justus ndyanabo
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 444
- 379
Ngoja tuje madikiteta wa uhuru wa habari mtatukoma nyie Jambo Leo
Kuna sumu humo, kuwa mwamgalifu ndugu.mimi huwa nafungia samaki aitwaye PONO
Majipu Factory Construction in ProgressWanaomwombea mabaya rais wetu washindwe na walegee .
Mashetani wakubwa
ajira hakuna piaa
Kabla sijachangia naomba kuuliza, hivi mmiliki wa Jambo Leo ni nani?Ngoja tuje madikiteta wa uhuru wa habari mtatukoma nyie Jambo Leo
Ha Ha, Kumbe Namba Imesambaa Nchi NzimaNipo huku kijijini msibani wanakijiji waliokua washabiki wa ccm kindakindaki hawana hamu na hii serikali hadi raha, wanadai no money circulation biashara zao wengi wamekata mitaji na wengine wametoa watoto wao kwenye shule binafsi kwa kuwa hawana pesa tena za kulipia ada, wananchi wengine wanalalamika ndugu zao waliokua wanawapa misaada mbalimbali baadhi yao wameacha kuwasaidia toka mjini na wengine wamepunguza misaada kwa %90 hawa waliopunguziwa misaada wengi ni wazazi wa watoa misaada na wengi hawataki kusikia hata neno magufuli, kuna jina wamempachika siwezi andika hapa make sina milioni kumi za kuchezea.
ni kweli wanakijiji wamechoka na wengi wanadai ikipigwa kura wapo radhi kumpigia hata mbwa kuliko kumchagua tena huyu tena, niliwauliza baadhi yao kwa nini walimchagua wakadai walitishwa kuwa wakimchagua mpinzani kutatokea vita na lowasa ni mwizi atawauza hadi wao na watahamishwa kusikojulikana.
Nikawauliza akitokea huyu mwizi mtamchagua? wakadai kwa hali ilivyo sasa wako Tayari kuchagua kitu chochote ili mradi huyu atoke madarakani, wewe mwanangu angalia nilivyo konda na sasa hivi ndio ana miezi nane, akimaliza miaka mitano je? Si nitakufa? Nimemnukuu mama moja wa makamo.
CCM wasipofanya marekebisho ya kiutawala natabiri hii ndiyo serikali itakayochokwa kwa mda mfupi kuliko serikali ya kikwete.
Hata mie natamani ningepiga kura jamani, lo! maana hii "hapa kazi tu" bila kuwa na sera madhubuti ya kitaifa ndo matokeo yake ni matamko tu pengine labda ingeeleweka hivi "Hapa Matamko Tu"![]()
hili gazeti siku zake zinaweza kuwa zinahesabika
=====
Kupotosha ni kawaida yenu, JK aliachia nchi genge la walafi, JPM anavunja Katiba na Sheria alizoapa kulinda, period!Uswahili. Maendeleo ni gharama, si lelemama. Hapa ndio kwanza hatujafika katikati ya trela, baadaye picha halisi ianze. Kuna watu, wengi tu, walihamia mijini kwa kuwa pesa iliyokuwa ikivuja serikalini iliteremkia huko. Sasa JPM ameziba nyufa zote kwenye kuta na sakafu ya Serikali wakati walionufaika na uvujaji huo wakiwa bado wamekinga bakuli, hawajajua wala kujiandaa kurudi walikotoka au kubadilisha tabia na mwelekeo kuwa kuzalisha halisi. Itachukua muda kundi hili kubwa kujitambua na kuchukua uamuzi sahihi. Na ndio maana haishangazi kuona mtu juzi alisema anaipinga serikali ya JK kwa kuendekeza rushwa, leo JPM anashughulikia rushwa, mtu huyo huyo anadai bora utawala wa JK. Na corrupt state beneficial owners wanaunga mkono, si haba.
Gazeti la ManjiHili gazeti ndo la Mzee wa mtama,au?
