Uswahili. Maendeleo ni gharama, si lelemama. Hapa ndio kwanza hatujafika katikati ya trela, baadaye picha halisi ianze. Kuna watu, wengi tu, walihamia mijini kwa kuwa pesa iliyokuwa ikivuja serikalini iliteremkia huko. Sasa JPM ameziba nyufa zote kwenye kuta na sakafu ya Serikali wakati walionufaika na uvujaji huo wakiwa bado wamekinga bakuli, hawajajua wala kujiandaa kurudi walikotoka au kubadilisha tabia na mwelekeo kuwa kuzalisha halisi. Itachukua muda kundi hili kubwa kujitambua na kuchukua uamuzi sahihi. Na ndio maana haishangazi kuona mtu juzi alisema anaipinga serikali ya JK kwa kuendekeza rushwa, leo JPM anashughulikia rushwa, mtu huyo huyo anadai bora utawala wa JK. Na corrupt state beneficial owners wanaunga mkono, si haba.