Mastory ya Bey
Wahanga wa vita ya pili ya dunia pamoja na machungu makubwa waliyopata kutokana na vita,walikuja baadae kujigundua wamekuwa watu zaidi
Kuna mambo ambayo hapo awali hawakuyapa kipaumbele katika maisha,kwa lugha nyingine waliyachukulia poa huenda kwa kutoona umuhimu wake
Lakini machungu ya vita na uzoefu walio upata wakajifunza kuyathamini maisha,wakajifunza kuthamini mambo madogo madogo ambayo hapo awali yalionekana sio chochote kwao
Waliona umuhimu wa kuwa na amani katika maisha yao,huenda hapo awali walipo ona sehemu nyingine ya dunia kuna machafuka walichukulia poa tu
Na huu mfano tunaweza kujichukulia sisi wenyewe Watanzania,tunapoona machafuko ya majirani zetu Congo,wakiwa wanatembea kana kwamba wanaandamana wakiwa na mizigo yao ,tunachukulia poa kabisa,lakini hatujui machungu ambayo wenzetu wanapitia
Tunapowaona majirani zetu Kenya wakimwaga damu tunawaona mashujaa na vidume,lakini katu tusiombe haya yatukute,kwani hakika tutajua thamani ya kuwa na amani
Kwahiyo wakati wa vita vya dunia,waathirika waliona jinsi watu walivyoteswa,kubakwa na kuuwawa,hii iliwaathiri sana hasa pale kumbukumbu zilipo wajia vichwani mwao
Lakini baadae walikuja kuwa watu imara,kimtazamo,kifikra na waliyaona mambo au maisha katika tofauti kabisa
Hapa tunajifunza kwamba kwa kila machungu ambayo tunapitia nyuma yake kuna somo kubwa sana tunajifunza,kwa kila maumivu na machungu tunayopitia ni mchakato wa kufikia sehemu fulani katika maisha yetu
Tufahamu kwamba haijalishi ni hali gani tunapitia kwasasa,ni maumivu kiasi gani yanatukuta kwa sasa,lakini mwisho wa siku,tutakuja kuwa tofauti kabisa,tutakuwa watu ambao wenye uzoefu mpya na maono mapya
But don't look for trouble,let matatizo yakutafute wewe,kwa njia hiyo yatakufundisha kitu fulani maishani