JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mastory ya Bey

Part 1

Story: “Mzigo wa Zamani”

Fatma alikuwa msichana mchangamfu, mwenye ndoto ya kuwa mwalimu. Lakini siku moja, alipokosea kusahihisha mtihani akiwa msaidizi wa mwalimu, mwanafunzi mmoja alipata adhabu kwa kosa ambalo halikuwa lake. Fatma alipojua ukweli, aliogopa kusema. Muda ukapita, na akahisi lawama kubwa moyoni.

Miaka ilivyopita, alikosa kujiamini, alijilaumu, na kujihisi hastahili mafanikio. Kila alipopata nafasi, alijiambia: “Nakumbuka nilivyomuumiza yule mtoto, siwezi kuwa mwalimu bora.”

Siku moja kwenye kongamano la walimu, alimkuta yule mwanafunzi akiwa mtu mzima na mfanikio makubwa. Kwa aibu na huzuni, Fatma alimuomba msamaha. Yule mwanafunzi akacheka kidogo na kusema:
“Nilishasahau hilo kitambo. Mengine ni changamoto za maisha tu. Usijichomee moto wa zamani, Fatma.”

Fatma alilia kwa hisia. Toka siku hiyo, aliamua kuachilia mzigo wa kujilaumu na kuanza upya.

Somo: Kujilaumu ni kama kubeba mzigo wa mawe — haukusaidii kufika mbele. Ukishatubu au kuomba msamaha, jikubalie, jifunze, na songa mbele kwa matumaini.


Part 2

Story: “Usijilaumu Milele”

Zuhura alikuwa msichana mwerevu sana, lakini siku moja alipata matokeo mabaya shuleni. Alijilaumu kwa miezi kadhaa: “Ningeamka mapema,” “Nisingefungua simu,” “Nilikuwa mzembe.” Polepole alianza kujiona hana thamani. Alijitenga, akaacha ndoto zake za kuwa daktari.

Mwalimu wake mmoja alipoona hali hiyo, alimuita na kumuuliza:
“Zuhura, kama mtoto mdogo ateleza na kuanguka, utamkemea au utamsaidia kuinuka?”
Zuhura akajibu: “Nitamsaidia ainuke.”
Mwalimu akasema: “Hivyo ndivyo unavyopaswa kujiangalia. Umeanguka, sasa inuka na ujisamehe.”

Maneno yale yalimgusa. Alianza kujifunza tena taratibu, akapata marafiki wapya waliomtia moyo, na miaka miwili baadaye alifaulu na kujiunga na chuo cha udaktari.

Somo:
Kosa moja si mwisho wa safari. Kujilaumu kupita kiasi hukufunga. Lakini kujifunza, kutubu, na kuendelea mbele ndio ushindi wa kweli.

Methali ya leo: “Aliyeanguka si aliyeshindwa, bali ni yule anayekataa kusimama tena.”
 
Tajir haiitwi hivyo expert wangu,hapo unafeli

Tajiri anaombwa ahudhurie kama ikimpendeza

Tajir Bantu Lady nimetumwa nifikishe ujumbe,yule mtu aliyelala jana anaomba ikikupendeza ukaribie jukwaani tafadhali

Asante
Bantu Lady ni tajiri kwako,ila kwangu ni mwanangu sana. Alafu nammudu kivyovyote na Hana noma maana ni mzungu wa roho.

Niitie Bantu Lady tafadhali,mkuu kabla sijapitiwa na usingizi.
 
Nukuu ya leo

"Usikubali makosa yako ya jana yaibe tumaini lako la leo — kila alfajiri ni nafasi mpya kutoka kwa Allah."
Nukuu ya leo 🌅

Inakukumbusha kuwa kila siku ni neema, na hakuna sababu ya kubaki kifungoni mwa jana. Anza upya kwa imani.
Mkuu

Nafatilia michango yako sana,unaonyesha ni mtu wa dini sana,ila uki-engage kwenye mada senditiza dini unakuwa humble sana. Huna kauli mbaya.. I salute 🫡 you for that, Buddy.

Nyumbani ni Lindi- kilwa?
 
Back
Top Bottom