Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 580
Source : Mwananchi kwenye habari ya DCI Manumba .......
......
"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.
Chadema ni taasisi..Hivyo hata kama Zitto akitoka na atoke...Hakika Chadema itaendelea kuwepo...na itazidi kupata umaarufu...Whos Zitto By then..Let Him go even 2day..Hell....Alafu wee...Kubwajinga ni Jinga Kweli kweli do u think Chadema ni Zitto only,...Jinga Kabisa wewe.....Na Mwandishi wetu
7th December 2009
Asema zipo njama kuhamisha ajenda ya ufisadi
Adai kunasa mawasiliano ya Zitto na mwingine
Ajigamba Chadema hakina mgogoro, kipo imara
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na Zitto Kabwe.
Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, amesema kuna vita kali sasa ya baadhi ya watu kufanya njama za kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuzungumzia masuala ya mbunge wao, Kabwe Zitto.
Nadhani sasa Watanzania wanatakiwa wakaelewa naona sasa kuna vita kali ya kuiondoa ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, na sasa wanataka kutuelekeza kumjadili mtu, Zitto.
Na mimi nasema hatuhitaji kujadili watu isipokuwa chama, alisema Dk. Slaa wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: Chadema hakina mgogoro na kipo imara na hiyo ilithibitika wakati na baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Septemba, mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu madai ya Zitto kutembea na barua ya kujiuzulu Chadema, Dk. Slaa alisema ofisi yake haijapata barua, maelezo yoyote au ushauri kutoka kwa Zitto unaoelezea suala hilo.
Hatuwezi kuendelea na mambo haya ya kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuanza sasa kujadili suala la mtu binafsi, kama ambavyo sasa inaanza kujitokeza, alisema.
Alisema Chadema ni taasisi itaendelea kuwepo hata kama yeye ama Mbowe (Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho) au Zitto wataondoka katika chama hicho.
Alisisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote licha ya baadhi ya watu kuanza kudhoofisha ajenda hiyo.
Akifafanua kuhusu suala la Zitto, Dk. Slaa alisema siku moja saa 1:00 jioni kabla ya Mkutano Mkuu wa Chadema uliopita, alipata nafasi ya kuzungumza na mama ya Zitto, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Shida Salum, aliyemhakikishia kwamba Zitto hahusiki na mambo hayo.
Siku moja kabla ya Kamati Kuu, niliongea na mama yake Zitto na akanihakikishia kwamba hahusiki na mambo haya yanayojitokeza ya kukichafua chama, alisema.
Alisema alielezwa na mama huyo kuwa wapo watu wanaomtumia Zitto kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kwamba mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayo password ya anuani ya barua pepe ya Zitto ambayo anaitumia kuandika taarifa mbalimbali alizoeleza zinaonyesha kama vile zinatoka kwa Zitto.
Lakini alisema baada ya mazungumzo na mama huyo, kesho yake gazeti moja lilikuwa na habari ya Zitto kukanusha kwamba hahusiki na suala la David Kafulila isipokuwa watu wametumia jina lake.
Dk. Slaa aliongeza baada ya mazungumzo hayo, asubuhi yake alipata taarifa za barua pepe kutoka kwa Mtanzania mwema zinazoonyesha mawasiliano kati ya Zitto na mtu mmoja (jina linahifadhiwa).
Bila kueleza kwa undani taarifa mbalimbali zilizokuwemo katika barua hizo pepe, alisema kwa kifupi kwamba zilikuwa zikionyesha mawasiliano ya kichama kati ya mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam na Zitto ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Ujerumani.
Alisema baada ya kuzisoma aliwasiliana na mkazi huyo wa Dar es Salaam akitamka athibitishe iwapo mawasiliano hayo ya barua pepe yalikuwa ya kwake au la.
