Hapo vip!!
Binafsi tokea mwanzo niliamini jamuhuri wapo sahihi na ni wakweli dhidi ya Mbowe,na hii inadhihirishwa katika maeneo haya.

Kwanza upeleleze wa Kingai sio wa mchezo mchezo ni mtaalam mwenye udhoefu wa muda mrefu katika maswala ya upelelezi na hii kesi ya Mbowe upelelezi wake ni umeanza muda mrefu sana sio juzi tokea mwa 2020.

Pili, ushahidi ya wakina Mahita ni ushahidi mzito sana...ni watu ambao ni mapapa wa system kwa muda..na serikali imewaanda hawa watu kwa pesa nyingi sana na kwa muda mrefu ili waweze kuisaidia taifa.

Tatu,Tanzani ni nchi bora sana Duniani kwa upelelezi na wapelelezi ni hawa waliompeleleza Mbowe..hivyo upelelezi wao ni wakitaalamu kama majibu ya Dactari

Nne,hukumu ndogo dhidi ya kesi ya mbowe ni ushahidi tosha ya kwamba upelelezi ni wakitaalam na u.efuata sheria.

Tano..gaidi sio mpaka mtu alipue bomu au ateke watu ndio anakuwa guidi...juzi uingereza jamaa mmoja alikuwa na mikakati ya kumteka mbunge tu basi akatuhumiwa kama gaidi.

Nimalize kwa kusema acheni ushabiki wa itikadi kwenye hili..wakina Kingai na wengine hawana interest yeyote dhidi ya kesi ya mbowe bali wanamshughulikia kama muhalifu yeyote mwenye makosa.
Sijaona Cha maana ulichoeleza zaidi ya maneno Mengi kama mzaramo,
Kama Huyo Kingai na Mahita ni makachelo waliobobea kama ulivyosema,weka CV zao tuone kama wamewahi kupata mafunzo nje,kwenye nchi kama Israel,UK,USA,au Cuba
 
Kichwa cha uzi nilidhani ndani nitakutana na ushahidi usiotia shaka! Nadhani wewe ni mbunge wa jimbo la hai kwa sasa, unamsagia kunguni mwenyekiti asijekutoka akagombea kukutoa kwenye jimbo.

Ukiachana na wale wanaopata maelekezo kutoka juu, sidhani kama mtanzania mwenye akili timamu anaweza kushabikia kufungwa kwa mbowe.

Maslahi yenu ninini enyi watu? Kwa muda mrefu sasa tunateseka kwa kukosekana kwa sauti ya upinzani bungeni, na bado!
Naona ametaja majina tu na kusifia sijaona ushahidi
 
Kutaka kuifanya nchi isitawalike,ni Jambo baya,Kama kweli alitaka iwe hivyo,kamwe asionewe huruma,alipwe sawasawa na usafi/uchafu wa mikono yake.
 
Bongo kuna upelelezi gani? Wanachokosea hapa TZ ni kuacha tracks lakini usipoacha tracks hakuna mpelezi bongo atakujua.
 

Wafilipi 4:4-7​

Neno: Bibilia Takatifu​

4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu ufahamike kwa watu wote. Bwana anakaribia kuja. 6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu
HAhahaha😂 hii ni kwa ajiri ya mbowe au?
Mungu anajua nia yake ilivyokua ovu sasa wewe hapo unamhangaikiana vifungu vya biblia?
Alisababisha kifo cha chacha wangwe na aqwilina na wengine huko arusha kwa vibomu vyake na wengine wakawa vilema.
Usimjalibu mungu kwenye mambo ya kishetani bwashee.
 
Kama nilivyoacha kufuatilia Media za ndani za nchi hii, ndivyo ambavyo nimeacha kufuatilia hii kesi feki ya kamanda wetu na sielewi wenzangu wanapata wapi nguvu na muda wa kuifutilia.

Chombo kinachoendesha hii kesi, kina watu wenye sifa kama za wale walioko kwenye ile tume ya kuvuruga uchaguzi,, hivyo hakuna kinachostahili kuitwa kesi.

Wakifanikiwa kumfunga Mwenyekiti, moja ya impact yake inaweza kuja kuwa ni kususia shughuli za hiki chombo kwa kesi zingine zote zinazowahusu makamanda wetu kwa siku using usoni.

Hata hivyo, Mungu ana makusudi kwa kila jambo na kumfunga huyu kamanda wetu ndio unaweza kuwa ni mwanzo wa anguko la hawa watu wasio na maarifa na pia kifungo hicho kitakuwa ni justification na catalyst ya kuendelea kudai katiba mpya

Hawa watu maarifa ni zero kabisa!
 
Nakuhakikishia akina Adamoo wangetumia mwezi mzima kukata Miti Ili iangukie Barabarani kutokea Morogoro Hadi Iringa.

Baada ya hapo lingeanza zoezi la kulipua masoko na "masheli" ya Dar ,Mbeya Arusha, Mwanza na kwingineko.

Baada ya hapo msako ungeanza Ili kumlaza Sabaya .
Jumla ya matumizi laki 6
Hii inahusisha per diem na nauli.kwa makomandoo wanne.
Badoo haijafahamika kama hiyo laki6 inahusisha malipo ya kazi yote.
 
Polishi wetu ni wazuri sana kwenye utengenezaji wa muvi na matukio! Ila safari hii naona wamechemka mbaya! Yaani mpaka watoto wachanga wanatambua fika hii kitu ni ya kubambikia!!
 
Nakuhakikishia akina Adamoo wangetumia mwezi mzima kukata Miti Ili iangukie Barabarani kutokea Morogoro Hadi Iringa.
Baada ya hapo lingeanza zoezi la kulipua masoko na "masheli" ya Dar ,Mbeya Arusha, Mwanza na kwingineko.
Baada ya hapo msako ungeanza Ili kumlaza Sabaya .
Jumla ya matumizi laki 6
Hii inahusisha per diem na nauli.kwa makomandoo wanne.
Badoo haijafahamika kama hiyo laki6 inahusisha malipo ya kazi yote.
Wangekata miti na bastora 😃😃
 
HABARI...

kwanza nikiri mara yangu ya kwanza kupiga kura ni 2020 na niliwapa CCM..

pili nikiri maovu yote ya uchaguzi nayafahamu na kuyafurahia (upande wa nafasi ya uraisi) maana upinzani bado unasafari ndefu kukamata nchi.

tatu nikiri kuchukizwa na kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni kama taifa tuliteleza na ni kosa ambalo hata CCM wanalijua na halitojirudia.

KWENYE MADA.
leo MBOWE anakabiliwa na kesi ugaidi lakini ni ukweli kwamba hii kesi haina mashiko na hakuna ugaidi wa aina hii na ninachojua mimi (mimi) kitengo cha ugaidi (CT) hakifanyi kazi kwa staili hii (wachache watanielewa) na kama kingefanya kazi kwa stail hii TANZANIA lingekua lango la magaidi.

CT wana ramani zao, mipaka yao, uongozi wao, safari zao, wahisiwa wao, watuhumiwa wao, mawasiliano yao, selo zao, silaha zao na mengine mengi ambayo hayawezi kuwa wazi kama huu upuuzi unaoendelea.

watanzania, CCM, raisi SAMIA, wabunge, mawaziri, viongozi wa dini n.k kuna siku MBOWE atakufa je tutaongea nini katika msiba wake??

je spika wa bunge utatoa taarifa gani kuhusu mbowe??

viongozi CCM katika mazishi mtavaa sare gani na mtatoa hotuba gani??

MAMA SAMIA kama utaenda msibani utawaambia nini watanzania na familia ya mbowe kwa kipindi hicho??

CHADEMA mtatoa hotuba ya aina gani siku hiyo.??

je serikali itatoa mchango gani katika mazishi yake???


binadamu huzaliwa na mwisho wake ni kufa hata MBOWE atakufa niliowataja fikirieni hili maana siku yaja.

MWISHO:

SIKU HIYO TUTAKUA WANAFIKI TULIOPITILIZA.
 
Hutaki wapinzani wakae ikulu lakini unawaamini wawepo bungeni, uko sawa kweli kichwani?

Yani unawaamini wapinzani wakatunge sheria bungeni, lakini ile kazi nyepesi ya kuwepo ikulu yenye wasaidizi wa kila aina huwaamini kama wanaweza kuifanya vizuri!
 
Back
Top Bottom