Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Lazima tukubali kuwa kuna watu wanaweza kufanya wanaovyotaka kwenye game pamoja na maelekezo ya Coach. Kocha anaweza kuwaambia wachezaji wapokea mpira ni pass hakuna kuvuta wala chenga lakini kuna wachezaji wanaojiamini na wenye kipaji wanaaminika na timu wanajua kamwe hawatakuja kutolewa wnacheza wanavyotaka.

Leo Hii RA, EL, wanaweza kufamfadhiri Mnyika, moto utakao waka hautakuwa CCM bali wapinzani ndio watakao aanza kuraluana na makucha wakiulizana kwanini umefadhiriwa na EL au RA, kwasababu RA na EL ni vigogo wasioweza kuguswa ndani ya CCM. si unaona sasa hivi magazeti yao yameandika vizuri kuhusu Zitto, umeona kuna maneno CCM? maneno yapo kwa wanachama wa CHADEMA

Zitto kutoa magari kumfadhiri Kafulila anfanya hivyo anajiamini, kwani anajua asset alizowekeza ndani ya CHADEMA, hawawezi kumgusa, si waliona moto wake walipomkataza kugombea uenyekiti ha ha ha Lakini shida inakuja kwa Kafulila na NCCR-Mageuzi, Je urafiki wa Kafulila na Zitto utadumu kwa muda gani? Hautahatarisha nafasi ya Kafulila ndani ya NCCR-Mageuzi huko Mbeleni.

BInafsi naona kufufuka kwa NCCR-Mageuzi, si Ajabu siku mkasikia Mh. Zitto anaongoza NCCR -Mageuzi na wana rudi kwenye nafasi yao ya 1995 and beyond, wee tusubiri, hili fukuto la CHADEMA halitazima hivi hivi let 2011 come (uchaguzi upite)

NO,

Zitto yuko njiani kuelekea CCM.

and

Hell NO

Zitto ndiye amekutana na moto hadi anatishia kujiondoa JF. Ha ha ha, who is smiling now - burger king or McDonald?
 
Huyu Dr. Slaa anatia aibu. Yeye na utu uzima wake, Ph.D yake na umaarufu wake anapelekeshwa na form six failure? Amekwisha huyu, siku zake zinahesabika.


Haya ni maneno ya mwandishi na Slaa hajasema lolote kuhusiana na maamuzi yet unaweza kusema hovyo kama vile wewe umemsikia Slaa anasema ? Hujui kwamba hii nk vita na magazeti yako kazini ?
 
NO,

Zitto yuko njiani kuelekea CCM.

and

Hell NO

Zitto ndiye amekutana na moto hadi anatishia kujiondoa JF. Ha ha ha, who is smiling now - burger king or McDonald?
Yuko huru..kufanya hivyo kikatiba..are teriffied with that move...
 
Yuko huru..kufanya hivyo kikatiba..are teriffied with that move...

Nenda kwenye shule zinazoanza na St .. ukajifunze lugha hii kama una mpango wa kuitumia hapa. Haya mambo ya kutumia muda wako wote madrassa kutengeneza suicide bombs ndiyo yanakuabisha sasa.
 
Nenda kwenye shule zinazoanza na St .. ukajifunze lugha hii kama una mpango wa kuitumia hapa. Haya mambo ya kutumia muda wako wote madrassa kutengeneza suicide bombs ndiyo yanakuabisha sasa.
Wewe mwehu uko terrified na zitto mpaka huna raha utalia go on crying...
 
Bluray pllllllliiiiiiiiz

wewe ulikua unabishana na jamaa hapa unamtetea zitto mpaka ukamwita erratic geneous. leo una kana na watu wakauliza mbona uko detered hivyo au unalipwa. if i remember in your own words if only zitto angejua whats best for him ange kuajili.

Haa hii sasa kama ile cimena ya gwyneth paltrow kila siku ni mpya ya jana yote kaya sahau mjomba tafadhali.