Alisema alifanya hivyo kwa kumtumia ujumbe na baada ya muda mkazi huyo alimpigia Dk. Slaa, na akathibitisha kwamba anazitambua barua hizo na mawasiliano hayo yalikuwa ni ya kwake.
Lakini baadaye katika mazungumzo yao ya simu, mkazi huyo wa jijini alimweleza Dk. Slaa kwamba ameingilia mawasiliano yao binafsi, jambo ambalo alilipinga.
Nilimweleza mkazi huyo kwamba sijaingilia mawasiliano binafsi, kwa kuwa taarifa zilizokuwa zikizungumzwa katika barua hizo zilikuwa zikikihusu Chadema na kwa maana hiyo hazikuwa binafsi, alisema.
Alisema baadaye mkazi huyo alimjibu Dk. Slaa kwamba anafanya kazi katika kampuni kubwa na kwamba Dk. Slaa hataiweza na afadhali aache.
Aliongeza baada ya gazeti moja kuchapisha habari za Zitto jana, alimtumia Zitto ujumbe wa barua pepe akitaka maelezo kuhusu habari hizo zilizodai kuwa anatembea na barua ya kujiuzulu Chadema.
Dk. Slaa alisema tangu alivyomtumia ujumbe huo jana asubuhi, hajapata majibu yoyote hadi alipowasiliana na Nipashe saa 11:00 jana jioni.
CHANZO: NIPASHE 12/07/2009
Strong point Kigogo,na aende zake!huyu aondoke bana anatuvuruga tu akili hapa...Kwani ZITTO nani?he is just another sisimizi ..nenda mwana kwenda wafuate wenzio wakina kafulila
Wanasiasa wa Tanzania bwana, yaani mtu anatoa an open ended statement kama hiyo. Mbunge wa kutumainiwa huyu.
Aliyekuwa anajenga suspense kwa kusema "I'm gonna do a song, that you have never heard before" alikuwa James Brown, na ile ilikuwa showbizz, sasa hizi rants za ki showbizz zinatoka wapi katika siasa zetu?
What am I talking about, as if Siasa is not the low end of showbizz.
Sasa hapa kawaachia watu interpretation.Wanaotaka kusema Zitto anataka kunywa vidonge sawa, wanaotaka kusema Zitto anataka kumcharanga mtu risasi sawa, maana kasema anataka kufanya kitu ambacho hakijawahi kufikiriwa bila kukisema specifically, hata kutoa hint tu.
Huyu huyu mtu analalamika waandishi wanavyomuandika, halafu hapo hapo anawapa an open ended quotation, open to any interpretation, ammunition for some more malicious articles.Huyu mtu yuko serious kweli au ana enjoy hii attention (any publicity is good publicity style)?
Emotional instability ikikufanya uwe controlled na story badala ya wewe kui control story unaonyesha jinsi usivyo na uwezo wa kuongoza.
May be uamue kujinyonga ndo tutakushangaa, mengine yoyote utakayoamua ni ya kawaida tu kwa binadamu, we hautakuwa wa kwanza kuamua yafuatayo.
- Mkuu Lunyungu, heshima mbele sana toka niingie JF sijawahi kuona ukiwa emotional like this, ninasema hivi kama kuna waliokuelewa hakuna wa kunizidi, na umenikumbusha tulipoongea kwa simu last time ukiwa kwenye uchaguzi Biharamulo, bado sijahau swali moja uliloniuliza kwamba all the games CCM played katika kuidhinisha ugombea wa Oscar, ili iwe nini?
- Maneno yako yote hapo juu ni 100% right, Chadema ikifa then itakuwa nini? Sidhani kama wengi tunajiuliza maswali serious namna hii, nimesema mara kwa mara kwamba kama sio Chadema, leo serikali ya CCM ingekuwa inatuchapa viboko bara barani!
