Ikulu, Dodoma: Humphrey Polepole na Waziri Kindamba waapishwa

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan anawaapisha viongozi aliowateua kama ifuatavyo:
  1. WAZIRI KINDAMBA WAZIRI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  2. HUMPHREY HEZRON POLEPOLE kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.
Mbwa huwa habweki akiwa na nyama mdomoni, if you know you know.
 
Angemteua hata Lukuvi.
Lukuvi na beshte yake kabugi wamepotezwa kwenye ulingo wa siasa. Chezeya mama wewe....
Acheni fitna na roho mbaya, husuda za kiafrika hata hao uliowataja wangepewa hiyo nafasi lazima mngekuja na mabandiko mengi sana humu.

Hakuna aliye sahihi machoni penu, kila mtu si sahihi na hata angeteuliwa mtu mpya asiyefahamika ahahahaa, mngeandika "kaokotwa wapi huyu?"

👉🏾 Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
 
Hahahahaha

Balozi Humphrey Polepole

Akitoka kuapishwa anapelekwa chuo cha Diplomasia miezi kadhaa kufundishwa maadili ya Balozi ili aache tabia yake ya kucheza singeli na viduku na na ku post mitandaoni pamoja na kukebehi Mamlaka

Hili linaitwa Kufuli kwa hisani ya Bi Mkubwa wa Makunduchi
 
Huyo mtu kwisha habari yake inakuja barua nyingine yakutengua uteuzi akalime magimbi huko kwao Mpitimbi. Huwezi kushindana na mamlaka.
Haya mambo ya kuheshimu mamlaka ndio hutengeneza maraisi miungu huku afrika. Raisi anapaswa kupingwa ndani na nje ya chama.
Hiyo ndio demokrasia.
 
What's this..?.

"Mh. Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia, utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe na tutazungumza kwa urefu..." Samia says.
 
Hii nchi utafikiri tupo kwenye The Godfather na Kina Michael Corleone...

Na hizo ndio moja ya Offer ambazo ni very difficult ku-refuse...

Sio kwamba nasifia bali nasikitika sababu Taifa halipaswi kuendeshwa hivi

Nani alistahili kuwa Balozi Malawi?
 
Back
Top Bottom