JamboLeo: Watanzania wakosa imani na 'Rais'

JamboLeo: Watanzania wakosa imani na 'Rais'

Tulieni watanzania nilazima wote tutaishi Sawa ngojeni JPM aseti mambo mtafurahi tu wengi walizoea kujimilikisha nakutamba.Izo zama hatuzitaki kitaeleweka tu natutamfurahia kamanda wetu JPM.Mwaweja sana wangosha
 
Wanachato wanaimani na Magu. Serkal ya vwanda imeanza kazi yake chato. Nyumban kwa magu pamekuwa kama white house.
 
Jambo leo wamegundua ukweli unalipa kuliko kujipendekeza
 
Kusema ukweli, maisha yamekuwa magumu maradufu kwa watu wote, watumishi wa umma ndio usiseme, wananchi wa kawaida ni kelele biashara haziendi....
Mh. Rais aangalie hali hii inakuaje, maana hali mbaya sana mitaani
Kwa nini mnasahau mapema hivi?
Rais.alisema wanaoishi kama malaika watajiunga na waTZ wanaoishi kama mashetani.
Limetimia. Tushangilie.
 
Ili ujue mambo ,/facts yalivyo kwenye Siasa za Tz kukupitia media,ni lazima pia uwajue Wamiliki wa vyombohivo! Unakumbuka Jambo Leo Miezi 9 nyuma walikuwa wanaandikaje, Fuatilia pia uandishi wa Nipashe ulivobadilika miezi kama minne iliyopita! Hiyo ndiyo Siasa ,who get what,when and how! Siwapigii debe ,magazeti objective kwakiwango cha kuridhisha ni Mwananchi na Majira !na kiasi fulani Raia Mwema ! Vinginevyo fuata mrengo ima wa tanzania Daima+Mtanzania+wenzao ...au Uhuru/habari Leo+ Raia Tanzania ....!

mimi wala mwananchi naona liko ki kenya kenya zaidi na dhani kuna mtu wao walikuwa wanampigia debe
Raia mwema na jamhuri ndo naona magezeti bora kwa sasa
 
Ben Saaanane:

Haya naandika Ukweli tena kwa dhati kabisa.

Inawezekana Uhakiki wa Vyeti Uanzie Ikulu ?

Ni Hivi,Kuelekea Maadhimisho ya Mwaka 1 baada ya Uzinduzi wa "Urais wa Push-Ups na Kusakata Rhumba Majukwaaani"

Imeshakua Balaa mtaani.Watu wameshaamua kama Mbwai Iwe Mbwai tu. Yaani Gazeti la Jambo Leo limeamua Kubamiza Headline "Watanzania Wakosa Imani na "Rais". Push-Ups si lolote ,Si Chochote .Vitisho tu.

Yaani wameamua kuweka Utafiti wao Hadharani. Subiri usikie kuwa Sheria mpya ya Takwimu kifungu namba 19 kimekiukwa na gazeti hilo kwa hiyo tunachukua hatua zifuatazo........!

All in Watanzania wameshtuka.Miezi 9 tu yupo nyang'anyang'a

Maana niliwahi kuandika "Misingi ya Urais sio kusakata Rhumba na Pushups majukwaani"-Wasomi Uchwara wakanibishia

Kisha miezi 5 baadae Mhusika Mwenyewe akasema "Kazi hii ni nzito sana ,wakati mwingine najuta kwanini hata niliutaka Urais".Alisema kwa kinywa Chake Mwenyewe.Simjaribu.

Lissu alisema tutamshinda mahakamani na tutamshinda nje ya mahakama.Juzi tumemshinda Mahakamani .Sasa huku nje tuendelee

Kwanza Kuzuia Mikutano ya hadhara namuunga mkono maaana ndio Silaha yake ya Mwisho na Kutisha watu kwa Vyombo vya Dola.Kwani mnadhani angefanyaje kama alijinadi kwenye kampeni kwa Kusakata Rhumba Jukwaani na Push-Ups?

Hivi mnataka katika Mikutano ya Hadhara mkawaeleze wananchi kuhusu ahadi zake wakati ilikua zilongwa mbali,Zitendwa Mbali. ? Haiwezekani kumuweka majaribuni kiasi hicho

Aliahidi kwa kasi sana.Kasi ya Magufuli

1:Nitamaliza Mgogoro wa Zanzibar akiwa anahutubia Bunge lakini baada ya Mwezi Mmoja akapinga

"Mgogoro wa Zanzibar siwezi kuingilia.Kuna mamlaka na tume yake.Atakayeleta Fyokofyoko atakiona cha Mtema kuni".

2:Aliahidi kupambana na Rushwa lakini baadae majuzi hapo akapinga

"Nimempa Trafiki Elfu 5 kwa ajili ya ku-brush Viatu"

Rushwa ikabatizwa jina jema

3 Akiwa Mapumzikoni Geita Alipobanwa kuhusu Mshahara wake akaahidi "Nikirudi Dar nitatoa vielelezo vya malipo ya Mshahara wangu hadharani"

Leo miezi minne Kimya! Yaaani Kimyaaaah! Sasa mnataka mkawaeleze Wananchi?

4:Halafu alipoumbuka hadharani ilikua hivi

"Ni Tanzania Pekee Mwanafunzi anaweza kupata Division Four na kwenda Chuo Kikuu halafu mwanasiasa anamtetea.Hao Wanasiasa ni Vi-La-ZA kama wao"

Bintiye aliwahi kupata Div.IV na Yupo Chuo kikuu UDOM. Yaani hajakanusha,Chuo au Familia Kimyaaah! Aibu hii ndio unataka Upeleke kule?

5: Akiwa Kule Mtwara tarehe 3 Septemba mida ya Jioni Uwanja wa Mashujaa akasema "Nitashusha bei ya vifaa vya ujenzi.Lengo langu pia nyumba za Tembe ziondoke na watanzania waishi maisha bora "

Vifaa vya ujenzi hadi sasa ni ghali na mbaya zaidi kawaambia wananchi waliokumbwa na mafuriko kule Kahama kuwa "Serikali yangu haiwezi kuwajengea nyumba wakati ninyi mmekaa tu"

6:Aliaahidi kupambana na Ufisadi .Sakata la Lugumi Kimyaaah.

-Utekelezaji wa Maazimio ya ESCROW kimyaa.Ndio kwanza IPTL imeendelea kulipwa mabilioni

-Hatua kwa Wanunuzi wa kivuko kibovu kama ripoti ya CAG ilivyoonesha kimyaaah.Maana yeye alikua Waziri mwenye dhamana.Sasa si jipu litumbuliwe?

-Akamfukuza kazi Dr.Hoseah kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU. Lakini mimi nikasema tatizo sio Hoseah bali Sheria na TAKUKURU kutokuwa Independent .Sasa mkurugenzi mpya anaendana na kasi ya Magufuli? Ha ha ha! Wananchi wakaelezwe ?

8: Akasema "nitatoa elimu Bure" na Pia matatizo ya mikopo yatakua Historia.Leo hadi baadhi ya watumishi wanachangishwa madawati naMikopo ya Wanafunzi tatizo liko palepale

9: "Bei ya Sukari itakua bei nafuu na napiga marufuku Sukari kuagizwa kutoka nje"

Leo Bei ya Sukari Wananchi hawahitaji kukumbushwa. Lakini baadae alipiga "Serikali yangu itaagiza sukari kufidia pengo la uhitaji"

10:Nitasimamia Utawala bora wa Sheria .Kisha akaja na " Magari binafsi yanayoingia barabara ya Mwendokasi yang'olewe tairi kisha yapelekwe kituo cha polisi na pale mtapata biashara.Wakija kuuliza kesho yake waambieni yalikuja yenyewe"

11: "Mimi nitakua Rais wa Wanyonge"

Kisha Wanyonge wa kule Msimbazi na Jangwani wakabomolewa nyumba bila fidia na bila decent measures na wengine wakapata fadhaa na majanga mengine

Wanafunzi wa UDOM wakafukuzwa bila staha bila utu kwa makosa yaliyofanywa na serikali.Wakatelekezwa na kudhalilika .Wakalia,Wakaomboleza.Watoto zaidi ya 7,000 wana ndugu ,Jamaa na marafiki waliosononeka.Mnataka mkawakumbushe hasira?

12: "Nitalinda Umoja wa Kitaifa"

-Ghafla akasema "Napenda Vijana Serikalini maana wazee ni wala Rushwa"

Yaaani hii ilikua haina tofauti na Ramli Chonganishi na yale ya wale wanaoua Vikongwe

-Halafu akasema Marufuku mikutano ya siasa hadi 2020

Yaani vyama vya Siasa visipate haki yao kisheria na kikatiba.Akajikuta amezalisha Operesheni UKUTA

Taifa lipo Kwenye Tension

13: Tangu atangaze kuwashusha Wanadamu waishi kama Shetani hata viongozi Decent wa Dini wameacha kujihusisha nae .Labda katika Maombi tu

14: "Tumefika hapa kwa sababu ya Kulindana ,Hilo kwangu halipo na Watanzania mniombee.Kuna majipu nitayatumbua.Nimejitoa Mhanga"

Kisha ghafla akaja na kaulimbiu "Wazee Wangu Mkapa na Kikwete nitawalinda .Pumzikeni kwa Raha Mustarehe"

15: "Kuna mtu anaibia Serikali Milioni 7 kila Dakika ". Wah hebu chukua Milioni 7X60X24 (Siku moja) upate jibu. Halafu kwa sababu huyo mtu ameshakamatwa sasa tuseme tangu akamatwe zimeokolewa Sh. ngapi na zimeelekezwa wapi

16: "Tanzania ya Magufuli ni ya Viwanda"

Hadi sasa Vimejengwa viwanda Vitatu

i) Kiwanda Cha Kuhamia Dodoma

ii) Kiwanda cha UKUTA

iii) Tundu Lissu Democratic Machine Tools

iv) Mikia Productions

iv) Majipu Factory Construction in Progress

Ha Ha ha!

Narudia "Misingi ya Urais sio kusakata Rhumba na Push-Ups Jukwaani". Kama anabisha basi Mnara ujengwe alipozindulia kampeni za Push-Ups.

Aluta Continua,Victory Ascerta....

Ben Saaanane
 
Naona kuna michoro ya takwimu pembezoni mwa hizo picha, yawezekana ndio ushahidi wenyewe huo. Halafu kama wametumia njia za kitafiti za kisayansi zinazokubalika na jumuiya ya utafiti wa kisayansi kwa ufasaha sioni tatizo katika habari hii ingawaje sijaisoma mbali ya kuona hii picha.
Utafiti umefanywa na Afrobarometer tena ripoti ilizinduliwa na Waziri wa nchi Muungano na Mazingira January Makamba.
 
1470567184604.jpg
 
mbona hakuna hata mmoja aliyeleta habari kamiliinaeleza kitu gani....
 
Na mpaka muda huu kuna wanachuo wamegomea kwenda mafunzo kwa vitendo(field) kwa kutopewa hela zao kwa wakati, uliza UDSM yaani ni shida kweli!
 
Hiyo heading tu inatutosha wananchi inaotugusa moja kwa moja haina haja yakulifungua ndani!
 
Yani unajiona umeweka uzi wa kisomi kweli!

Hivi hayo ndio mawazo mbadala wa ccm kweli?

Hii nchi ina laana gani? Kweli think tank wa chama unawezaje kuandika mipasho kama hii? Na kujiita wewe ndio mbadala ccm?

Mungu turehemu
 
Watu walishatabiri kwamba huyu brother wangu atakaa madarakani kwa awamu moja tu ya miaka mitano. Now the dream is coming true. Brother kachokwa haraka sana. Kachuja, kachujuka.
 
Back
Top Bottom