- However: Kuharibika kwa hewa huko Chadema sasa hivi, ninawalaumu sana wazee wa huko kwa kukosa busara nzito za kuendesha siasa za taifa kichama, hakuna modern tactics, hakuna smart political strategies, huko Chadema inaonekana wanachama na viongozi wanajiendea tu na kufanya anything, I mean mwanachama mdogo sana na wa kawaida ana nguvu za ajabu za hata kuweza kuitisha press conf. na kusema siri nyingi za chama, sasa you wonder amezijuaje kama zinatakiwa kuwa siri tena za juu?
- Freeman amejitahidi sana lakini na yeye anafika mahali anahitaji msaada, bado ni mchanga pia kisiasa na hasa busara za siasa za taifa, mnamnyima Zitto uenyekiti, sawa mlitakiwa kutathmini matokeo bila kuwa bias, mlihitaji a devil advocate wa kuweza kuwaambia msiyoyataka, kwamba Zitto ni maarufu na yuko juu sana kisiasa, sasa kwa sababu hamumpi uenyekiti, basi mpeni hata umakamu, au kama hamumutaki kwenye chama, basi mruhusuni agombee mkamchinje kwenye majukwaa na uwe ndio mwisho wake kisiasa, lakini kwa mnayoyafanya sasa hivi, sio siri kwamba mna safari ndefu sana kwa sababu mmeshindwa kutathmini the effect ya Zitto na kukosa uenyekiti, sasa mzimu wenu wenyewe unawala!
- Sijawahi kuona siasa foolish kama hizi mnazozifanya sasa, unamnyima kiongozi maarufu wa chama chako kugombea nafasi kubwa, halafu unaanza kumnyanyasa kwa njia za kijinga jinga ambazo hata ukiulizwa na wenye akili nyingi huwezi kuzi-defend, wala kuzi-define ukaeleweka, hujui kwamba in-the process unazidi kumjenga, huku ukikaribisha unwanted attention ndani ya chama chako, sasa unaona kina Manumba wameshaanza kujisogeza pole pole, the next thing utamsikia Hosea akija huko kunusa nusa halafu mtaishia kulaumu kila mtu isipokuwa nyinyi wenyewe ambao ndio hasa chanzo cha huu upuuuzi!
- Mkuu Lunyungu, hapa niko na wewe kwamba Chadema wanahitaji kuweka sawa nyumba yao, a house divided against itself haiwezi kusimama na kutusaidia taifa, wazee huko Chadema hebu kaeni chini na Zitto, mumsikilize anasema nini na anataka nini, sio lazima mumpe kila kitu anachotaka lakini ikibidi mkutane kati kati basi, na kufanya hivyo kwenye siasa sio kushindwa wala ujinga ndio smart modern politics zinavyotaka, ninarudia tena maneno yangu ya juzi kwamba Chadema, kukua kwenu na kufa kwenu, sasa hivi kunategemea mtakavyo -deal na hii ishu ya Zitto, msim-underestimate huyu mtajimaliza wenyewe, sasa ondoeni hizi habari zenu kwenye media kwanza, waiteni wale wote waliojitoa muone kama mnaweza kuwarudisha chamani un-conditionally, na ndugu yangu Freeman kama haya maji ni mazito mno basi busara hapa ni kuachia ngazi ikibidi kwa manufaa ya chama.
- Hivi Chadema mmeshawahi ku-imagine mkifa mtakuwa mmetufanyia nini wanachi wa Tanzania? I mean inasikitisha sana eti! Dr. Slaa kwa kusema haya uliyoyasema hadharani exactly unategemea ku-accomplish what? Mawasiliano ya siri ya Zitto yanayolindwa na sheria ya jamhuri kama haki zake za kibinadam wewe umeyapataje kama hukuvunja haki zake kisheria? Hivi huko chadema hakuna washauri wa siasa wala sheria?
Respect.
FMEs!
DCI: Zitto, tuletee tuhuma za chademaNa Ramadhan Semtawa
SIKU chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kulalamika kuingiliwa kwenye anuani yake ya barua pepe, Jeshi la Polisi limesema kuingilia mawasiliano ya faragha ya mtu ni jinai na kumtaka mwanasiasa huyo atoe taarifa polisi ili waanze kulishughulikia.
