Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Hapo ndipo busara za wazee wa chama zinapohitajika.

Nadhani mzee mtei na waasisi wenzake hawatoachia hali hii iendelee kama kweli wanajali maslahi ya chadema.

lakini vile vile hali hii inatukumbusha kwamba busara walizotumia kumshauri zitto ajitoe kugombea uenyekiti huenda hazikukubaliwa na zitto isipokuwa alishinikizwa.

lakini yote kwa yote wazee wasipoingilia kati mapema sakata hili chadema kutatimka vumbi hivi karibuni.

Mungu awanusuru na kimbunga kinachowanyemelea.
 
hivi ndivyo tunavyojiandaa kuelekea uchaguzi 2010??
 
Asema zipo njama kuhamisha ajenda ya ufisadi
Adai kunasa mawasiliano ya Zitto na mwingine
Ajigamba Chadema hakina mgogoro, kipo imara





Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na Zitto Kabwe.




Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, amesema kuna vita kali sasa ya baadhi ya watu kufanya njama za kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuzungumzia masuala ya mbunge wao, Kabwe Zitto.
“Nadhani sasa Watanzania wanatakiwa wakaelewa…naona sasa kuna vita kali ya kuiondoa ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, na sasa wanataka kutuelekeza kumjadili mtu, Zitto.

Na mimi nasema hatuhitaji kujadili watu isipokuwa chama,” alisema Dk. Slaa wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: Chadema hakina mgogoro na kipo imara na hiyo ilithibitika wakati na baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Septemba, mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu madai ya Zitto kutembea na barua ya kujiuzulu Chadema, Dk. Slaa alisema ofisi yake haijapata barua, maelezo yoyote au ushauri kutoka kwa Zitto unaoelezea suala hilo.

“Hatuwezi kuendelea na mambo haya ya kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuanza sasa kujadili suala la mtu binafsi, kama ambavyo sasa inaanza kujitokeza,” alisema.

Alisema Chadema ni taasisi itaendelea kuwepo hata kama yeye ama Mbowe (Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho) au Zitto wataondoka katika chama hicho.

Alisisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote licha ya baadhi ya watu kuanza kudhoofisha ajenda hiyo.

Akifafanua kuhusu suala la Zitto, Dk. Slaa alisema siku moja saa 1:00 jioni kabla ya Mkutano Mkuu wa Chadema uliopita, alipata nafasi ya kuzungumza na mama ya Zitto, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Shida Salum, aliyemhakikishia kwamba Zitto hahusiki na mambo hayo.

“Siku moja kabla ya Kamati Kuu, niliongea na mama yake Zitto na akanihakikishia kwamba hahusiki na mambo haya yanayojitokeza ya kukichafua chama,” alisema.

Alisema alielezwa na mama huyo kuwa wapo watu wanaomtumia Zitto kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kwamba mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayo password ya anuani ya barua pepe ya Zitto ambayo anaitumia kuandika taarifa mbalimbali alizoeleza zinaonyesha kama vile zinatoka kwa Zitto.

Lakini alisema baada ya mazungumzo na mama huyo, kesho yake gazeti moja lilikuwa na habari ya Zitto kukanusha kwamba hahusiki na suala la David Kafulila isipokuwa watu wametumia jina lake.

Dk. Slaa aliongeza baada ya mazungumzo hayo, asubuhi yake alipata taarifa za barua pepe kutoka kwa Mtanzania mwema zinazoonyesha mawasiliano kati ya Zitto na mtu mmoja (jina linahifadhiwa).

Bila kueleza kwa undani taarifa mbalimbali zilizokuwemo katika barua hizo pepe, alisema kwa kifupi kwamba zilikuwa zikionyesha mawasiliano ya kichama kati ya mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam na Zitto ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Ujerumani.

Alisema baada ya kuzisoma aliwasiliana na mkazi huyo wa Dar es Salaam akitamka athibitishe iwapo mawasiliano hayo ya barua pepe yalikuwa ya kwake au la.

Alisema alifanya hivyo kwa kumtumia ujumbe na baada ya muda mkazi huyo alimpigia Dk. Slaa, na akathibitisha kwamba anazitambua barua hizo na mawasiliano hayo yalikuwa ni ya kwake.

Lakini baadaye katika mazungumzo yao ya simu, mkazi huyo wa jijini alimweleza Dk. Slaa kwamba ameingilia mawasiliano yao binafsi, jambo ambalo alilipinga.

“Nilimweleza mkazi huyo kwamba sijaingilia mawasiliano binafsi, kwa kuwa taarifa zilizokuwa zikizungumzwa katika barua hizo zilikuwa zikikihusu Chadema na kwa maana hiyo hazikuwa binafsi,” alisema.

Alisema baadaye mkazi huyo alimjibu Dk. Slaa kwamba anafanya kazi katika kampuni kubwa na kwamba Dk. Slaa hataiweza na afadhali aache.

Aliongeza baada ya gazeti moja kuchapisha habari za Zitto jana, alimtumia Zitto ujumbe wa barua pepe akitaka maelezo kuhusu habari hizo zilizodai kuwa anatembea na barua ya kujiuzulu Chadema.

Dk. Slaa alisema tangu alivyomtumia ujumbe huo jana asubuhi, hajapata majibu yoyote hadi alipowasiliana na Nipashe saa 11:00 jana jioni.




CHANZO: NIPASHE
 
(Haya ndiyo maneno latest ya Mbunge Zitto Kabwe dhidi ya CHADEMA;likely hali si shwari ndani ya CHADEMA,SOMA MWENYEWE HAPA CHINI)

Malalamiko ya Zitto yalitokana na taarifa iliyotolewa na chama hicho kilichodai kuwa ofisa habari aliyetimuliwa, David Kafulila anatumia anuani ya barua pepe ya Zitto visivyo halali. Kafulila na Zitto ni marafiki wakubwa.


"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.


Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema na kwamba "wanapaswa waniache nipumzike na kufanya mambo yangu".


"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha," alisema.

Katika kuonyesha kuchukizwa na baadhi ya taarifa alizoziita za kizushi zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si Mwananchi), Zitto, alisema:

"Faragha yangu ni faragha yangu, Zitto ni Zitto kama yeye na siyo mali ya Chadema.


Akizungumzia uhusiano wake na Kafulila aliyehamia NCCR-Mageuzi kutoka Chadema, Zitto alisema: "Siku zote msimamo wangu umekuwa kwa wale wanaokandamizwa... na katika hili David (Kafulila) ndiye anayekandamizwa."


Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema katika kufanya mambo yake.


"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha yangu."

"Msimwandame Kafulila. Mumwache mtoto wa watu. Mmeshamwita sisimizi inatosha. Msijaribu kunigombanisha na Kafulila. Sitaki... sitaki... sitaki," aling'aka Zitto

CHANZO;Gazeti la Mwananchi
 
Hivi kila siku ziittooooo ziti mpakka lini. Halafu kuna wadau vimeo humu ndani ya blog hii wanadhani hii ni blog ya CHADEMA may be mwanzilishi ni kad wa chadema lakini si kila wa humu ni chadema. after all kumtaja mtu mmoja kila siku ni kutumikishwa kwa hiari ni lazima mmkosoe kwanza huyo zito ndipo tutaenda sawa.
si mnakumbuka ya MR SIXX aliibuka na tuhuma kibao kumbe yeye ni namabri 1 tena anakumbatia upumbavu. hebu tafutenei kwanza ukombozi wa fikra binafsi ndipo upiganie ya wengine. sometimes nakasirika siingii katika maoni. leo nilikuja na jipya lakini haya mara dr slaa mara zito mara oohh chadema mwananchi upumbavu mtupu hatupo hapa kushabikia chadema wala mtu tuseme yatupasayo kusema.
mbona tunamkosoa makamba na kumwacha mzee wa nchi, mbona tunamkosoa Rostam na kumsifia zito hamkumbuki aliyosema selelii kuhusu sitta, lowasa akukweti na rostam, au hamkusikia kwa vile wote ni ccm. tuache ushabiki wa kijinga kama huu. nadhani ifikie wakati tuwe na ukombozi wa fikra zetu kwanza tuwe wa kutumikishwa kama wale wanaojivunia historia ya utumwa bagamoyo ambayo inawaweka utumwani hata leo hii.
hivi ni lini tutaamka, tunayo ya kujadili, kwa mfano kwa nini kampeni za hakisawa ni nyingi sana tutaja chinjana, tumechoka amani na huo ndo ukweli, uzazi wa mpango bila kuangalia athari kwa maambukizi mapya ya ukimwi. mume ataka watoto mke amefunga uzazi, suala ni watoto haijalishi mama ni nani, athari yake maambukizi mapya. haaaaaaaataratibu macho na masikio yangu yamechoka kumsikia zito. ni mnafiki, mwongo, mla rushwa na tapeli.
 
Sijui mh Zitto anamtishia nani? akiwa ni mtanzania huru anaweza kufanya maauzi yoyote anayopenda, hii ikiwa ni pamoja na kujiuzulu Chadema na kujiunga na NCCR au CCM. Lakini ni vizuri kwa kuwa itatusaidia mapema kujua true colors za wanasiasa ambao tunadai kuwa wanapromise ya kuleta new politics Tanzania. Kuna wengine wameimba kwa miaka 20 haki,usawa rushwa ni adui, lakini ukweli ni kuwa ni kinyume na wanayosema.

Long live Tanzania-ufisadi utashindwa tu.
 

Kaka bora umetukumbusha .....mwaka 1994....mrema alijiunga na NCCR....waliofaidika ni NCCR kwani aliwatoa kuwa kikundi kidogo cha wasomi [pressure group]....hadi kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania....na kupata karibu asilimia 40 ya votes ,mwaka 1995...wabunge zaidi ya 20 etc ...haijapata tokea hadi leo....sasa mtu anayesema MREMA aliuwa NCCR sijui anatumia vigezo gani....mimi nadhani NCCR ilimuuwa mREMA na baada ya hapo ...hakijaweza kukurupuka tena..labda iwapo watafanikiwa kumpata ZITTO kidogo watapata ka airtime .....lakini mwisho wa siku kitamuuwa kisiasa.

Nasema hivyo nikijuwa kuwa watu wengi humu walikuwa NCCR Enzi hizo na kuna waliopoteza ajira na resources kwa ajili ya kukijenga lakini mwisho wa siku ...ccm ikapenyeza chokochoko kama wanavyofanya kwa CHADEMA sasa ....CHama kikawa hakikaliki......na ikapelekea mrema kukimbia ..na kuwaachia chama .....matokeo yake ni wazi...wale waliokuwa wakiendesha ...choko choko ndani ya nccr mageuzi wote wamekuwa rewarded..masumbuko lamwai,ngawaiya,nsaguswako,festus limbu, etc...james mwakyoma...

Nayaweka haya ili watu wajuwe historia ya ukandamizaji wanaofanyiwa wananchi....MREMA huyo alienda chama cha TLP...kilikuwa chama kinachokufa ......pamoja na kuwa alikuwa ameshaishiwa nguvu kikapata kauhai kidogo......bado akafuatwa na Leo hii Leo Lekwama ...ameshanunuliwa yupo CCM [kila mtu ana bei yake...he compromised for less]...Pamoja na kasoro za wazi za mrema ukweli ni kuwa alihujumiwa...

Msisahau ile style ya kuhujumu wapinzani ...ndio imeanza tena kuelekea 2010......na watch this space...Watu kama ZITTO hana makosa ila ukweli ni kuwa anawindwa na ccm ili kuyumbisha upinzani...na ni lazima akipenda awe imara ...ipo siku atakuta waliokuwa wakitumiwa kumuwinda ....wanakuwa rewarded.....!!

Meanwhile wapenda demokrasia wajiandae kwa tamko loolote...kwani lolote litakalotokea halitakuwa ajabu...tofauti na wakati mwingine ...CHADEMA waanaonekana kuwa firm kwa ku avoid media.....ila ni MUHIMU WAKAAZA ZIARA YA KUWAANDAA WANANCHI PSYCHOLOGICALLY dhidi ya vita wanayopigwa ...,kuepuka media..,kuepuka kujibizana especially wajiepushe sana kumuongelea ZITTO ambaye anaonekana ndio anataka kufanywa na maadui wa chadema [zitto akiwemo] kama chambo cha mgogoro......

Wananchi wamechezewa sana .........na wanakata tamaa sana pale viongozi wao waliowaamini wanapowaacha......hembu jiulizeni ..mtu kama walid kabourou....watu walikuwa wakishinda relwe kigoma kumsubiri.....kama mfalme....alipoamua kuwaacha watu wake tena bila hata kuwa consult..waliumia sana....KWANINI WAPINZANI HAWAWAIGI CCM ....WAO WANAGOMBANA WANAVUANA NGUO ...LAKINI HAWAHAMI CHAMA ....KWA NINI WANASHAURI WAPINZANI WAKIGOMBANA WAHAME!!!??
 
Binafsi napenda Zitto anyamaze asijibizane na Media kabisa hii inazidi kujenga uhasama kati yake na wanachama wengine wanajua ni kweli kumbe propaganda za wabaya wa Chadema ni bora Zitto akasimama yeye kama yeye kuliko kuyumbishwa na maadui wa chama.
 
tukiwa "ndani ya kumi na mbili" hawa watatu watapata kazi sana kufanya kazi pamoja kuelekea uchaguzi mkuu mwakani. Mbowe, Slaa, na Zitto. Hawawezi kulima shamba pamoja kama hawajafungwa kongwa pamoja. Ningekuwa na uwezo ningewafungia hawa watatu kwenye kisiwa kimoja mahali fulani na hawarudi hadi wawe wamekumbatiana na kukubaliana.
 
Jamani nimeona article inayosema Zitto yuko mbioni kujiuzulu Chadema katika Mwananchi! Cha kushangazwa article hiyo wameitoa ghafla! Sasa najiuliza kulikoni?
Huu mtindo wa kubadili heading unaanza kuniboa! We moderator anzisha thread zako kama hii ni 'jamii forums' sioni ni kwanini uondoe baadhi ya articles zenye maslahi ya taifa au kuzibadili vichwa vya habari kuku-suit wewe madhalani hazimkashifu mtu!

NB: Pls dont use my name kuweka article yako au heading that's a crime dont put words in my mouths! Kuwa mstaarabu!!
 
Wamwache Zitto na Kafulila wake wakafulie huko NCCR, watajiju.
 


KABISA ...!! WATANZANIA WAMESHAUMIA VYA KUTOSHA ..KUWABEBA WATU...KUWAUNGA MKONO...MWISHO WANAWAACHA SOLEMBA!! SI VEMA.....ikiwa ni kweli kuna wazo kama hilo kwa zitto na ikiwa kweli yeye ni mpenda mageuzi itapendeza kama atahama bila kuyumbisha wananchi wa kawaida....lakini sitaki tukio la NCCR LIRUDI kwani kuna wananchi walijiapiza kuwa hawatakaa tena waunge mkono wapinzani ...kwa kuwa waliwadanganya ...wakawaunga mkono mwisho wakapewa pesa wakawakimbia ......na huo ndio umekuwa mtaji wa ccm siku zote .....kuwa WAPINZANI WANAGOMBANA NA HAWANA MSIMAMO!!....kumbukeni ya MSABAH SALUM na kisa cha kutekwa nyara....!!
 
Kweli siasa za TZ ni ngumu sana, hivi viongozi wa CHADEMA hamuoni kama mnalikoroga hapa?

Mukianza kujibizana kwenye magazeti jua mwisho wa hilo jambo haupo tena.

Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji, jifungieni sehemu mpaka Mwafaka upatikane.

Jino kwa jino haitasaidia kabisa kwenye hili. Kwa maendeleo ya maana, Tanzania inahitaji chama/vyama vya upinzani imara. Kinachotokea hakifurahishi kabisa hasa mnapofanya haya mambo wakati ambao watu wangetegemea muungane vizuri ili kutumia weakness ya CCM kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Vita vya panzi, ni furaha ya kunguru, angalieni kunguru wamejaa kila sehemu, msipokuwa waangalifu, hao kunguru watashiba mwaka huu.
 


mmezidi na ma thread yenu ya zitto bora tu yameunganishwa yote pamoja mweeeeee
 

hivi na marando nae amesepa?
 
kwajinsi watu walivomkalia kooni huyo zitto, inaonekana watu wanataka uamuzi wa namna fulani kutoka kwa zito, kwanini msimuche huyo zitto akae chini, amue mwenyewe..
by the way uamuzi anao mwenyewe na anaujua, hizi kelele ni usumbufu wa bure tu.
 

Ni wazi upeo wako wa spinning bado mdogo sana. Moja; Chuki kati ya Mbowe na Kafulila (nimetumia neno kati kwani naamini wote wawili ni wakosa katika hili) hazijaanza na uchaguzi mkuu bali muda mrefu sana kutokana na misimamo ya wazi ya Kafulila kuhusu Mbowe na reaction ya Mbowe kuhusu Kafulila. Wote hawa hawajawahi kuficha chuki kati yao. Pili; Siasa za makundi ndani ya CHADEMA hazikuwa katika hali ya uadui na ufitini wakati huo 2008 kama zilivyo sasa mara baada ya Zitto kuthubutu kushindana na Mbowe katika UENYEKITI. Mwanzoni hali hiyo ilikuwa chinichini lakini mara baada ya Zitto kujulinakan kuwa anagombea Uenyekiti na kama hali inavyojionyesha waziwazi sasa, chuki, fitina na ushindani wa kimakundi umekuwa wa wazi zaidi kama ilivyo katika CCM.

Ni wapi mimi nilisema kuwa Heche alitaka kumchoma kisu Zitto Kabwe. Angalia sasa unajikuta ukisema hata yale yaliyofunikwa. Unataka nikuletee ushahidi kwani wewe umeshajiona ni Mwanasheria na JF ni mahakama siku hizi? Ni lini uliwahi kuleta mashahidi wa wawili ama watatu wanaothibitisha kuwa ROSTAM anahusika na WIZI wa EPA? Hivi hayo aliyoyafanya Heche aliyafanya kwa Kificho na sio kwenye uwanja w wazi kabisa akizungukwa na mamia ya WANACHADEMA? Yaani kitendo cha Heche kusema magazetini kuwa hakufanya hilo tayari kimeshathibitisha kuwa hilo halikufanyika. Unataka kutuambia kuwa kwa kuwa ROSTAM alishasema magazetini kuwa hakuhusika na RICHMOND, DOWANS na EPA basi tayari ni thibitisho kuwa yeye ni innocent?

Hata kipofu asiyesoma magazeti wala mitandao kama JF atakushangaa. Mlianza kutumia majina vivuli na sasa mmefikia hata kutumia majina yenu kama alivyofanya KINABO na hata magazeti yenu bila hata kujificha mkiiamini kuwa mnanafasi ya kushinda. Acheni kujidanganya, vita dhidi ya Zitto hamtaiweza kamwe…..

Huna tofauti na kina SOPHIA SIMBA na MAKAMBA. Badala ya kujibu hoja unakimbilia kudai MATUSI na UASI. Ni wapi mimi nimetukana CHADEMA ama hata kiongozi wenu? Uweje niwe muasi wakati kamwe sijawahi kuwa MWANACHAMA wenu….Mnadhani ninyi tu mna haki ya kusema mapungufu ya CCM lakini yakisemwa yenu basi inakuwa ni WIVU, MATUSI na UASI? Nasikia wewe ndio unajiona kuwa MASTER OF SPINING wa CHADEMA.


Mnajiona ninyi tu ndio wenye haki ya kumzushia, kumfitini na hata kumkejeli Zitto lakini wengine hawana haki ya kumtetea. Yaani mna asilimia SABA tu ya wapiga kura tayari mnataka kuleta udikteta wa wanyonge, mkiwa Wababe sijui itakuwaje? As long as mnaendeleza kampeni chafu yenu dhidi ya Zitto I will stand up on you no matter what. Mkitaka ukimya wangu, LEAVE ZITTO ALONE..

Hili nakubali nilikosea. Ni kweli Muslim Hassanali amefanya kazi ya kisiasa Kigoma Kusini lakini pia Kafulila amekuwa na mchango mkubwa pia….

Umemtuhumu tena mwandishi wa habari kuwa anagenge laki lenye vita dhidi ya Zitto, unaweza kutupa ushahidi wa tuhuma zako hata kama ni wa kimazingira
Tafadhali usinipeleke huko. Unajua wazi kuwa ninakujua wewe, namjua Kinabo na connection zenu wote na CHADEMA, mmefikaje huko, mnaoperate vipi na kadhalika. Kinabo alikuja na jina lake na kutoa madai yake ambayo kwangu niliona kuwa ni mwendelezo wa vita ya kimakundi dhidi ya Zitto. Kama alivyotoa madai yake na mtazamo wake nami nina haki ya kutoa madai yangu na msimamo wake. Ukitaka ushahidi hata wa kimazingira ni kunipush mimi kumwaga mchele kwenye viapanga wengi. I am not as insensitive and reckless as u r.


Unaweza kuyaeleza hayo maono ya mbali?
Hata nikukueleza siamini kama umeshafikia ukomavu wa kisiasa wa kuweza kuelewa. Natambua kuwa ni hamasa na sio dira, itikadi na mitizamo mipana na endelevu iliyokuvutia kuingia katika siasa na zaidi CHADEMA. Na huu ndio upungufu mkubwa ambao vijana wengi tunao na kushindwa kujenga aina ya siasa itakayotusaidia sisi kutekeleza wito wa kizazi chetu ambao wote tulipaswa kutilia mkazo na sio hizi petty, egoistic and selfish short term interests. .


Hili na mengine ambayo nimeyaacha kwa makusudi, nakupa muda ujirudi kabla name sijachagua kufuata mkondo huo kukujibu. Jana nimewasialiana nawe kistaarabu na kuzungumza na Mnyika na viongozi wako wengine kwa undani sana. Naamini wamekutumia ujumbe. Nikirudi tena na kukuona unaendelea na haya matusi ya wazi na kuwahusisha wasio husika nami sitakutukana lakini ni wazi nitawahusisha pia watu wa karibu wako. Nakuapia kuwa sio tu itawaumiza wao bali hata chama chako kitu ambacho bado najizuia kukifanya hata katika hali mliyofikia…..


omarilyas
 
Ambacho nakijua , taarifa toka ndani ya chumba fulani cha habari katika haya magazeti ya mafisadi , ni kwamba habari ya kujiuzuru zito Imeisha pewa kichwa cha habari, wanasubiri huyo jamaa aamue kujiuzulu waijazie jazie maneno tu basi.
Kwa hiyo mh Zitto ameukabidhi muskakabali wake mikononi mwa mafisadi? Maana kwa kauli hii mafisadi ndio wanaoonekana kuratibu ubaadae wa Zitto.
 
Siasa za Tanzania inaelekea kila mtu ana bei yake, na wakikushindwa watatumia kila mbinu wahakikisha wanakubomoa!
 

- Hapana hili limekorogwa na Chadema wenyewe sasa walinywe wenyewe bila kusingizia mtu wa nje!

Respect.


FMEs!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…