Hospitali Binafsi ziache masihara na afya za Watanzania

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
BY MWANDISHI HURU

Takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32 zinaeleza kwamba kutokupokea mgonjwa kisa hitilafu ya bima ni kuvunja makubaliano.

Ifike hatua wafanyabiashara wa Tanzania waache kufanya masihara na afya za Wananchi, huu uhuni wa wafanyabiashara ufanyike kwenye mambo mengine sio kwenye Afya zetu. Kitendo cha hospital binafsi kutoa tamko la kusitisha huduma kwa wagonjwa kwa Masaa 48 kisa kutaka faida kubwa kutoka NHIF sio sahihi hata kidogo, hili peke yake linaonesha dhahiri shahiri hospitali hizi hazina huruma na afya za watanzania.

Bila kupapasa macho kila mmoja ni shahidi kwamba dawa na vifaa tiba vinavyouzwa kwenye hospitali binafsi ziko juu sana, Mfano Mtoto anaweza kuumwa homa tu dawa ukaambiwa elfu 50 wakati wao wanauziwa na serikali elfu 8 hapo bado bili ya kumwona Daktari zaidi ya elfu 60, Wakati ukienda hospital za serikali unatibiwa chini ya hapo, huu ni zaidi ya uhuni

Pongezi nyingi ziende kwa serikali kupitia Waziri wake wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kutoa tamko ambalo lipo wazi sana na liliweka mbele maslahi ya Watanzania

"Hatutamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka sheria ya kutoa huduma hivyo naomba wabadilishe matangazo yao isipokua mgonjwa wa dharura, tujikite kwenye kuwahudumia watanzania fedha Baadae" Amesema Waziri Ummy

Tayari Kamati ya Kitaalam iliyoundwa inaendelea na majadiliano hivyo hospitali zote ziendelee na kutoa huduma kama kawaida. Aliongeza Waziri Ummy

Binafsi natoa pongezi kwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa kuja na mpango wa dharura wa kuhudumia wagonjwa kupitia bima ya NHIF wale wataopata usumbufu kwenye hospitali binafsi, hii ni kubwa sana na imeonesha mfano wa kuingwa.
 
dawa ukaambiwa elfu 50 wakati wao wanauziwa na serikali elfu 8
Someni kwanza kabla hamjafungua nyuzi. Nani kakwambia hospitali binafsi zinauziwa dawa na serikali? Toka lini?

Takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32 zinaeleza kwamba kutokupokea mgonjwa kisa hitilafu ya bima ni kuvunja makubaliano.
Umeisoma hiyo sheria? Usiropoke. Hii sheria inahusu mgonjwa wa dharura (Emergency Care) mfano Unconcious patient (Mgojwa aliyepoteza fahamu au yupo altered), Convulsing patient (Mgonjwa aliye katika hali ya kifafa) n.k ambao hata kama hana bima wala pesa, lazima umpatie huduma kwanza ndipo swala la malipo lifuate.

Hii sheria haimaniishi mgonjwa kaja anatembea kisa bima haifanyi kazi umpe huduma bure.

This is a free market, huna haki ya kumlazimisha mtu akupe huduma kwa bei unayotaka wewe
 
BY MWANDISHI HURU

Takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32 zinaeleza kwamba kutokupokea mgonjwa kisa hitilafu ya bima ni kuvunja makubaliano.

Ifike hatua wafanyabiashara wa Tanzania waache kufanya masihara na afya za Wananchi, huu uhuni wa wafanyabiashara ufanyike kwenye mambo mengine sio kwenye Afya zetu. Kitendo cha hospital binafsi kutoa tamko la kusitisha huduma kwa wagonjwa kwa Masaa 48 kisa kutaka faida kubwa kutoka NHIF sio sahihi hata kidogo, hili peke yake linaonesha dhahiri shahiri hospitali hizi hazina huruma na afya za watanzania.

Bila kupapasa macho kila mmoja ni shahidi kwamba dawa na vifaa tiba vinavyouzwa kwenye hospitali binafsi ziko juu sana, Mfano Mtoto anaweza kuumwa homa tu dawa ukaambiwa elfu 50 wakati wao wanauziwa na serikali elfu 8 hapo bado bili ya kumwona Daktari zaidi ya elfu 60, Wakati ukienda hospital za serikali unatibiwa chini ya hapo, huu ni zaidi ya uhuni

Pongezi nyingi ziende kwa serikali kupitia Waziri wake wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kutoa tamko ambalo lipo wazi sana na liliweka mbele maslahi ya Watanzania

"Hatutamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka sheria ya kutoa huduma hivyo naomba wabadilishe matangazo yao isipokua mgonjwa wa dharura, tujikite kwenye kuwahudumia watanzania fedha Baadae" Amesema Waziri Ummy

Tayari Kamati ya Kitaalam iliyoundwa inaendelea na majadiliano hivyo hospitali zote ziendelee na kutoa huduma kama kawaida. Aliongeza Waziri Ummy

Binafsi natoa pongezi kwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa kuja na mpango wa dharura wa kuhudumia wagonjwa kupitia bima ya NHIF wale wataopata usumbufu kwenye hospitali binafsi, hii ni kubwa sana na imeonesha mfano wa kuingwa.
...niliandika andiko la namna hii jana, kiufupi serikali iwachukulie hatua
 
Je kama huyo mtu ameshavunja mkataba na NHIF inakuaje.
Unalazimishaje mtu atoe huduma wakati humnunulii dawa,humlipii pango wala mishahara?
Watu waache kutafuta vifungu vya kubana watu. Serikali inakataa kutoa fedha kutoa kiasi ambacho wamiliki wahospitali wanaona kinakidhi mahitaji.
Siasa hazifai wapunguze ubishi waache sekta binafsi ifanye kazi wao hawawezi wafanye zaidi siasa
 
BY MWANDISHI HURU

Takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32 zinaeleza kwamba kutokupokea mgonjwa kisa hitilafu ya bima ni kuvunja makubaliano.

Ifike hatua wafanyabiashara wa Tanzania waache kufanya masihara na afya za Wananchi, huu uhuni wa wafanyabiashara ufanyike kwenye mambo mengine sio kwenye Afya zetu. Kitendo cha hospital binafsi kutoa tamko la kusitisha huduma kwa wagonjwa kwa Masaa 48 kisa kutaka faida kubwa kutoka NHIF sio sahihi hata kidogo, hili peke yake linaonesha dhahiri shahiri hospitali hizi hazina huruma na afya za watanzania.

Bila kupapasa macho kila mmoja ni shahidi kwamba dawa na vifaa tiba vinavyouzwa kwenye hospitali binafsi ziko juu sana, Mfano Mtoto anaweza kuumwa homa tu dawa ukaambiwa elfu 50 wakati wao wanauziwa na serikali elfu 8 hapo bado bili ya kumwona Daktari zaidi ya elfu 60, Wakati ukienda hospital za serikali unatibiwa chini ya hapo, huu ni zaidi ya uhuni

Pongezi nyingi ziende kwa serikali kupitia Waziri wake wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kutoa tamko ambalo lipo wazi sana na liliweka mbele maslahi ya Watanzania

"Hatutamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka sheria ya kutoa huduma hivyo naomba wabadilishe matangazo yao isipokua mgonjwa wa dharura, tujikite kwenye kuwahudumia watanzania fedha Baadae" Amesema Waziri Ummy

Tayari Kamati ya Kitaalam iliyoundwa inaendelea na majadiliano hivyo hospitali zote ziendelee na kutoa huduma kama kawaida. Aliongeza Waziri Ummy

Binafsi natoa pongezi kwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa kuja na mpango wa dharura wa kuhudumia wagonjwa kupitia bima ya NHIF wale wataopata usumbufu kwenye hospitali binafsi, hii ni kubwa sana na imeonesha mfano wa kuingwa.

Ng'ombe analazimishwa kunywa maji?
 
Back
Top Bottom