Mastory ya Bey
Je ni sahihi kuendelea kuwa na namba ya ex wako?
Jibu linaweza kuwa ndio au hapana itategemeana na mahitaji ambayo yanaweza kuwepo baada ya mahusiano kufa
Ila jibu la kwanza si sawa kuendelea kuwa na namba ya ex wako,kwanza unakuwa nayo ili iweje? Unatarajia nini toka kwa ex wako?
Je haupo tayar kumove on na mahusiano mapya? Au bado upo njia panda huku unataka na huku unataka
Sikia msomaji wangu,lililo la busara ni kumove on,futa namba ya simu,na liepuke lolote ambalo bado linaweza kuwa kikwazo kwako cha kusonga mbele,kumbu kumbu yoyote ambayo itakuwa sababu ya kukufanya ushindwe kumove basi malizana nayo mara moja ili uwe free kusonga mbele
Heshimu hisia zako na songa mbele,kwani mlivyoamua kuachana si mlikuwa na akili timamu bila kushurutishwa na yeyote yule mpaka mkayafikia hayo maamuzi? Sasa kinachokufanya ushindwe kumove on nini?
Fanya maamuzi ya busara na songa mbele kamwe usiangalie nyuma
Upande wa pili kwa nini uwe na namba ya ex wako,hii itategemeana na mko matured kiasi gani,kwa maana ya kwamba now ni stickly business that's all na si vinginevyo,na mtatafutana kwa mambo nje ya mapenzi
Mfano nijizungumzie mie binafsi,nina ex wangu ambaye yupo kwenye fani ya huduma za kiafya,huyu huwa namtafuta pale ninapotaka huduma hiyo na kupata huduma ya VIP. na nje ya hapo hakuna la ziada,ni just business
Kwahiyo huenda ukawa na namba ya ex ambaye akawa msaada kwako kwa huduma fulani lkn hakikisha hakuna zaidi ya hapo,hakuna kuchekiana time to time,ni pale tu unapo hitaji msaada fulani basi
Hapo unaweza kuwa na namba ya ex wako,kama analeta leta shobo basi fasta malizana nae mapemaaaa.