Mkuu,

Tuko pamoja sana. Ile film inaitwa 50 First Dates (2004) na amecheza Adam Sandler (Myahudi) na bibie Drew Barrymore kama Lucy Whitmore.
 
Mkuu,

Tuko pamoja sana. Ile film inaitwa 50 First Dates (2004) na amecheza Adam Sandler (Myahudi) na bibie Drew Barrymore kama Lucy Whitmore.

sawasawa ndio hii umeona jama alivyokua na kazi kila siku kuanza tena somo.
 
Mkuu Geoff, wewe angalia obsessive scenarios ni zitto asubuhi mpaka asubuhi!! Think about it we are slowly acquiring British bull-shit ya ku-dwell na kitu kimoja mpaka inaboa

LOL! labda kwa sababu walitutawala!
 
Haya ni maneno ya mwandishi na Slaa hajasema lolote kuhusiana na maamuzi yet unaweza kusema hovyo kama vile wewe umemsikia Slaa anasema ? Hujui kwamba hii nk vita na magazeti yako kazini ?

Mkulu Lunyungu,
Siku hizi hili gazeti la Wakenya ndio pekee lililobakia kuaminika wanayosema. Wakishaandika wewe subiri tu uone matokeo yake.

Hata hivyo, Dr. Slaa yumo humu mtandaoni, akisingiziwa anaweza kujibu mapigo.
 
Mkuu nadhani huwezi kuweka conclusion kwenye hilo, kwani wanasema wanachama watarudisha kadi lakini bado hawajarudisha kadi, hatujui mtu ametumia kigezo gani kupima kuwa mamia wataudisha hizo kadi na pia kama kweli litatokea hilo kwa hiyo hakuna haja ya mtu kuja kueleza lolote hapa kwani hakuna aliyerudisha kadi bado kwa maana hiyo ni sahihi kusema CHADEMA Kigoma Bado shwari maana hatuna evidence bado

Hizo namba tunazoweka ni utabiri wetu. Subiri kidogo hayawi hayawi yatakuwa.
 
Whatever it is let the people decide on whatever they want. Quiting from one party to another it's normal. Even zitto Kabwe is free to anywhere he likes.
 
Zitto aifadhili NCCR-Mageuzi kupitia kwa Kafulila
zittokabwe.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, ambaye anamuunga mkono aliyekihama chama hicho.
broken-heart.jpg
Na Elizabeth Ernest

NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ametangaza kumuunga mkono swahiba wake David Kafulila kugombea ubunge jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi na tayari ametoa magari matatu kwa ajili ya kumsaidia kujiimarisha jimboni huko.

Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka kwa watu walio karibu na Zitto na Kafulila vinasema kwamba, kiongozi huyo wa Chadema ameamua kumuunga mkono Kafulila ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoka mikononi mwa CCM na kwenda upinzani.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, NCCR-Mageuzi ilishika nafasi ya pili huko Chadema ikishika nafasi ya tatu kwenye matokeo ya ubunge. Katika uchaguzi wa mwaka 2000, jimbo hilo lilichukuliwa na NCCR-Mageuzi kabla ya 2003 kuchukuliwa na CCM katika uchaguzi mdogo.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni, Chadema kilijizolea viti 12, NCCR-Mageuzi 11 na CCM kilipata viti 20. Kulingana na takwimu hizo, upinzani uliongoza.

Mwaka 2005 kama Chadema ambacho kilishika nafasi ya tatu kingeiunga mkono NCCR-Mageuzi, Jimbo hilo sasa lingekuwa katika mikono ya upinzani kwa kuwa kura za kambi hiyo zilikuwa nyingi kuliko za CCM.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Zitto anaamini kwamba, Kafulila ndiye aliyejenga Chadema kama chama ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano na NCCR-Mageuzi katika maeneo ambayo chama hicho kina nguvu.

