea kuvimba sana mpaka nikawa siwezi kuvaa viatu, nikawa navaa yale mayeboyebo ya kipindi 😅 (sijui kama mnayukumbuka maana sasa hivi kuna Crocs )
Hali ya miguu ilikuwa mbaya mpaka nikasafiri kurudi jijini Dar es Salaam, nikaenda Hospital nikaambiwa inatakiwa nifanyiwe operation 😥 nililia sana na sikuwa na uwezo wa kuhoji lakini nilikuwa nalia mpaka ikashindikana. Sasa basi kuna Uncle wangu ni Mganga ( Mganga kweli 😂 maana kuna Waarabu walikuwa wanatoka Oman, Bahrain na nchi za Gulf walikuwa wanamfuata na Mimi nilikuwa naitwa kwenda kuwa mtafsiri 😂😂😂 kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili mpaka Kisukuma.
Nikamwambia sitaki kuchanwa miguu mimi naomba unisaidie , basi kikachinjwa kifaranga cha kuku nikakitemea mate mdomoni hatimaye mwili wangu wote ukawa ndani ya kile Kifaranga ndio akaanza kuangalia kuna nini ndani ya mwili ? Ikaonekana Figo zangu zilikuwa chafu na ndio maana miguu ilikuwa inavimba na huo uchafu ni uchawi niliolishwa.
Basi akanipa dawa ya kunywa kwenye uji siku tatu tu nikawa naona mabadiliko ndani ya siku 7 nikapona kabisa miguu.
ShesRise_1 kama nilivyo sema hapo awali Uchawi ni dhana ambayo Tukio linaonekana, Tafsiri ipo lakini Ushahidi hakuna. Kwa kisa hiki wadau mnasemaje ?