JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya usiku

WANANDOA NA HAKI YA TENDO LA NDOA


Leo kalamu ya mlinzi wa zamu inaangalia swala zima la tendo la ndoa kwa wanandoa

Hii ni haki ya msingi sana kwa wanandoa,maana hata msingi mzima wa ndoa umejengewa hapo,haki zote tulikuwa tunapata majumbani kwetu,lakini haki hii ndio ikawaunganisha mwanaume na mwanamke waishi pamoja ili kukidhi matamanio yao

Kwa maana kwamba baada tu ya kufunga ndoa kila mmoja anastahili kupata haki hiyo pasina masharti yoyote yale au bila vikwazo vyovyote vile

Lakini bahati mbaya iliyopo ni kwamba hutokea baadhi ya wanandoa kutumia silaha ya tendo la ndoa kukomoana pale inapotokea sintofahamu kati yao

Basi mwanandoa mmoja wapo hutumia silaha hiyo kumnyima mwenzake unyumba kwakuwa tu kuna haja au mambo fulani hayajatekelezwa

Hakika mbele ya Mungu hili ni kosa kubwa sana,sijui upande wa ukristo huko,lakini kwa ufahamu wa dini ya kiislamu,kwa mwanamke ambaye anaitwa na mumewe kitandani kisha akakataa basi hakika hulaaniwa na Malaika usiku kucha

Sasa usione hili ni jambo dogo,hawa viumbe hawana dhambi kwahiyo dua zao mbele ya Mola wao huwa ni zenye kupokelewa,kama ambavyo huwaombea watu wema dua kwa Mungu,na Mungu hupokea dua zao

Lakini lingine kuna hatar kubwa sana ya kuwa sababu ya mwenza wako kwenda nje kupata faraja huko,nawe utakuwa sehemu ya uovu huo,kwasababu umesababisha mwenza wako akazini kwakuwa wewe hukumpa haki yake

Kwahiyo mjue kwamba kinachowaunganisha wanandoa msingi wake ni hilo tendo,sasa iweje tena mnyimane mautamu wakati kwa hiari yenu wenyewe mmeamua muishi pamoja kama mume na mke

Kama kuna tokea sintofahamu yoyote basi zungumzeni na myamalize lkn msitumie haki yenu ya msingi kuanza kukomoana

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom