Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
na Irene Mark
DAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.
Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.
Taarifa hizo zilitokana na mawasiliano ya Zitto na watu walio karibu naye ambao juzi waliliambia gazeti hili wanachokiita ukweli wa madai ya mbunge huyo kumuunga mkono Kafulila katika harakati zake mpya akiwa NCCR-Mageuzi, kiasi cha kumpatia magari matatu kwa ajili ya kuzunguka maeneo kadhaa ya Jimbo la Kigoma Kusini katika siku chache zijazo.
Jana Kafulila aliiambia Tanzania Daima kuwa kama ni hivyo, Zitto ni mzushi, kwani hajawahi kumpa neno la siri la kufungua anuani ya barua pepe yake, wala hafahamu lolote kuhusu anuani hiyo.
Katika toleo la jana, gazeti hili lilkuwa na habari kuwa Zitto alimkana Kafulila, na kwamba mbunge huyo amekiandikia barua chama chake (CHADEMA) kukijulisha msimamo wake binafsi, kwa maelezo kuwa wanaomhusisha na kauli za Kafulila wana nia ya kumchonganisha (Zitto) na uongozi wa CHADEMA.
Kauli kama hii ilitolewa na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto, katika mahojiano yake na gazeti la MwanaHALISI wiki mbili zilizopita, akisema mwanawe anatumiwa na watu wenye lengo la kuvuruga chama na kumgombanisha mwanawe na uongozi wa chama chao.
Katika kauli yake ya juzi, Zitto alinukuliwa akiwaeleza watu walio karibu naye kuwa hata taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu yeye kumbeba Kafulila zinamnukuu bila kumhoji yeye.
Lakini jana Kafulila alisema: Huo ni uzushi unaotengenezwa password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi. Wakati huo huo, aliyevuliwa cheo cha Ofisa Mwandamizi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Juju Danda, jana alitangaza rasmi kujiunga NCCR-Mageuzi kama Kafulila.
Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi, alisema.
Am fed up with this debate.Let me stay away and discuss other issues.
Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kuwa haiwezekani na itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama kulingana na katiba ya chama.Kafulila ndiye alisema kapewa magari matatu na naibu katibu wa CHADEMA ili akapige kampeni kwa chama cha NCCR dhidi ya vyama vingine CHADEMA kikiwemo
Mkuu tafakari kwanza,mimi sina chama lakini napenda fairness regardless,na ukweli ndio pia muhimu.
Kwanza uzingatie Zitto bado ni CHADEMA,na madai yako kwamba Kafulila keshajiendea zake NCCR na bado hawajaridhika hayana mantiki kwasababu Kafulila ndiye alisema kapewa magari matatu na naibu katibu wa CHADEMA ili akapige kampeni kwa chama cha NCCR dhidi ya vyama vingine CHADEMA kikiwemo.Kwahiyo kama habari hizo ni za kweli then CHADEMA lazima watakuwa concerned na pengine kumwuliza naibu katibu mkuu wao if all this is true.Na ndio maana Zitto akakanusha habari hizo,then ikasemekana kuwa Zitto kasema Kafulila ana password yake,huwezi kujua alibanwa ndani ya chama,Kafulila akaibuka akasema Zitto mzushi,sasa nani kamfata nani?Tulia na tumia busara,reasoning na reality vitake over emotions,you will then see where i am coming from.
Kuna mwanadada mmoja kanipigia simu anasema yeye na Kafulila walikuwa darasa moja na yeye wiki hii Jumamosi anapata cheti baada ya kumaliza degree yake na Kafulila alikwua virus hata darasani . Sijajua ukweli wa habari hizi ina hata wa darasani kwake wanasema jamaa ni troublesome.
Jmushi1,
Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kwamba itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama.
Wanaboidi,
Kilichotokea kimetokea na haya yote mazungumzo ni baada ya habari kwani Kafulila hakufukuzwa bali alivuliwa cheo chake na Zitto hakupinga hatua hiyo.. hakuna mahala Zitto amesema Chadema au Dr. Slaa amefanya makosa kumwengua Kafulila ktk wadhifa isipokuwa ni waandishi wenye chuki binafsi ndani na nje ya Chadema wanaojaribu kukiharibu chama kwa kupitia mgogoro huu. Ajabu ni kwamba wote hawa walikuwa tayari wamezivua nguo zao kuyakoga maji haya machafu, sasa kinachonishinda kuelewa ni kwamba Kafulila kaondoka, bado mnamfuafuta aliko na maneno mengi kuendelea kuhakikisha Zitto pia anaondoka Chadema...
Hii inatisha sana na pengine inanipa sura kamili ya vichwa vya wanachama wa Chadema..
Jmushi1,
Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kuwa haiwezekani na itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama kulingana na katiba ya chama.
Wanaboidi,
Kilichotokea kimetokea na haya yote mazungumzo ni baada ya habari kwani Kafulila hakufukuzwa bali alivuliwa cheo chake na Zitto hakupinga hatua hiyo.. hakuna mahala Zitto amesema Chadema au Dr. Slaa amefanya makosa kumwengua Kafulila ktk wadhifa isipokuwa ni waandishi wenye chuki binafsi ndani na nje ya Chadema wanaojaribu kukiharibu chama kwa kupitia mgogoro huu. Ajabu ni kwamba wote hawa walikuwa tayari wamezivua nguo zao kuyakoga maji haya machafu, sasa kinachonishinda kuelewa ni kwamba Kafulila kaondoka, bado mnamfuafuta aliko na maneno mengi kuendelea kuhakikisha Zitto pia anaondoka Chadema...
Hii inatisha sana na pengine inanipa sura kamili ya vichwa vya wanachama wa Chadema..
Ndio maana nasema kuwa hakuna jipya hapa maana wote ni wazushi tuMkuu wangu this is politics, Kafulila ameondoka na anatoa tuhuma ambazo Chadema kama chama wanaziktaa sasa ulitaka Chadema wafanye nini?
Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.
Huo ni uzushi unaotengenezwa password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi.
Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi,
come join club whea we talk real life.....wachana na hizi mambo za kuchosha akili bila faida
Inaelekea harakati za kuhakikisha upinzani hautoi changamoto kubwa kwa CCM katika uchaguzi wa 2010 zinaanza kufanikiwa, tena kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.
Baada ya muda mfupi tu, tutaanza kuelewa kuwa CHADEMA, chama kilichoonekana kuwa usumbufu kwa CCM kitaangamia na kuwa kama baadhi ya vyama vingine vya upinzani.
CCM ina uwezo mkubwa kwa kweli. labda na bahati ya ajabu. Kila wapinzani wanachokifanya wakati kama huu ni kuhakikishia CCM ushindi wa nguvu tu.
Punguza jazba mangi, twende taratibu tutafika tu. Tangu lini umejitoa chadema chalii angu!!??au ndo umeanza kuwakana wenzako?
Jitahidi kufanya homework yako vizuri, isome hiyo makala ya huyo mwandishi vizuri, soma katikati ya mistari halafu uje unionyeshe ni wapi tanzania daima wamezungumza na zitto na akawaeleza kwamba kafulila ana password yake kama si majungu ya tanzania daima &co., Na hata kama aliwahi kumpa password yake kutokana na ukaribu wao, bado siamini kwamba zitto ni mzembe kiasi cha kuzungumza jambo kama hilo mbele ya watu.
kwahiyo usiwe na shaka chalii angu ninakuona vizuri sana "where you coming from".
Kafulila kaondoka zake kwenda nccr na ametangaza kuingia kilingeni kupambana na chadema kwahiyo msiweweseke, jipangeni mkakabiliane nae huko huko kwenye battle field, haya makelele mnayoendelea kupiga inaonyesha ni kiasi gani kafulila amewashika pabaya.
Mkuu umeuvaa mkenge vizuri...Mkuu wangu this is politics, Kafulila ameondoka na anatoa tuhuma ambazo Chadema kama chama wanaziktaa sasa ulitaka Chadema wafanye nini?
umegundua kama kanjanja kama alivyo willy edward
iritating....Kafulila (kafulia), Zitto, Makamba, Simba khaaaaa! Masikio yanauma nawish kungekuwa na mahali ambapo sitasikia huu upupu anymore!!