Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
HM HAFIF,
huna point wewe.unaonekana ni mhindi tu mshangiliaji.tuachie nchi yetu we nenda kaangalie kina amitha bartchan na mithun then ukalale.AFRICA IS FOR AFRICANS,BLACK AFRICANS..
 

Other ni kuwakomalia haachii ngazi kitu ambacho wananchi hawafikirii mpaka wachukue uamuzi ambao wananchi hawakufikiria.
 
Mie nafikiri atambadili dini TUMAINI na BARUBARU ili waungane na David Kafulila kwenye chama chake kipya na dini yake ya Kikristo (kama sikosei).

Tumaini na Barubaru anzeni kujifunza kusali na MASHOGA wa ANGLICAN hihiiiiiiii 🙂

Ila mkiwa huko mkae vizuri maana mkijisahau, kinyani kimewapitia kati ya miguu.

Tumaini na Barubaru .............................. wenye wivu wajinyonge 🙂
 
Unaongee nini wewe?
nafikiri kichwa chako nimejaa hewa??
 
Hii picha utadhani wanaambiana;
S:Bwa mdogo, hii message iliyoko humu ni ya kwako au ya sisimizi?
Z: We mzee vipi? Niachie nasema, ohoo!

teh teh teh teh
Hii kali sana
 

Yap kama wanakuzingua sana mkuu zito we ishia tu huko huko German then uongeze nguvu ya kurusha makombora ya masafa marefu na mbali kama mzee Mwanakijiji....
.....
 

Tatizo ni baadhi ya watu kutotaka kusoma yale wasiyopenda. Kama habari si sahihi, anayeweza kukanusha ni Zitto. Na si kukanusha tu bali kulishitaki gazeti la mwananchi kuandika uongo dhidi yake (Zitto). Sisi wengine kuanza kulishambulia gazeti la mawananchi hatutendi haki.
 
Zitto atoke atupishe na chama chetu...hatuwezi kujenga nidhamu ya chama kwa kuwa na watoto wajeuri jeuri tu kwa umaarufu walioupata ndani ya CHADEMA..Atoke akiache chama chetu na hakitakufa ....maamuzi yasiyofikirika ndo yapi?na ayafanye basi
 

Uchambuzi wako unafanana kabisa na jina lako.Mbona wewe hujakaa kimya halafu unamtaka Dr Slaa kukaa kimya!

Hivi unafahamu kuwa ukimya unaweza kutafisirwa kuwa ni a silent yes?Tongoza msichana halafu akae kimya....ni rahisi zaidi kusema hapana kuliko ndio,and for that matter ukizushiwa jambo kisha ukakaa kimya watu wanaweza kuhitimisha kuwa umeafikiana na tuhuma hizo.Mfano mwepesi ni wa Tiger Woods....

Sophia Simba anavyoendekeza mipasho huko UWT na as Waziri mwenye dhamana ya kupiga vita ufisadi,ni sawa kwako.Makamba anapotukana wana-CCM wenzie kwa vile tu wanasema Kikwete dhaifu,ni sawa kwako.JK alivyorudi leo na kuongea pumba kuwa wanaomtaka awajibike wana chuki nae,ni sawa kwako.Ila Slaa,as Katibu Mkuu wa Chadema,wadhifa unaompa jukumu kama la Makamba,akisema inakuwa nongwa.

Yani kuna watu kama wamerogwa na CCM.Yaani pamoja na mateso yote haya,ujambazi wote huu,dharau zote hizi,bado kuna wanaotaka kuiona CCM ikiendelea kutubaka milele huku vyama vingine vikinyong'onyea....

Safari ya ukombozi wa Mtanzani bado ni ndefu san with reference ya mentalities kama za Kubwajinga
 

Zitto fatigued yet?
 


- Mkuu Lunyungu, heshima mbele sana toka niingie JF sijawahi kuona ukiwa emotional like this, ninasema hivi kama kuna waliokuelewa hakuna wa kunizidi, na umenikumbusha tulipoongea kwa simu last time ukiwa kwenye uchaguzi Biharamulo, bado sijahau swali moja uliloniuliza kwamba all the games CCM played katika kuidhinisha ugombea wa Oscar, ili iwe nini?

- Maneno yako yote hapo juu ni 100% right, Chadema ikifa then itakuwa nini? Sidhani kama wengi tunajiuliza maswali serious namna hii, nimesema mara kwa mara kwamba kama sio Chadema, leo serikali ya CCM ingekuwa inatuchapa viboko bara barani!

- However: Kuharibika kwa hewa huko Chadema sasa hivi, ninawalaumu sana wazee wa huko kwa kukosa busara nzito za kuendesha siasa za taifa kichama, hakuna modern tactics, hakuna smart political strategies, huko Chadema inaonekana wanachama na viongozi wanajiendea tu na kufanya anything, I mean mwanachama mdogo sana na wa kawaida ana nguvu za ajabu za hata kuweza kuitisha press conf. na kusema siri nyingi za chama, sasa you wonder amezijuaje kama zinatakiwa kuwa siri tena za juu?

- Freeman amejitahidi sana lakini na yeye anafika mahali anahitaji msaada, bado ni mchanga pia kisiasa na hasa busara za siasa za taifa, mnamnyima Zitto uenyekiti, sawa mlitakiwa kutathmini matokeo bila kuwa bias, mlihitaji a devil advocate wa kuweza kuwaambia msiyoyataka, kwamba Zitto ni maarufu na yuko juu sana kisiasa, sasa kwa sababu hamumpi uenyekiti, basi mpeni hata umakamu, au kama hamumutaki kwenye chama, basi mruhusuni agombee mkamchinje kwenye majukwaa na uwe ndio mwisho wake kisiasa, lakini kwa mnayoyafanya sasa hivi, sio siri kwamba mna safari ndefu sana kwa sababu mmeshindwa kutathmini the effect ya Zitto na kukosa uenyekiti, sasa mzimu wenu wenyewe unawala!

- Sijawahi kuona siasa foolish kama hizi mnazozifanya sasa, unamnyima kiongozi maarufu wa chama chako kugombea nafasi kubwa, halafu unaanza kumnyanyasa kwa njia za kijinga jinga ambazo hata ukiulizwa na wenye akili nyingi huwezi kuzi-defend, wala kuzi-define ukaeleweka, hujui kwamba in-the process unazidi kumjenga, huku ukikaribisha unwanted attention ndani ya chama chako, sasa unaona kina Manumba wameshaanza kujisogeza pole pole, the next thing utamsikia Hosea akija huko kunusa nusa halafu mtaishia kulaumu kila mtu isipokuwa nyinyi wenyewe ambao ndio hasa chanzo cha huu upuuuzi!

- Mkuu Lunyungu, hapa niko na wewe kwamba Chadema wanahitaji kuweka sawa nyumba yao, a house divided against itself haiwezi kusimama na kutusaidia taifa, wazee huko Chadema hebu kaeni chini na Zitto, mumsikilize anasema nini na anataka nini, sio lazima mumpe kila kitu anachotaka lakini ikibidi mkutane kati kati basi, na kufanya hivyo kwenye siasa sio kushindwa wala ujinga ndio smart modern politics zinavyotaka, ninarudia tena maneno yangu ya juzi kwamba Chadema, kukua kwenu na kufa kwenu, sasa hivi kunategemea mtakavyo -deal na hii ishu ya Zitto, msim-underestimate huyu mtajimaliza wenyewe, sasa ondoeni hizi habari zenu kwenye media kwanza, waiteni wale wote waliojitoa muone kama mnaweza kuwarudisha chamani un-conditionally, na ndugu yangu Freeman kama haya maji ni mazito mno basi busara hapa ni kuachia ngazi ikibidi kwa manufaa ya chama.

- Hivi Chadema mmeshawahi ku-imagine mkifa mtakuwa mmetufanyia nini wanachi wa Tanzania? I mean inasikitisha sana eti! Dr. Slaa kwa kusema haya uliyoyasema hadharani exactly unategemea ku-accomplish what? Mawasiliano ya siri ya Zitto yanayolindwa na sheria ya jamhuri kama haki zake za kibinadam wewe umeyapataje kama hukuvunja haki zake kisheria? Hivi huko chadema hakuna washauri wa siasa wala sheria?

Respect.


FMEs!
 
Wabe,

With quotes kama hizo unawezaje kuwalaumu waandishi tu? Zitto naye anajiweka katika hali ya kuandikwa vibaya mwenyewe.

Bluray kweli kabisa,

Ndio maana nikamuunga mkono Lukule kuwa dawa ya waandishi ni kukaa kimya kabisa 'mkapa style'!

Kweli inawezekana kabisa Zitto aliwasiliana nao, na pengine kwa nia njema kabisa,lakini waandishi kazi yao ni ...kutoa habari. Bila kuwaza how this might cause confusion
 


Julius Kambarage Nyerere alisema kwamba ukila nyama ya mtu, utaendelea kuila tu .... sasa ndicho anachofanya Slaa.
 
Unaongee nini wewe?
nafikiri kichwa chako nimejaa hewa??

Kama huelewi ninachoongea, sasa unafikiri vipi kichwa changu kimejaa madudu?

Subiri kuungana na Kafulila, uwe Mu-Anglican.

Wale Waarabu wa Loliondo uliosema NDIYO WANAUME mambo yatakuwa jambo...............
 
Hivi Chadema mmeshawahi ku-imagine mkifa mtakuwa mmetufanyia nini wanachi wa Tanzania? I mean inasikitisha sana eti!
maneno mengi ya busara sana, haya machache ndo yananiuma sana, tangu juzi nimetafakari sana juu ya usaliti huu.

chadema mpo katika njia ya kutusaliti, kusaliti umma, hii ni dhambi kubwa sana. Huku ni kuwa vinja moyo Watanzania.

Mkuu FMES asante kwa
 

FMES,sizijui siasa za ndani za chadema,hata hivyo mimi mwenyewe nilijiuliza sababu hasa za kumshauri Zitto asigombee uenyekiti,naweza tu ku guess kwamba walidhani angeweza kumshinda Mbowe?Nildhani wangeachwa wapiganie kura kwa hoja.Kwa mantiki hiyo,kama sababu ni ya kuogopa kwamba Zitto angeweza kushinda,then ni wazi kuna mgawanyiko na hata pengine mgogoro kama kuna dalili zozote zinazoonyesha kwamba Zitto hajaridhishwa na mwenendo mzima.
Hata hivyo kwenye highlight ni kwamba kiutaratibu email ya institution ama organization ni mali ya organization hiyo na kuna policies and procedures zinazo guide matumizi yake,na hivyo haishangazi kama zikiwa monitored.
 
Kwanza nakubaliana kabisa na wale waliosema kuwa kile kinachoendelea sasa hivi ndani ya Chadema dalili nzuri sana ya USALITI wa hali ya juu kwa UMMA wa WATANZANIA. Chadema nawashauri msivunje matumaini ya watanzania, la sivyo laana itawarudia siku moja.

Pili, mi nadhani kinachoendelea sasa hivi ndani ya Chadema ni vita ya wenyewe kwa wenyewe. Unless mtu awe na tangible evidence kunishawisi kuamini kwamba Zitto ndo chanzo cha mgogoro, it doesn't make sense to me. It makes more sense kuamini kwamba mgogoro huu unaanzishwa na watu wengine ndani ya chama kwa lengo la kumkata makali Zitto, na yeye anakuwa "dragged in" ili ajinase kwenye mtego na baadae aonekane yeye ndo tatizo. Hata sijioni wa ajabu kudhani kwamba Katibu Mkuu aliwafukuza wale watumishi bila kumshirikisha wala kumtaarifu msaidizi wake, sioni ajabu kabisa!! Lengo: Ku-crate chance ya tofauti ya mawazo ili baadae mbuzi wa kafara alaumiwe akisema tofauti na wakubwa.

Mheshiwa Zitto: Inaonekana kuna mtego huko nyumbani kwenu. Angalia, umelengwa kukunasa na kukukata makali. Uwe mjanja kama nyoka. Lengo la haya yote ni wewe, na sababu ni kwa kuwa ulitaka kugombea uenyeketi.
Mimi siyo mwanachama wa chama chochote.
Asante.
 

May be uamue kujinyonga ndo tutakushangaa, mengine yoyote utakayoamua ni ya kawaida tu kwa binadamu, we hautakuwa wa kwanza kuamua yafuatayo

a) Kuhamia CCM au chama chochote unachoona watakusikiliza
b) Kujivua uanachama na kuachana na uwakilishi wa wananchi wa jimbo lako walikokuchagua
c) Kujivua vyeo vyote kwenye CHADEMA na kubaki mwanachama wa kawaida tu

I suggest you go for for option C. itakufanya uheshimike zaidi ingawa CHADEMA wanaweza kukutimua wakitaka kama watakuwa na uhakika kuwa ulikuwa unakisaliti chama kwa maslahi yako binafsi - ndo ukubwa huo mzee.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…