JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Nyimbo ni nyingiiii ila kwa leo tuishie na huu wimbo wa paul Clement: Mwaminifu

Huu wimbo alinidedcate rafiki angu wa kipindi hichoo anaitwa Eva niliupenda toka siku ya kwanza nausikiliza mpaka kesho nitaendelea kuupenda,, na mimi leo nausimulia hapa labda utafanyika baraka kwa watu wengine pia 🙏👇
 
🎶🎶 Unawasi wasi hofu na mashaka unahisi moyoni kama Mungu kakuacha maana unaona hausogei wala hauendelei uko pale pale kila siku uko vile vile,,,, Mungu alianzisha safari na ataimaliza ahadi zote alizo sema atazitimiza maana alikujua kabla haujazaliwa kabla haujajijua

Na Mungu hawezi kukuacha njiani, safari yako aliianzisha mwenyewe asingetaka angekuacha mwanzoni unapo kwenda yeye anajua...
 
Nakumbuka mwaka 2020 nikiwa kwenye basi narudi nyumbani Dar kutokea Morogoro; kupitia spika za basi nilikuwa nasikia wimbo uliokuwa na maneno haya kwa uchache:
"Akisema atakubariki,
Hakuna atakayezuia,
Kwani yeye ndiye Mungu,
Mwenye baraka zote."

Muimbaji ni yule aliyeimba pia
"Naliaaa 'pole'
Naliaaa 'pole sana!'"

Haikuwa mara ya kwanza nasikia huo wimbo ila hiyo siku ulinibariki na kunifariji mno. Nilikuwa nimepoteza matumaini na mipango yangu ilikuwa imefeli pakubwa.. lakini baada ya kuusikiliza ule wimbo nilijikuta napata nguvu mpya ya kuendelea kupambana.
 
muimbaji anaitwa Jenifar mgendi
 
Back
Top Bottom