Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 17,815
- 33,486
hili gazeti siku zake zinaweza kuwa zinahesabika
=====
Ben Saaanane:
Haya naandika Ukweli tena kwa dhati kabisa.
Inawezekana Uhakiki wa Vyeti Uanzie Ikulu ?
Ni Hivi,Kuelekea Maadhimisho ya Mwaka 1 baada ya Uzinduzi wa "Urais wa Push-Ups na Kusakata Rhumba Majukwaaani"
Imeshakua Balaa mtaani.Watu wameshaamua kama Mbwai Iwe Mbwai tu. Yaani Gazeti la Jambo Leo limeamua Kubamiza Headline "Watanzania Wakosa Imani na "Rais". Push-Ups si lolote ,Si Chochote .Vitisho tu.
Yaani wameamua kuweka Utafiti wao Hadharani. Subiri usikie kuwa Sheria mpya ya Takwimu kifungu namba 19 kimekiukwa na gazeti hilo kwa hiyo tunachukua hatua zifuatazo........!
All in Watanzania wameshtuka.Miezi 9 tu yupo nyang'anyang'a
Maana niliwahi kuandika "Misingi ya Urais sio kusakata Rhumba na Pushups majukwaani"-Wasomi Uchwara wakanibishia
Kisha miezi 5 baadae Mhusika Mwenyewe akasema "Kazi hii ni nzito sana ,wakati mwingine najuta kwanini hata niliutaka Urais".Alisema kwa kinywa Chake Mwenyewe.Simjaribu.
Lissu alisema tutamshinda mahakamani na tutamshinda nje ya mahakama.Juzi tumemshinda Mahakamani .Sasa huku nje tuendelee
Kwanza Kuzuia Mikutano ya hadhara namuunga mkono maaana ndio Silaha yake ya Mwisho na Kutisha watu kwa Vyombo vya Dola.Kwani mnadhani angefanyaje kama alijinadi kwenye kampeni kwa Kusakata Rhumba Jukwaani na Push-Ups?
Hivi mnataka katika Mikutano ya Hadhara mkawaeleze wananchi kuhusu ahadi zake wakati ilikua zilongwa mbali,Zitendwa Mbali. ? Haiwezekani kumuweka majaribuni kiasi hicho
Aliahidi kwa kasi sana.Kasi ya Magufuli
1:Nitamaliza Mgogoro wa Zanzibar akiwa anahutubia Bunge lakini baada ya Mwezi Mmoja akapinga
"Mgogoro wa Zanzibar siwezi kuingilia.Kuna mamlaka na tume yake.Atakayeleta Fyokofyoko atakiona cha Mtema kuni".
2:Aliahidi kupambana na Rushwa lakini baadae majuzi hapo akapinga
"Nimempa Trafiki Elfu 5 kwa ajili ya ku-brush Viatu"
Rushwa ikabatizwa jina jema
3 Akiwa Mapumzikoni Geita Alipobanwa kuhusu Mshahara wake akaahidi "Nikirudi Dar nitatoa vielelezo vya malipo ya Mshahara wangu hadharani"
Leo miezi minne Kimya! Yaaani Kimyaaaah! Sasa mnataka mkawaeleze Wananchi?
4:Halafu alipoumbuka hadharani ilikua hivi
"Ni Tanzania Pekee Mwanafunzi anaweza kupata Division Four na kwenda Chuo Kikuu halafu mwanasiasa anamtetea.Hao Wanasiasa ni Vi-La-ZA kama wao"
Bintiye aliwahi kupata Div.IV na Yupo Chuo kikuu UDOM. Yaani hajakanusha,Chuo au Familia Kimyaaah! Aibu hii ndio unataka Upeleke kule?
5: Akiwa Kule Mtwara tarehe 3 Septemba mida ya Jioni Uwanja wa Mashujaa akasema "Nitashusha bei ya vifaa vya ujenzi.Lengo langu pia nyumba za Tembe ziondoke na watanzania waishi maisha bora "
Vifaa vya ujenzi hadi sasa ni ghali na mbaya zaidi kawaambia wananchi waliokumbwa na mafuriko kule Kahama kuwa "Serikali yangu haiwezi kuwajengea nyumba wakati ninyi mmekaa tu"
6:Aliaahidi kupambana na Ufisadi .Sakata la Lugumi Kimyaaah.
