Mastory ya Bey
Leo bwana nikiwa town nikajikuta huyu hapa kwa fundi viatu,four angle yangu ilihitaji kuzungushiwa uzi maana sori kama ilianza kubanduka hivi
Kama unavyojua wabongo hatuna baya linapokuja swala la kupiga mastory,tukaongelea mada mbali mbali,mwisho wa siku tukaangukia kwenye No reforms No election
Kikubwa ambacho wadau kwa kauli moja,wamepinga sana majirani zetu wa Kenya kutaka kuingilia maswala yetu ya ndani
Wadau walihoji ya kwao yana washinda iweje waje kwetu kutaka kutuchafulia amani ya nchi yetu
Wao hawapati haki yao yoyote kwanza lazima wamwage damu,je hiyo ndio siasa? Alihoji mwamba mmoja
Mwamba mwingine akasema unajua wakenya wengi wamesoma lakini hawana kazi,ndio maana wanastress sana,hivyo hawana raha na nchi yao na wako wako confused,so wanaona tuko hapi pamoja na kula ugali na tembele lkn mwisho wa siku tunaishi kwa amani bila machafuko
Akaendelea kusema kama kuna watu wana msoto wa maisha basi ni Wakenya,wengi wao wanaishi kwenye mabanda ya bati,nadhani machakosi ni mfano mmoja wapo
Wadau wakaendelea kusema si unaona wenzetu Wakongo,kutwa kuchwa wanatembea na magodoro,hiyo yote ni kutokana na machafuko nchini mwao,kwahiyo tujifunze kutoka kwa wenzetu
Wadau wakaendelea kusema ifike kipindi Viongozi wa dini waache kuzungumzia mambo ya siasa,kwasababu wataanza kutugawa kutokana na dini zetu,na kila familia ya Watanzania tumechanganya,je si tutaanza kubaguana ndugu kwa ndugu kwasababu kuna waislamu na wakristo
Vile vile wakasema wenzetu wanabaguana kwa makabila huko kwao Kenya,ndio maana fujo na kumwaga damu ni sehemu ya maisha yao
Hivyo Watanzania tusiingie kwenye mtego wao,wapambane na shida zao watuache na maisha yetu
Wadau wakasema Watanzania tuache kabisa kushabikia hao Wakenya na kuwaona ni mashujaa,hao wako na shida mingi sana
Ni bora tuonekane ni waoga lakini mwisho wa siku watoto wetu na familia zetu waendelee kuishi kwa amani