JamboLeo: Watanzania wakosa imani na 'Rais'

JamboLeo: Watanzania wakosa imani na 'Rais'

Uswahili. Maendeleo ni gharama, si lelemama. Hapa ndio kwanza hatujafika katikati ya trela, baadaye picha halisi ianze. Kuna watu, wengi tu, walihamia mijini kwa kuwa pesa iliyokuwa ikivuja serikalini iliteremkia huko. Sasa JPM ameziba nyufa zote kwenye kuta na sakafu ya Serikali wakati walionufaika na uvujaji huo wakiwa bado wamekinga bakuli, hawajajua wala kujiandaa kurudi walikotoka au kubadilisha tabia na mwelekeo kuwa kuzalisha halisi. Itachukua muda kundi hili kubwa kujitambua na kuchukua uamuzi sahihi. Na ndio maana haishangazi kuona mtu juzi alisema anaipinga serikali ya JK kwa kuendekeza rushwa, leo JPM anashughulikia rushwa, mtu huyo huyo anadai bora utawala wa JK. Na corrupt state beneficial owners wanaunga mkono, si haba.
Uko sawa ndugu naomba unisaidie sasa hapa;

ameziba kwa wale waliokua zina wavujia (waliokua wanazipata kiuraisi) sasa mbona hata sisi wa halali bado mambo magumu????

Hizo zilizokua zinavuja why zisi chonge dawati??? Maana nimechangia 30000/= ya dawati!!!!!!

Hizo zilizokua zinavuja why zisisaidie kununua mbegu za kilimo kwa msimu ujao, rejea waziri wa kilimo tangazo lake la juzi kuwa bajeti iliyotengwa ni ndogo ivyo wakulima wajiandae kujigharamia wenyewe!!!!

Izo zilizo kua zinavuja kwanini zisi saidie kulipa deni la MSD ili zahanati zetu zipate dawa na vifaa vya tiba kwa wakati????


Izo zilizokua zina vuja kwanini zisi pelekwe kwenye kasi ya kujenga ama kupima maeneo ya viwanda kwenye mikoa ama wilaya mbalimbali hapa nchini????


Jiulize maswali ya fuatayo; toka tunapambana na ufisadi na kuwakamata hawa mafisadi mpaka wa milion 7 kwa sekunde, ni kiasi gani cha fedha kimesha rudishwa na kimepelekwa kwenye changamoto ipi????

Juzi nimesikia serkali imepunguza kulipa watumishi hewa na zaidi ya bilioni 20 zimeokolewa toka mwezi wa 3 ukipiga hesabu nisawa na bilioni 150 mpaka sasa serikali yetu imefanikiwa kuokoa!!!! Hizo zimeeelekezwa wapi???? Kwanini izo nafasi sasa zisitangazwe ajira kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira????

Au kama ajira sio sasa hivi kwanini zisipelekwe moja kwa moja kwenye uboreshaji miondombinu ya shule kama vile dawati na uongezwaji wa vyumba vya madarasa???? Ili watoto wetu wasome vizuri!!! Au kwanini zisinunue mbegu na pembejeo za kutosha kwa wakulima wetu???

Mwisho maelezo yangu ni kwamba, thamani ya hela yetu kwa sasa haimach na mfumuko wa bei ama maisha tunayo ishi!!!!! Serikali na shauri iachane na mambo ya siasa na matamko ya kila siku!!!!!! Iki wasikia wapinzani wanaongea isikie yale mazuri na mengine kupuuzia!!!!! Ijikite kuzitatua changamoto za maisha ya watu kwa kuwa na kipaombele na dira inayo itekeleza!!!!!!

Watu wakipata unafuu wanao utarajia upinzani hata ukeshe na maandamano watu wanelewa huto muona mtu kwenye maandamano wala mikutano maana shida zake zinatatuliwa!!!


Nakila waziri afanye kazi sio kila siku kumchosha mkuu wa nchi atoe tamko ndio watu wakatekeleze jambo fulani!!!!! Inafika mahala sasa watu wanasema "MAGUFULI akija!!!!!!! " hii ni mbaya sana!!!! Inapaswa kuwa kawaida yetu kutimiza wajibu na sio mpaka mh rais aje!!!!
 
Kama mambo yenyewe ni haya, kamwe hataruhusu chama chochote cha upinzani hasa CHADEMA, CUF, ACT na NCCR Mageuzi kufanya mkutano wa hadhara, kwa maana anajua kwamba haya yaliyoorodheshwa na Ben Saanane ndiyo yanayokwenda kusemwa. Ni afadhali aonekane dikt*t@ kuliko kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Ben Saanane ni mtu mwenye chuki na mshabiki mkubwa wa Bw Mbowe na his gang of four, na huwa kila mara anavutia kwake, wala simlaumu, chadema wakijinyia hutasikia akisema hapa pananuka, lakini ccm wakipiga chafya utasikia akisema wantawanya BIRD FLU.