-Utekelezaji wa Maazimio ya ESCROW kimyaa.Ndio kwanza IPTL imeendelea kulipwa mabilioni
-Hatua kwa Wanunuzi wa kivuko kibovu kama ripoti ya CAG ilivyoonesha kimyaaah.Maana yeye alikua Waziri mwenye dhamana.Sasa si jipu litumbuliwe?
-Akamfukuza kazi Dr.Hoseah kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU. Lakini mimi nikasema tatizo sio Hoseah bali Sheria na TAKUKURU kutokuwa Independent .Sasa mkurugenzi mpya anaendana na kasi ya Magufuli? Ha ha ha! Wananchi wakaelezwe ?
8: Akasema "nitatoa elimu Bure" na Pia matatizo ya mikopo yatakua Historia.Leo hadi baadhi ya watumishi wanachangishwa madawati naMikopo ya Wanafunzi tatizo liko palepale
9: "Bei ya Sukari itakua bei nafuu na napiga marufuku Sukari kuagizwa kutoka nje"
Leo Bei ya Sukari Wananchi hawahitaji kukumbushwa. Lakini baadae alipiga "Serikali yangu itaagiza sukari kufidia pengo la uhitaji"
10:Nitasimamia Utawala bora wa Sheria .Kisha akaja na " Magari binafsi yanayoingia barabara ya Mwendokasi yang'olewe tairi kisha yapelekwe kituo cha polisi na pale mtapata biashara.Wakija kuuliza kesho yake waambieni yalikuja yenyewe"
11: "Mimi nitakua Rais wa Wanyonge"
Kisha Wanyonge wa kule Msimbazi na Jangwani wakabomolewa nyumba bila fidia na bila decent measures na wengine wakapata fadhaa na majanga mengine
Wanafunzi wa UDOM wakafukuzwa bila staha bila utu kwa makosa yaliyofanywa na serikali.Wakatelekezwa na kudhalilika .Wakalia,Wakaomboleza.Watoto zaidi ya 7,000 wana ndugu ,Jamaa na marafiki waliosononeka.Mnataka mkawakumbushe hasira?
12: "Nitalinda Umoja wa Kitaifa"
-Ghafla akasema "Napenda Vijana Serikalini maana wazee ni wala Rushwa"
Yaaani hii ilikua haina tofauti na Ramli Chonganishi na yale ya wale wanaoua Vikongwe
-Halafu akasema Marufuku mikutano ya siasa hadi 2020
Yaani vyama vya Siasa visipate haki yao kisheria na kikatiba.Akajikuta amezalisha Operesheni UKUTA
Taifa lipo Kwenye Tension
13: Tangu atangaze kuwashusha Wanadamu waishi kama Shetani hata viongozi Decent wa Dini wameacha kujihusisha nae .Labda katika Maombi tu
14: "Tumefika hapa kwa sababu ya Kulindana ,Hilo kwangu halipo na Watanzania mniombee.Kuna majipu nitayatumbua.Nimejitoa Mhanga"
Kisha ghafla akaja na kaulimbiu "Wazee Wangu Mkapa na Kikwete nitawalinda .Pumzikeni kwa Raha Mustarehe"
15: "Kuna mtu anaibia Serikali Milioni 7 kila Dakika ". Wah hebu chukua Milioni 7X60X24 (Siku moja) upate jibu. Halafu kwa sababu huyo mtu ameshakamatwa sasa tuseme tangu akamatwe zimeokolewa Sh. ngapi na zimeelekezwa wapi
16: "Tanzania ya Magufuli ni ya Viwanda"
Hadi sasa Vimejengwa viwanda Vitatu
i) Kiwanda Cha Kuhamia Dodoma
ii) Kiwanda cha UKUTA
iii) Tundu Lissu Democratic Machine Tools
iv) Mikia Productions
iv) Majipu Factory Construction in Progress
Ha Ha ha!
Narudia "Misingi ya Urais sio kusakata Rhumba na Push-Ups Jukwaani". Kama anabisha basi Mnara ujengwe alipozindulia kampeni za Push-Ups.
Aluta Continua,Victory Ascerta....
Ben Saaanane