Zitto, ambaye yuko Ujerumani ambako anasoma, alikaririwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akidai kuwa anaingiliwa mawasiliano katika anuani yake ya barua pepe (e-mail), kitu alichosema ni aghalabu kufanywa hata na Idara ya Usalama wa Taifa.
Zitto, ambaye juzi alituma barua pepe kwenye gazeti hili kulalamikia kitendo hicho huku akitangaza kutembea na barua ya kujiuzulu uongopzi Chadema, alieleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho alidai kinafanywa na chama chake.
Hata hivyo, DCI Manumba alipoulizwa jijini Dar es Salaama jana kuhusu malalamiko ya Zitto, alijibu: "Sisi hutujapata rasmi malalamiko hayo, lakini akileta tutachunguza kwa kuwa si sahihi kuingilia mawasiliano ya mtu."
Kwa mujibu wa DCI Manumba, mawasiliano ya barua pepe na mengine ni faragha hivyo ni makosa kwa mtu yeyote kuingilia mawasiliano ambayo hayamhusu.
"Kwa kawaida ni makosa kuingilia mawasiliano ya mtu siku zote tukipata taarifa kama hizo tunachoweza kufanya ni kuchunguza kuthibitisha kwanza kwani ni suala kitaalamu zaidi," alifafanua DCI Manumba.
DCI aliongeza kwamba, siku zote wamekuwa wakichunguza malalamiko yote yanayofikishwa kwao kama yanahusiana na uingiliaji wa faragha ya mtu ikiwemo mawasiliano yake.
Alifafanua kuwa iwapo mlalamikaji akifikisha malalamiko yake, wao huwa hawasiti kuchunguza bila kuangalia jambo lenyewe lina mlengo gani.
"Ni sawa na mtu akimpiga mkewe sisi tukiletewa taarifa, kwanza tunachunguza halafu tunachukua hatua za kisheria kwa mhusika baada ya kujiridhisha. Kwa hiyo hata yeye (Zitto) akileta tutachunguza," aliongeza.
"Siku zote tunafanyia kazi taarifa zinazotufikia, kama kuna mtu anazo taarifa akileta kwamba mawasiliano yake yameingiliwa tutafanyia kazi tukio hilo ili kujiridhisha."
Malalamiko ya Zitto yalitokana na taarifa iliyotolewa na chama hicho kilichodai kuwa ofisa habari aliyetimuliwa, David Kafulila anatumia anuani ya barua pepe ya Zitto visivyo halali. Kafulila na Zitto ni marafiki wakubwa.
"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.
Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema na kwamba "wanapaswa waniache nipumzike na kufanya mambo yangu".
"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha," alisema.
Katika kuonyesha kuchukizwa na baadhi ya taarifa alizoziita za kizushi zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si Mwananchi), Zitto, alisema: "Faragha yangu ni faragha yangu, Zitto ni Zitto kama yeye na siyo mali ya Chadema.
Akizungumzia uhusiano wake na Kafulila aliyehamia NCCR-Mageuzi kutoka Chadema, Zitto alisema: "Siku zote msimamo wangu umekuwa kwa wale wanaokandamizwa... na katika hili David (Kafulila) ndiye anayekandamizwa."
Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema katika kufanya mambo yake.
"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha yangu."
"Msimwandame Kafulila. Mumwache mtoto wa watu. Mmeshamwita sisimizi inatosha. Msijaribu kunigombanisha na Kafulila. Sitaki... sitaki... sitaki," aling'aka Zitto
SRC
MWANANCHI
cHADEMA WAMECHANGANYIKIWA.CHAIRMAN KIDATO CHA NNE NA KATIBU ANA MZIGO FEKI(PhD).KAZI KUBWA.