“Zitto amekwisha weka bayana kuwa katika Uchaguzi Mkuu ujao upande wa jimbo hilo anamuunga mkono Kafulila kwa kuwa anaamini atashinda na kuimarisha upinzani,” kilisema chanzo cha kuaminika.
Maelezo hayo ya Kabwe yamekuja huku Kafulila akijiandaa kwenda jimboni humo kuhutubia mikutano ya hadhara akitumia magari ya Zitto.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa Kafulila ambaye sasa ni mwanachama wa NCCR-Mageuzi ataanza ziara yake mkoani humo Desemba 8, mwaka huu akiwa na viongozi wa kitaifa wa NCCR-Mageuzi.

Kwa mujibu wa habari hizo, Kafulila pia anatarajia kuzungumza na wanachama wa Chadema mkoani Kigoma na kuzunguka maeneo mbalimbali kwa magari ya Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Kafulila aliliambia gazeti hili jana kuwa atatumia magari ya Zitto kwa kuwa ni rafiki yake wa karibu.

“Mimi na Zitto ni marafiki wa siku nyingi, tayari nimezungumza naye na amekubali kunisaidia kama rafiki yake wala sijakodisha," alisema Kafulila jana na kuongeza:

"Amenipa magari yake kwa ajili ya usafiri kwa sababu nitaondoka na watu wangu huku Dar kwenda Kigoma”.

Alifafanua kuwa jambo kubwa analokwenda kufanya Kigoma ni kuwaeleza wanachama wa Chadema sababu zilizomwondoa kwenye chama hicho na hatima yake kisiasa.

Zitto hakupatikana jana kuzungumzia ufadhili wake kwa Kafulila na taarifa iliyopatikana kutoka kwenye familia yake ilieleza kuwa yuko masomoni Ujerumani.

Alipoulizwa kuhusu magari hayo, mama wa mzazi Zitto, Shida Salum alisema kuwa Kafulila na Zitto ndio wanaostahili kuzungumzia suala hilo.

"Mimi siwezi kusema chochote, hawa ni marafiki nadhani wenyewe ndio wanaoweza kuzungumza zaidi," alisema.

Awali mmoja wa wanachama wa Chadema atakayekuwa katika ziara hiyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alieleza kuwa msafara huo utakuwa na magari manane; matatu ya Zitto Kabwe na magari matano ya NCCR-Mageuzi

"Magari hayo yatabeba watu mbalimbali wakiwemo wanachama wa Chadema zaidi ya 50 ambao watatangulia kwa ajili ya kwenda kuandaa mazingira ya kumpokea Kafulila na msafara wake na katika maandamano maalum yaliyoandaliwa kwa ajili yake," alisema mwanachama huyo na kuongoza:

"Kimsingi Kigoma yote hakuna mwanachama wa Chadema aliyefurahishwa na kitendo kilichofanywa na viongozi wa chama hicho kuwaengua na wote wana hamu kubwa kumsikiliza Kafulila".

Alisema katika ziara hiyo, wanachama hao wanatarajia kurudisha kadi za Chadema na kujiunga rasmi na chama cha NCCR-Mageuzi.
Takribani wiki moja na nusu iliyopita, Dk Slaa alifuta nyadhifa za afisa habari wa chama hicho, David Kafulila pamoja na Afisa Mwandamizi wa Bunge na Halmashauri, Danda Juju na kuwa wanachama wa kawaida ambapo baada ya uamuzi huo, Kafulila na Juju kwa nyakati tofauti walitangaza kujiengua katika chama hicho huku Kafulila akijiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi.

Kafulila na Juju walifutwa nyadhifa zao kwa madai kuwa walikuwa wakitoa habari za chama hicho kwa vyombo vya habari kinyume na taratibu, jambo ambalo walilipinga vikali na kudai kuwa walifanyiwa hivyo kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuzungumza ukweli na kutetea haki kwa maslahi ya chama.