Mbona mimi si miongoni mwa hao lakini sina imani na 'Rais'! Sababu zangu ni kuwa hata kama angetelemsha 'mana' toka juu,hawezi kutuongoza kwa sheria za mfukoni mwake. Ili kuwa na imani na Rais lazima kuwe na mjumuiko wa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kwenda kitandani ukiamini kwamba Kiongozi Mkuu yu makini katika kuheshimu Sheria na utawal bora.Hapana jamani twende mbele turudi nyuma,
Nimechunguza maudhui ya hili gazeti nimegundua yanawakilisha kundi lililo ndani ya chama ambalo limeathirika na ujio wa Mwenyekiti mpya.
Kundi ambalo lilikuwa linanufaika na udhaifu wa serikali iliyopita, mirija imekatwa sasa wanaanza chokochoko kwa mgongo wa wananchi kuwa hawana imani na rais kumbe wao ndio hawana imani na Magufuli kama atalinda maslahi yao. Tuseme Hapana.
Haiwezekani Magufuli kaza uzi, ukiona mtu anapiga kelele gizani juwa jiwe limempata.
Ni kweli maisha yanakuwa magumu tutaumia kwa kipindi kifupi lakini binafsi bado nauona mwanga huko mbeleni.
Wananchi tuweni na akili za uchambuzi, wale waliofanya maisha yetu yawe duni kwa kujitajirisha wao na watoto wao ndio hao hao wanataka kutumia hali ngumu iliyopo kufifisha jitihada za rais.
Inakuwaje hali ngumu yetu waione leo kwani awamu iliyopita tulikuwa na hali nzuri?
Kwa hili niko na rais, he is doing a wonderful job ambayo haikuwahi kuonekana awamu iliyopita, ni wavivu, wazembe, wezi, waliozoea madili tu ndio watakaomwona hafai.
Ukisoma vizuri nilicho kisema sijaomba hizo pesa zilizo vuja zinifikie!!Hello ndugu, pesa zilizokuwa zikivuja zilishaliwa kwa takriban miaka 30; zimeacha pengo ambalo serikali ya JPM, hata ungekuwa unaongoza wewe huwezi kuliziba kwa miezi 8. Kwa hiyo unachotakiwa kufahamu ni kuwa government money leakages have been water tight sealed. Pili ni kuwa pesa mlizokuwa mkipata kutokana na manunuzi mafisadi/wezi wa mali ya umma sasa hamuwezi kuzipata tena kwa kuwa hawanazo za kutumia kama ilivyokuwa zamani. Kwa hiyo walipokoza, nanyi mnakosa pia. Hali hii kwenye nadharia ya uchumi inaitwa contractive multiplier effect. Jitahidi uwe na ujuzi unaotakiwa ili uweze kuingia katika mfumo wa uchumi wa nchi (mzalishaji mali) nawe utaweza kuwa sehemu ya washiriki wa pato la taifa. Kulalama kuomba mafisadi warudi kuendesha uchumi wa nchi hakutasaidia kitu. Ni Kazi Tu.
Pesa za umma zilizokuwa zikivuja zilikwisha mwagika na kupotea. Pesa za umma ambazo zinazokombolewa kwa sasa zinaziba mapengo yaliyosababishwa na mivujo iliyokuwa imekithiri. Utaratibu wa kuziba mapengo unapitia mfumo rasmi, hivyo si muda mrefu tutaanza kuona matokeo (chanya) yake. Labda nikukumbushe kisa cha shirika Fulani la umma kununua kalamu ya wino kwa njia ya public procurement kwa shilingi 5000, wakati aina hiyo hiyo ya kalamu katika kibanda nje ya shirika hilo, inauzwa shilingi 300. Hoja iliyokuwa ikitolewa kuhalalisha wizi huo ni kuwa zabuni ya manunuzi hayo ilifanyika kwa mujibu wa sheria husika (PPA No.7/2011). Lakini pia juzi juzi tu tumesikia kiwanja ekari moja huko halmashauri ya Arumeru, Arusha ikiuzwa kwa shilingi billioni moja (1,000,000,000) wakati wenyeji katika eneo hilo hilo wanauza ekari moja kwa bei ya kati ya shilingi laki 3 na laki 5. Suala hili liko TAKUKURU kwa sasa. Mivujo ilikuwa mingi hasa.Nimesema kwa kua hazivuji tena (zipo mahala) kwanini sasa zisiende kutatua changa moto ya madawati au miundombinu ya madarasa au madawa au dawa na vifaa vya hospitali????