JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Chachandu Special

Screenshot_20250915-225019_Google.jpg

Jina kamili: William Samoei arap Ruto

Tarehe ya kuzaliwa: 21 Desemba 1966

Mahali: Sambut, Kaunti ya Uasin Gishu, Kenya

Safari yake:

Alisomea Botany na Zoology katika Chuo Kikuu cha Nairobi na baadaye akapata PhD ya Ekolojia ya Mimea.

Aliingia siasa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kupitia KANU, akihusishwa na Youth for KANU '92.

Ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Waziri wa Kilimo na Waziri wa Elimu ya Juu.

Mnamo 2013–2022, alikuwa Naibu Rais wa Kenya chini ya Uhuru Kenyatta.

Mnamo Agosti 2022, alishinda uchaguzi na kuwa Rais wa 5 wa Kenya kupitia chama cha UDA chini ya muungano wa Kenya Kwanza.

Ruto anajulikana kwa falsafa yake ya “hustler nation”, akijitambulisha kama mtu aliyepanda kutoka maisha ya kawaida kijijini hadi kufikia Ikulu.
 
Mastory ya Bey

My people, mwanamke anaweza kukubali kuolewa na wewe lakini haimaanishi kwamba anakupenda

Anaweza kuamua kukuzalia mtoto lakini haimaanishi anakupenda

Anaweza kukwambia anakupenda sana lakini ikawa ni story tu au maneno ya mdomoni tu

Anaweza kukutambulisha kwa ndugu zake au akakumbatia au kukubusu hadharani usifikir ndio kwamba anakupenda

Mwanamke anayekupenda kwa dhati ni yule ambaye yupo pamoja na wewe katika kupambana kwako,yupo pale kukusapoti katika struggle zako,na kuhakikisha yupo pamoja na wewe mpaka mfikie malengo yenu pamoja

Ukimpata mwanamke wa namna hii basi usimuache akupotee mkamate kwa mikono miwili na ulimlinde asije akakuponyoka
 
LEO KATIKA HISTORIA
Haya ni matukio muhimu yaliyotokea duniani tarehe 15 Septemba katika historia (leo katika historia):

1835 – HMS Beagle ilifika Galápagos, ambapo Charles Darwin alianza kuchunguza viumbe waliomsaidia kuunda nadharia ya evolution.

1916 – Vita vya Kwanza vya Dunia: Jeshi la Uingereza lilitumia mashine ya kivita (tank) kwa mara ya kwanza vitani huko Somme, Ufaransa.

1935 – Sheria za Nuremberg zilipitishwa Ujerumani na Adolf Hitler, zikitoa misingi ya ubaguzi wa kisheria dhidi ya Wayahudi.

1963 – Jeshi la Malaysia lilianzishwa rasmi baada ya taifa hilo kuundwa.

2008 – Benki kubwa ya Marekani Lehman Brothers ilifilisika, tukio lililochochea mgogoro mkubwa wa kifedha duniani.

2022 – William Ruto aliapishwa rasmi kama Rais wa 5 wa Kenya mjini Nairobi.
 
Mastory ya Bey

My people, mwanamke anaweza kukubali kuolewa na wewe lakini haimaanishi kwamba anakupenda

Anaweza kuamua kukuzalia mtoto lakini haimaanishi anakupenda

Anaweza kukwambia anakupenda sana lakini ikawa ni story tu au maneno ya mdomoni tu

Anaweza kukutambulisha kwa ndugu zake au akakumbatia au kukubusu hadharani usifikir ndio kwamba anakupenda

Mwanamke anayekupenda kwa dhati ni yule ambaye yupo pamoja na wewe katika kupambana kwako,yupo pale kukusapoti katika struggle zako,na kuhakikisha yupo pamoja na wewe mpaka mfikie malengo yenu pamoja

Ukimpata mwanamke wa namna hii basi usimuache akupotee mkamate kwa mikono miwili na ulimlinde asije akakuponyoka
Kama ulishafikia malengo peke yako na unataka kuoa utaangalia nini?😊
 
Back
Top Bottom