Yeye Leo kufunguliwa minyororo tumwache arukeruke kwenye GARDEN YA VILA YA BWANA MKUBWA WAKE.

Huyu ni mshabiki tuu.
20160807_055451.jpg


hili gazeti siku zake zinaweza kuwa zinahesabika

=====
 
Neno watanzania kwny hicho kipeperushi wasio kuwa na imani na Magu wanamaanisha Wakwepa kodi,wezi, mafisadi, wazembe na Waabudu Mikutano na Maandamano ya kisiasa
Binafsi naona Rais atashindwa hatimaye kubaki kutoa kauli za vitisho lakini for economic growth sioni muelekeo vema.Nachokiona sasa wapigaji watatengemeza mitandao ndani ya Chama na nje na wanamjua kuwa rais hana kifua cha uvumilivu hivyo asiposema hadharani watajua hana taarifa.Misingi iko kwenye loophole za sheria. Jiulize tokea tumbua majipu ianze miezi nane iliyopita nani kahukumiwa?.
Wakurugenzi wa NIDA, TRA, TPA, TRL, million saba Kwa dakika, wanaopokea mishahara 17..
President must change strategies other wise.....
 
We have been talking about this :"Africa needs strong Institutions but not strong people ". There is no good leader in Weak institutions.
 
Watanzania wengi wamechoka na kile kibwagizo cha 'Hapa Kazi Tu!' wakati mtaani hakuna Kazi wala Ugali, ni njaa tupu.
Wakati wa kampeni Ahadi zilikuwa ni hizi.
1/Elimu bure.
2/Viwanda.
3/Ajira kwa vijana.
4/Kushuka kwa bei za bidhaa muhimu.

Sasa vipaumbele vimegeuka na kuwa.
1/Kuongeza Kodi mpya.
2/Kutokusafiri nje.
3/Kutumbua majipu.
4/Kuzuia bunge live.
5/Kuchangia madawati.
6/Kupambana na UKUTA.
7/Kuhamia Dodoma.
 
Kama mambo yenyewe ni haya, kamwe hataruhusu chama chochote cha upinzani hasa CHADEMA, CUF, ACT na NCCR Mageuzi kufanya mkutano wa hadhara, kwa maana anajua kwamba haya yaliyoorodheshwa na Ben Saanane ndiyo yanayokwenda kusemwa. Ni afadhali aonekane dikt*t@ kuliko kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Je,ni ya uongo?
 
20160807_055451.jpg


hili gazeti siku zake zinaweza kuwa zinahesabika

=====


Kuna mahali ambapo siwezi kupata JAMBO LEO...lakini kuna mtu kanidokeza kuwa eti contents zake kwa habari hiyo hazihusiani na utawala wa sasa wa awamu ya tano...labda ndiyo maana wame-quote 'Rais'...hata hivyo picha iliyopo ni ya JPM...hivyo kama ni kweli contents hazihusiani na kichwa cha habari then uwezekano wa kufungiwa upo...huwezi kuandika kiujanja ujanja 'Rais'...lakini sijui waliosoma contents za gazeti hilo tunaomba watuhabarishe...
 
20160807_055451.jpg


hili gazeti siku zake zinaweza kuwa zinahesabika

=====

Kulia na kucheka yote ni kelele tu .....
Hata hayo uliyoandika na kujinasibu sana kuwa nilisema.... Zote ni kelele tu..... Hizo ni hira zenu za kutaka kumzoofisha Rais wetu mpendwa....
MShindwe na Mlegee na tena kwaJina la YESU .......
Haitakuwa na hatakoma kuacha kuisimamia Katiba.... Mtaenda tu hata kwa bakora kwani Mlizoea kuwababatiza kiaina Watanzania.....
 
Wewe hata baba yako hapo nyumbani mambo yote aliyokuahidi au kuyapanga aliyatekeleza at Once.... Acheni mambo yenu tujadiliane kwa fact na kwenye ukweli pazungumzwe Ukweli.... Hivi jamani hamuoni mambo yanayofanyika au ndo mmejipanga kubishia kila jambo jema linalofanywa? Shame On You Guys - Nchi itajengwa na sisi wote, Hii ndiyo tabu / shida kubwa ya wa TZ kujifanya wanajua kila jambo kumbe hata makwao wanakotoka shida tupu..... Acheni hizo bwana ....
 
Back
Top Bottom