Kuna habari nyingine ambazo zinachochea migogoro zaidi. Kafulila ni mwanasiasa mchanga, nadhani hajui siasa ni nini. Kwa mwendo anaokwenda nao anaweza kujikuta anajimaliza mwenyewe bila kujua.
Tatizo ninaloliona, kijana anataka kuwa kwenye media akifikiri kwamba inampandisha chati, lakini ukweli ni kwamba media inamuongezea maadui badala ya kumjenga.
Ingekuwa ni busara angeenda huko Kigoma Kusini akasema na wananchi wa huko ambao ndiyo wapiga kura wake. Kuweka habari hizi kwenye magazeti ni kama vile anatumia jina la Zitto kuomba aungwe mkono na supporters wa CHADEMA jimboni. Pia in a way, ni kama anamchonganisha Zitto na CHADEMA.
Anaongelea kuchukua jimbo wakati serikali za mitaa viti 20 vimeenda CCM, na wao (CHADEMA + NCCR) walipata viti 23, je ana uhakika gani kwamba waliopigia kura CHADEMA na NCCR wote watampa kura yeye?
Hakutakiwa ku-reveal details za hiyo safari yake wala support anayoipata toka kwa Zitto. Pili, kutoa habari kama hiyo kunamfanya ajiweke kwenye mazingira ya utata kwa kuwa aligoma kurudisha kadi ya CHADEMA (kama taarifa hizo zilikuwa sahihi). Je, ana uhakika gani kwamba NCCR-Mageuzi watampa nafasi ya kugombea kwenye hilo jimbo? Asije akashangaa ikifika wakati wa uteuzi wakamtema kwa sababu nyepesi sana kwamba hawana imani naye.
Zitto, mshauri rafiki yako kwamba kwenye siasa na hasa kabla hujajenga jina unatakiwa kuwa makini sana. Jina linajengwa kuanzia jimboni kwako na siyo kuanzia kwenye magazeti. Wanaopiga kura ni wananchi wa jimboni, sio sisi wasoma magazeti. Hizo habari za kwenye magazeti zinatoa mwanya wa wapinzani wengine wanaonyemelea hilo jimbo kutafuta njia za kukumaliza kirahisi zaidi.
Atakuja kushangaa atakapokuja kujikuta jina lake limepigwa red na chama chake na wala asijue ilikuwaje. Kwani aliyegombea Ubunge 2005 kupitia NCCR amesema hataki tena kugombea?
Hizi siasa za kwenye magazeti tuwaachie wenyewe wanaojua, wengine naona tunazivamia tu bila kujua how to play the dirty game. Mimi sikumfahamu Zitto wala Mnyika kabla ya uchaguzi wa 2005, nimemfahamu Zitto baada ya kushinda na pia Mnyika nimemfahamu baada ya kuitikisa CCM jimboni Ubungo.
Kwa hiyo a good starting point ni sera zake huko jimboni kwake na siyo publicity kwenye magazeti. Atajimaliza kirahisi sana. Akomae na wapiga kura wa jimbo lake maana ndio watakaomchagua, sisi wengine ni wapiga domo tu.
Pia inahitaji understanding ya hali ya juu na ukomavu wa kisiasa CHADEMA kumwelewa Zitto kwamba hana nia ya kukihujumu chama chake. Pamoja na kwamba lengo ni kuimarisha upinzani, lakini ushirikiano wa dhati kati ya vyama vya upinzani haupo, wao wenyewe wanaonana kama maadui, lakini at personal level watu wanaweza kushirikiana lakini kwa njia za kimya kimya na siyo kuropoka magazetini kama jinsi dogo Kafulila anavyofanya.