Wapinzani wa Polepole wana upeo mdogo sana wa kifikra, muda si mrefu atawashangaza watu

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,398
3,907
Ndugu Humphrey Polepole,

Tarehe 28/11/2020 Ndugu Hamphrey Polepole aliteuliwa na Hayati Rais Magufuli kuwa Mbunge, hapo awali alikua ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa.

Baada ya kifo cha Rais Magufuli mambo yakabadilika.Tarehe 14/3/2022 Rais Samia akamteua Ndugu Polepole kuwa Balozi nchini Malawi.

Wapo 'wahuni' ambao walifurahia Polepole kuondolewa Bungeni, wakadai kwamba Polepole kuondolewa Bungeni basi watapumua kwani hatasikika tena, atakuwa ameuliwa kisiasa.

Baada ya kwenda Malawi kama Balozi tulitarajia angekua amepotea kama vile 'maadui wa Magufuli' walivyotegemea! Ila ikawa tofauti, Polepole akang'aa kuzidi hata alipokuwa Mbunge.

Jamaa akachapa kazi kisawasawa hadi wahuni wakakasirika! Katika mabalozi wote wa Tanzania ukianzia Ulaya, Amerika, Asia na huku Afrika basi ni Polepole pekee ndio alikuwa anasikika! Wahuni wakanuna.

Jana Rais Samia kamuhamisha Balozi Polepole toka nchini Malawi kwenda nchini Cuba. Sababu ya kumtoa Malawi na kumpeleka Cuba anayoijua ni mwenyewe Rais Samia na si mwingine yeyote, lakini cha ajabu sasa walewale 'wahuni' jana wakaanza kusherehekea tena kwa ngoma na kucheza kabisa.

Wahuni wanadai Polepole kupelekwa Cuba basi ndio kazimwa kisiasa kabisa!

Wanadai nchi sasa itakua mbali na masalia ya Mwendazake, yaani wanamchukia Magufuli, pia wanawachukia na wale washirika wa karibu wa Magufuli.

Wamesahau kuwa hata pale alipopelekwa Malawi walifurahia na ni wao waliotuambia kuwa Polepole angepotea kisiasa lakini kilichotokea hadi leo hawaamini, wakapigwa nyumbani na ugenini.

Mimi nawakumbusha tu kuwa hata huko Cuba Ndugu Polepole ataendelea kuwapelekea moto balaa, na watazidi kununa!

Wakitaka waondokane kabisa na Ndugu Polepole, yaani wasimsikie kabisa katika nchi hii basi njia ni moja tu, inabidi sasa wakubali kuingia kwenye 'mfumo' wa Ndugu Polepole ili wafundishwe Uzalendo. Mbali na hapo hakuna njia nyingine
 
Wapinzani wa Polepole?
😂😂😂
Mbona unamkuza sana huyo jamaa, hana lolote la kumfanya awe na wapinzani, wananchi wanafurahia tu alivyoshuka baada ya kujimwambafai sana enzi za Jiwe
 
Hahahha Polepole ndio amuangushe Rais wa JMT? mnachekesha sana. Awamu hii deep state ndio kina Rostam alafu eti bwana mdogo Polepole ndio apambane nao 😂😂😂😂. Hii nchi Ina vituko sana.
 
Porojo tu, hakuna mtu timamu anayeweza kuhangaika na huyo chakubanga
 
Kipaji na uwezo wa Polepole ni tishio kwa watawala. JPM ye aliamua kufanya nae kazi lakini kuna mambo kila mtu alisimamia imani yake.

Mungu akishakupa kibali mwanadamu anabakia kutapatapa dhidi yako.
 
Kipaji na uwezo wa Polepole ni tishio kwa watawala. JPM ye aliamua kufanya nae kazi lakini kuna mambo kila mtu alisimamia imani yake.

Mungu akishakupa kibali mwanadamu anabakia kutapatapa dhidi yako.
Wakat mwingine ni bahati na kudra za Mwenyezi MUNGU....

Sijaona chochote Cha kupigia mfano zaidi ya kauli na matamko akiwa pale CCM

MBONA TUNAO MFAHAMU JOHN JUSTIN PAMBALU,
Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA....
na ALIE WAI KUA DIWANI KATA YA BUTIMBA (MZA) KATIKA UMRI MDOGO KULIKO YEYOTE TANZANIA,
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA 2020...

Huyu bwana mdogo ni mzalendo MNO sijui kwanini walishindwa kumu ungisha JUHUDI kina bwana POLE POLE...
Huyu dogo CCM wange fanya mpango wa mshawishi wamchukue ni hazina ya TAIFA LETU 🇹🇿

Kipimo namba Moja ni UZALENDO wake Kwa CHADEMA sizani kama kuna msaka tonge yeyote ambae aliacha KUUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM....

Wampe hata UDC Ileje huko au namtumbo....
 
Back
Top Bottom