Mwigulu na uongozi unaoheshimu imani

Mwigulu na uongozi unaoheshimu imani

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
463
Reaction score
312
𝗠π—ͺπ—œπ—šπ—¨π—Ÿπ—¨ 𝗑𝗔 π—¨π—’π—‘π—šπ—’π—­π—œ π—¨π—‘π—”π—’π—›π—˜π—¦π—›π—œπ— π—¨ π—œπ— π—”π—‘π—œ

Kuna nyakati ambapo picha moja haiwezi kueleza falsafa nzima ya uongozi, lakini inaweza kutupa nafasi ya kutafakari kwa kina kuhusu uongozi, unyenyekevu, imani na Taifa. Picha ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika mazingira ya ibada ni miongoni mwa picha zinazobeba ujumbe huo.

Kama mwananchi ninayeamini katika Tanzania yenye amani, umoja na kuheshimiana, ninapomuona Waziri Mkuu akishiriki katika matukio mbalimbali ya dini, namuona kama kiongozi mwenye mamlaka anayeyaweka pembeni tofauti na kuonyesha heshima kwa taasisi za dini, imani na utu wa wengine.

Katika kipindi cha hivi karibuni, Dkt. Mwigulu amekuwa akionekana katika shughuli za madhehebu mbalimbali ya dini, si kwa kubagua, bali kwa kushiriki katika matukio yanayogusa maisha ya Watanzania.

Agosti 25, 2026, alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid la Kitaifa, akisisitiza umuhimu wa wema, huruma, upendo, kusaidiana, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania wa dini mbalimbali.

Juni 21, 2026, Kanisa la Anglikana Tanzania lilimtunuku Dkt. Mwigulu heshima ya Lay Canon, likitambua mchango wake katika kuhamasisha na kufanikisha uchangishaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Kanisa. Kilichovutia zaidi ni kwamba heshima hiyo ilitolewa kwa kiongozi ambaye si muumini wa Kanisa hilo, ishara kwamba mchango kwa jamii unaweza kutambuliwa hata unapovuka mipaka ya dhehebu.

Juni 28, 2026, Dkt. Mwigulu Nchemba alishiriki katika ibada maalum ya katika ibada maalumu ya kilele cha harambee iliyofanyika kwenye usharika wa Amani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati, mjini Singida. Harambee hiyo ambayo ni ya nne kufanyika, ililenga kukusanya sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya kuboresha vituo vya huduma za afya, kuimarisha vituo vya huduma za elimu, utumishi na uinjilisti vya Dayosisi hiyo ambavyo vinapaswa kukamilika ifikapo Desemba, mwaka huu.

Agosti 30, 2026, Dkt. Mwigulu alikuwa Mgeni Rasmi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Jimbo Katoliki la Mpanda, Katavi. Katika tukio hilo, alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika huduma za kijamii, maendeleo na ustawi wa wananchi, akitambua mchango wa Kanisa Katoliki katika elimu, afya na huduma za kiroho.

Agosti 10, 2026, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alikutana Ikulu ya Chamwino na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika mazungumzo yaliyogusa masuala ya kitaifa, imani, maendeleo, amani, mshikamano na mustakabali wa Taifa. Pia, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushauriana na kushirikisha viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya jamii katika masuala muhimu ya Taifa.

Rais anazungumza na viongozi wa dini. Waziri Mkuu anashiriki shughuli zao. Viongozi wa dini wanakutana na Serikali. Wananchi wanaendelea kupata huduma.

Tunapoona viongozi wakikutana na Waislamu, Wakatoliki, Waanglikana, Walutheri na madhehebu mengine, tunapaswa kuona zaidi ya tukio lenyewe, Ujumbe wa umoja, Daraja la mazungumzo, Heshima kwa uhuru wa kuabudu, Kwamba tofauti zetu za kiimani hazipaswi kuwa sababu ya kupoteza utu wetu wa pamoja kama Watanzania.

Kwa mtazamo wangu kama mwananchi, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba anastahili pongezi kwa kuendelea kutenga muda wake kushiriki katika shughuli za dini mbalimbali na kuheshimu nafasi ya taasisi za dini katika Taifa.

Na kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pongezi kwa kuendelea kuimarisha utamaduni wa mazungumzo, ushirikiano na kuheshimiana kati ya Serikali, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa jamii.
lv_0_20260831134017.jpg
 
Uchawa ni laana
 
Back
Top Bottom