Mkuu hilo swali la nani atawaongoza avengers baada ya iron man kufa unatakiwa ujue marvel bado hawajaweka wazi hadi hapo avengers 5 itakapotoka, hivyo marvel fans tunafanya kukisia tu wapo wanaosema ni doctor strange wengine wanasema captain marvel na wengine wanasema spider man.
Halafu kitu kingine unatakiwa ujue kuwa kiongozi wa avengers tangu mwanzo alikuwa ni captain america na siyo iron man na hili iron man mwenyewe aliwahi kulisema kwenye avengers age of ultron kuwa “actually he’s the boss, i just pay for everything and design everything, and make everyone look cooler” kwamba yeye iron man alikuwa anawapa tu financial and technological assistance ila hakuwa leader.
Kuhusu kwa doctor strange kama ulisikiliza vizuri script ya avengers infinity war kuna sehemu doctor strange alitekwa na ebony maw mtoto wa thanos, akapelekwa titan ambako iron man na spider man walienda kumuokoa na kukutana na guardians of the galaxy kisha wakamuua huyo ebony maw.
Huko doctor strange alitumia time stone kuangalia 14 million possible futures ambazo avengers wataingia kwenye conflict na thanos, na akagundua kati ya hizo futures ni moja tu ndiyo ambayo avengers watashinda hivyo akamuambia iron man na iron man ndiyo akaja kumuuliza vile kwenye endgame.
Alimuuliza “hey you said 1 out of 14 million we win yeah, tell me this is it” doctor strange akamjibu “if i tell you what happens, it won’t happen” akimaanisha kwamba hiyo inaweza isiwe ndiyo future alioiona, ila alipoona thanos anakaribia kusnap fingers na avengers wengine walikuwa wameshapigika akamuambia iron man kuwa ile ndiyo ilikuwa chance pekee ya yeye kuchukua stones na kusnap fingers.
Na ndiyo maana pale alinyanyua kidole kimoja kuonesha ishara kuwa this is the one and only future ambayo avengers wangeshinda, out of the 14 million futures ambazo aliziona.
Kuhusu captain america mkuu mbona inaeleweka, captain alirudisha zile infinity stones zote ila badala ya kurudi 2023 kama walivyokubaliana alirudi miaka ya nyuma ili akaishi na mke wake peggy carter.
Kilichomfanya asizeeke ni sababu alikuwa kwenye ice, ila alipoenda kuishi maisha ya kawaida alizeeka.