JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mastory ya bey​


Natumaini mmekuwa na siku nzur leo na hata kama kulitokea changamoto za hapa na pale,kikubwa upo hai ni neema kubwa sana hiyo

Hatupo kwenye dunia ya peke yetu kwamba utasikia kauli nzuri siku zote,utasikia maneno mazuri siku zote,laa! Kuna nyakati ambazo tunakutana na vichaa ambao sio lazima waokote Makopo ila kwa head hakuko sawa,hata hapa jf wapo wengi tu

My point is,maneno siku zote huwa hayaumi,matusi siku zote huwa hayaumi ila kinachouma ni tafsiri ambayo unaipa maneno hayo.

Ni kwa namna gani unayapa uzito hayo matusi na maneno mabaya ndio kadri unavyoathirika nayo,lakini ukijifunza kutoyapa uzito na ukayapuuza trust me hayakudhuru it's just like ur listening ur favorite music

Najua ninachozungumza nimejifunza hilo na now huwezi kunikera kwa maneno ya hovyo au matusi,kwakuwa siyapi kipaumbele wala siyawazi kabisa,nahisi kama unaniambia kauli ambayo haina nafasi kwangu na hivyo haihitaji kupewa uzito wowote ule

Kifupi nimemaster jinsi ya kufikiri na kuwaza majambo,nachagua kipi cha kukipa kipaumbele na kipi cha kukidharau, you too can learn na kuwa na peace of mind

Kumbuka hakuna yoyote atakaye humiza hisia zako unless uruhusu hilo litokee

Jifunze kuwaza tofauti
 

Quotes of the day​


Nukuu za Leo

1. “Mafanikio siyo mwisho, kushindwa siyo mwisho wa dunia; ni ujasiri wa kuendelea ndiyo unaohesabika.” – Winston Churchill 💪


2. “Njia pekee ya kufanya kazi kubwa ni kupenda unachokifanya.” – Steve Jobs ❤️


3. “Amini kwamba unaweza, na tayari umeshafika nusu ya njia.” – Theodore Roosevelt 🌈


4. “Usiangalie saa; fanya kama inavyofanya — endelea kusonga mbele.” – Sam Levenson ⏰


5. “Furaha si kitu cha kupokezwa, inatokana na matendo yako mwenyewe.” – Dalai Lama 🌺
 

Positive affirmations​


🌸 Positive Affirmations za Leo 🌸

1. Ninaamini uwezo wangu wa kufanikiwa katika kila ninachofanya. 💪


2. Kila siku inaleta fursa mpya ya kujifunza na kukua. 🌞


3. Mimi ni chanzo cha amani, upendo, na nguvu njema. 🕊️


4. Ninastahili mafanikio, furaha, na utulivu wa moyo. 🌺


5. Niko kwenye safari nzuri ya mafanikio na utimilifu. 🌈
 

Leo katika historia​


📅 Siku ya Leo Katika Historia — 13 Oktoba

Mnamo 13 Oktoba 1775, Baraza la Mabunge la Marekani lilipitisha azimio la kuanzisha Jeshi la Baharini (Continental Navy), ambalo baadaye likawa msingi wa Jeshi la Majini la Marekani.

Mnamo 13 Oktoba 1792, jiwe la msingi (cornerstone) la Ikulu ya Marekani (White House) liliwekwa na Rais George Washington.

Mnamo 13 Oktoba 2010, wahandisi walifanikisha kuwatoa watu 33 waliobebwa chini ya ardhi kwa siku 69 katika mgodi uliopita, tukio lililovutia dunia nzima.

Kwa kweli, siku ya leo nayo zimeonesha matukio ya kusisimua kama ajali ya ndege ya Uruguayan mnamo 1972 huko Andes ambapo watu wachache waliishi baada ya changamoto kubwa sana.
 

Mastory ya bey​


Ni majira ya usiku hope mpo gud kama kawa kama dawa,karibuni kijiweni ambapo mastory ndio mahala pake

Leo ningependa tuzungumzie ishu nzima ya kuwa na Dhana juu ya jambo fulani au mtu fulani,haya ni maradhi ya namna jinsi tunavyowaza na kufikiri

Tumejikuta tu automatic huwa dhana zetu huwa negative zaidi kuliko kuwa positive,ni mara chache sana itokee umdhanie mtu Dhana njema,ila mara nyingi huwa tunaangukia katika mtazamo hasi zaidi

Hii inatokana na makuzi yetu na namna tulivyoona wengine jinsi wanavyodhani nasi bila kujua tunaangukia upande ule ule

Mfano anaweza onekana mtu amevaa vizur tu wala hana baya na mtu,lakini watu utawasikia wanasema "anajifanya ana hela sana siku hizi au anajionyesha tu tumuone siku hizi yupo vizur"

Au mtu anaamua ajiongelee zake broken English basi waja hawakawii kuwa na dhana mbaya hawakawii kusema "huyu nae anajifanya kasoma au anataka tujue kuwa kaenda shule"

Hii na mifano mingine mingi ni udhibitisho tosha kwamba hakika watu wengi tumejikuta tumejaa dhana mbaya juu ya watu wengine

Sasa msomaji wangu wa Mastory ya Bey,tupo hapa kujifunza kuwaza na kufikiri tofauti,tuvunje minyonyoro na makufuli yote ambayo yamefunga fikra zetu na maono yetu juu ya kuwa na dhana mbaya

Ni wakati sasa wa kuanza kuwaza na kufikiria tofauti, tuwachukulie watu kama walivyo, tuache kuwa na dhana juu ya watu just tuwaangalie na kuwaacha kama walivyo, kwa vyovyote watakavyo fanya au kubehave is nothing to do with us at all,let's give them a break

Na tupende sana kuwadhania watu dhana nzuri,katika Uislamu inasemwa katika maandiko hakika baadhi ya dhana ni dhambi,wakati mwingine tunajichumia madhambi kwa kuwadhania watu vibaya

Next time if you feel like you wanna judge people just chill and tell urself isn't worth it

Jifunze kuwaza na kufikiria tofauti
 

Leo katika historia​


Hapa ni baadhi ya matukio ya kihistoria yaliyotokea tarehe 14 Oktoba:


---

🇹🇿 Katika Tanzania

14 Oktoba 1999 — Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa wa Tanzania, alifariki dunia kutokana na leukemia huko London, Uingereza.

Siku hii pia huchukuliwa nchini Tanzania kama Siku ya Mwalimu Nyerere, ambapo wananchi hukumbuka na kuheshimu urithi wake wa viongozi, elimu, na ujenzi wa taifa.



---

🌍 Kimataifa / Ulimwenguni

1066 — Vita vya Hastings: Walowezi wa Norman wakiongozwa na William the Conqueror waliwashinda Waingereza na kuanza udhibiti wa England.

1947 — Chuck Yeager alikuwa mwanadamu wa kwanza kuruka kwa kasi kubwa kuliko sauti (breaking the sound barrier) akiwa na ndege ya Bell X-1 juu ya Muroc Dry Lake, Marekani.

1964 — Martin Luther King Jr. alipata Tuzo ya Amani ya Nobel kwa juhudi zake za kuhimiza haki sawa na kusimamiza ubaguzi wa rangi.

1964 — Billy Mills, mwanafunzi wa Marekani, alishinda dhahabu katika mbio za 10,000m katika Michezo ya Olimpiki huko Tokyo — ushindi mkubwa kutokana na matabaka ya ushindani.
 

Ujumbe wa Leo​

🌞 Ujumbe wa Leo 🌞

Maisha ni safari yenye milima na mabonde. Usikate tamaa unapokutana na changamoto, maana mara nyingi ndizo zinazoandaa njia ya mafanikio. Kumbuka — hata giza nene zaidi halidumu milele; alfajiri huja tu baada ya usiku mrefu. ✨
 
Back
Top Bottom