JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Quotes of the day​


Here are some positive quotes to brighten your day 🌞✨

1. “Keep your face always toward the sunshine—and shadows will fall behind you.” — Walt Whitman


2. “Believe you can and you're halfway there.” — Theodore Roosevelt


3. “Start where you are. Use what you have. Do what you can.” — Arthur Ashe


4. “Happiness is not by chance, but by choice.” — Jim Rohn


5. “The only way to do great work is to love what you do.” — Steve Jobs


6. “Every day may not be good, but there’s something good in every day.” — Alice Morse Earle


7. “You are never too old to set another goal or to dream a new dream.” — C.S. Lewis


8. “Your attitude determines your direction.” — Unknown


9. “Don’t let what you cannot do interfere with what you can do.” — John Wooden


10. “Be the reason someone smiles today.” — Roy T. Bennett
 

Mastory ya bey​

Poleni kwa pilika pilika za kutwa nzima ya leo,kumekuchwa huku tulio angaziwa jua mchana tunaelekea kulala na walio funikwa na usiku wanaelekea kuamka ndio nidhamu ya ulimwengu hiyo.

Tumeshawahi kusikia neno wasi wasi wa mapenzi au huenda sisi wenyewe ndio ambao wahusika ambao ni wahanga wakubwa wa jambo hili

Kwanza ebu tujue kwanini huwa tuna wasi wasi wa mapenzi,kwa mtazamo wangu kuna mambo mawili

Mosi huenda watu ambao tunao sio hadhi yetu hivyo tunajua muda wowote watatukimbia au watakuwa na wapenzi wengine au hatuwapi kile wanachostahili hivyo tunahofia wakikutana na watakao wapa wanachostahili ndio tutawakosa mazima

Sasa solution ili kuondokana na wasi wasi wa mapenzi ni kuwa na mtu wa size yako,kihadhi,kimuonekano,kiuchumi na kadhalika,huyo mtaenda sawa

Pili, ukiwa na mweza hakikisha hajisikii mpweke,upweke sio mtu kuwa single bali upweke hasa ni mtu kuwa na mume au mke kisha akawa mpweke,hakuna mapenzi,hakuna furaha,hakuna mazunguzo na vicheko na kadhalika

Ukijitathimini na kujikagua vizuri utafanya maamuzi ambayo yatakuwezesha kuepukana na mawazo na fikra za wasi wasi wa mapenzi

Jambo lingine huenda umeyafanya yote hayo lakini mchawi jinsi unavvyowaza na kufikiria,yani umejiweka kuwaza katika mtizamo hasi tu muda wote,huenda kutokana na unayoyasikia vijiweni au kuwa na watu ambao siku zote mitazamo yao ni kuwaza negative tu

Kupitia Mastory ya Bey tunajifunza kuwaza na kufikiria tofauti

Anza sasa kuwaza na kufikiria tofauti

Bey
 

Mastory ya bey​

Mambo zenu,hope mpo gud wasomaji wangu nami nipo vizuri kwa uzito wa tano

Mastory yangu ya leo tutaangalia ni sababu zipi ambazo zinafanya kuwe na umuhimu wa kusahau machungu yaliyo pita

Mosi, hutupa amani ya ndani kwasababu machungu yaliyopita hutupa huzuni,hasira na hata kujikuta tunachukia maisha kwa ujumla wake,kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana tusahau au tupambane kuachana na machugu ya zamani

Pili, hutuwezesha kuishi kwa furaha ,unajua kumbukumbu mbaya za matukio ya zamani hutufanya tushindwe kuishi maisha yetu to the fullest,yani ingawa ni matukio ya zamani lkn huyafanya maisha yetu yasiwe na mvuto wala thamani,hutufanya tuwe wanyonge muda wote,lakini pale tutakapo azimia kusonga mbele na kusahau yalipita na kuyasamehe tunapata furaha

Hunufaisha afya ya akili na mwili pili,kumbukumbu mbaya za zamani hutupa msongo wa mawazo na hii hupelekea hata afya zetu kudhoofu,kwahiyo tunapo amua kupambana na kuachana na machungu ya zamani tunaimarisha afya zetu na kiwiliwili pia

Ni ishara ya kukua kiroho na kiakili pia,mtu anajua kwamba majaribu ni sehemu ya maisha,na maisha siku zote hayakupi unachotaka kwahiyo unakubaliana na fate au majaliwa yako. Vile unajifunza kwamba kwa jaribu ambalo unakutana nalo ni somo na elimu tosha inakuwezesha kufika mahala fulani katika maisha

Kwa kumalizia wasomaji wangu kila mtu hupitia changamoto mbali mbali katika maisha,tunachotofautiana ni namna gani tunazikabili na kuenda nazo sawa ili zisitunyime fursa ya kusonga mbele na kufurahia maisha yetu,kingine msomaji wangu ebu tujiulize kuna faida gani ya kuruhusu kuumizwa na mambo ambayo hatuwezi kuyabadilisha kwa maana yalishatokea tayari?

Anza kuwaza na kufikiria tofauti

Bey
 

Ujumbe wa Leo​

🌞 Ujumbe wa leo — 16 Oktoba 2025 🌿

“Usiruhusu machungu ya jana yakukoseshe amani ya leo. Kila siku ni fursa mpya ya kuandika ukurasa bora katika maisha yako.” ✨



Kumbuka:
Maisha ni safari yenye milima na mabonde, lakini nguvu yako iko katika uwezo wa kuamka tena kila unapojikwaa. Acha yaliyopita yapite, elekea mbele kwa matumaini mapya na moyo wa shukrani. 💪🌺
 
Back
Top Bottom