Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
katika maisha ya kisiasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu lakini katika hili kuna mtu au taasisi zilizo na maslahi ya kudumu na mh.Nafikiri zitto anayo maslahi ktk kuona chadema inakufa,lakini tutakaopata hasara ni sisi wanyonge wakwti yeye na wenzake wanafaidika .
 
Sasa kabla Zitto hajaiua chadema si chadema wampige chini.Chama cha nidhamu
 
Mmoja anatoka kigoma kusini, mwingine kigoma kaskazini, wa kusini aligombea uenyekiti wa vijana, aliposhinda badala ya kutanganzwa mshindi akaitwa sisimizi, wa kaskazini aligombea uenyekiti taifa, wazee wakamwambia achane fomu. huyu wa kusini na wa kaskazini ni marafiki damu damu, ni 'homeboys', wa kaskazini kaapa kumuunga mkono wa kusini kwa gharama yoyote ile. wa kusini kashatafuta hifadhi, wa kaskazini bado (kidichu) IZ T KILIA NAU?
Yeah.. very clear!
 
Kwa yote yanayomkamkabili Mh. Zito ni sehem ya matunda ya siasa changa ndani ya nchi na vyama vyenyewe. Zito siyo malaika hivyo kuwa na makosa ni moja ya sifa ya kibinadamu lakini ubinadamu wake unakamilika pale anapotambua makosa yake. Nimeuona wasifu huo kwa Zito pekee ndani ya CHADEMA, lakini ninafadhaishwa na utukufu wanaojivika wakuu wengine ndani ya CHADEMA!! Jamani tuwe wakweli kuwa kuna mmomonyoko usiojua nyakati ndani ya CHADEMA, CCM ni chama chenye matatizo makubwa ndani yake hapa nchini ila wao wana sifa mmoja ya kujivumilia katika nyakati maalum. Zito ni kijana mwenzetu, jasiri, mweledi na muungwana, nadhani wasaa umefika sasa kwake kujiweka sawa na kuangalia mbele kwa niaba ya maslahi ya Umma na siyo chama au genge la watu wachache.

Akibaki ndani ya CHADEMA sawa,Akienda CCM sawa, NCCR sawa, akirudi katika uanaharakati vema.

Wana Jf tusimuhukumu Mh.Zitto, tukiangalie CHADEMA kama taasisi dhidi mtu mmoja tu na nguvu wanayoitumia sasa.

All the best Mheshimiwa Zitto, binafsi ninakuunga mkono kwa maono yako kisiasa na kianaharakati. Big up Young Brother
Kati

FDR,

Nimekuwa nikisoma kila kinachoendelea humu. Ni kweli kuwa Zitto ni mtu wa maridhiano. Hili nampa sifa lakini sio maridhiano tunayoyataka TZ kwa sasa. Haya yaende DRC, Burundi na Somalia.

Kinachogomba hapa ni NIDHAMU na UAMINIFU. Zitto ameandika mengi (hasa wakati wa uchaguzi, mimi ndo nilijua upande wa pili wake na nilijidhihirisha kwa i was right kumpinga asiwe chairperson) na wengi hasa magazeti yamemsemea mengi.

Sina sababu ya kumuunga mkono na sina sababu ya kuungana na wengine CHADEMA lakini kama mzalendo halisi hii yote ni sababu ya Zitto. Mbowe amepakaziwa sana ni mwanahalisi tu ameweza kumhoji na akamaliza simply kuwa kuna taratibu za kichama za kumaliza matatizo yao.
 
sisimizi: braza z, tugombee uenyeviti na sisi mwisho wa reli taifa lijue tuumo.
z: emama wacha! Hilo wazo linaonesha kweli umeshiba mawese ya kwetu, mi nigombee uenyekiti taifa, na wewe uenyekiti bavicha!

wenye chama: uenyekiti hauendi popote palle, wewe sito jitoe na wewe sisimisi japo umeshinda, yezu na malia hamna matokeo.

naam, hapa ndipo gogoro lilipoanzia

bonge la ubunifu mpwa... Big up ile mbaya
 
......, sasa hivi kunategemea mtakavyo -deal na hii ishu ya Zitto, msim-underestimate huyu mtajimaliza wenyewe, sasa ondoeni hizi habari zenu kwenye media kwanza, waiteni wale wote waliojitoa muone kama mnaweza kuwarudisha chamani un-conditionally, na ndugu yangu Freeman kama haya maji ni mazito mno basi busara hapa ni kuachia ngazi ikibidi kwa manufaa ya chama.

