JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

huu wa Roland Robert,,, Faragha

🎶🎶🎶 Nimekuja faragha mahali la siri niseme nawe mambo ya moyo niseme nawe kwa siri si hadharani maana wanadamu watanisema,,,
Niseme nawe yanayo niudhi niseme nawe yanayo nisumbua niseme nawe yanayo nikatisha tamaa, niseme nawe yanayo utesa moyo wangu na yanayo niumiza niseme nawe yanayo nikatisha tamaa niseme nawe yanayo nitesa🎵🎵🎼....
 
huu wa Roland Robert,,, Faragha

🎶🎶🎶 Nimekuja faragha mahali la siri niseme nawe mambo ya moyo niseme nawe kwa siri si hadharani maana wanadamu watanisema,,,
Niseme nawe yanayo niudhi niseme nawe yanayo nisumbua niseme nawe yanayo nikatisha tamaa, niseme nawe yanayo utesa moyo wangu na yanayo niumiza niseme nawe yanayo nikatisha tamaa niseme nawe yanayo nitesa🎵🎵🎼....
Sizijui hizi nyimbo..
Ngoja nizitafute 🙏🏽
 
Israel Mbonyi: Kaa nami
🎵🎵 Ikiwa nimepata neema kwako unikumbukee jicho lako liwe juu yangu nyakati zote wema wako unisindikize Hadi tamatii hili ni ombi langu nakumwagia moyo nachoomba kaa nami ikiwa nimepata neema kwako.....

0107
 
Magret James: Unaweza
🎶🎶 Unaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya niombavyo,,,,, Zaidi ya nitakavyo unaweza kufanya unaweza Yesu zaidi ya tarajio unaweza kufanya unaweza yesu
 
Japhet zabron & Joel luaga: Sauti ya mwisho
🎶🎼🎼, Adui aweza kuwa na maneno ya kwanza ila neno la mwisho ni lako maumivu yaweza kuwa ni mazito kupitiliza ila neno lako ni zaid ya sindano.. Nitasubiri usiku huu nitasubiri kutapo kucha nitasubiri kwa imani nitasubiri kwa maombi ni neno lako moja nasubiri ukisema yatosha yatosha mwanangu
Bwana nasubiri nasubiri mimi nangoja nangoja sauti yako ya mwisho ikisema yatosha yaishe mwanangu....

0120ukisema hakuna wa kupinga
 
Martha Mwaipaja: Unasema nini
🎵🎵 Umbali huu umenileta mwenyew ili niendelee nakusikia, dunia ni ngumu kuishinda niishinde vipi nambie niendeleeje mwenyewe siwezi nakusikia mambo ni mengi vitu ni vingi sema niishi vipi nakusikia,

0130,, majibishano mimi yamenishinda nambie baba nakusikia, mapambano ya dunia yamenishinda mwenyewe nambie baba nakusikia,, mambo mengine siyawezi mimi.....
 
huu wimbo ulihit sana miaka mi5 au 4 iliyopita ila kwangu mpka leo bado haujachuja,, weekend ilikua karibu hostel na korido zote za kike walikua wanaplay huu wimbo😄😄😄🙌 na kipindi cha mitihani 🤣🤣

Patrick Kubuya: Moyo wangu
🎶🎶Moyo wangu usilie tena moyo wangu usibabaike unae Mungu mkuu sana unae Mungu muweza wa yote,, aliingia rohoni mwangu kanipa kutulia kanambia ewe mwanangu usilie lie tena ninajua shida zako mimi nitazitatua bila Yesu mimi ni mtu bure...
 
Rehema simfukwe huyu dada ana nyimbo nyingi mnoooo na nzuri hazichoshi kusikiliza
Mungu aendelee kumtunza maana ananibariki mno🤗
 
🎶🎶 Haya ni maombi yangu kwako wote ninao wapenda wasipitwe na neema yako,, basi ikiwa ipo ahadi ya kuingia rahani mwako sitaki kukosa na niwapendao🙏 mimi marafiki zangu na familia yangu tusipitwe na neema yako
 
Huyu baba Ambwene mwasonge ni kama ana sauti ya uponyaji kwenye nyimbo zake,, Nyimbo zote ni nzuri na nina zipenda mnooo ila huu "Nimeachilia" nina upenda mara miamoja

siku ukiwa na machungu hautamani kuzungumza wala kumshirikisha mtu unayo yapitia kaa mahali then sikiliza huu wimbo kwa utulivu utapata relief ya moyo na akili
 
🎶🎶 Sio kila kinachokuja kwako ni chako na sio kila kiondokacho kwako ni chako hata kama unavipenda sio vyako", vingine Mungu huviondoa ili wew ubaki salama iwe kazi nafasi mahusiano au cheo, japo vyaondoka kwa maumivu ila jifunze kuviacha viende na nafasi ya moyo wako mpe Mungu

Jifunze kuviacha viende jifunze kusema bai bai maana sio vyote vyakwako,, walitoka kwetu hawakua wa kwetu maana wangekua wetu wangelikaa nasi walifunuliwa ili tujue sio wote wa kwetu🎶🎶
 
Back
Top Bottom