Habari hizo zilidai kuwa katika mazungumzo hayo, Dk Slaa alisema kitendo cha Mbowe kumtaka atekeleze agizo lake la kuwafuta uanachama Kafulila na Juju amemfanya aeleweke vibaya kwa watu wake wa karibu.

Habari zilifafanua kuwa Dk Slaa alimweleza Mbowe kuwa shughuli nyingi ndani ya chama hicho anazifanya kwa kujitolea na kwamba kama ni Ubunge angeweza kuupata hata kama angekuwa mwanachama wa chama kingine na kusisitiza kuwa anayoshutumiwa na watu kuhusu uamuzi wa kuwavua nyadhifa Kafulila na Juju aliujua kabla.

Tangu Juju na Kafulila watangaze kujitoa Chadema, Mbowe hajawahi kuzungumza lolote licha ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake ambazo zilipigiliwa msumali na Juju ambaye alidai kuwa kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali(CAG) atakikagua chama hicho na kukuta mambo shwari atakuwa tayari kwenda jela.

Habari zaidi zilieleza kuwa mara baada ya kikao hicho, Dk Slaa wakati anatoka alikutana mlangoni na Muasisi wa chama hicho na Gavana wa kwanza mzalendo Benki Kuu ya Tanzania, Edwin Mtei alimwomba wazungumze, lakini Dk Slaa alisisitiza kuwa ana safari ila baada ya kuombwa kwa muda mrefu na Mtei alikubali. Inadaiwa kuwa mazungumzo yao yalidumu kwa saa mbili.

Habari hizo zilieleza kuwa maofisa wawili wa juu wa chama hicho (majina tunayo) wako katika hatua za mwisho za kujivua uanachama na inadaiwa kuwa mmoja wao ameshaandika barua ya kujivua uanachama kwa madai kuwa mchango wake katika chama umekuwa hauthaminiwi na kwamba shughuli zake nyingi zimekuwa zikifanywa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama hicho, John Mnyika.

Mwananchi lilipomtafuta Dk Slaa kuzungumzia suala hilo, alisema kuwa chama hicho hakiwezi kukaa na kujadili masuala ya Kafulila na Juju kwa madai kuwa ni ya kipuuzi.

“Hivi wewe una cheti kweli cha uandishi wa habari. Nikuulize swali kwamba, hapo kwenu Mwananchi wamefukuzwa watu wangapi tena bila hata uongozi kujua mbona hamuandiki, Chadema tuna mambo mengi ya msingi ya kuzungumza hatuwezi kukaa na kujadili suala la Kafulila na Juju” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“Maswali haya kuanzia leo iwe mwisho kuniuliza, sisi hatuwezi kukaa na kujadili upuuzi wa Kafulila na Juju, tena andika mwandishi wala usiogope; nasema ni upuuzi”

Dk Slaa alisema kuwa ndani ya Chadema mtu yeyote akifanya mambo kinyume na utaratibu lazima achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kufuata katiba ya chama hicho. Alisisitiza kwamba, mambo yote yanayozungumzwa kuhusu chama hicho hayana msingi na yanatolewa na watu wasioipenda Chadema na wanaotaka kukiona chama hicho kikipoteza dira.


nina wasiwasi na habari zinazoandikwa sasa na Mwananchi inaelekea RA ameshawadakisha!

I cant understand why people fail to figure out what is behind all this. Hizi ni pesa za mafisadi (CCM) zinafanya kazi. Hivi what did u expect? CCM waiache CHADEMA's popularity to linger into 2010 at its top gear? Hata hao CCM wenyewe wangejicheka. Am a CCM's dormant member and I know how our party machinery works. Target ya chama letu ni ku-identify opportunists (kama Zitto) kwenye opposition camp and use them. As simple as that.....
 
eeeh watu bwana ingieni na nyie kwenye siasa tuone mazuri na mabaya yenu
tunaongea wee vitendo hafifu
 
Lazima tukubali kuwa kuna watu wanaweza kufanya wanaovyotaka kwenye game pamoja na maelekezo ya Coach. Kocha anaweza kuwaambia wachezaji wapokea mpira ni pass hakuna kuvuta wala chenga lakini kuna wachezaji wanaojiamini na wenye kipaji wanaaminika na timu wanajua kamwe hawatakuja kutolewa wnacheza wanavyotaka.

