Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza Daktari aliyejimilikisha hospitali ya Amana kwa lengo la kujitajirisha achukuliwe hatua kali
Daktari huyo mwenye jina kapuni amebainika kutumia Vifaa vya Hospitali hiyo ambavyo vinamilikiwa na Serikali ili kuwatibu Wagonjwa lakini malipo yote alikuwa akiyapokea binafsi
Tuhuma dhidi yake zimetolewa na Mgonjwa kwa Wizara hiyo ambaye alilipishwa laki 7 na kuhudumiwa na Nesi huku akiwa amelazwa Gesti badala ya kulazwa kwenye Wodi za Wagonjwa na wala hakuambiwa anaumwa nini
Waziri wa Afya ameagiza hatua zote za kinidhamu zifuatwe katika kumshughulikia Daktari huyo. Ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dar es Salaam alipotembelea Hospitali ya Amana kujionea utendaji kazi.