FMEs!

FMES,

Unakumbuka wakati wa uchaguzi wa CHADEMA? Zitto alimwaga siri hapa. Unajua position yake? Maneno yote kwenye media hajawahi kuyakanusha. Naamini yana ukweli otherwise ngoja arudi bongo.

CHADEMA is a political party is not football club. Kitendo alichokifanya Kafulila na Juju halafu eti warafiki wa Zitto na habari ya Saed Kubenea? Nina wasiwasi mkubwa na Zitto. Zitto anacheza na akili zetu.
 
Hivi hawa kina Mbowe, Dr Slaa, Mtei, Mnyika si member hapa JF,mbona wamekaa kimya siku hizi hawachangii kabisa?
 
Zitto anapaswa kuwa makini na katika kipindi hiki na pia kama kweli ana malengo ya mbali ya kisiasa basi awe karibu sana na viongozi wake wakuu wa CHADEMA na hata kuwasikiliza na kushauriwa juu ya mambo yote ya kisiasa
 
Swali....Hivi ni Zitto tu anapaswa kuwa makini? Hao wengine wanaopita hapa na kwenye magazeti na sasa hadi kwenye LUNINGA wakiendeleza mkakati wao wa "KUMMALIZA" Zitto hawapaswi kuwa makini?

Hivi ungekuwa wewe ungekubali kuona kila unapojitahidi kuonyesha nia ya maridhiano wenzako wanachukulia hilo kama oppurtunity kwao na show of weakness kwako na kuendelea kukushambulia kwa fitina, majungu na hata kashfa kutumia wanachama, wapambe na hata watumishi wao, ungeweza kuonyesha huo umakini ama uvumilivu mnaomlazimisha Zitto kuendelea nao?

Acheni kudanganyika na hao wanaojifanya kuwa wana haiba ya mapenzi kwa Zitto wakati wanamuona ni "gatecrusher" na kauzibe kwa maslahi, ndoto na mikakati yao binafsi ya kisiasa...

Watu wanapofikia kuhack mawasiliano ya wanaomuita "mwenzao" na kujigamba katika vyombo vya habari.....that is the highest level of irresponsibility and insensitiveness to the interests of their party and the whole national agenda (Democratic progress, anti corruption and social economic development) which they like showing that they are championing...

Ndugu zangu, hata kama mna mitizamo tofauti, mmechagua makundi, mmekinzwa na prejudices, mnajaribu kulinda matumaini ya "utume" wa CHADEMA katika kujenga upinzani madhubuti....bado mna jukumu la kuwa objective na ku-question ukweli na ustaarabu kutoka pande zote mbili na sio kwa upande wa Zitto tu....

omarilyas
 
Kumbuka hii ni politics na pia kama akina Dr. Slaa wanapeleka majungu ni humo humo ndani na hawayatoi nje. Ndo maana mtu kama mimi aka sisimizi naona kama nyie ndo wabaya. Msema sana, mbona hao hawasemi? Mbona hakanushi yale yanayozungumzwa?
 
Tanzania, Zitto hakiachi Chadema Mwandishi wetu Juma Nkamia
08/12/2009

Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Zitto Kabwe Zubeiri anasema, licha ya hali ya kutoelewana ndani ya chama chake, hatojiondoa na kwamba hizo ni hisia tu za watu.
kabwe-zitto_0.jpg
Kabwe Zitto Mbunge wa Chadema akiwahutubia wafuasi wa chamaAkizungumza na Sauti ya Amerika, Zitto amesema "kwa sababu watu wamezoea kwamba watu wakigombana, wasipoelewana ndani ya vyama, basi ni lazima mtu atoke ajiunge na chama kingine. Kwa hiyo Siondoki Chadema na ninaendelea kua mwanachama wa Chadema."
Mbunge huyo alisema ni jambo la kawaida kwa watu kutoelewana na kwamba kuna tofauti ya mitizamo ndani ya chama. Anasema kuna tofauti za mitizamo kuhusiana na suala la demokrasia ndani ya chama,kuhusu uwajibikaji ndani ya chama, kuna suala la kuheshimiana ndani ya chama lakini siyo tofauti za kumwezesha kukihama chama hicho.
Zitto anasema "sikujiunga mimi na Chadema labda kwa sababu nilikwenda kwenye kura za maoni za chama kingine nikakataliwa ndipo nikapata hasira na nikajiunga na Chadema, hapana. Nilijiunga na Chadema kutokana na kuamini misingi ya Chadema, walakini ni wazi kabisa kwamba ni lazima ifikiye wakati viongozi inapokua hamuelewani, ni lazima moja apishe nagfasi ya wengine watekeleze majukumu yao."
Amesema ikiwa ataondoka, basi ataondoka kakutoka uwongozi lakini si uwanachama. Na anasema hamini nadharia ya kuhama chama, kama vile alivyo pinga kuhama kwa Thomas Kashilila na kujiunga na NCCR Mageuzi.

source.VOA/SWAHILI

Omary, whats the meaning ya hiyo yenye red?
Wote tunajua kuwa alieenguliwa kwenye kura za maoni CCM na kuingia CHADEMA ni Dr.Slaa, sasa Zitto anafikisha ujumbe gani hapo?
Ina maana yeye hadhamini mchango wa watu wengine ambao walikuwa nje ya CHADEMA hapo kabla?

Mshauri najua huwa anakusikiliza kuwa uongozi ni pamoja na matamshi unayotamka yanaweza yaakamfanya mtu mwingine akawa na hasira na badala ya kiusema mazuri juu yako akawa anasema mabaya juu yako na ikifikia hapo ujue kuwa mabaya ni mengi kuliko mazuri na mabaya yana tabia ya kupendwa kusikilizwa zaidi ya mazuri.
 
Kumbuka hii ni politics na pia kama akina Dr. Slaa wanapeleka majungu ni humo humo ndani na hawayatoi nje. Ndo maana mtu kama mimi aka sisimizi naona kama nyie ndo wabaya. Msema sana, mbona hao hawasemi? Mbona hakanushi yale yanayozungumzwa?

Atakanushaje pengine yuko chini ya amri sasa hivi. Siasa ni mbaya hasa ukijichanganya.
 
Omary, whats the meaning ya hiyo yenye red?
Wote tunajua kuwa alieenguliwa kwenye kura za maoni CCM na kuingia CHADEMA ni Dr.Slaa, sasa Zitto anafikisha ujumbe gani hapo?

Ina maana yeye hadhamini mchango wa watu wengine ambao walikuwa nje ya CHADEMA hapo kabla?

Mshauri najua huwa anakusikiliza kuwa uongozi ni pamoja na matamshi unayotamka yanaweza yaakamfanya mtu mwingine akawa na hasira na badala ya kiusema mazuri juu yako akawa anasema mabaya juu yako na ikifikia hapo ujue kuwa mabaya ni mengi kuliko mazuri na mabaya yana tabia ya kupendwa kusikilizwa zaidi ya mazuri.

Hapana kaka, ni wazi Zitto alikuwa ansisitiza loyality yake kwa CHADEMA.

Lakini hata hivyo ni muhimu kujua kama mahojiano hayo yalifanyika kabla ama baada ya Dr Slaa kusema aliyoyasema mbele ya waandishi na hata katika luninga ambapo alifikia kumhukumu Zitto kuwa kwa kuwa hajibu hizo tuhuma zao basi moja kwa moja anakuwa na hatia na vijeme vingine kadhaa. Mbaya zaidi akamuingiza mama yake Zitto kwa mambo ambayo yalisemwa katika mazingira ya kuaminiana.

Jamani Zitto anaheshimu sana wazee sio tu wa CHADEMA bali hata walioko CCM. Na ni mengi ameyafanya ama amekubali kuyafanya kutokana na heshima aliyonayo kwao. Sasa wakati mwengine Wazee nao huwa wanakuwa na jukumu la kulinda heshima hiyo. Wanaposhindwa na kurudiarudia kumgonga vijembe kijana wao Zitto, tusitegemee na yeye ataendelea kunyamaza tu. Inafika mahala na yeye Zitto uvumilivu unamshinda. Kama umewashinda wazee hao ni wazi kijana kama yeye yupo prone zaidi kushindwa pia....

Ndio maana nikasema, uvumilivu, umakini na ustaarabu ni jukumu la wote....

omarilyas
 
Atakanushaje pengine yuko chini ya amri sasa hivi. Siasa ni mbaya hasa ukijichanganya.

Sasa huyohuyo mnataka awe makini, asijibizane, awe mvumilivu na bado mnataka kumhukumu kwa kukwepa kufanya msiyoyataka....kukanusha - kujibizana na hao wanaomtuhumu na kumfitini kila kukicha. hivi akiamua kujibizana nao atakuwa anajenga ama kubomoa chama chake? hivi leo Dr Salim akisimama na kuanza kukanusha yote waliyo na wanayoendelea kuchimba, kumfitini na kumkashifu atakuwa anajenga ama anabomoa CCM. Ina maana kunyamaza kwake ni ishara ya kuwa na hatia.....this is worse than mob justice we see being legitimized in our streets...Tuepuke na utamaduni huu wa kuwahukumu watu kwa ukimya, ustahi, umakini na hata uvumilivu wao. Tusipofanya hivyo tutakuwa tunaendeleza utamaduni wa siasa chafu/hovyohovyo unaweka mizizi katika nchi yetu...

omarilyas
 
Josephat Isango

NITASEMA ukweli daima, ili taifa la Tanzania, linufaike liendelee kudumu. Ni tendo la ukatili sana, ambalo hufanywa na wale tu wenye dhamiri za pekee, ambao kwa kawaida tunaweza tukawaita kwa jina moja tu la ukatili.

Nahitaji ujasiri wa pekee sana, usio na dalili ya hofu kuwadhulumu watu pesa ya kununulia sanda siku ya msiba, hapo kutakuwa na maswali mengi sana kwa sisi wanafalsafa.

Ina maana huyu mtu hajui unyeti wa jambo hili? Na kama anajua kwanini anafanya hivi? Aidha, amekusudia au hajui analolitenda.

Kama anajua anafanya nini mbona anaendelea?

Mateso makubwa yaliyopo kwa Watanzania kwa miongo mingi sasa, yanahitaji wanasiasa makini, wasiotaka kutekeleza matakwa yao binafsi ila matakwa ya Watanzania.

Tumeteseka sana, tunazidi kuteseka, huku kila mmoja akijaribu kuonyesha kuwa kuna ombwe la uongozi katika nchi yetu.

Lakini kwa busara tu hatuwezi kukaa bila uongozi, sasa inapokuwa wale waliotuhadaa tukawaamini tukawapa dhamana wanatusaliti katika wakati muhimu tuwaeleweje?

Akili ya Zitto Kabwe imehasiwa sasa, inatazama kwa macho ya makengeza. Au kama haijahasiwa na kuona kwa macho ya makengeza basi kuna mkakati maalumu wa makusudi wa kuharibu harakati za ukombozi wa Watanzania zinazofanywa na mwanasiasa huyu kijana.

Zitto, Mbunge kijana na mwanasiasa machachari aliyeibukia CHADEMA anawachanganya Watanzania. Aliwahadaa Watanzania wakamwamini, wakajua ni kijana mpiganaji, asiyehongwa na yupo kwa ajili ya wanaoteswa, au wanaokandamizwa. Na kweli ni mzalendo anayepigania ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa mafisadi.

Tupo msibani katika safari ya ukombozi, tumechanga pesa ya kununua sanda, Zitto anataka kutudhulumu kwa kuwa kabla ya msiba tulimwamini kuwa ni mwaminifu, ni wa nyumbani, na pesa kiduchu ya kununua sanda isingeweza kumtia kiwewe apate tamaa ya kutusaliti.

Zitto anajua alivyokuwa kivutio kwa Watanzania kwa kukubali kusimaishwa ubunge kwa kusimamia ukweli. Zitto anajua wazi umaarufu wake ulivyoporomoka baada ya kutetea Dowans, kampuni dada ya Richmond iliyo kampuni ya kitapeli.

Zitto hana shaka kuwa umaarufu wake ndani ya chama ulivyoporomoka baada ya kuhusishwa na njama za kuharibu kwa makusudi uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ili ahakikishe kuwa kipenzi chake David Kafulila anashinda uchaguzi hata kwa njia zisizo halali?

Vijana wakajiuliza, tutalaani vipi vitendo vibaya vya CCM ikiwa vitaota mizizi katika chama makini? Wakapiga kelele, msimamizi wa uchaguzi akafuta matokeo, na Zitto akatoka ukumbini kwa aibu.

Sasa mjadala umeanzia tena kwa Kafulila huyu huyu, ambaye ametenguliwa kuwa Ofisa Habari wa chama, imekuwa gumzo, tena uongozi wenyewe ni wa kuteuliwa.

Hivi iliandikwa wapi kuwa Kafulila ni lazima awe kiongozi tu katika CHADEMA, na kuwa akiondolewa uongozi itakuwa dhambi?

Hatuwezi kufikiri kuwa yule aliyekuwa amemteua ndiye aliyekuwa na uwezo wa kutengua uteuzi? Kwani Kafulila alikuwa kiongozi kwa kupigiwa kura? Na hata kama angekuwa kiongozi wa kupigiwa kura, je, anapotenda kinyume cha utaratibu asingeonywa?

Imefikia hatua tuhoji sasa, je, Zitto anataka tuamini kipi? Yeye ndiye aliyefundisha na kuwasadikisha Watanzania kuwa CHADEMA ni chama safi, na ni yeye huyo huyo anaibuka na mikakati mibovu kuibomoa.

Haihitaji mwekezaji kutoka nje ya Tanzania kuelewa kuwa Zitto anasaliti Watanzania katika safari ya ukombozi.

Kila mara Zitto anasema yupo pamoja na wanyonge na wanaoonewa.

Ifike mahali tujiulize, yupo pamoja nao lini? Yupo pamoja nao wapi? Yupo pamoja nao kwanini?

Na yupo pamoja nao yeye na nani? Na je, yupo pamoja nao kwa kujitegemea au anategemezwa?

Zitto yupo pamoja na Watanzania katika kukomboa nchi kwa kuwa yupo na Kafulila tu?

Watanzania wameipenda CHADEMA, Zitto ni shahidi kuwa siku alipoonyesha kutofautiana na Mbowe, siku walipopatana baada ya uchaguzi kuna mama mmoja pale Dar es Salaam alipowaona katika msafara alishuka katika gari lake la kifahari akibubujikwa machozi na kuwakumbatia huku akiwabariki na kuwatakia mema katika safari ya ukombozi.

Ilikuwa ni mojawapo ya ishara, kati ya ishara nyingi za Watanzania kuamini kuwa CHADEMA sasa ni mkombozi wao, wala hakuna anayesema mkombozi wao ni Freeman Mbowe, wala Arfi, wala Dk. Slaaa, wala Zitto Kabwe, wala Kafulila, wala Tundu Lissu.

Ila tumaini lao ni CHADEMA, maana CHADEMA bila Mbowe, Dk. Slaa, na wengine bado inawezekana na itaendelea kuwepo. Hii ni taasisi.