Leo Hii RA, EL, wanaweza kufamfadhiri Mnyika, moto utakao waka hautakuwa CCM bali wapinzani ndio watakao aanza kuraluana na makucha wakiulizana kwanini umefadhiriwa na EL au RA, kwasababu RA na EL ni vigogo wasioweza kuguswa ndani ya CCM. si unaona sasa hivi magazeti yao yameandika vizuri kuhusu Zitto, umeona kuna maneno CCM? maneno yapo kwa wanachama wa CHADEMA

Zitto kutoa magari kumfadhiri Kafulila anfanya hivyo anajiamini, kwani anajua asset alizowekeza ndani ya CHADEMA, hawawezi kumgusa, si waliona moto wake walipomkataza kugombea uenyekiti ha ha ha Lakini shida inakuja kwa Kafulila na NCCR-Mageuzi, Je urafiki wa Kafulila na Zitto utadumu kwa muda gani? Hautahatarisha nafasi ya Kafulila ndani ya NCCR-Mageuzi huko Mbeleni.

BInafsi naona kufufuka kwa NCCR-Mageuzi, si Ajabu siku mkasikia Mh. Zitto anaongoza NCCR -Mageuzi na wana rudi kwenye nafasi yao ya 1995 and beyond, wee tusubiri, hili fukuto la CHADEMA halitazima hivi hivi let 2011 come (uchaguzi upite)

historia ya NCCR mageuzi itajirudia kiufikia mwaka 2010-that is devide and rule ...kwa kiasi kikubwa kuna nguvu kubwa ya pesa na PR inawekezwa NCCR kwa sasa........je historia ya watu wa kigoma itajirudia????......

KUMBUKENI NCCCR YA MREMA ILIVYOKUWA HOMA LA JIJI......JE VIJANA WA SASA WANAWEZA KUTUFIKISHA KWENYE MOTO WA 1995 MWAKANI???

HISTRIA YA USALITI NI USALITI ....WAPINZANI WANAVUNJWA VUNJWA!
 
Mnapoteza maana ya demokrasia.... kama wapinzani wanaungana mkono kuiondoa CCM madarakani, kinawauma nini? Wawe wa CUF, CHADEMA, TLP au NCCR, wakiungana na kusaidiana, kuna tatizo? Mimi namuunga mkono Zitto kwa kumsaidia Kafulila, kwa kuwa ametamka wazi malengo yake... wapinzani walipokuwa wanahasimiana, mlilalamika. Sasa wanaungana, mnalalamika tena? MNATAKA NINI ninyi binadam MSIOTOSHEKA? Mkiletewa mvua, mnalalamika, mnataka jua! Mkiletewa jua, mnalalamika, mnataka mvua! Waacheni waungane!

Hongera Zitto na Kafulila kwa kuweka MFANO BORA wa ushirikiano katika mapinduzi ya kisiasa nchini! Na wengine nao wafuate mfano wenu!

./Mwana wa Haki
 
Hivi kuna ubaya gani Zitto akimuunga mkono Kafulila ( mkimbizi wa kisiasa) kupambana na CCM? Kama Zitto na Kafulila ni marafiki huo urafiki wao hauwezi futika kwa vile Kafulila amefulia na kijiunga na NNCR-Mageuzi. Ni wajibu wa marafiki kusaidiana. Labda urafiki wao ni kama ule wa JK na EL ambao haukuanzia barabarani. Hata hivyo mimi nilidhani kuimarika kwa upinzani ndio kukua kwa Demokrasia hapa nchini.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom