UTEUZI: Rais Samia ateua Balozi mmoja na kumhamisha Humphrey Polepole kuwa Balozi nchini Cuba

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya vituo kwa Mabalozi wawili (02) na uteuzi wa Balozi mmoja (01) kama ifuatavyo:

1. Amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu Balozi Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Malawi.

2. Amemteua Balozi Lt. Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

3. Amemteua Bw. Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi nchini Uturuki. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Bakari alikuwa Konseli Mkuu nchini Dubai.

FsyyKAdaUAAWg6-.jpeg
 
View attachment 2575203
Tuliosomea Cuba tunaelewewa.
Mr pole pole kapelekwa mbali na Tz kusudi kuvuruga zile movements zake za chini chini.

Maana ilikuwa haipiti mwezi bila kuja Tz.

Next stage watamla kichwa kabla ya 25.
Japo, hii itakuwa risk kwa SSH.
Maana watamrahisishia mipango yake.
 
Masikini Polepole anapelekwa kwenye njaa tu. Mama kaona bado anafanya kazi kisiasa katupwa kisiwani mbali sana!
 
Tuliosomea Cuba tunaelewewa.
Mr pole pole kapelekwa mbali na Tz kusudi kuvuruga zile movements zake za chini chini.

Maana ilikuwa haipiti mwezi bila kuja Tz.

Next stage watamla kichwa kabla ya 25.
Japo, hii itakuwa risk kwa SSH.
Maana watamrahisishia mipango yake.
Movement zipi Mkuu? Polepole ni nzi tu CCM hakuwa hata na miaka 5 so Hana hiyo power mnayofikiria anayo. Kahamishwa Ili tu asipige kelele awe busy muda wote ila Sio kwamba ana uwezo wa kushawishi chaguzi za 2025.

Kama kinana, makamba, membe n.k walikua na miaka zaidi ya 40 CCM walitulizwa na JPM walipotaka kumuondoa 2020 ndio sembuse Polepole na Bashiru waliokaa 5 years pekee?? Mkuu CCM Ina wenyewe na ndio waliokamata serikali so hao kina Kabudi, Polepole na Bashiru ni wageni tu
 
Polepole ameponzwa na kitendo Cha kutaka kupoka madaraka ya amiri Jeshi mkuu kwa kutamka salamu ya "himahima" Tanzania....ni kwa wale wanajeshi waliokuwa wanaenda Malawi kutoa msaada. Akilenga umaarufu binafsi wakati akijua wale wameenda kwa amri ya SSH. Mwanajeshi anatakiwa kumtii amiri Jeshi pekee,au bosi katika mfumo wa kijeshi.

Pia muda mwingi alikuwa anazurura tu Tanzania bila kufanya kazi. Mara Yuko Sinza, mara Mbeya. Sasa ngoja akajifunze maisha Mapya na watu wasiojua kingereza au kiswahili.

Sasa hivi akipost jambo Instagram linapata likes kumi au mia, message hazifiki 50. Muda utasema, na Diblo Dibala anahaha tu. Diblo Dibala ndiye mgombea pendwa wa Polepole ...bado Wana Nia ya kurejesha utaratibu wa kutupa watu baharini, kuteka, na kubambika kesi, kujizolea fedha kwenye akaunti za watu.
 
Back
Top Bottom