Wananchi wamewekeza katika sera nzuri za chama, hawajawekeza kwa watu moja moja. Watu wanapita, wanazeeka, wanafariki, wanajiondoa uanachama n.k. hivi ilikuwaje Zitto akawekeza akili zake kuwa mafanikio katika CHADEMA ni mpaka kafulila awe ofisa habari wa chama pale makao makuu, na kuwa akiondolewa inabidi yeye aandike barua ya kuacha madaraka yote, yakiwamo ya ubunge? Kama Zitto haamini haya, apite sasa katika maeneo alipokuwa maarufu anone kama hatazomewa.

Ifike mahali Zitto aache tabia ya uvuguvugu. Awaambie Watanzania anataka nini? Yupo pamoja nao katika safari ya ukombozi au amewaacha. Na kama amewaacha aeleze kwa nini anaacha wakati huu uchaguzi mkuu unapokaribia?

Ifike mahali Watanzania tujiulize, kijana huyu amegeukaje haraka hivi? Inawezekena hakuwa mpiganaji makini na mzalendo, au amenunuliwa na CCM, na kama hajanunuliwa basi anataka anunuliwe muda huu na CHADEMA kwa lengo la kuwalingishia wana CHADEMA umaarufu ambao wamempatia, kwa ushirikiano wao alipokuwa kabla na wakati akiwa mbunge ndani ya chama.

Hivi Zitto angeweza kufundisha mambo ambayo yeye mwenyewe hayasadiki? Kama hakuyasadiki kwa nini alifundisha? Ni mfano wa wachezaji fulani maarufu ambao wanaweza kuringa kucheza siku ya mechi kwa visingizio kibao ili wabembelezwe, wanunuliwe, na wapewe peremende na maji ili kuwaomba waingie uwanjani. Hawachezi kwa uzalendo, wanacheza kwa kuwa wamepewa pipi, hivyo siku tukikosa pipi hawatashirikiana nasi. Si wachezaji wa kutumainiwa.

Ilikuwaje Zitto ashindwe kuamini kuwa nguvu kazi ya vijana wenye ushirikiano ndani ya CHADEMA waliokuwa wakifanikisha kumpatia yeye ushindi katika mambo muhimu apeleke bungeni, ndio wale wale wanaofanikisha kutafuta mawasiliano kutoka kwa marafiki zake wanaoandaa njama za kuiangamiza CHADEMA kwa kuwa wamelipwa ili kuzorotesha nguvu ya ukombozi?

Zitto inafaa ajulikane sasa, kama ni wa moto au baridi, lakini vinginevyo kwa uvuguvugu alionao, si muda mrefu Watanzania watamtapika katika siasa za ukombozi.

Safari ya ukombozi ni ndefu, Watanzania wamechoka, na hawatahofia mawimbi yoyote, kwani ndiyo safari ya ngalawa yetu ya umma.

Umaskini wa Watanzania, na haja ya ukombozi wao vitakuhukumu. Tafakari chukua hatua, kama upo tayari kutudhulumu pesa ya kununulia sanda katikati ya msiba ili tukuelewe.

Tutakuelewa tu upo upande gani na kwa nini.

Wala haihitaji mwekezaji kujua kuwa ama umehongwa, ama unataka kuhongwa!

Ni dhambi gani kubwa unayotaka kuitaja kuwa ndiyo chanzo cha kupoteza uzalendo wako, ili uwaache Watanzania katika safari yao ya ukombozi?

Kusingizia kuacha siasa ni kutuambia kuwa ulichokuwa unakitafuta umekipata, na hauna haja tena na ukombozi wa Tanzania. Hata hivyo wanafalsafa tunakutakia kila jema katika maamuzi, na tunakuomba radhi kwa kukuambia ukweli. Maana ni heri ya ukweli unaouma kuliko uongo unaofurahisha. Tulaumiane katika ukweli, kuliko kupendana katika fedheha.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom